ECG The Jesus Nation Church Kilimanjaro Branch

ECG The Jesus Nation Church Kilimanjaro Branch Church

DAY 04 -HUKUMU YA HAMAN Esta 6:1 “Usiku ule mfalme hakupata usingizi; akaamuru aletewe kitabu cha maandiko ya taarifa, n...
13/08/2026

DAY 04 -HUKUMU YA HAMAN

Esta 6:1 “Usiku ule mfalme hakupata usingizi; akaamuru aletewe kitabu cha maandiko ya taarifa, nayo yakasomwa mbele ya mfalme.”

Mordekai alifanya kazi ya kumlinda Mfalme kutoka kwa Bigthana na Tereshi lakini hakupata heshima anayostahili kwa muda mrefu, hii inalandana na maisha ya kawaida kuwa mtu anaweza kufunga kitabu chako na usipate yale ambayo unastahili.

Kuna roho zimeapa kuwa kitabu chako kisifunguke kwenye maisha yako na kuna namna ambayo Shetani anaweza kubadilisha kurasa za kitabu chako mfano kwenye kitabu cha biashara anaweza akakuwekea kwenye kurasa zako madeni, hasara n.k. na hii hupelekea unakuwa kwenye sehemu moja bila mafanikio. Lakini Mordekai hakusimama bila maombi aliomba na Mungu alimuheshimisha upya.

Maombi machache ya kusimama nayo siku ya leo
- Kufungua kitabu chako kilichofungwa na Roho za Haman miaka na miaka kiende kufunguka leo
- Kila heshima yako iliposhushwa ikarejee kwenye maisha yako (Modekai alichukuliwa kwa hali ya kawaida kutokana na kazi alikuwa anaifanya lakini baada ya kitabu chake kufunguka heshima ilirudi )

NI MAOMBI YANGU KWAKO KUWA KILA KITABU CHAKO KILICHOFUNGWA( NDOA, HABARI NJEMA, FURAHA, AMANI, HESHIMA, BIASHARA) KIKAFUNGUKE NA KILA KURASA MBAYA ZILIZOWEKWA NA SHETANI ZIKACHANIKE KWA JINA LA YESU
MAOMBI YA MCHANA BADO YANAENDELEA NSSF GHOROFA LA NNE KUANZIA SAA SITA NA NUSU MCHANA MPAKA SAA NANE KAMILI MCHANA (12:30pm-2;00pm).
Prophet Shepherd Bushiri
Prophetess Mary Bushiri
ECG The Jesus Nation Church Tanzania
Mtalemwa Dionis Rweyemamu
Boneka Adolph Boneka

DAY 03    HUKUMU YA HAMAN VITA YA HAMAN NA MORDEKAI Esta 6;1 Usiku ule Mfalme hakupata usingizi akaaamuru kitabu cha maa...
12/08/2026

DAY 03 HUKUMU YA HAMAN
VITA YA HAMAN NA MORDEKAI

Esta 6;1
Usiku ule Mfalme hakupata usingizi akaaamuru kitabu cha maandiko ya Taarifa nayo yakasomwa mbele yake.

Roho ya Haman inaficha ukweli kuhusu wewe, lakini unapokuwa mwaminifu kwa Mungu na kuyatii maagizo yake yeye huwa mwaminifu kwa na hukuvisha mavazi ya kifalme.
Kuna watu ni wazuri kwenye kuongea na kusababisha ushawishi na uchonganishi wa kiovu kwa watu wengine , na hii huinua chuki kwa watu wanaokuzunguka ama watu waliokuwa wakikuheshimu wamekuwa hawakuheshimu tena.
Lakini kupitia biblia Modekai alipompasha habari Esta, hawakusimama kimwili walifunga na kuomba kwa takribani siku tatu ili wapate jawabu kutoka kwa Mungu. Na Mungu alisimama na Mordekai. Hii inamaana ya kwamba neno la Mungu ni kweli na amini na wakati wake hauwezi kupingwa wala kuzuiliwa

“LAZIMA UJUE KUWA HAKUNA VITA INAYOPIGWA KIMWILI LAZIMA UWE MUOMBAJI NA MSOMAJI WA NENO“
MAOMBI YANAENDELEA TENA SIKU YA KESHO NSSF JENGO LA UCHUMI KUANZIA SAA SITA NA DAKIKA 45 MPAKA SAA NANE MCHANA.
Prophet Shepherd Bushiri
Prophetess Mary Bushiri
ECG The Jesus Nation Church Tanzania
Boneka Adolph Boneka

DAY 2 HUKUMU YA HAMAN Roho Ya Haman ni roho inayotunga sheria kwaajili ya kuchonganisha wengine, kuchelewesha baraka za ...
11/08/2026

DAY 2 HUKUMU YA HAMAN
Roho Ya Haman ni roho inayotunga sheria kwaajili ya kuchonganisha wengine, kuchelewesha baraka za watu n.k Kupitia biblia tunamsoma Haman alisimama k**a kikwazo cha Modekai kupokea Baraka ya kazi aliyokuwa ameifanya Esta 3;6; Zifuatazo ni baadhi ya kazi chache
1. Roho Ya Haman inatamka, hutoa matangazo au matamko ili yafanye kazi kwenye maisha yako ili yaharibike
2. roho ya Haman husimama kuweka alama ya uharibifu kwenye familia Kuna hali ambayo imezoeleka kuwepo kwenye familia mfano magonjwa, kutokuolewa, kusoma na kutokupata kazi, Aibu, Kukataliwa, Mauti n.k
3. Roho ya Haman husimama kuongea au kutoa repoti mabaya kwa watu wengine mfano kazini ili ufukuzwe kazi,
4. Roho ya Haman husimama kupanga maovu kwenye maisha yako ili usifike kwenye hatima yako

