Tumaini la utukufu ulimwenguni.

Tumaini la utukufu ulimwenguni. Serving Souls to Heaven.

HAPPY NEW MONTH.MWEZI WA KUANZA KUONEKANA KILA JAMBO LILILOKUWA LIMEFICHWA NA ADUI KWAKO.ANDIKO KUU Mwanzo 8:5[5]Maji ya...
01/10/2025

HAPPY NEW MONTH.

MWEZI WA KUANZA KUONEKANA KILA JAMBO LILILOKUWA LIMEFICHWA NA ADUI KWAKO.

ANDIKO KUU

Mwanzo 8:5
[5]Maji yakapunguka-punguka hata mwezi wa kumi; mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.

Kilele humaanisha ukamilifu wa kitu, Kila UBORA na MAFANIKIO Yako yaliyokuwa haya onekani, ni neema ya Mungu Tena iko Kwa ajili ya kuanza kuonekana OCTOBER.

THE MONTH OF COMPLETION OF GOD'S DIVINE ORDER.

THE MONTH OF REIGN

AMUA KUTAFUTA WAPI UMEKWAMA NA SIO KUSUBIRI KILELE KWAKO KIFIKE.
SIO RAHISI KWA WATU WARAHISI BALI NI RAHISI KWA WATU WAGUMU WANAO AMUA KUFANYA KITOFAUTI NA MWANZO WAO.

DAILY HOPE________________________________________________ *MONDAY 15 SEPT 2025.*  *UJUMBE:* *KUWA WAKILI MWAMINIFU WA M...
15/09/2025

