Amedeus J.Shio Ministries

Amedeus J.Shio Ministries This Ministry on Facebook, Generally Focuses on Christian Transformation through Simplified Teaching

17/02/2023

!

Huwezi kuhubiri Neno la Msalaba wakati umejaa uoga, ustaarabu na hekima ya dunia hii!

Injili ni Upuuzi usioingia akilini!

Kwanza Inakwaza kiburi chetu wanadamu!

Na Ukihubiri k**a ilivyo lazima uonekane mpuuzi!

Hujui maadili wala Haki!

Ukitaka kuonekana wa maana hubiri watu kua na maadili mazuri ili waingie mbinguni

Hubiri watu kuacha dhambi ili Mungu awakubali!

Hio ndio hekima ya dunia hii, fanya mema upate mema! Ishi kwa haki upewe haki!

Huwezi kuingia mbinguni kirahisi tu, fanyia kazi kupata mbingu! Matendo mabaya = Jehanam, Matendo mabaya = Motoni!

Ni simple hivyo, hekima ya dunia inakudai wewe ufanye ndio upate!

Usipohubiri hivyo, wewe ni mtenda dhambi, mwana wa majoka na kuzimu na una promote ulimwengu kuendelea na maovu!

Hujui haki ya Mungu!

Ndio sababu wengi kwa njaa na kiu ya kukubalika na ulimwengu hawahubiri msalaba wanahubiri maadili

Wamekataa msalaba, wamebatilisha nguvu yake! Wanataka ulimwengu uwatambue ni wahudumu wa haki ili hali ulimwengu haukumtambua Bwana wetu (1Yoh 3:2-3)

Ni akili na hekima kuhubiri na kuwasema watu dhambi na makosa yao, hapo inaonyesha wewe unachukia dhambi na maovu!

Tena onyesha ghadhabu na hasira unapohubiri - unakua ni mtu usiye na mchezo na Mungu kabisa, mtu wa haki!

Vinginevyo? Utapigwa mawe, utatengwa na masinagogi! Utaonekana mwana mpotevu!

Yes!

Utasemaje imani tu katika kristo inamwingiza mtu mbinguni?

Hai make sense kwa logic wala hekima za dunia hii!

Ni upuuzi uliopingwa na kudhihakiwa na wasomi wakubwa na wanafalsafa wa Kigiriki zamani zile za Paulo mpaka wanazuoni wa leo!

Ni upuuzi mkubwa uliokua kwazo kwa wayahudi wote! Wao walitaka ishara kubwa sio imani!

Kwamba dhambi zinaondolewa kwa imani pekee juu ya “msalaba” wa Kristo? (Luka 24;47, Marko 16:15-16) - Upuuzi!

Kwamba mtu anaokolewa pasipo kufanya kitendo cha haki? (Efeso 2:8-10, Rumi 5:17), - Upuuzi!

Kwamba Mungu aliupatanisha ulimwengu na nafsi yake katika Kristo asiwahesabie makosa? (2Kor 5:19) - Upuuzi!

Kwamba imani yako tu kwa dhabihu ya Kristo inakutakasa na kukukamilisha milele? (Waebrania 10:10-14) - Upuuzi

Kwamba Jina la Yesu ndio pekee linaokoa!? (Mdo 4:12) - Upuuzi!

Kwamba mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria? (Gal 2:16) - Upuuzi!

Kwamba uzima wa milele ni kwa imani tu katika Yeye? (Yohana 3:16) - Upuuzi!

Eti aaminiye hahukumiwi? (Yohana 3:17) - Upuuzi tu!

Yaani anayeamini stori kua Mungu alifanyika mwili akawa mtoto wa Mariamu na Yusuphu, akasulubiwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu akafufuka siku ya tatu… anaokoka!! (Rumi 10:9-10)- upuuzi!

Kwamba huyo amevuka mautini na kuingia uzimani! Hivyo tu? Pasipo kazi yeyote? Pasipo kutenda haki? (Yohana 5:24-26)

Huo ni upuuzi!

Yaani unataka kusema kwamba Mungu anamhesabia haki asiye mtaua kwa msingi wa imani katika Kristo pekee? (Rumi 4:1-6) - Upuuzi!

Tena unasema; Eti hapana hukumu ya adhabu juu ya hao walio katika Kristo Yesu? (Rumi 8:1-2)

Upuuzi kabisa, uwe ndani ya Yesu una makosa halafu usihukumiwe?! Acha mchezo!!

Watu wa maadili na utamaduni wanakuona unavuta bangi, wewe ni mhuni; unahamasisha dhambi na maovu!

Upuuzi gani huo unasema?

Lakini ajabu ni kwamba: Paulo aliteswa na kutukanwa kwa upuuzi wa hili Neno

Mitume walikimbizwa huku na huku na kuuwawa sababu ya kuhubiri wokovu kwa imani tu katika Jina la Yesu!

Walifia upuuzi huu!

Ajabu zaidi ni kua Mungu mwenyewe ndiye aliyependa kua mpuuzi! Amepuuzia dhambi na makosa yetu; kwa ajili ya Kristo asamehe na kutokukumbuka tena (Waebrania 8:12)

Mungu alipenda kuokoa ulimwengu kwa upuuzi wa Neno hili la msalaba!

Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa wa lile neno linalohubiriwa.
-1 Wakorintho 1 : 21

Hatuna cha kufanya bali kuhubiri msalaba wa Yesu!

Chanzo cha amani na wokovu wetu!

Msalaba asili ya mema, tunatua mzigo hapo!

K**a Paulo tunasema:

Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.
-Warumi 1 : 16

Hatuoni haya, Hatuoni aibu, hatuogopi…

Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni , bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
-1 Wakorintho 1 : 18

Ndiyo nguvu iokoayo, wala sio lifestyle zetu!

Na hivyo tunadumu kuhubiri upuuzi huu!

Bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi;
-1 Wakorintho 1 : 23

Bali waoga na wasioamini katika upuuzi wa Injili sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto!

