22/09/2020
JUMAPILI TAREHE 20/09/2020.
MCH: DEBORA UDIBO.
SOMO: KUSAMEHE NA KUSAMEHEWA.
MATHAYO 18:15-35
katika maisha ya sasa ya watu wengi, kinacho wasumbua wengi ni swala la Kusamehe na kutangaza msamaha.. Kutosamehe inapelekea mengi k**a magomjwa na hata uadui. Watu wa Mungu tunatakiwa tuelewe kwamba Usiposamehe tuu hasira na ghadhabu ya mungu inakuwa juu yako. Kwa sababu hata Mungu wetu ni Yule ambaye hutusamehe kila mara. KWA NINI USHINDWE KUSAMEHE?
Mwana wa Mungu elewa na jua kwamba msamaha ni uzima. Ukitaka maisha marefu na yenye amani ,furaha na yaliyo funguka , basi jifunze kusamehe. Wewe k**a mwana na mtoto wa Mungu lazima kujifunza sifa,tabia na amri za Mungu..Mungu mwenyew ana amuru kwamba ili kwamba yeye atusamehe basi na sisi yatupasa kusamehe wengine.
Samehe ili Uchanue, ustawi,na uwone mtembeo wa Mungu Katika maisha yako.Kuwa na amani na watu wote. Kwa namna hiyo unaiponya mwenyewe. Ukitaka kuwa mtu aliye mwepesi wa kusamehe chunguza sifa za na utaratibu wa Mungu.
Mwana wa Mungu pale unaposhindwa Kusamehe au kutangaza msamaha basi tafuta msaada kutoka patakatifu pa Mungu.