DAILY HOPE
________________________________________________

*MONDAY 15 SEPT 2025.*

*UJUMBE:* *KUWA WAKILI MWAMINIFU WA MUNGU.*

*Luka 12:42*
```Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye WAKILI MWAMINIFU, mwenye BUSARA, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?``` .

WAKILI ( steward ) ni mtu ambaye amepewa nafasi ya kuwa msimamizi wa mali, nyumba au kitu chochote Kwa ajili ya mtu mwingine ( bosi).

Sifa kuu mbili za uwakili ni uaminifu na busara, Leo tunatizama Kwa suala la uaminifu tu.

YESU alitumia hili akiwa anamaanisha Kwamba ni nani ambaye ataweza kusimama Kwa uaminifu amweke kwenye utumishi awahudumie wengine Kwa mali zake, fedha zake, nguvu zake pamoja na Muda.

Mwamini unahesabika k**a WAKILI kwasababu

na mali zote umepewa na MUNGU

na vipawa ulivyonavyo umepewa na Yesu.

@ umepewa muda (siku za kuishi) na MUNGU

@ umepewa mwili na Mungu

MUNGU anataka mtu atakaye weza kutumia muda aliopewa, nguvu, mali na karama Kwa ajili ya kuujenga ufalme wa Mungu.

✍️Ukiwa wakili usiyekuwa mwaminifu sahau kuaminiwa na MUNGU Kwa mambo makubwa katika utumishi. Utumishi sio madhabahuni tu inaweza kuwa ni ofisini na biashara

✍️Ukiwa wakili usiyemwaminifu, ni wazi kuwa utakosa taji mbinguni.

*OMBA NAMI.....*

Baba Asante Kwa neno asubuhi ya Leo, Ikiwa ni wiki nyingine niweze nikawe wakili mwaminifu Kwa Kila Dak ya muda wangu ulionipa kuwa hai, nitumie nguvu zangu Zote Kwa ajili ya ufalme wa Mungu, mali zangu na karama Ili nikutumikie Kwa viwango vyako.
Asante Yesu Kwa neema na baraka zako. AMINA.


*Joel Osteen..*  *What follows  "I AM "* 📍Mimi ni masikini.. roho ya umasikini inaanza kukujia.📍Mimi ni mzee- uzee unaan...
01/08/2025

*Joel Osteen..*
*What follows "I AM "*
📍Mimi ni masikini.. roho ya umasikini inaanza kukujia.
📍Mimi ni mzee- uzee unaanza kukujia 🤣🤣
📍Mimi nitakufa tu- roho ya mauti inaanza kukujia
📍Mimi staolewa- roho ya kukataliwa inaanza kukujia🤣
📍Mimi staoa - wadada wanaanza kukukimbia hata k**a unawasalimia Bwana asifiwe 🤣🤣 ( shetani buana)
📍Mimi stafaulu - roho ya kufeli inakujia Kwa Kasi🤣

JIFUNZE KUJITAMKIA MANENO YA BARAKA KWA ULIMU UNAUMBA.
📍Mimi nimebarikiwa - baraka zinaanza Kuja kwako
📍Mimi nitaolewa mwaka huu - kibali kinaanza kujia🔥
📍Mimi nitaoa mwaka huu - mchumba kutoka Kwa Mungu anakuja🔥
📍Mimi stakufa - afya inakujia
📍Mimi ni HB / BT - UZURI UNAKUJIA🤣🤣

✍️IKIWA UNAKIRI PAMOJA NAMI MAMBO MAZURI NIONE LIKE ZA KUTOSHA KATIKA JINA LA YESU....

GOD CAN CHANGE YOUR TEARS INTO JOY.UMA UKPAI ni mwinjilisti na mchungaji mkubwa wa uamsho hko Nigeria wakati akiwa akija...
05/05/2025

GOD CAN CHANGE YOUR TEARS INTO JOY.

UMA UKPAI ni mwinjilisti na mchungaji mkubwa wa uamsho hko Nigeria wakati akiwa akijana familia yake ili mfukuza nyumbani sababu ya kuokoka, basi ikabidi ahamie kanisani Kwa machozi na maumivu makali sana, wakati akiwa anaishi kanisani alikutana na mchungaji wake akamweleza Hali yake inayomkuta badae mchungaji alimchukua akawa anakaa naye nyumbani kijana UMA. akiwa Kwa mchungaji wake alikaa Kwa muda na maisha yalikuwa mazuri sasa akasahau maumivu na machozi ya kipindi Cha nyuma. badae kijana UMA alibadika kwani alianza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na dada mmoja ambapo alikuwa akikutana na hyo dada kwenye jumba Moja ambalo lilikuwa halijaisha kujengwa. siku si nyingi alik**atwa na taarifa kumfikia mchungaji ambaye alikuwa mlezi wake sasa baada ya kufukuzwa nyumbani kwao. mchungaji aliamua kumfukuza kijana UMA kwani aliona k**a kijana amemdharirisha sana na kanisa Kwa ujumla. kijana UMA maumivu na machozi yalirudi yakiwa mara mbili yake sababu hakuwa na pakula chakula Wala kulala, UMA aliamua kukaa kwenye lile jumba alilokuwa akitumia kufanya mapenzi na yule dada, usiku mchana alianza kuomba Toba na kumlilia Mungu amrudie tena. MUNGU alimjilia Tena akajaa Roho mtakatifu, watu waliopita karibu walivutwa na nguvu za Mungu katika lile jumba alokuwa akikaa.
