UMOJA DAIMA MEDIA

UMOJA DAIMA MEDIA UMOJA DAIMA MEDIA
Official account
We are Christian media organization owned by ELCT NORTHERN DIOCESE

Usharika wa Ngarony, Jimbo la Siha, KKKT Dayosisi ya Kaskazini wamefanya ibada maalumu ya kuwaombea na kuwaaga wanafunzi...
02/09/2026

Usharika wa Ngarony, Jimbo la Siha, KKKT Dayosisi ya Kaskazini wamefanya ibada maalumu ya kuwaombea na kuwaaga wanafunzi wa darasa la saba, kutoka shule za Msingi za Ngarony na Mese.

Ibada hii ililenga kuwaombea wanafunzi hao ili wakafanye vyema katika Mitihani ya Taifa ya darasa la saba inayotarajiwa kufanyika mwezi Septemba, 2026.

02/09/2026

Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo, ameweka wakfu gari aina ya Toyota Land Cruiser la Jimbo la Kilimanjaro Mashariki pamoja na pikipiki sita zinazotolewa kwa ajili ya Wachungaji wa baadhi ya Sharika za Misioni za Dayosisi.

Ibada hiyo imefanyika leo katika Makao Makuu ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini, ambapo Askofu Shoo amewapongeza wanajimbo la Kilimanjaro Mashariki kwa hatua ya kumpatia Mkuu wa Jimbo chombo hicho cha usafiri. Askofu Shoo amesema gari hilo linapaswa kutumika kwa matumizi yaliyokusudiwa ili kuwezesha utekelezaji wa shughuli na majukumu mbalimbali ya Jimbo.

Akizungumzia pikipiki hizo sita, Askofu Shoo amesema Dayosisi imeweka mpango wa kununua pikipiki kila mwaka kwa ajili ya kuwawezesha Wachungaji na Wainjilisti wanaohudumu katika maeneo ya Misioni na Sharika zinazokabiliwa na changamoto kubwa ya usafiri. Amesema hatua hiyo inalenga kurahisisha huduma za kiroho na kijamii katika maeneo ambayo usafiri umekuwa changamoto kwa watumishi wa Kanisa.

Aidha, Askofu Shoo ameipongeza Idara ya Misioni na Uinjilisti ya Dayosisi, iliyo chini ya Msaidizi wa Askofu, Mch. Deogratius Msanya, kwa juhudi zake katika kuhakikisha Wachungaji na Wainjilisti wanapata nyenzo muhimu za kuwawezesha kufikisha huduma katika maeneo mbalimbali. Amesema fedha zinazotumika katika mpango huo zinatokana na sadaka za Epifania, ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha kazi ya Misioni na Uinjilisti ndani ya Dayosisi.

Askofu Shoo amewataka Wachungaji waliokabidhiwa pikipiki hizo kuzitumia kwa uadilifu mkubwa na kwa kuzingatia malengo yaliyokusudiwa. Kwa upande wake, Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Mashariki, Mch. Calvn Koola, amemshukuru Mungu kwa siku hiyo na kwa hatua ya Askofu Shoo kuweka wakfu gari la Jimbo.

01/09/2026

Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Mch. Deogratius Msanya, amewakaribisha wageni kutoka Sinodi ya Nebraska Marekani, wakiongozwa na Askofu Johnson Scott, waliotembelea Ofisi Kuu za Dayosisi ya Kaskazini leo, Septemba 1, 2026.

Sinodi ya Nebraska ni rafiki na mshirika wa muda na Dayosisi ya Kaskazini, huku mahusiano yao yakijengwa katika misingi ya urafiki, upendo na umoja katika Kristo.

Akizungumza mara baada ya utambulisho, Askofu Johson Scott wa Sinodi ya Nebraska amesema amefurahi kushiriki pamoja na waumini na viongozi wa Dayosisi ya Kaskazini katika Sala ya Asubuhi.

Askofu Johnson amesema amefurahishwa kusikia kutoka kwa mhubiri wa siku hiyo kwamba mahusiano kati ya Dayosisi ya Kaskazini na Sinodi ya Nebraska si ya kimradi pekee, bali ni mahusiano ya kifamilia na kirafiki.

Amesema anakubaliana na mtazamo huo kwa kuwa mara kadhaa wanapokutana, hukutana k**a marafiki na watu wanaounganishwa na huduma ya Kanisa, huku wakitambua kwamba wao ni kaka na dada katika Kristo, licha ya kuhudumu katika maeneo tofauti.

Aidha, amesema mahusiano hayo ni sehemu ya juhudi za kujenga mahusiano ya Kikristo duniani kote, jambo ambalo, kwa mujibu wake, linampa Mungu furaha na utukufu.

Awali, Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Mhandisi Z. S. Moshi, akimkaribisha Msaidizi wa Askofu na ujumbe kutoka Sinodi ya Nebraska, amesema Dayosisi ya Kaskazini na Sinodi ya Nebraska zina mahusiano yaliyojengwa katika urafiki na upendo wa Yesu Kristo.

01/09/2026

Tazama wanafunzi kutoka Kusirye-U English Medium wakionyesha uwezo mkubwa.

Tukio hili ni onesho mbele ya waalimu na waalikwa waliofika katika warsha ya elimu iliyoandaliwa na Shule ya Kusirye-U katika kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.

Shule hii iko chini ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini.

Usharika wa Ngarony, Jimbo la Siha, Dayosisi ya Kaskazini, umeendelea kuhubiri Injili kwa njia ya michezo, ikiwa ni sehe...
31/08/2026

Usharika wa Ngarony, Jimbo la Siha, Dayosisi ya Kaskazini, umeendelea kuhubiri Injili kwa njia ya michezo, ikiwa ni sehemu ya kuwafikia vijana na jamii kwa ujumla kwa kutumia vipaji na michezo.

Jana, Jumapili tarehe 30 Agosti 2026, Usharika wa Ngarony umepata nafasi ya kuhubiri Injili kupitia mchezo wa kirafiki wa soka kati ya vijana wa Ngarony na Kashashi, uliofanyika katika Uwanja wa Ngarony.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa na kuvutia mashabiki kutoka maeneo mbalimbali. Hata hivyo, timu hizo ziligawana pointi baada ya kumalizika kwa mchezo kwa sare ya bao 1-1.

Kupitia michezo k**a hii, Usharika wa Ngarony unaendelea kutumia fursa ya michezo kuwaunganisha vijana, kukuza vipaji na, zaidi, kuwafikishia ujumbe wa Injili kwa vitendo na kuwahamasisha vijana kumjua Mungu na kushiriki katika huduma za Kanisa.

InjiliUwanjani

31/08/2026

Kila kiongozi anatakiwa kusikiliza ujumbe huu kutoka kwa Mchungaji James Nkya wa KKKT Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini.

31/08/2026

Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Kati, Mch. Javason Mrema, akihubiri katika Ibada ya Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Mtaa wa Msandaka, Usharika

31/08/2026

Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Kati, Mch. Javason Mrema, akihubiri katika Ibada ya Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Mtaa wa Msandaka, Usharika wa Msaranga Mandaka, Jumapili, Agosti 30, 2026.

31/08/2026

Mchungaji James Nkya akiongea katika Semina ya wanawake viongozi wa Umoja wa wanawake Jimbo la Kilimanjaro Kati, KKKT Dayosisi ya Kaskazini, alieleza kuwa moja ya sifa ya kiongozi ni kutunza siri.

Address

P. O Box 195
Moshi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UMOJA DAIMA MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to UMOJA DAIMA MEDIA:

Shortcuts

Share