Acha uoga!

Amini Kristo!

Hubiri msalaba wa Kristo!

Tukutane kazini

Felician Makarios Phos
Kainos Creation Church (KCC)
0742107009

17/01/2023

JAMBO JIPYA LA KUSHANGAZA DUNIANI…!

Kusema kua “kunena kwa Lugha” kwa mujibu wa Biblia sio maneno yasioeleweka kwa ufahamu (supernatural speech) bali ni maneno “mapya ya Agano Jipya!”

Like “wewe umezaliwa na Mungu” , “mwamini ni mtakatifu”

Ati hapo ndio kunena kwa lugha mpya!!

Bros..!

Hutaki kunena kwa Lugha basi kaa kimya endelea kuomba “kimaskini” ili hali u “tajiri” katika usemi wote!

Huwezi kuyapa maana tofauti unayoona wewe maneno ya maandiko yaliyotumika kwa jambo mahususi!

Paulo anatumia sura nzima kueleza lugha supernatural ambayo akili ya mwanadamu haina matunda na kufundisha kua itahitaji another supernatural gift ya fasiri ya lugha ili kutoa maana ya kilichozungumzwa katika roho then unakuja na maneno “cheap” like…

Kunena kwa lugha sio kuongea maneno yasioeleweka…!

Are you fine?

Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.
-1 Wakorintho 14 : 2

- Hakuna asikiaye (hakuna anayeelewa)
- mambo ya siri katika roho yake (sio akili yake)

Nami NATAKA ninyi NYOTE mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa AFASIRI, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.
-1 Wakorintho 14 : 5

- Anataka wote tunene kwa lugha ( mana yake kila mwamini anaweza kunena kwa Lugha)

- Anaelekeza anenaye kwa Lugha mbele ya kusanyiko AFASIRI ili kanisa lielewe na kujengwa (mana yake halielewi bila FASIRI ya Lugha)

Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.
-1 Wakorintho 14 : 14

- Anasema kuomba kwa Lugha ni Roho yake huomba (ni kuomba kwa roho)

- Anasema kwamba akili hapo haielewi (haina matunda) mtu anapoomba kwa lugha!

Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.
-1 Wakorintho 14 : 26

- Anasema KILA MMOJA ANA lugha, ana Tafsiri! Hakuna aliyebaguliwa, hakuna aliyenyimwa! Ni wewe tu ukiamua kutembelea “umaskini” ili hali u tajiri! Ni wewe tu na ujinga wako!

Iko clear, Lugha ni ya rohoni, na haieleweki na akili ya mwanadamu! Sio kisukuma wala kichina - definitely sio lugha za wanadamu!

Na hii habari ya kusema, watu watasema kwa lugha tu endapo “Roho” ata taka yeye, “as the spirit wishes”;

Hii nayo ni confusion ilio very unnecessary!

Yaani Paulo atumie sura nzima kuelekeza kanisa namna ya ku operate katika karama ambayo wahusika hawana utawala nayo? Atakua timamu kweli?

Utaelekezaje saa mwamini atulie kimya angoje mwingine anene ikiwa Roho ndio anaamua sa ngapi na kiasi gani unene kwa lugha?

Utaelekezaje mwamini kutamani sana karama za roho (kunena na kufasiri etc) ikiwa ni k**a Roho apendavyo?

Utaelekezaje kua nataka ninyi nyote mnene kwa lugha ikiwa ni mapenzi ya Roho?

Utasemaje “msizuie kunena kwa lugha” ikiwa ni mapenzi ya Roho?

Utaelekezaje anenaye na afasiri ikiwa sio uwezo wala uamuzi ulio kwake bali wa Roho?

Some confusions are stupidly unnecessary!!

K**a mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.
-1 Wakorintho 14 : 27

Hee!! Kwa hio hapo Paul anamwelekeza Roho namna ya ku control wanenaji? Yaani aliandika haya maelekezo kwa Roho aliyeko Korintho!

Some people are not fine at all!

Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue.
-1 Wakorintho 14 : 29

Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze.
-1 Wakorintho 14 : 30

Maandiko yote hayo yanaonyesha usukani upo kwa mwenye karama na sio kwa Roho “k**a apendavyo”

Ni k**a wewe upendavyo!

Unaweza amua kukaa kimya au kunena! You are in control!

Iko wazi k**a jua la mchana!

Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.
-1 Wakorintho 14 : 38

Amen!

Felician Makarios Phos
Kainos Creation Church (KCC)

07/10/2022

NISEME KIDOGO KUHUSU

1. Ndoa ni muunganiko wa kidunia tu na sio wa mbinguni

2. Ni ya dunia lakini ni takatifu na yenye baraka ya Mungu

3. Ndoa ni uchaguzi, siyo lazima.

4. Unaoa unayemtaka, ni uchaguzi wako isipokua katika Bwana

5. Kubaki single pia ni uchaguzi, SIYO dhambi.

6. Ndoa ni kwa ajili ya procreation.. (uzazi na malezi)

7. Ndoa ni kwa ajili ya kutumikia mahitaji ya ki-ngono ili kuondoa ngono isiyo na utaratibu, uasherati.

8. Majukumu ya mume ni kumpenda mkewe

9. Majukumu ya mke ni kumtii mumewe

10. Majukumu ya mume ni kumridhisha mke wake katika "ibada" ya ndoa.

11. Majukumu ya pamoja ni malezi ya watoto (ikiwa wapo)

12. Majukumu ya mume ni kusababisha mimba (k**a wanahitaji watoto)

13. Majukumu ya mke ni kubeba mimba mpaka wakati wa kujifungua

14. Majukumu ya mume ni kuongoza familia na kuitunza (yaani mke na watoto wake)

15. Majukumu ya mke ni kumsaidia mume kutimiza majukumu ya kifamilia na kimaisha

16. Kimsingi ndoa haisaidii huduma ya mtu kwa Bwana just by default, kwa wengi inaongeza Jam! Kua Single pia sio faida ya moja kwa moja kwa huduma- katika hali zote unaweza kufaidika au kupigika kihuduma.