UMA UKPAI alipata neema Tena akarudi kanisani ambapo alitumika akihubiri mikutano pale kijijini watu walifunguliwa miujiza ikitendeka. katika historia ya watumishi wa Mungu walowahi Kutokea Nigeria na Dunia Kwa ujumla kijana UMA UKPAI ni mmoja wapo ambae sasa anakanisa kubwa na chuo Cha biblia hko nchini.

KUMBUKA. EWE KIJANA........

MUNGU NI MUNGU WA REHEMA, MUNGU ANAWEZA KUKUTAKASA TENA.

RUDI KWAKE KWA TOBA NA MGEUKO WA NDANI WA KUAMUA KUACHA NJIA MBAYA.

.
.

MAMBO YAKAYOKUSAIDIA KUWA NA UFANISI KATIKA HUDUMA YA VIJANA.Ili uwe na Ufanisi katika kuwahudumia vijana inabidi uwe na...
05/05/2025

MAMBO YAKAYOKUSAIDIA KUWA NA UFANISI KATIKA HUDUMA YA VIJANA.

Ili uwe na Ufanisi katika kuwahudumia vijana inabidi uwe na mambo yafuatayo ;

1. HUDUMA YA VIJANA NI KURITHISHA MAARIFA YA KIMUNGU KIZAZI KIMOJA KWENDA KINGINE.

Mungu amekupa agizo hilii wewe uwaandae watumishi wakubwa wajao. Ukiwa k**a mwl au mchungaji wa vijana, Mungu amekupa neema ya kuwarithisha shuhuda na matendo makuu ya Mungu uliyoyaona katika maisha Yako.
Zaburi 48:12-13
[12]Tembeeni katika Sayuni, Uzungukeni mji, Ihesabuni minara yake,
[13]Tieni moyoni boma zake, Yafikirini majumba yake, Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja.
Zaburi 71:17-18
[17]Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu; Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo.
[18]Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako.
Zaburi 78:4,6
[4]Hayo hatutawaficha wana wao, Huku tukiwaambia kizazi kingine, Sifa za BWANA, na nguvu zake, Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya.
[6]Ili kizazi kingine wawe na habari, Ndio hao wana watakaozaliwa. Wasimame na kuwaambia wana wao.
Mambo ya Walawi 3:17
[17]Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa.
Huduma ya vijana ni Mwendelezo wa kufanya kile ambacho Mungu anafanya kwenye kizazi hiki kiweze kufanyika hata Kwa kizazi kinachokuja. Ipo hasara kubwa sana ya kuacha watoto wasipate kujua matendo makuu ya Mungu aliyoyatenda kwani hii ndyo sababu ya kuinuka kizazi kisicho mjua Mungu kabisa.
Waamuzi 2:7-11
[7]Watu hao wakamtumikia BWANA siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioendelea siku zao baada ya Yoshua, hao waliokuwa wameiona hiyo kazi kubwa ya BWANA yote, aliyokuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.
[8]Kisha Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa BWANA, akafa, naye alipata umri wa miaka mia na kumi.
[9]Nao wakamzika katika mpaka wa urithi wake katika Timnath-heresi, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi.
[10]Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua BWANA, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.
[11]Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya BWANA, nao wakawatumikia Mabaali.

Kizazi kisicho mjua Mungu ni kizazi gani?
🌷Ni kizazi kisicho jua matendo makuu ya Mungu baba na ukuu wake.
🌷Ni kizazi chenye maarifa mengi ya kidunia kuliko ya Ki-Mungu
🌷Ni kizazi chenye ukaidi.

Inafaa sana vijana wadogo wajifunze utumishi. Kwani ipo faida kubwa ya kutumika ukiwa kijana mdogo.