KESHO TUNAENDELEA NA MAOMBI HAPA ,NSSF GHOROFA YA 4 KUANZIA SAA SITA NA DAKIKA 45 (12;45pm) MPAKA SAA NANE MCHANA.
Prophet Shepherd Bushiri
Prophetess Mary Bushiri
ECG The Jesus Nation Church Tanzania
Mtalemwa Dionis Rweyemamu
Boneka Adolph Boneka

HUKUMU YA HAMANI -DAY 01 Roho Ya Haman ni roho inayotunga sheria kwaajili ya kuchonganisha wengine, kuchelewesha baraka ...
10/08/2026

HUKUMU YA HAMANI -DAY 01

Roho Ya Haman ni roho inayotunga sheria kwaajili ya kuchonganisha wengine, kuchelewesha baraka za watu n.k Kupitia biblia Esta 2;1 Modekai alitoa taarifa kuhusu kifo cha Mfalme lakini, lakini taarifa zilipofika kwa Mfalme hazikufika kwa jina la Modekai zilifika kwa jina la Haman.
Lakini pia Esta 3;1-10 inaeelzea namna Haman alivyotumia nafasi yake ya kuwa karibu na Mfalme na akaweza kupokea cheo badala ya Modekai
Hii inamaana kubwa sana, kuna watu wanafanyakazi lakini matokeo ya kazi walizofanya hupokea wengine, hivyo wengine wamekuwa wakisimama aidha kwenye hasara, kubaki sehemu moja bila maendeleo.

Na ndio maana Wiki Hii Hapa NSSF GHOROFA YA 4 KUANZIA SAA SABA MCHANA Tutakuwa Tukifanya Maombi na kila Haman kwenye maisha Yako lazima aachie Nafasi yako na Maisha yako hayatabaki k**a ulivyo.
Prophet Shepherd Bushiri
Prophetess Mary Bushiri
ECG The Jesus Nation Church Tanzania
Boneka Adolph Boneka

Kwa Neema ya Mungu, ni wiki nyingine Mungu ametupa tutaenda kuwa na maombi ya HUKUMU YA HAMANI. Yapo Mambo mengi kwenye ...
09/08/2026

Kwa Neema ya Mungu, ni wiki nyingine Mungu ametupa tutaenda kuwa na maombi ya HUKUMU YA HAMANI. Yapo Mambo mengi kwenye maisha yako ambayo Hamani ameyazuia, au kufanya usahaulike kwenye milango ya baraka zako
Wiki hii pale NSSF GHOROFA YA NNE, MIMI BISHOP BONEKA, Nitakufundisha na tutaomba pamoja yule Hamani alieshikilia maisha yako ataachia na utakuwa huru KWA JINA LA YESU

USIKOSE JUMATATU HADI IJUMAA SAA SABA MCHANA , PIA TUTAKUWA LIVE KWENYE ACCOUNT YA YOUTUBE (apostle boneka)
Prophet Shepherd Bushiri
Prophetess Mary Bushiri
ECG The Jesus Nation Church Tanzania
Boneka Adolph Boneka

LIVE UPDATE | SUNDAY SERVICE | SUNDAY OF FRESH FIRE | PARACH SESSION | PASTOR FREDYParach ni Kitabu cha maombi ya kila s...
09/08/2026

LIVE UPDATE | SUNDAY SERVICE | SUNDAY OF FRESH FIRE | PARACH SESSION | PASTOR FREDY

Parach ni Kitabu cha maombi ya kila siku kilichoandaliwa na Bba yetu wa kiroho Major 1(Prophet Shepherd Bushiri) Kwaajili ya kukuza imani na kiwango cha kulifahamu neno la Mungu.
Prophet Shepherd Bushiri
Prophetess Mary Bushiri
ECG The Jesus Nation Church Tanzania
Mtalemwa Dionis Rweyemamu
Boneka Adolph Boneka

LIVE UPDATE | SUNDAY SERVICE | SUNDAY OF FRESH FIRE | INTERCESSION | LEV SEBASTIAN Ibada Imeshaanza kwa Maombi ya nguvu ...
09/08/2026

LIVE UPDATE | SUNDAY SERVICE | SUNDAY OF FRESH FIRE | INTERCESSION | LEV SEBASTIAN

Ibada Imeshaanza kwa Maombi ya nguvu kuandaa ibada kubwa ya mstari wa maombezi. Bado hujachelewa karibu sana na mUNGU ATAKUHUDUMIA

Mathayo 13:13
Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.
Prophet Shepherd Bushiri
Prophetess Mary Bushiri
ECG The Jesus Nation Church Tanzania
Mtalemwa Dionis Rweyemamu
Boneka Adolph Boneka

Address

Moshi

Telephone

+255784572929

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ECG The Jesus Nation Church Kilimanjaro Branch posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to ECG The Jesus Nation Church Kilimanjaro Branch:

Shortcuts

Share