17. Kuishi katika ndoa ni karama, k**a huna usilazimishe! Siyo dhambi

18. Watoto ni matokeo ya wazazi wao, (seed form principle) hawatoki mbinguni

19. Watoto wakiwa vilaza au smart ni combination yenu au ukoo wenu, SIYO BWANA! Chagua mwenza vizuri

20. Mungu hajawahi Unganisha wanandoa! Usitafute kiki! Mmeunganishana wenyewe!

21. Kufeli ama kufaulu katika ndoa sio kipimo cha "spirituality" ya mtu kwa kua ndoa inahusisha nia (will) na vipaumbele vya mwenza ambavyo huamua matokeo ya afya ya ndoa na huwezi kutawala nia ya mwingine.

22. Viumbe vipya wenye akili wanaoa katika Bwana na ku take advantage ya muunganiko kwa ajili ya Bwana!

Tutaendelea mwakani...
🍻🍻

Makarios

17/08/2022

Disagreements isn't betrayal, friends disagree. However anyone who doesn't mind teaming up with people whom he knows don't like you has betrayed you.

A friend could disagree with you but they don't hand you over to shame, mockery, in perfidy without a sense of further commitment.

He won't suddenly become the rallying point for those who dislike you.

Betrayal means to hand your friends over to shame, hurt and ensure they lose respect with others.

To betray is devilish.

You give away confidential information.

Secrets.

They don't care what you lose.

True friends stay true to you even when you have disagreements.

If you think this is too tough for Friendships, then may you experience judas in your life.

Amen

August 17,2021
Rev Onayinka

22/09/2021

📡📡📡📡📡📡📡📡📡📡

*MWAMINI ANA MSAMAHA WA MILELE.*

🔓🔓🔓🔓🔓🔓🔓🔓🔓🔓

ambaye katika yeye *tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi*;
Kol 1:14 SUV

Katika yeye huyo, kwa damu yake, *tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi*, sawasawa na wingi wa neema yake.
Efe 1:7 SUV

Kwa kuangalia maandiko K**a hayo juu tunaona kuwa Mwamini tayari anao msamaha wa dhambi.

Huu msamaha wa dhambi umetolewa kupitia ukombozi ulio katika Kristo Yesu.

Kwa dhabihu ya Kristo iliyotolewa Mara moja tu, Mwamini amepata msamaha wa Milele.
K**a jinsi ukombozi ulivyotolewa Mara moja tu, ndivyo msamaha ulivyotolewa Mara moja tu.

Msamaha huo uliotolewa kupitia dhabihu ya Yesu, tunaupokea Leo kwa kuamini tu.
Mtu Yeyote anaposikia injili na kuamini, Mara moja anaupokea msamaha huo.

Kwa hivo msamaha unapokelewa kwa Mtu kuamini injili tu, na si vinginevyo.
Msamaha hauombwi kila Mtu anapokosea; msamaha unapokelewa Mara moja tu Mtu anapoamini injili.

Hii ndio maana sio sahihi kwa Mwamini kufanya Maombi ya kuomba msamaha, kuomba rehema, au Maombi ya kujitakasa. Kufanya hivyo Ni ishara ya kuikana kazi ya Yesu ya msalaba. Huwezi kuomba kitu ulichokwisha kupewa tayari.

Msamaha wa dhambi tulikwisha kupewa miaka zaidi ya 2,000 iliyopita, kabla hata hatujazaliwa. Tulisamehewa in advance.
Tulisamehewa dhambi zote tulizokwisha tenda, tunazotenda leo, na tutakazotenda kesho (incase).

Wacha nikazie vizuri hapa: dhambi haziondolewi au kufutwa kwa maneno, dhambi zinaondolewa kwa Damu. Kwa hiyo kufikiri kuwa ukitumia maneno yako kuomba msamaha ndio dhambi zinaondolewa Ni kujidanganya Sana.

"ambayo ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi ya dhambi kumkamilisha mtu aabuduye, Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na *pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo*."
Ebr 9:9‭, ‬22 SUV

Ondoleo la dhambi linafanyika kwa kumwaga Damu ndugu, sio kwa maneno yako, relax.

"tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na *kutuosha dhambi zetu katika damu yake*,"
Ufu 1:5 SUV

Yesu alifanya hiyo kazi tayari; alimwaga Damu yake Mara moja ili sisi tuondolewe dhambi. Kwa Damu ya Yesu tuna msamaha wa Milele.

Una msamaha wa Milele, mpendwa, tembea katika uhalisia wako.

"Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu *mMEsamehewa dhambi zenu*, kwa ajili ya jina lake."
1 Yoh 2:12 SUV

Je! Bado huelewi hata Sasa?!

Nijulishe.

Bro. Amedeus J. Shio
Kainos Creation Church
(22/09/2021)

21/04/2020

Na, Amedeus J. Shio

*TOFAUTI ILIYOPO KATI YA NAFSI, ROHO, NA MWILI.*

📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖

1 Wathesalonike 5 : 23 - Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi *nafsi* zenu na *roho* zenu na *miili* yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

📡📡📡📡📡📡📡📡📡📡

Hili andiko👆👆
Limeweka wazi kabisa kuwa mtu amegawanyika sehemu tatu. Yaani ili uwe mtu ni lazma haya mambo matatu yawepo: Nafsi, roho, na mwili.

Mtu ni roho, anayo nafsi, na anaishi katika mwili.

Mtu sio nafsi wala sio mwili.
Ndio maana mtu akifa tunasema mwili wa marehemu. Tunaamini mtu mwenyewe hayupo hapo, huo ni mwili wake tu. Yeye mwenyewe anakuwa keshaondoka zake.

Mwili ni nyumba ya mtu, yaani roho. Mwili ukipata shida k**a magonjwa au ajali, mtu huamua kuondoka-maana nyumba imeharibika.