Daudi alimuua Goliati akiwa. Kijana mwenye umri wa miaka 15 na 17, Yusufu aliota ndoto kubwa akiwa kijana wa miaka 17, yohana aliyekuwa mwanafunzi wa Yesu alianza kimfuata Yesu akiwa na miaka 16. Pia hata Yesu mwenyewe alianza kukaa barazani na kuhojiana neno la Mungu akiwa na miaka 12.

2. KUWA KIONGOZI AMBAYE NI MFANO WA KUIGWA ( Role Model)

K**a mtumishi uliyeitwa kutumika Kwa vijana, unapaswa kuwa mfano kwako Kwa kuyaishi Yale unayofundisha. Watoto na vijana wote hujifunza hasa Kwa mifano, Kwa hyo wewe utakuwa mtu wa kuigwa k**a utakuwa na tabia Inayoendana na kile unachokisema.
Mara nyingi Yesu alifundisha Kwa kuonyesha mfano halisi ili nao wafanye, Paul anasema nifuateni Mimi k**a ninavyo mfuata kristo.
Maeneo matatu ya chaguzi za maisha ya vijana unapaswa kuwasaidia.

i. Vocational choice ( uchaguzi wa fani au kazi ya kufanya )
Vijana hujiuliza sana nitafanya kazi gani kwenye maisha Yangu? ( who am I going to do with my life ).
K**a mtu uliyeitwa kufundisha vijana unapaswa kuwaongoza vijana wawe na chaguzi zilizo sahihi Kwa kuwasaidia kujua nini Mungu ameweka ndani Yao kufanya wawapo hai.

ii. Life- mate choice ( uchaguzi wa mwenza wa maisha).
Vijana wengi hupata shida sana kujua nani atamuoa au ataolewa naye ( who am I going to marry)
Simama ukiwaelekeza ili wawe kufanya maamuzi yaliyosahihi katika eneo Hilo.
iii. Value selection ( Nini wataamini kwenye maisha Yao yote?)
Hii inahusu ni kitu gani Wana amini na kukishika K**a hukumu ya utu wao wa ndani.
Vijana wengi hukosa mwelekeo thabiti wa kiimani ambapo hufanya Kila mmoja awaze na kuamua kivyake tu. Wengi wao wakiishia kuamini miungu kwenye maisha Yao.
Waelekeze chaguzi iliyosahihi ya kumwamini Yesu kristo katika maisha Yao Kwa kuwaonyesha uzuri wa kuwa na Yesu kwenye maisha Yao pia kuwafundisha juu ya hukumu ya Mungu Kwa watu wote wasio mwamini kristo kwani yeye ndye njia pekee ya kweli na uzima .

3. KUFUNDISHA NENO LA MUNGU( Teaching God's word)

Mathayo 28:19-20
[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
[20]na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Andiko hili linatupa agizo kuu la kufanya kwetu Kwa MUNGU, kuwafundisha wengine amri za Mungu yaani neno la Mungu k**a sisi alivyotufundisha.

Kwanini tunapaswa kufundisha neno la Mungu Kwa vijana?

I. Huduma ya vijana imejengwa katika fundisho la neno la Mungu. Ambapo itawasaidia Kujenga msingi imara ( solid foundation) Kwa ajili ya maisha Yao.
Msingi imara Kwa vijana unajengwa Kwa neno la Mungu, kijana akijaza neno la Mungu itampa Kushinda majaribu na Hila za adui shetani.
Luka 6:46-49
[46]Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?
[47]Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake.
[48]Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.
[49]Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa.

Mfundishe kijana neno la Mungu ili dhoruba na mafuliko yakija asianguke katika jina la Yesu...
Mambo mhimu ya kujua na kujiandaa k**a mtumishi Kwa vijana.

Katika filosofia ya kigiriki walimu walipaswa kujua mambo haya wanapokuwa wanaenda kufundisha, hatuna budi nasisi kuweza kuyajua haya ili yatusaidie katika kuwajenga vijana katika neno la Mungu.

I. Pathos
Maana yake ni kwamba mwl. Anapaswa na shauku ya ndani ( deeply passion) ya kutaka kufundisha vijana.
Mara nyingi watu hufundisha waooo na vijana sababu tu wanaona hawana kazi na wapo tu huru, unakuta unaenda kufundisha ukiwa k**a umelazishwa bila kuwa na mwito na msukumo wa ndani wa kutaka kuwajenga watoto walijue neno la Mungu.
