Apostle Allen Kipangula Teachings

Apostle Allen Kipangula Teachings HUU NI UKURASA UNAOTUMIWA NA MTUMISHI WA MUNGU APOSTLE ALLEN KIPANGULA KUFUNDISHA NENO
0756057068

KWA NINI UNAPASWA ULINDE MOYO WAKO KWA WIVU MKUBWA.1. MOYO WAKO NI KWENYE MAISHA NI  K**A  INJINI ILIVYO KWENYE GARI. Mi...
29/05/2026

KWA NINI UNAPASWA ULINDE MOYO WAKO KWA WIVU MKUBWA.

1. MOYO WAKO NI KWENYE MAISHA NI K**A INJINI ILIVYO KWENYE GARI.


Mithali 4:23
[23]Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

👉Ubora wa maisha ya mtu unategemea sana kinachoendelea kwenye moyo wake.

Mfano; Nebukadreza alikua mfalme anayesimamia ufalme wa Babeli, moja kati ya ufalme mkubwa duniani lakini kuanguka kwake kulitegemea mabadiliko ya moyo wake tu.

Danieli 4:15-16,33
15 Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi;
16 MOYO WAKE UBADILIKE, USIWE MOYO wa BINADAMU, na APEWE MOYO wa MNYAMA; nyakati saba zikapite juu yake. 33 Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, AKALA MAJANI k**a NG'OMBE, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata NYWELE ZAKE ZIKAKUA, zikawa k**a manyoya ya tai, na kucha zake k**a kucha za ndege.

👉Angalia mambo yaliyompata Nebukadreza, kwa kweli ni mambo mazito sana lakini chanzo ni BADILIKO LA MOYO; toka MOYO WA MWANADAMU na KUWA NA MOYO WA MNYAMA

Badiliko la moyo lilisababisha

a)Apoteze heshima ya kifalme na heshima k**a mwanadamu kiasi cha kufukuzwa mbali na mwanadamu.

b)Ghafla hata yeye mwenyewe alianza kufurahia maisha tofauti na wanadamu ; alianza kula majani ya kondeni, akaacha kujitunza akawa mchafu ana kucha ndefu,nywele ndefu n.k

c)Kwa miaka 7 maisha yake yalisimama;aliishi k**a kichaa alipoteza uwezo wa kufanya shughuli yoyote k**a mwanadamu.

👉Kuna watu wanaishi maisha magumu sana unaweza kufikiri namna ya kuwasaidia ni KUWAPA FEDHA lakini hawa watu hawahitaji fedha wanahitaji BADILIKO LA MOYO.

👉Ungepata nafasi ya kuonana na Nebukadreza akiwa anakula majani ungehisi hana hela kumbe ana ufalme unaotawala ulimwengu ila tatizo pekee ni kwamba AMEPOTEZA MOYO SAHIHI.

👉HAKUNA MAOMBI YANAWEZA KUGEUZA HALI MBAYA YA MTU IKIWA HAKUNA BADILIKO LA MOYO

👉Daniel alimwombea Nebukadreza ili yasimpate mabaya aliyokua ameyaona kwenye ndoto hata hivyo miezi miwili baadaye mabaya yote yalimpata Nebukadreza kwa sababu moyo haukubadilika.

Kuna mtu nilimwombea hakupona nikajiuliza nakosea wapi ? Nikamwombea tena na tena haponi. Roho Mtakatifu akaniambia ana moyo mbovu; hayuko tayari kusamehe. Nilipomwambia alilia kwa uchungu sana na baada ya kusamehe akapona jumla.

👉Kuna watu hawahitaji maombi wanahitaji badiliko la moyo tu.

Nebukadreza hakupona kwa kuombewa alipona kwa badiliko la moyo kwa kuamua kukubali kuwa aliye juu ndiye anatawala.

Danieli 4:24-25, 34
24 tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme;
25 ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani k**a ng'ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote.
34 Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;

Usiufanye moyo wako kuwa mgumu, geuka leo ili na maisha yako yageuke.