Kwa hiyo kufa ni hali ya mtu kuamua kuuacha mwili kwa sababu mbalimbali k**a magonjwa, ajali, nk.

Mtu ni roho, anayo nafsi, na anakaa katika mwili (usisahau hii).
Bwana Yesu asifiwe!

Naamini mpaka hapo tumeelewana.

Ngoja tuzame tena kidogo kuchambua hizi mambo:👇👇

*1.* Nafsi (soul).
Nafsi sio kitu cha kushikika.
Nafsi ina vitu vitatu ndani yake👇

a). Akili (mind).
b). Utashi (will).
c). Hisia (emotions).

ndio center ya nafsi.
Kuna akili za aina mbili: conscious mind, na subconscious mind.

Hii subconscious mind ndio kwenye lugha ya biblia tunaita moyo.
Labda nitachambua hili kiundani kwenye somo linalojitegemea.
Maana wengi wakiona neno moyo kwenye biblia, wanadhani ni roho inazungumziwa.

Anyway, twende mbele kidogo👇

ni ule uhuru tuliopewa na Mungu k**a wanadamu, kufanya maamuzi bila kusukumwa.
Yaani ni kwamba, Mungu hakutaka amwendeshe mwanadamu k**a robot; alitaka mwanadamu awe huru kimaamuzi. Ndio maana akampa free will( Utashi binafsi).
Kwa sababu hiyo mwanadamu ana uwezo wa kuamua hata kumkataa Mungu, na Mungu wala hawezi kuingilia maamuzi yake.

Adam, kwa mfano alichagua mwenyewe kumwasi Mungu. Wala shetani hakumlazimisha. Ni maamuzi yake binafsi.
Hiyo ndiyo nguvu ya mwanadamu.

K**a sio utashi tuliopewa, Mungu angelazimisha wanadamu wote tukoke.
Lakini sasa hawezi fanya hivyo sababu ametugea free will.

Anakuwekea mbele yako uzima na mauti, halafu anakuambia chagua. That's the power of will.

ndio Hisia(emotions). Mwili unapata hisia zake kupitia milango mitano ya fahamu: ngozi, pua, ulimi, masikio, na macho.

*2.* roho (spirit).
Hii si ngumu kuelewa naamini. roho ndio wewe mwenyewe. Ni ile pumzi ya Mungu.
roho ndiyo iliyoumbwa kwa mfano na sura ya Mungu- kwa kuwa Mungu ni roho.

roho imetoka kwa Mungu mwenyewe. Namaanisha wewe umetoka kwa Mungu moja kwa moja. Mwili wako ndio umetoka mavumbini. Ila wewe hujatoka mavumbini, umetoka kwa Mungu. God is your genuine source.

roho ndiyo itaenda mbinguni au kuzimu baada ya kutengana na mwili(kifo).

Hata hivyo unapaswa kujua mara tu roho itokapo katika mwili, Mungu huipa hiyo roho mwili mwingine wa kiroho.

Huu mwili wa kiroho ndio utaenda aidha kuishi na Bwana milele(k**a uliokoka), au kuungua jehanam milele(k**a uligoma kuokoka).

*3.* Mwili (body).
Mwili ndio nyumba ya roho kuishi hapa duniani.

Mungu, shetani, malaika na mapepo ni roho ambazo hazina mwili wa kuishi nao hapa duniani.
Ndo maana shetani ilibidi atumie mwili wa nyoka kutimiza agenda yake duniani.

Yesu naye ilibidi apewe mwili kimiujiza kupitia kwa mariamu, ili atimize na yeye agenda yake ya ukombozi duniani.

Mtu ni roho yenye mwili.

Ok, naamani kwa summary ya mafundisha haya umepata kitu.

Siwezi andika kila kitu humu, msijechoka kusoma bule.

Barikiwa sana, katika jina la Yesu.

Prepared by,

Amedeus J. Shio
0766 120 520

31/03/2020.

19/04/2020

Na, Amedeus J. Shio

*DINI NI MPANGO WA MWANADAMU KUMTAFUTA MUNGU.*
*WOKOVU NI MPANGO WA MUNGU KUMTAFUTA MWANADAMU.*

📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖

Luka 19 : 10 - "Kwa kuwa *Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.*"

📡📡📡📡📡📡📡📡📡📡

Dini zote duniani zinajitahidi kumtafuta Mungu kwa namna moja au nyingine.

Hata wazee wetu wa zamani(traditional religions) nao walijaribu kumtafuta Mungu kupitia mizimu na matambiko mbali mbali, kuabudu miti mikubwa, mawe nk.

Wahindu na wengine wengi huabudu hata wanyama na viumbe wengine wakidhani kuwa ndiyo miungu.

Zipo dini zinazomtafuta Mungu kupitia Muhamad, Buddha, Mariam, Musa nk..

Hizo zote ni jitihada za kumtafuta Mungu wa kweli.

Hata hivyo, cha kusikitisha ni kwamba, hakuna dini iliyofanikiwa kumpata Mungu wa kweli.

Dini zote zimekuwa zikipapasa papasa tu.

Kumjua Mungu wa kweli ilibidi mpaka yeye Mungu mwenyewe ajifunue kwetu.

K**a Mungu asingejifunua mwenyewe kwetu, basi mpaka leo tungekuwa bado tunapapasa tu.

Mungu amejifunua kwetu kupitia Kristo Yesu.
👇👇
Yohana 3 : 16 - Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Hatuwezi kumjua Mungu wa kweli pasipo Kristo Yesu.

Yesu alikuja duniani kumfunua na kutujulisha Mungu wa kweli.

Ukimjua Yesu umemjua Mungu.

Ukimwamini Yesu umemwamini Mungu.

Kwa nini?

Kwa kuwa Mungu alikuwa ndani ya Yesu.
Ukimwona Yesu umemwona Mungu.
👇👇
2 Wakorintho 5 : 19 - "yaani, *Mungu alikuwa ndani ya Kristo,* akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho."

Kwa maana hiyo mtu yeyote anayemkataa Yesu, amemkataa Mungu.