K**a mwl. Na mtumishi wa MUNGU Kwa watoto na vijana Jenga shauku na Nia dhabiti ya kutaka kufundisha vijana.

ii. Logos
Logos maana yake neno la Mungu, unapaswa kujiandaa vizuri Kwa neno la Mungu, usikurupuke na kwenda kufundisha vijana hakikisha una neno ulilojiandaa kuwafundisha watoto siku hyo.

iii. Ethos
Imani na matendo Yako Kwa kufuata kile unachofundisha. Mwl. Unapaswa kukiishi unachofundisha kijana. Yesu alifundisha mambo ambayo ni maisha yake ya Kila siku.

4. PANGA SHUGHULI ZITAKAZO WASHIRIKISHA WOTE KWA PAMOJA.

Waebrania 10:24
[24]tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri;
Mwl. Au mchungaji wa vijana panga matukio ambayo yatawafanya vijana wote washiriki, hii inaweza kupangwa Kwa kusudi la kujuana na kufahamiana zaidi kwani vijana wakifahamiana ni rahisi kujengana Kwa tabia njemaa. Pia inapunguza Kwa kuwa na makundi au urafiki na. Watu ambao hawana Imani sawa yaani hawajaokoka. Kumbuka vijana wengi huharibika sababu ya kuwa na shughuli za pamoja na vijana ambao hawajaokoka huko nje.
1 Wakorintho 15:33
[33]Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
K**a mazungumzo mabaya yanaharibu tabia njema, pia mazungumzo mazuri yanaweza Jenga tabia nzuri zaidi Kwa vijana.
Shughuli hizi ni pamoja na ;
.Michezo (. Kuimba, dance ) Chakula Drama.

5. WAPE NAFASI YA KUTUMIKA ( opportunities for Christians services)

Baada ya kuwafundisha vijana wape nafasi ya kutumika kanisani, inaweza kuwa kwenye kanisa la watoto au kanisa kubwa k**a kufanya usafi kanisani, kupanga viti na kutoa sadaka pia hata huduma za nje k**a ushuhudiaji na umisheni.
Kusudi la Yesu wakati akiwa duniani ilikuwa ni kuwafundisha wanafunzi ili wawe k**a yeye, ndivyo ilivyo kwetu pia,. Tunafundisha vijana ili wafanye k**a sisi tunavyofanya.
Yesu alifundisha Kwa njia ifuatayo ambayo nasisi yaatupasa kuifuata ili kuwakuza vijana kwenye utumishi.

I. Unafundisha, yeye akisikiliza
ii. Nafanya, yeye Akiwa anaangalia.
iii. Anafanya nikiwa namwangalia, ( hapa akikosea namrekebisha ili afanye Kwa ubora zaidi)
iv. Anafanya na kuniletea taarifa.

6. FANYA KILA JAMBO KWA KIASI.

Fanya kwa kiasi mambo yote k**a vile mafundisho ya biblia, shughuli za nje, kutumika na maombi.
Hii ni Kwa sababu vijana Wana kikomo Cha umakini ambao wanaweza kuwa nao wakati wa kujifunza biblia, kuomba, na kutumika. Kwa hiyo Fanya Kwa kiasi tu ili wawe na shauku ya kukusimiliza kesho Tena. Ukifundisha Kwa muda mrefu itafika wakati hawata kuelewa unachofundisha.

SOMA ZAIDI KITABU
EFFECTIVE YOUTH MINISTRY

.
.

MISEMO YA WATU WENGI. Muda ukifika Namimi nitafanikiwa.Swala la muda tu nami ntaishi na mke wangu vizuri.Muda ukifika na...
20/03/2025

MISEMO YA WATU WENGI.

Muda ukifika Namimi nitafanikiwa.

Swala la muda tu nami ntaishi na mke wangu vizuri.

Muda ukifika nami ntakuwa nahuduma kubwaaa........

Sasa naomba utakafakari vizuri, wakati unasema ni suala la muda tu,

📍Je unaona hayo mafanikio sasa toka moyoni au ni hisia tu( emotiona) ?

📍Je unafanya nini kuhakikisha unaifikia kesho Yako iliyobora zaidi k**a unavyosema?

Makaburi yamejaza watu waliokuwa wanasubiri muda ufike waone mafanikio ( destiny) lakini sababu hawakuweza kuyaona toka moyoni na kufanya hatua kufikia kesho waliishia hapo walipoishia bila kuona mafanikio Yao .

Kuwaza kuhusu kufanikiwa kesho ni suala jingine na kufanikiwa kwenyewe ni suala jingine.
MUNGU ndye aliyeweka mafanikio ndani Yako,
Efeso 1:3