Unaweza ukapewa mtaji, ukawa na maarifa na ukaweka bidii lakini usifanikiwe kwa sababu ya moyo mbaya.

Nitaendelea....sehemu ya pili

Apostle Allen Kipangula 0756 057 068
ABC GLOBAL MOSHI

[SEHEMU YA NNE] NAMNA YA KUMSHUGHULIKIA SHETANI K**A SIMBA ANGURUMAYEANDIKO LA MSINGI.1 Petro 5:8-9[8]Mwe na kiasi na ku...
07/03/2026

[SEHEMU YA NNE] NAMNA YA KUMSHUGHULIKIA SHETANI K**A SIMBA ANGURUMAYE

ANDIKO LA MSINGI.

1 Petro 5:8-9
[8]Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa msh*taki wenu Ibilisi, k**a simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
[9]Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.

Kuna ufanano mkubwa kati ya Shetani na simba kiutendaji.

Kulingana na picha iliyotumiwa katika 1 Petro 5:8–9. Mtume Petro hakusema Shetani ni simba halisi, bali “k**a simba angurumaye”, akitumia mfano kueleza tabia na namna anavyofanya kazi.

Tutazame kwa pamoja namna simba anavyofanya kazi.

4. Simba hulenga kula / kumeza mawindo

Lengo la simba kukaa karibu na kundi la swala, pundamilia, nyumbu au nyati SIO KUOMBA MSAMAHA WALA KUJENGA URAFIKI NAO bali ana nia ya DHATI YA KURARUA na KULA MAWINDO.

Kuna wakati simba anaweza kumk**ata mnyama mdogo na akaanza kumchezea bila kumla hii haina maana ameokoka ni mtego anataka mama wa yule mnyama mdogo ajitokeze na mwisho awale wote.

Ndivyo pia Shetani anavyotafuta:
-Atakuvuta kwa raha ya dhambi kabla hajakuharibu jumla.

-Atakuacha uendelee kutenda dhambi huku ukiimba, ukihubiri, na uendelee na maisha mazuri ili usahau madhara ya dhambi mpaka utakapokua umezama sana , umezoea dhambi na huwezi kuziacha hapo ndipo utajua SHETANI SIO BABU YAKO WALA BIBI YAKO

-Unapopewa rushwa, kufurahia raha ya ngono na mambo ya namna hiyo usije kusahau ukweli huu lengo la shetani lipo pale pale ANAMTAFUTA MTU AMMEZE!

Baada ya muda utagundua
-Ameharibu imani yako.

-Amekuangusha kiroho.

-Amekutenga na Mungu wako.
-Amekuharibia maisha yako jumla!

Yohana 10:10
[10]Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

-Delila alikua anambembeleza Samsoni ili ampe siri ya nguvu zake, alipodanganywa na kutoa siri alik**atwa, akatobolewa macho, akapewa kazi ngumu ya kusaga ngano na mwisho akafa.

Mwisho wa dhambi sio raha,ni MAUTI.
Yakobo 1:14-15
[14]Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
[15]Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa MAUTI.

SHETANI SIO BIBI YAKO WALA BABU YAKO NI ADUI YAKO UKICHEZA NAYE UTALIA WEWE!

Sehemu ya 5 inakuja......

Apostle Allen Kipangula
0756 057 068
ABC GLOBAL MOSHI

[SEHEMU YA TATU] NAMNA YA KUMSHUGHULIKA NA SHETANI K**A SIMBA ANGURUMAYEANDIKO LA MSINGI.1 Petro 5:8-9[8]Mwe na kiasi na...
07/03/2026

[SEHEMU YA TATU] NAMNA YA KUMSHUGHULIKA NA SHETANI K**A SIMBA ANGURUMAYE

ANDIKO LA MSINGI.

1 Petro 5:8-9
[8]Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa msh*taki wenu Ibilisi, k**a simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
[9]Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.