Njia ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu ni moja tu, nayo ni Yesu.

Bila Yesu hakuna mbingu. Ukimkataa Yesu umemkataa Mungu, na kwa hivo unasubiriwa na Jehanam ya moto.

Hakuna njia nyingine ya kumwona Mungu. Ni Yesu tu.
Haijalishi unaamini nini, wala una dini gani.
Yesu ndiyo njia pekee ya kumwona Mungu.
👇👇
Yohana 14 : 6 - "Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; *mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi."*

Na hapa kinachohitajiwa ni kuokoka, yaani, kumwamini Yesu k**a Bwana na mwokozi wa maisha yako.

Yesu ndiye ndia pekee ya kuokolewa na kumwona Mungu.
Hakuna kiongozi wa dini yoyote duniani mwenye uwezo wa kukupeleka kwa Mungu wa kweli.
Ni Yesu pekee.
👇👇
Matendo ya Mitume 4 : 12 - *"Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote,* kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."

K**a bado hujaokoka, fanya uamuzi huo mara, uokoke.
Yesu alikufa kwa ajili yako ili wewe uwe hai kupitia Yeye.

Wokovu sio aina ya dini mpya. Wokovu ni maisha mapya ndani ya Kristo.

K**a hujaokoka na unatamani kuokoka na upewe neema ya kuacha dhambi na kuishi matakatifu, wasiliana nami kwa number zifuatazo👇👇

Prepared by:

Amedeus J. Shio
0766 120 520

30/03/2020.

07/04/2020

Na, Amedeus J. Shio

*MAVAZI YA KUJISITIRI KWA MWANAMKE NI YAPI?*

JE! SURUALI NI VAZI LA KUJISITIRI?

📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖

1 Timotheo 2 : 9 - *"Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri*, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;"

📡📡📡📡📡📡📡📡📡📡

Biblia inaposema mavazi ya kujisitiri ina maana gani hasa?🤒

Hebu tuchek hizi version za kiingereza👇👇

"In like manner also, that women adorn themselves in *modest apparel*, with shamefacedness and sobriety; not with broided hair, or gold, or pearls, or costly array;"
1 Timothy 2:9 KJV

"I also want the women to *dress modestly*, with decency and propriety, adorning themselves, not with elaborate hairstyles or gold or pearls or expensive clothes,"
1 Timothy 2:9 NIV

Likewise, I want women to adorn themselves modestly and appropriately and discreetly in *proper clothing*, not with [elaborately] braided hair and gold or pearls or expensive clothes,
1 Timothy 2:9 AMP

Kwa kuchunguza hili andiko👆👆
tunagundua neno mavazi ya kujisitir linazungumzia Mavazi ya adabu(Modest apparel). Na mavazi ya adabu ni yale yanayoficha sehemu nyeti(private parts).

Unavovaa sketi au gauni jiulize Je! Sehemu nyeti zimefichika?
Ukivaa suruali jiulize pia je! Mtu anaweza kuona sehem zangu nyeti?
K**a yanakusitiri, safi, endelea kuvaa. K**a hayasitiri, achana nayo.

Tuzungumze kidogo swala la mwanamke kuvaa suruali.👇

Hakuna mahali biblia imekataza mwanamke kuvaa suruali, wala hakuna mahali biblia imesema kwamba suruali ni vazi la mwanaume.

Suruali kwenye mazingira flani huwa ndio vazi zuri la mwanamke kujisitiri kuliko hata sketi na magauni.
Chukulia mazingiza yafuatayo👇👇

-Kwenye michezo mingi ya wanawake
-Wanawake maaskari.
-Shamba dress kwa wanafunzi wa k**e.
- Wanawake wafanyakazi wa Tanesco.
- Wanawake magundi mechanic nk..
- Manesi na madaktari.
- Watoto wadogo wa k**e.
Nk..

👆👆
Nimetolea hayo maeneo k**a mfano; lakini yako mengi.
Mazingira k**a hayo, Suruali hufaa sana katika kumsitiri mwanamke.

Suruali haina dhambi kabisa. Ila inategemea tu ni suruali ya aibu au ya heshima( naamini naeleweka nikisema hivyo).

Kuna suruali wanawake wakivaa, zinasababisha ajali za barabarani nk.🐒

Hata sketi nyingine zikivaliwa huleta madhara hayo hayo.

Kwa hiyo tuko huru kuvaa mavazi yoyote ilamradi tu hayatuondoi kwa Yesu.
🤸‍♂️🤸‍♂️
Mambo ya mavazi yanategemea utamaduni na maadili ya mahali husika(Cultural aspect).

Kuna tamaduni wanawake ndio wanavaa suruali na wanaume wanavaa sketi.

Tamaduni za kina haruni makuhani walivaa magauni, na wengine wengi walivaa sketi. Je! Na sie wanaume wa leo tuvae magauni na sketi??😅
Japo kuna nchi kadhaa wanaume wanavaa sketi. Mfano nchi ya *Fiji*. Nenda ka-google utaona mwenyewe.👌

Suruali zilizotajwa kwenye biblia si k**a hizi zetu, zilikuwa ni kaptula.

Someni biblia muelewe jamani.👇👇

Kutoka 28 : 42 - "Nawe wafanyie suruali za nguo ya kitani, ili kufunika tupu ya miili yao; *suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani;*"

Suruali zao zilishonwa toka kiunoni hadi mapajani. Kwa hiyo kimsingi alikuwa anazungumzia kaptula. Suruali toka lini ikaishia pajani?🤷‍♂️

Na pia kitu kuvaliwa na kina haruni, daniel nk. Haimaanishi ndio sheria wote tuvae hivo.

K**a ni hivo tupigilie makanzu k**a Yesu.
Tusichanganye kweli na uongo wapendwa.

Yesu na mitume walivaa makanzu. Je! Na sisi tupigilie makanzu? Je! Tuseme kanzu ndo vazi la kiume au?

