06/10/2021
ASILI YA SALA YA SALAMU MARIA KATIKA BIBLIA....
SOMA KWA MAKINI...
Inaletewa kwenu kwa hisani ya Riziki Kavishe, Jimbo Katoliki Moshi, Christ the King Parish.
___________________________________________________
Katika uchanganuzi wa sala hii karibu tuwe pamoja nikichambua neno moja Baada ya lingine.
SALAMU MARIA UMEJAA NEEMA, BWANA YU NAWE.
Neno hili tunalipata kupitia injili ya Luka 1:28 pale Malaika Gabriel alipomwamkia Bikira Maria akisema
"Salamu uliyepewa neema, Bwana yu nawe" hii ni salam ya kipekee aliyoipokea Bikira Maria yenye Habari njema kutoka kwa Mungu.
UMEBARIKIWA KULIKO WANAWAKE WOTE, NA YESU MZAO WA TUMBO LAKO AMEBARIKIWA.
Maneno haya tunayapata katika Injili ya Luka 1:42 pale Elizabeth alipomwambia Maria
"Umebarikiwa wewe katika wanawake wote, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa". Hii ni wazi kwamba Bikira Maria alibarikiwa kuliko wanawake wote kwa kuwa alikuwa ni Mteule wa pekee wa Mungu, atakayetuletea Mkombozi.
MARIA MTAKATIFU MAMA WA MUNGU.
Maneno haya tunayapata katika Injili ya Luka 1:43 akisema:-
" Hata Mama wa Bwana anijilie mimi?"
Ni ishara wazi kuwa, kumbe Bikira Maria alikuwa ni Mama wa Mungu, aliyetuletea Mkombozi.
UTUOMBEE SISI WAKOSEFU, SASA NA SAA YA KUFA KWETU.
Naneno haya pia twayapata katika kitabu cha Yakobo 5:16 pale Mungu anapotuambia
"Ungamianeni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, Mpate Kuponywa". Kumbe tunaalikwa kuombeana sisi kwa sisi, pia kushiriki kitubio.
AMINA.
Neno amina limekuwa ni shukurani, likimaanisha na iwe hivyo, linatuashiria kuwa maombi yetu na yapokelewe k**a tulivyoomba.
Wengi wamekuwa wakidai sala hii imeandikwa wapi katika Biblia, Kanisa Katoliki hatubaatishi wala Hatuoteshwi ndoto za Mchana, wala hatukariri Biblia, bali twaielewa na kufundisha kweli ya Mungu, si k**a wenzitu walivyozoea kukosoa bila kuichambua Biblia kwanza, huo ndio ukweli uliotoka katika maandiko Matakatifu na ya Kweli.
Nanyi mtaijua kweli, nayo kweli itawaweka huru.
WENU KATIKA KRISTO
RIZIKI KAVISHE