Kuna ufanano mkubwa kati ya Shetani na simba kiutendaji.

Kulingana na picha iliyotumiwa katika 1 Petro 5:8–9. Mtume Petro hakusema Shetani ni simba halisi, bali “k**a simba angurumaye”, akitumia mfano kueleza tabia na namna anavyofanya kazi.

Tutazame kwa pamoja namna simba anavyofanya kazi.

3. Simba hushambulia kwa ghafla.
-Shetani muda wote hutafuta muda utakaolala na kujisahau.

Anasubiri muda utakaokua;
-Umeacha kuomba
-Umeacha kufunga
-Umeacha kukesha
-Umeacha kusoma Neno.
-Umeanza kupuuza umuhimu wa ibada na kuhisi upo salama nje ya kanuni za Mungu, hapo ndipo hushambulia kwa ghafla.

Mathayo 13:24-25
[24]Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;
[25]lakini watu WALIPOLALA, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
1 Wathesalonike 5:3
[3]Wakati wasemapo, KUNA AMANI na SALAMA, NDIPO UHARIBIFU UWAJIAPO KWA GHAFULA, k**a vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala HAKIKA HAWATAOKOLEWA.

Simba anaweza kujificha kisha kushambulia kwa haraka bila mawindo kutarajia.

Shetani pia mara nyingi hujaribu kwa ghafla kupitia:

-majaribu
Mwanzo 39:11-12
[11]Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani;
[12]huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.

-mawazo mabaya.

Luka 22:3-4
[3]
Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara.
[4]Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao.

-mazingira yasiyotarajiwa.
Shetani atamtumia huyo huyo unayemwita kaka yangu au dada angu katika Bwana kukuangusha usipokua makini. -Jifunze kumwamini Mungu wanadamu ni vyombo dhaifu (unstable) -Usijiamini kupita kiasi

Sehemu ya nne inakujia.....

Apostle Allen Kipangula
0756 057 068
ABC GLOBAL MOSHI

[SEHEMU YA PILI] NAMNA YA KUMSHUGHULIKA NA SHETANI K**A SIMBA ANGURUMAYEANDIKO LA MSINGI.1 Petro 5:8-9[8]Mwe na kiasi na...
07/03/2026

[SEHEMU YA PILI] NAMNA YA KUMSHUGHULIKA NA SHETANI K**A SIMBA ANGURUMAYE

ANDIKO LA MSINGI.

1 Petro 5:8-9
[8]Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa msh*taki wenu Ibilisi, k**a simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
[9]Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.

Kuna ufanano mkubwa kati ya Shetani na simba kiutendaji.

Kulingana na picha iliyotumiwa katika 1 Petro 5:8–9. Mtume Petro hakusema Shetani ni simba halisi, bali “k**a simba angurumaye”, akitumia mfano kueleza tabia na namna anavyofanya kazi.

Tutazame kwa pamoja namna simba anavyofanya kazi.

2. Simba huzunguka akitafuta mawindo dhaifu

â—ŹSimba mara nyingi huchagua mnyama aliyedhoofika, aliyejitenga, au asiye makini.

Ndivyo pia Shetani:

-hutafuta mtu asiyekesha kiroho, aliye mbali na ushirika wa waamini wengine, au mwenye imani dhaifu.
👉Ndiyo maana andiko linasema: “mwe na kiasi na kukesha.”
-Kuwa makini na mlango wowote wa dhambi kumbuka mazungumzo mabaya huharibu tabia njema (1kor15:33) na taa ya mwili ni jicho likitiwa giza kwa kutazama vitu vichafu maisha yako yote yatapoteza mwelekeo.

👉Usijitenge na ibada au makusanyiko ya wana wa Mungu kufanya hivyo ni kujihatarisha na kumpa shetani nafasi ya kukushambulia.

Maandiko yanasema:
-Waefeso 4:27
[27]wala msimpe Ibilisi nafasi.

-Waebrania 10:25
[25]wala tusiache kukusanyika pamoja, k**a ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

-Waebrania 3:12-13
[12]Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.
[13]Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.