Jamani, swala la mavazi ni cultural sio spiritual. Ni swala linalotegemea maadili ya jamii husika katika utamaduni waliopo nao. Huwezi kuweka msimamo wa aina moja kuhusu lipi vazi sawa na lipi si sawa kidunia. Dunia ina mchanganyiko wa tamaduni mbalimbali, hivyo tegemea pia misimamo na maadili kutofautiana.

Ukiona jamii flani wanakataa aina flani ya mavazi, ni kwa lengo tu la kutunza maadili ya kile wanachokiamini, sio sheria ya Mungu ya jumla.

Kitheolojia utamaduni ambao hauathiri imani unaruhusiwa kuendelea. Ila utamaduni unaokinzana na imani ndio hupingwa.

Kwenye kumbukumbu la torati, tunaona wayahudi wanakatazwa kuvaliana mavazi kwa sababu, mwanaume ukivaa vazi la mwanamke aliye kwenye siku zake, na wewe unakuwa najisi siku saba.

Ndo maana wakapewa lile agizo la kutokuvaliana mavazi.

Hebu tuone👇👇

Kumbukumbu la Torati 22 : 5 - *"Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke;* kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako."

Anaposema yampasayo, anamaanisha, ambayo si ya kwake. Yaani, unachukua kwa mfano nguo ya mkeo unaivaa; au mwanamke unachukua nguo ya mumeo unavaa. Ndicho walichokatazwa.
Hilo andiko halizungumzii fashion au style ya nguo.

Kwa hivo wapendwa tusipindishe maandiko ili kuhubiri tunayoyataka. Tunapaswa kuihubiri kweli ya biblia k**a ilivyo.

Mambo ya msingi kuangalia kwenye swala la mavazi:👇👇

1. Je! Mavazi hayo yanasababisha makwazo kwa wengine?
K**a ndio, basi usiyavae.
K**a kweli umeokoka, utajua kipi ni kwazo na kipi sio kwazo.
Hata k**a ni suruali utajua ipi ni kwazo, ipi sio kwazo.(unahitaji moyo wa kiasi).

Japo kuna wanaume hata uvaaje bado kwao ni kwazo tu kwa kuwa wana roho za ukahaba zinawasumbua.
Aina hii ya wanaume wanahitaji kufunguliwa(deliverance).

2. Je! Haya mavazi yanakuathiri mahusiano yako na Mungu?
K**a ndio, achana nayo.
K**a unaweza yavaa na bado mahusiano yako na Mungu yakabaki salama, haina shida, vaa.

3. Je! Mavazi hayo yamepingwa kwenye biblia?
K**a yamepingwa usivae, k**a hayajapingwa, vaa.

Nimalize kwa kusema Roho Mtakatifu ni mwaminifu. Ukimwomba akuongoze hata kwenye mavazi atafanya hivyo.

K**a kweli umeokoka somo hili bila shaka limekuwa sana baraka kwako. Limekuweka huru katika Roho Mtakatifu atupaye kuwa na kiasi.
Sijalifundisha k**a mwalimu wa mahadili ya eneo fulani, bali k**a mwalimu na mchambuzi wa Biblia.
K**a unaipenda biblia umelifurahia, ila k**a ulishazoea kila kitu mpaka uwekewe sheria ndio zikuongoze, kazi sana.
Wanaoongozwa na Roho wa Mungu(sio sheria za kibinadamu), ndio wana wa Mungu.
Sheria husaidia mara nyingi kwa nje, lakini hutengeneza wanafiki wa hali ya juu.

Ukipinga kuongozwa na Roho na kung'ang'ania kuongozwa na sheria, una shida sana.
*Sisi tunaongozwa na Roho Mtakatify kwa kutumia sheria mpya iliyo ndani ya Kristo Yesu katika Neno la Mungu;* sio sheria za kujitungia tu wenyewe na vimisimamo vyetu bibafsi.

Pia nishauri, tuondoe swala la kuhukumu watu kwa aina ya mavazi. Tukatae mavazi ya aibu, lakini tusimamie biblia.

Culture is dynamic. Kilichoaminika na kukubalika miaka ya zamani ni tofauti na sasa. Especialy katika nyakati hizi za mchanganyiko wa
tamaduni na maadili.
Usipofunguka katika hili utapata shida sana. Utabaki tu kusema yule anahubiri huku kavaa suruali? Anaenda motoni. Sijajua ni moto upi unazungumzia!!🤒

Nikikuuliza culture yetu ya kiafrika mavazi yetu ni yapi sijui utajibuje?
Maana hata kuvaa suti tumeiga waingereza.🤷‍♂️

Tutoke katika maisha ya torati ya Musa, tuingie kwenye Neema na kweli, wapendwa.
Bila kuibadili neema hiyo kuwa ufidadi.

Yuda 1 : 4 - "Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, *wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi,* nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo."

Tuache udini tufundishe kweli ya biblia.

Prepared by,

Amedeus J. Shio
0766 120 520

31/03/2020.

06/04/2020

Na, Amedeus J. Shio

*HIVI MWAMKE KUJIPAMBA NI DHAMBI?*
*NI KWELI BIBLIA IMEKATAZA MWANAMKE KUJIPAMBA?*

📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖

Isaya 61 : 10 - Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, k**a bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na *k**a bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.*

📡📡📡📡📡📡📡📡📡📡

Hivi kuvaa hereni, mikufu, bangili, vikuku, ni dhambi?
Kusuka rasta na mitindo mingine ya nywele nayo ni dhambi?
Kupaka rangi, shedo, wanja, poda nk. Nako ni dhambi?

Upi ukweli wa mambo haya?🤔

Baada ya kuyachunguza maandiko kwa mda mrefu, k**a mwanafunzi wa biblia, na kupata uhakika wa mambo yale yaliyokuwa tata kwangu, naligundua ukweli ufuatao.👇

Kibiblia, hakuna dhambi yoyote katika hayo.
Biblia haijakataza mwanamke kujipamba.

Wanaokataza kujipamba ni watu tu kwa aidha kukosa tafsiri sahihi ya maandiko, au kuridhisha nafsi zao.