Hutengenezi mafanikio mengine nje na Yale uliwekewa na Mungu ndani Yako,

Ninaposema Kesho uione toka moyoni, ni kuona mafanikio ( baraka) katika eneo husika aliyoiweka Mungu ndani Yako.
MUNGU amekuumba ili ufanikiwe katika eneo Fulani la maisha Yako.

Nini Cha kufanya ili kesho Yako iwe halisi?

1. WEKEZA katika maarifa kwenye Hilo eneo.
Maarifa ni pamoja na ;
Kujua ahadi za MUNGU katika eneo Hilo
Kujua nguvu iliyopo katika eneo Hilo itakayokupa kufanikiwa.
Kujua mipaka Yako, kwamba nini unapaswa kufocus.
2. Anza kutenda.
Unahitaji nguvu ya kuanza kutenda, huwezi jikuta tu umekuwa jitu la Imani hafu hujapambana na vipepo. Daudi asingemuua goriati k**a asingekuwa ameanza vita maporini na Simba na dubu, huko hko Sirini kusikokuwa na watu wengi wanaokuangalia Fanya Kwa kiwango Cha ubora wako hata wengine wanaona nothing your doing.

Huwezi jikuta tu umemiliki kampuni kubwa, hata hujawahi kufanya biashara yeyote. Fanya hata iwe ni kidogo, AMINI, FANYA KWA UBORA NA FANYA KWA MWENDELEZO.

mtoto mdogo siku Zote hawezi beba gunia la mpunga, akibeba debe Moja msifie amefanya kazi kubwa kulingana na nguvu Zake.

E A. Adeboye
Yesterday and today

Let there be light

DOMINION OVER THE FORCES OF DARKNESS.Mwanzo 1:26And God said, Let us make man in our image, after our likeness: and let ...
24/02/2025

DOMINION OVER THE FORCES OF DARKNESS.
Mwanzo 1:26
And God said, Let us make man in our image, after our likeness: and let them have DOMINION OVER the fish of the sea, and over the fowl of the air, and over the cattle, and over all the earth, and over every creeping thing that creepeth upon the earth.

1. You must have knowledge of God
🔥Size of your God, his Truth
Psalms 82:5 They know not, neither will they understand; they walk on in darkness: all the foundations of the earth are out of course.

Danieli 11:32 And such as do wickedly against the covenant shall he corrupt by flatteries: but the people that do know their God shall be strong, and do exploits.
2 . Know yourself
🔥Who are you?
Zaburi 82:6
I have said, Ye are gods; and all of you are children of the most High.

.

GIZA LA
UMASIKINI, MAGONJWA, DHAMBI, HALITAISHINDA NURU KAMWE.
GIZA HUTAWEZA KUSHINDA NDANI YANGU.




THE CHALLENGING COUNTERFEIT Satan constantly is challenging God's power in the universe.  He is the challenging counterf...
15/02/2025

THE CHALLENGING COUNTERFEIT

Satan constantly is challenging God's power in the universe. He is the challenging counterfeit because he actually poses no threat to God.

Satan was originally created by God as a beautiful angel named Lucifer. Read about his original state and position in Ezekiel 28:12-17. But Satan rebelled against the power and authority of God. He wanted to be as God Himself. You can read the story of his rebellion in Ezekiel 28:17 and Isaiah 14:12-15. God could have struck Satan down and killed him for such rebellion. But if He had brought down the first enemy in this way, there would have been the possibility of another rebellion and the history of Heaven would have been clouded with similar disasters. Instead, God cast Satan out of Heaven and allowed his claims to power to have complete trial on earth. God also cast out other angels who participated in Satan's rebellions. They are now evil angels known as "demons" or "devils" at work in the world today.