USIKOSE IBADA KWA SABABU YOYOTE ILE.

"Huwezi kuacha kupumua kwa kiteteo cha kuchoka—utakufa"

Sehemu ya tatu inakujia....

Apostle Allen Kipangula
0756 057 068
ABC GLOBAL MOSHI

[SEHEMU YA KWANZA] NAMNA YA KUMSHUGHULIKA NA SHETANI K**A SIMBA ANGURUMAYEANDIKO LA MSINGI.1 Petro 5:8-9[8]Mwe na kiasi ...
07/03/2026

[SEHEMU YA KWANZA] NAMNA YA KUMSHUGHULIKA NA SHETANI K**A SIMBA ANGURUMAYE

ANDIKO LA MSINGI.

1 Petro 5:8-9
[8]Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa msh*taki wenu Ibilisi, k**a simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
[9]Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.

Kuna ufanano mkubwa kati ya Shetani na simba kiutendaji.

Kulingana na picha iliyotumiwa katika 1 Petro 5:8–9. Mtume Petro hakusema Shetani ni simba halisi, bali “k**a simba angurumaye”, akitumia mfano kueleza tabia na namna anavyofanya kazi.

Tutazame kwa pamoja namna simba anavyofanya kazi.

1. Simba hunguruma kuogopesha mawindo yake

â—ŹSimba hutumia kunguruma ili kutisha na kuvunja moyo wa mawindo yake kabla hajayashambulia.
â—Ź Hofu inamfanya anayewindwa akose uelekeo asielewe cha kufanya maana hajui adui yuko wapi au hata akijua aogope.

👉Vivyo hivyo, Shetani hutumia hofu, vitisho, na mawazo mabaya ili kumfanya mtu awe dhaifu kiroho.
👉Anajaribu kumfanya mtu aogope, akate tamaa, au aache imani.

👉Mtu akishashambulia na hofu anapoteza imani kwa Mungu na Neno lake.
👉Anaanza kutafuta mbinu za kimwili za kumsaidia na hapo ndipo anapopoteza pambano kwa kuingia uwanda ambao shetani yuko vizuri zaidi.

UKWELI WA KUKUSAIDIA.

Ukiona simba ananguruma ujue yafuatayo.
1. Simba hunguruma pale anapohisi kutishiwa au kuogofywa na kitu.

2. Simba hutumia mngurumo pale anapohisi adui yake ni mkubwa au ana uwezo kumzidi.

3. Simba hutumia mngurumo pale ambapo hajui mawindo yako wapi anataka hofu iyatoe mawindo mahali pake pa maficho na salama ili ayaone na kushambulia.

4. Simba hutumia mungurumo k**a njia ya kuonyesha nguvu zake ili yamkini amtishe hata mnyama aliye na nguvu kuliko yeye.

5. Mngurumo wa simba hauui kinachopelekea kuua ni kitendo ambacho mnyama anayewindwa atafanya k**a mwitikio wa hofu.

UNAPOHISI KUOGOPA AU KUTISHWA NA ADUI KWA NAMNA YOYOTE FANYA YAFUATAYO:

1. Mpinge kwa kutumia Damu ya Yesu na Neno la ushuhuda.
-Muonyeshe ulishatakaswa kwa damu ya Yesu,ulishaokolewa kutoka nguvu za giza, uko huru na hakuna cha kukudhuru.
-Achilia maandiko kinyume chake , Neno la Mungu ndio makombora rohoni dhidi ya adui .
-Kufyatua kombora tumia Neno imeandikwa na liachilie hilo andiko !
Mathayo 4:10-11
[10]Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
[11]Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.

Ufunuo wa Yohana 12:11
[11]Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.

Zaburi 107:1-2
[1]Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
[2]Na waseme hivi waliokombolewa na BWANA,
Wale aliowakomboa na mkono wa mtesi.