Yaani mtu anaweza akakataza kitu kwa kuwa tu yeye binafsi hapendi..na kwa sababu anataka aaminike, anatafuta maandiko ya kumuunga mkono hoja yake, hata kwa kuyalazimishia.
👇👇
Yeremia 23 : 16 - "Bwana wa majeshi asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria; huwafundisha ubatili; *hunena maono ya mioyo yao wenyewe;* hayakutoka katika kinywa cha Bwana."

Biblia inasema tunapaswa kuhubiri neno la Mungu kwa uaminifu.👇👇

Yeremia 23 : 28 - "Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na *yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu.* Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana."

Tusilitangue neno kwa mapokeo yetu ya kidini. Tuache mapokeo ya kidini, tuhubiri ukweli wa biblia.👇👇

Marko 7 : 13 - *"huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana;* tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo."

Lengo la somo hili si kushawishi watu kujipamba, bali ni kuuleza ukweli wa swala hili katika biblia.

K**a nilivoeleza hapo juu, narudia tena kusema, kujipamba sio dhambi kibiblia.

Mwanamke ni kawaida kabisa kujipamba, na biblia haijakataza swala hilo.

Lakini kabla ya kujipamba jiulize maswali yafuatayo👇👇

*1.* Je! Kujipamba kwangu kunaharibu mahusiano na ukaribu wangu na Mungu?

Mathayo 18 : 8 - "Basi mkono wako au mguu wako *ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe;* ni afadhali kuingia katika uzima hali umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele."

K**a kwa sababu ya kujipamba unachelewa kanisani, unashindwa kujiachia ukiwa kwenye maombi, unashindwa kumwabudu Mungu kwa kuogopa kuharibu make-up, nakushauri ni bora uache.
Bora uache kujipamba kuliko kuharibu mahusiano yako na Mungu.

Paulo aliiona hiyo hatari kwenye kanisa moja, akaamua kuwaonya kwa hilo. Aliona walikuwa wakijipamba lakini mahusiano yao na Mungu hayakuwa mazuri.

Walikuwa wakiacha kutilia mkazo mambo ya rohoni, badala yake wako busy na mambo ya mwilini k**a kuvaa mavazi ya gharama nk..
Tunasoma, 👇👇

1 Timotheo 2 : 9 - "Vivyo hivyo *wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;"*

Ukisoma hapo kwa makini👆utagundua paulo hakukataza kujipamba. Anasema, *"Wanawake na wajipambe"* , kwa hiyo Hakukataza wasijipambe.
Ila alitaka wazingatie katika kujipamba kwao, mambo matatu:
🔐Mavazi ya kujisitiri
🔐Adabu nzuri
🔐Moyo wa kiasi

Hebu tuone na Petro anasemaje 👇👇

1 Petro 3 : 3 - 4 "Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu."

Petro anasisitiza mambo mawili katika kujipamba: roho ya upole, na roho ya utulivu.

Hajakataza kujipamba. Alimaanisha waanze na mapambo ya ndani kwanza(moyoni), ndipo kujipamba kwa nje kutakuwa na maana.

Wao walijipamba tu nje, lakini ndani yao hawakuwa sawa.

Ok, ngoja labda nikuletee tafsiri ya kiingereza kwenye hiki kifungu, utanielewa tu..👇👇

"Your adornment must not be *merely external*—with interweaving and elaborate knotting of the hair, and wearing gold jewelry, or [being superficially preoccupied with] dressing in expensive clothes; but let it be [the inner beauty of] the hidden person of the heart, with the imperishable quality and unfading charm of a gentle and peaceful spirit, [one that is calm and self-controlled, not overanxious, but serene and spiritually mature] which is very precious in the sight of God."
1 Peter 3:3‭-‬4 AMP

Naamii umeona neno merely hapo. Hilo neno limetumika kuonesha kujipamba kwenu kusiwe kwa nje peke yake, yaani kusiwe kujipamba ambako hakuna maana, bali ili kulete maana changanyeni na mapambo ya ndani.

Me nafkiri umeelewa bhana, labda uwe ulijiandaa kutokuelewa..😅

Najua kuna watu dini zimewaingia kiasi kwamba hata kuwaelimisha kweli ya Mungu inakuwa shida kweli. Wameshaweka ngome zao tayari. Watu wa namna hii ni kazi sana.

Ukitaka kuelewa kweli halisi ya biblia ni lazma uvue udini kwanza.

Anyway, tuendelee na somo letu jamani..

Tunza mahusiano yako na Mungu. Angalia mapambo na makeup ambazo hazikuondolea Uhuru wako na Kristo.

Hapa ndipo wengine hupata kitu tunaita personal conviction ya kuacha kabisa kujilamba. Kuna watu Mungu huwazuilia kabisa kujipamba.
K**a na wewe Roho Mtakatifu anakushuhudia kutokujipamba, mtii. Lakini usilazimishe na wengine wawe k**a wewe; umekatazwa wewe kibinafsi.

Ukiamua kujipamba sawa, na ukiamua kutojipamba sawa; cha muhimu tunza mahusiano yako na Mungu.

*2.* Je! Kwa nini nataka kujipamba?(motive behind).

Watu hujipamba kwa sababu mbalimbali:👇

*A).* Kujipamba kwa ajili ya miungu migeni.
👇

Mwanzo 35 : 4 - "Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu."

Hizo pete za masikioni zinazozungumziwa hapo ni hereni(rings). Lakini walizivaa hizo hereni k**a kinga(hirizi). Ndio maana ilibidi waziondoe ili kutembea na Mungu.

Hebu tusome kwenye tafsiri ya kiingereza, 👇👇

"So they gave Jacob all the [idols and images of the] foreign gods they had and *the rings which were in their ears [worn as charms against evil],* and Jacob buried them under the oak tree near Shechem."
Genesis 35:4 AMP

Naamini umeona hapo👆, walivaa hereni k**a kinga(charms). Otherwise, wasingekuwa na haja ya kuzivua.