Shortly after God created the first man and woman, the battle began on earth. You can read of the first challenge in Genesis chapter 3. The fall of Adam and Eve into sin was rooted in rebellion against the authority and power of God. Adam and Eve sought knowledge equal to that of God. With such knowledge would come power. From this time on, Satan has challenged the authority of God on earth.

Through sin, Satan seeks to draw men and women to allegiance to himself instead of God. The Harvestime Institute course, "Spiritual Strategies: A Manual Of Spiritual Warfare," deals with the subject of Satan in detail.

If you are taking the Institute courses in their suggested order, you have already studied this course. If not, we suggest you obtain it to assist in understanding this enemy and specific spiritual strategies to overcome his power. One of the chief methods of Satan in challenging God's power is to counterfeit it.

A counterfeit is an imitation of something and is designed to deceive. For example, counterfeit money is made to look like real money. Criminals pass it off to others as real money to deceive them. Satan counterfeits the power of God. He imitates God's power to deceive people. He uses his angels (demons) to help him accomplish this goal.

Satan and his demons sometimes appear as good instead of evil. We are warned: And no marvel; for Satan himself is transformed into an angel of light. Therefore it is no great thing if his ministers also be transformed as the ministers of righteousness: whose end shall be according to their works. (II Corinthians 11:14-15) In the final days of time on earth, this imitation of God's power by Satan will increase.

Through signs and wonders, he will deceive many: Even him, whose coming is after the working of Satan, with all power and signs and lying wonders. And with all deceivableness of unrighteousness in them that perish: because they received not the love of the truth, that they might be saved. And for this cause God shall send them strong delusion, that they should believe a lie. (II Thessalonians 2:9-11) This Scripture reveals how Satan works.

He counterfeits the power of God with "all power and signs and lying wonders." The only way you can detect his deception is by the truth of the Word of God.

For more lessons visit ;
HARVESTIME INTERNATIONAL INSTITUTE


SIRI YA UWEKEZAJI.zipo aina mbalimbali za uwekezaji, lakini Leo nataka tuangalie uwekezaji Mmoja tu wa ufalme wa MUNGU.U...
31/01/2025

SIRI YA UWEKEZAJI.

zipo aina mbalimbali za uwekezaji, lakini Leo nataka tuangalie uwekezaji Mmoja tu wa ufalme wa MUNGU.

Uwekezaji wowote katika eneo lolote unamatokeo Yake, ukiwekeza negatively utapata matokeo negative results, ukiwekeza positively utapata positive results.

Uwekezaji ni suala la MCHAKATO. Hakuna mtu aliyekeza Kwa muda mfupi tu na akapata matokeo makubwa.

Uwekezaji unahitaji watu wanaolenga shabaha( focused).

Uwekezaji unahitaji watu wanaoweza kuona picha kubwa ya kitakachozalishwa na uwekezaji wao.

Uwekezaji unahitaji watu waliokubali kuficha thamani Yao Kwa muda wote wakiwa wanawekeza. Maana WAKATI WA UWEKEZAJI SIO MUDA WA KUONYESHA KILE UNACHOWEKEZA HADHALANI.

YOHANA MBATIZAJI Aliwekeza Kwa kiwango Cha juu Sanaa hata kabla ya Kutokea kwake akihubiri.
Luka 1:80
Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli.

Huwezi tokea na kuleta mabadiliko bila kukaa na kuwekeza Sirini Kwana , YOHANA MBATIZAJI Aliwekeza Sanaa katika MUNGU alimtafuta sana MUNGU ndyo maana tunakuja kuona matokea Yake alipotokea wana wa Israel.

IPO siri kubwakatika kuwezeka Rohoni , YOHANA alifunga aliomba usiku na mchana,