2. Mkabili na kumkemea kwa mamlaka ya jina la Yesu.
-Our enemy is powerless against the authority of the name of Jesus.
Luka 4:41
[41]Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye Kristo.

Wafilipi 2:9-11
[9]Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
[10]ili kwa jina la Yesu KILA GOTI LIPIGWE, la VITU vya MBINGUNI, na VYA DUNIANI, na VYA CHINI YA NCHI;
[11]na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Yakobo 4:7
[7]Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

Sehemu ya pili inakuja...

Apostle Allen Kipangula
0756 057 068
ABC GLOBAL MOSHI

[SEHEMU YA KWANZA]UTAJIRI WA KWELITRUE RICHESMAANDIKO YA MSINGILuka 16:11[11]Basi, k**a ninyi hamkuwa waaminifu katika m...
26/02/2026

[SEHEMU YA KWANZA]UTAJIRI WA KWELI

TRUE RICHES
MAANDIKO YA MSINGI

Luka 16:11
[11]Basi, k**a ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli?
If therefore ye have not been faithful in the unrighteous mammon, who will commit to your trust the TRUE RICHES?

Ufunuo wa Yohana 3:17-18
[17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
[18]Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

Katika dunia hii yenye ushindani wa utajiri wa vitu ambapo watu wameshindana kumiliki nyumba magari na ndege na sasa wanakimbizana kumiliki watu, ni rahisi sana kupoteza uelekeo na ukajikita kufukuzia kinachodaiwa ni utajiri na ukasahau kwa habari ya utajiri wa kweli.

Ukisoma Neno la Mungu na kulitafakari kwa kina utagundua kuwa ;

1.Utajiri wa kweli si fedha, dhahabu au mali mtu anazoweza kuwa nazo ingawa utajiri wa kweli huvuta hivyo vitu pia.

2. Mtu anaweza kuwa na mali zinazothaminiwa katika dunia hii na bado akawa maskini.

3. Utajiri wa vitu (mali) mara nyingi hutumika kufunika umaskini halisi ambao mtu anao , umaskini ambao huambatana na unyonge, mashaka, hofu, upofu na uchi (kukosa utukufu wa Mungu).
ambaye hajaoga anaweza kuuficha uchafu wake kwa kujipaka mafuta na kuvaa nguo nzuri lakini haitachukua muda kwa harufu mbaya kumuumbua kuwa ni mchafu ndivyo kwa mtu aliyemaskini anayejisitiri kwa vitu.

Utajiri wa kweli ni nini ?

Utajiri wa kweli ni mvuto wa kimungu (thamani) anaoweka juu ya mtu unaowalazimisha watu wamtendee mema na kumhudumia kwa mali zao.

Isaya 43:4
[4]Kwa kuwa ulikuwa wa THAMANI machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.

Tuangalie mifano angalau miwili.

a)Mfano wa mfalme Suleiman.

Mungu alimtokea kwenye ndoto na akamwambia AMEMPA utajiri(sio atampa) na hii ilikua baada ya Suleman kuomba apewe hekima.

1 Wafalme 3:11-13
[11]Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu;
And God said unto him, Because thou hast asked this thing, and hast not asked for thyself long life; neither hast asked riches for thyself, nor hast asked the life of thine enemies; but hast asked for thyself understanding to discern judgment;
[12]basi, tazama, nimefanya k**a ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu k**a wewe, wala baada yako hatainuka mtu k**a wewe.
Behold, I have done according to thy words: lo, I have given thee a wise and an understanding heart; so that there was none like thee before thee, neither after thee shall any arise like unto thee.
[13]Na mambo yale usiyoyaomba NIMEKUPA, MALI na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme k**a wewe, siku zako zote.
And I HAVE ALSO GIVEN THEE that which thou hast not asked, both RICHES, and honour: so that there shall not be any among the kings like unto thee all thy days.

Kwahiyo Sulemani aliamka kutoka kwenye ndoto ni tajiri lakini hakua na mali yoyote mkononi kutoka kwenye ndoto hiyo maana Mungu alisema NIMEKUPA.

Utajiri hapa ulikua ni mvuto wa kiungu ambao Mungu aliweka juu ya Sulemani ili watu wamtendee mema k**a ambavyo tunaona kwenye andiko linalofuata.

1 Wafalme 10:1,3,10
[1]Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani juu ya jina la BWANA, ALIKUJA ILI AMJARIBU KWA MASWALI YA FUMBO.
[3]Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala hakukuwa na neno alilofichiwa mfalme asimwambie.
[10]Basi akampa mfalme TALANTA ZA DHAHABU MIA na ISHIRINI, na manukato mengi, mengi sana, na vito vya thamani; wala haukuja tena wingi wa manukato, k**a hayo malkia wa Sheba aliyompa mfalme Sulemani.

Zingatia yafuatayo;
1. Malkia wa Sheba hakua na tatizo lolote analohitaji kutatuliwa na Suleman alikuja kumjaribu ili kupima uwezo wake k**a ni kweli ana uwezo k**a avyosikia.

2. Chochote ambacho Malkia alimpa Sulemani hakikua ni malipo ya kutatuliwa changamoto ilikua ni zawadi ya kumuonyesha namna anavyomkubali.

Sasa tuachane na zawadi nyingine tupige mahesabu thamani ya dhahabu pekee kwa fedha za kitanzania.

1talanta=26kg
120talanta =3120kg
Ambazo ni sawa na
3120,000grams.

1gram (dhahabu safi) =Tsh419,500/=

Kwahiyo
3120,000gram=Tsh1,308,240,000,000

Tirioni 1.3 za kitanzania mtu kapewa k**a malipo ya Interview ya siku moja hatujapigia mali nyingine ambazo alipewa.

Mara zote mali hutoka mikononi mwa maskini wenye mali na kuwaelekea matajiri wasio nazo lakini wenye utajiri wa kweli.

Mfano wa pili:Mwanampotevu

Mwanampotevu alikua ni maskini anayeishi kwa baba tajiri.

Yeye alijua kwa kuondoka na mali nyingi alizopewa na baba yake tayari amekua tajiri.

Ilichukua muda mchache kuufunua umaskini wake aliokua anauficha kwa mali za baba yake.

Luka 15:13-16
[13]Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati.
And not many days after the younger son gathered all together, and took his journey into a far country, and there wasted his substance with riotous living.
[14]Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye AKAANZA KUHITAJI.
[15]Akaenda akashik**ana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
[16]Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala HAPANA MTU ALIYEMPA KITU.

MAMBO YA KUZINGATIA.
i)Utajiri wa vitu unaweza kuisha.
ii)Utajiri wa vitu unaweza kuliwa na watu waliokuzunguka.
iii)Utajiri wa Vitu unaweza ukapukutika kutokana na majanga (mf njaa) na ukapotea.
iv)Ni utajiri wa kweli pekee ndio unaweza kustahimili na kudumu nyakati zote.

Mwana mpotevu hakua na utajiri wa kweli (thamani/mvuto wa kiungu) ndio maana mali zilipoisha hakukua na mtu wa kumpa kitu kiasi kwamba hata aliyemwajiri kumlishia nguruwe wake hakumpa chakula.

Hii ni zero mvuto.

Kuna watu sasa ni matajiri wa vitu lakini hawana utajiri wa kweli, wana marafiki wengi kwa sababu ya mali ila zikipotea hizo mali ndio utagundua ni maskini wa kutupwa.

K**a hujajitajirisha kwa Mungu hata k**a ni tajiri wa mali ni suala la muda tu utagundua ni maskini aliyebahatika kuwa na vitu.

Ukiona mtu anasema nilipokua na hela nilikua na marafiki wengi niliwasaidia lakini baada ya kufilisika hakuna hata mmoja anayenikumbuka , ujue huyu mtu alikua maskini tangiapo.