YOHANA alijitenga na Dunia (DHAMBI)
YOHANA alisoma gombo la chuo(neno la MUNGU)
YOHANA alijifunza kumsikiliza Roho mtakatifu akiwa maporini.

DAVID IBIYEOMIE (Founder of salvation ministries)

David ibiyeomie Aliwekeza sana katika MUNGU hata kabla ya Kutokea kuanza kanisa. Ndyo maana alipotokea alikuwa na kitu Cha kuwapa watu.

DUNIA INAHITAJI MAJIBU, UKITAKA KULETA MAJIBU KWA ULIMWENGU HUU,
KAA SIRINI,
WEKEZA KATIKA MUNGU.
JIFUNZE KUMSIKIA BABA,
JIFUNZE KUJIDHABIHU,
JIFUNZE KUMTOLEA MUNGU,
JIFUNZE KUTEMBEA NA MUNGU.
JIFUNZE SIRI ZA NGUVU ZA MUNGU.

HAKIKA UKIJATOKA DUNIA ITASEMA ULIKIWA WAPI KULETA MAJIBU YETU.



.

20/11/2024

NGUVU ZA MUNGU

Zaburi 105:4
"Mtakeni Bwana na NGUVU ZAKE; utafuteni uso wake siku zote"

Kwenye andiko hili la msingi tunayaona mambo kadhaa;

1. Kuna uhusiano wa moja kwa moja na kumtafuta Mungu kila siku na kiwango cha nguvu zake utakachotembea nacho.
-UKIWA na consistency (muendelezo) wa ushirika na Mungu, utakuwa mtu mwenye nguvu za Mungu wakati wote, na UTAKUWA ukijazwa nguvu zake kila iitwapo leo, Bali UKIWA mtu wa mara moja moja, utakuwa na UPAKO wa msimu tu!

2. Nguvu za Mungu hazikunyeshei k**a mvua au kukuangukia k**a jua; Ni mpaka UZITAKE NA KUZITAFUTA!
Watu wote tuna haki sawa MBELE ZA MUNGU katika Kristo Yesu lakini ni wale tu walioamua KULIPA GHARAMA YA KUZITAFUTA NA KUZITAKA NGUVU ZA MUNGU ndio wanatembea katika UPAKO MKUBWA maishani mwao!

3. Hauwezi kutafuta nguvu za Bwana na usikutane na Bwana kwanza; Hivyo unavyotafuta nguvu za Mungu itakufanya umsogelee na kuwa karibu na Mungu, inakuza mahusiano na ushirika wako na Mungu.
HAKUNA MTU MWENYE KUWEKEZA KUTAFUTA NGUVU ZA MUNGU AMBAYE MAHUSIANO YAKE NA MUNGU YATAKUWA YA KUSUASUA, AUTOMATIC UTAJIKUTA UNAKUA MNO KIROHO PIA!

4. Ukilisoma hilo andiko unaona kuna neno NGUVU ZAKE ikiwa na maana Mungu ana nguvu zaidi ya moja (ana nguvu za aina mbalimbali).

Waefeso 6:10
"Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika UWEZA WA NGUVU ZAKE"

Hapa tunapata yafuatayo;

1. Biblia haituruhusu kuridhika na kiwango cha nguvu za Mungu; Inatutaka TUZIDI KUWA HODARI katika nguvu za Mungu.
Ukiona mtu anafurahia nguvu ya Mungu kidogo aliyonayo na hakazani kufika kwenye kimo, urefu, upana na kina cha Kristo, ujue huyu mtu amefilisika.

2. Tunaendelea kuona waziwazi kuwa UNAANZA NA BWANA halafu ndipo Uweza wa nguvu zake unaachiliwa juu yake.
Hii ina maana wote watafutao nguvu za Mungu, wana nafasi ya kukutana na Mungu na ukikutana na Mungu maisha yako yamegeuka.

AINA ZA NGUVU ZA MUNGU;

1. Nguvu za kuwa shahidi mwaminifu wa Yesu (Matendo 1:8, Matendo 4:33).
Hizi ni nguvu maalum za kukusaidia:
i) Kukuthibitisha ya kuwa

Mabadiliko katka ulimwengu huu, hayabadili uweza Na ukuu wa Mungu tuliyenae, yeye anaweza yote,  yeye anajua yote, yeye ...
04/09/2024

Mabadiliko katka ulimwengu huu, hayabadili uweza Na ukuu wa Mungu tuliyenae, yeye anaweza yote, yeye anajua yote, yeye ni yuleyule JANA, LEO NA HATA MILELE.

''for with God nothing shall be impossible ''

.

Una shida yoyote kwenye maisha yako? Nenda miguni pa yesu, soma neno la Mungu, utapata majibu ya kila swali lako
13/04/2024

Una shida yoyote kwenye maisha yako?

Nenda miguni pa yesu, soma neno la Mungu, utapata majibu ya kila swali lako

Address

Bomang'ombe
Moshi
SOMALIA

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tumaini la utukufu ulimwenguni. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Tumaini la utukufu ulimwenguni.:

Share