Mfano wa tatu:Yesu alipozaliwa.
Yesu alipozaliwa kwa nje alikua ni maskini lakini ndani tajiri kumbuka utajiri wa kweli sio vitu ni mvuto au thamani ya kiungu juu ya mtu inayoweza kuvuta watu na vitu.

Yesu alikua na utajiri wa kweli!

Utajiri wake uliwafanya mamajusi kutoka mashariki ya mbali kusafiri kwa siku kadhaa ili tu wamwone na kumsujudia.

Walipomfikia hawakumpa "baby diapers" walimletea dhahabu na manukato yaliyomfanya baba yake Yusufu asiwaze kusafiri kwenda Misri kukaa huko na kurudi baada ya Herode kufa.

Mathayo 2:1-2,10-11
[1]Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
[2]Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
[10]Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno.
[11]Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.

Tafuta kuutafuta UTAJIRI WA KWELI na utajiri wa mali utakujilia.

Niishie hapa kwa sasa...

Apostle Allen Kipangula
0756 057 068
ABC GLOBAL MOSHI

2. MALEZI YA KIROHO ni NJIA YA MUNGU ya KUWAANDAA WATU NA KUWAFANYA KUWA BORA KWENYE WALICHOITIWA.Matendo ya Mitume 18:2...
09/02/2026

2. MALEZI YA KIROHO ni NJIA YA MUNGU ya KUWAANDAA WATU NA KUWAFANYA KUWA BORA KWENYE WALICHOITIWA.

Matendo ya Mitume 18:24-26
[24]Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko.
[25]Mtu huyo alikuwa AMEFUNDISHWA NJIA YA BWANA; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye ALIJUA UBATIZO wa YOHANA TU.
[26]Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila WALIPOMSIKIA WAKAMCHUKUA KWAO, WAKAMWELEZA NJIA YA BWANA KWA USAHIHI ZAIDI.

Hata k**a unasikia moto unawaka au msukumo wa kuwa mtu fulani kwenye maisha itakugharimu kukaa chini ya malezi kuwa mtu huyo.

Hauwi mtu fulani kwa kuwa umetamani kuwa, unakuwa kwa sababu umetengenezwa kuwa.

HABARI NJEMA KWA WATU WA KILIMANJARO.Mchungaji kiongozi wa kanisa la Assembly of Believers Church Moshi anakukaribisha k...
07/02/2026

HABARI NJEMA KWA WATU WA KILIMANJARO.

Mchungaji kiongozi wa kanisa la Assembly of Believers Church Moshi anakukaribisha kwenye ibada maalumu ya UJAZO WA ROHO MTAKATIFU, UPONYAJI NA KUFUNGULIWA.

YESU ATAWAFUNGUA WOTE:
â—ŹWANAOTESWA NA DHAMBI NA WANASHINDWA KUACHA.

â—ŹWALIOFUNGWA KWENYE TABIA SUGU K**A ULEVI, UVUTAJI SIGARA/BANGI/MADAWA YA KULEVYA.

â—ŹWALIOVUNJIKA MIFUPA ITAUNGWA NA WATATEMBEA.

â—ŹWANAOTESWA NA MAGONJWA SUGU K**A KISUKARI, SARATANI, SHINIKIZO LA DAMU N.K

â—ŹWANAOTESWA NA MADENI SUGU YASIYOLIPIKA.

TUKUTANE MOSHI, MJOHORONI UKUMBI WA CHAKITO.

SAA 2 KAMILI ASUBUHI.

TUTAKUA NA IBADA MOJA TU.

MJULISHE YEYOTE ALIYEKO MOSHI ASIKOSE NEEMA HII.

Unayekuja nijulishe kwa namba zifuatazo

APOSTLE ALLEN KIPANGULA
0756 057 068 /0711 990 492

MCHUNGAJI KIONGOZI-ABC MOSHI

Address

Kiboriloni
Moshi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Apostle Allen Kipangula Teachings posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Apostle Allen Kipangula Teachings:

Shortcuts

Share