Kuvaa hereni sio dhambi. Ilamradi huvai k**a hirizi ya kukulinda. Unavaa ili upendeze.

Kuna watu wanasema ati mapambo ni miungu. Sijui wanasoma biblia gani?!🤷‍♂️

Hiyo miungu hapo kwenye hilo andiko hayakuwa mapambo jamani, vilikuwa vinyago(idols), na vijisanamu) tu. Walikuwa wamevibeba mikononi.
Someni hilo andiko vizuri mwelewe.👆

Usivae pete, hereni, mikufu, vikuku, ama chochote kwa lengo la kulata majini ya bahati, kuvuta mpenzi wako, kukulinda nk..hayo ni machukizo kwa Mungu.
Huko ni kujiungamanisha na miungu migeni.

Jipambe tu kwa lengo la kupendeza inatosha.

*B).* Kujipamba kwa sababu unahisi Mungu kakuumba vibaya. Yaani unajipamba kwa lengo la kumkosoa Mungu. 👇

Warumi 9 : 20 - "La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, *Kwani kuniumba hivi?"*

Kubali ulivyoumbwa mpendwa. Usijichukie kwa kuwa wewe ni mweupe ama mweusi, au ulitaka kuwa na kichwa cha aina flani.

Usijipambe kwa lengo hilo. Ni lazma ujikubali kwanza, ndipo ujipambe.

Pamba uzuri aliukupa Mungu.

Vyovyote ulivyo, wewe ni mzuri tayari kwa asili. Usipojikubali hivyo, kuna shida si ndogo.

Mapambo hayana maana ya kukupa uzuri ambao huna, bali kupamba uzuri uliopewa na Mungu tayari.
Sema amen, k**a umenielewa..💪

Kujipamba sio kubadili uumbaji wa Mungu, kujipamba ni kupendezesha uumbaji wa Mungu.

Kwanza huwezi kujibadili hata hivyo. Labda ufanyiwe scientific procedures.

Narudia, jikubali kwanza ndipo ujipambe.

Mwanzo 1 : 31 - *"Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana.* Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita."

Kila unapojitazama kwenye kioo, jisemee hili andiko👇

Zaburi 139 : 14 - *"Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.* Matendo yako ni ya ajabu, *Na nafsi yangu yajua sana,"*

Bwana Yesu asifiwe..👍

*C).* Kujipamba kwa ajili ya kuwanasa wanaume au ukahaba. Tunao mfano wa mwanamke Yezebeli. Yeye alijipamba kwa ajili ya ukahaba. Tunasoma, 👇👇

2 Wafalme 9 : 30 - "Hata Yehu alipofika Yezreeli, *Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake,* akachungulia dirishani."

Huyu Yezebeli alijipamba kwa sababu ya ukahaba. Je! Wewe unajipamba kwa sababu gani?

Hata leo makahaba hujipamba vile vile ili waweze kunasa wanaume kwa urahisi, na wanafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kujipamba ukiwa na nia mbaya k**a hii ni bure kabisa katika ukristo wako. Utaona k**a wanaume wanakusifia lakini wanakudanganya tu wakuchezee na kukuacha. Hebu soma hapa..👇👇

Yeremia 4 : 30 - "Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, *ujapojipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri bure tu; wapenzi wako wanakudharau; wanakutafuta roho yako."*

Kujipamba ili uangushe wanaume, biblia inasema, wanaume hao wanakudharau tu. Huna lolote. Hiyo ni nia mbovu kabisa.

Usijipambe kwa mavazi ya kikahaba👇

Mithali 7 : 10 - "Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana *mavazi ya kikahaba,* mwerevu wa moyo;"

Vaa mavazi ya kujisitiri(modest apparel).
Hata k**a ni suruali, iwe ya kusitiri(modest).

Uwe na nia njema unapojipamba. Hakikisha kwa ujumla wake, unajipamba kwa utukufu wa Mungu.👇

1 Wakorintho 10 : 31 - "Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, *fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.*"

Wakolosai 3 : 17 - "Na *kila mfanyalo,* kwa neno au kwa tendo, *fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu* Baba kwa yeye."

1 Wakorintho 6 : 20 - "maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, *mtukuzeni Mungu katika miili yenu.*"

Hakikisha unajipamba ili upendeze kwa lengo la kumtukuza Mungu. Otherwise recheck the motivation behind adornment.

Bila shaka tumeelewana hapo.

*3.* Je! Kujipamba kwako kunakwaza wengine?

Je! Unajipamba kiasi cha kuwafanya watu wasiendelee mbele na Yesu?

Luka 17 : 1 - "Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini *ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!"*

Jifunze kujipamba kwa kiasi mpendwa.

Biblia inasema tuwe na kiasi katika mambo yote.👇
2 Timotheo 4 : 5 - "Bali wewe, *uwe na kiasi katika mambo yote,* vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako."

Mambo yote ni pamoja na kujipamba. Jipambe kwa kiasi.

Utajuaje hicho kiasi ndio sawa?!

Roho mtakatifu atakuambia. We mwulize kila unapojipamba, utapata ushuhuda wa Roho ndani yako.

Warumi 8 : 14 - "Kwa kuwa wote *wanaoongozwa na Roho wa Mungu,* hao ndio wana wa Mungu."

Ukijifunza kujipamba kwa kiasi, huna haja ya kuwekewa sheria.

Wagalatia 5 : 23 - "upole, *kiasi; juu ya mambo k**a hayo hakuna sheria."*

Bila shaka umenelewa kwa uzuri. Hallelujah!

Hayo yalikuwa ni baadhi ya maswali machache ya kujiuliza kabla ya kuchukua msimamo wa kujipamba.

Mwanamke kujipamba sio dhambi. Tusifiche ukweli kwa sababu za kifarisayo.

Wanawake wengi wanaokatazwa kujipamba kwenye dini zao, mioyoni mwao wanatamani ila basi tu. Wameamua tu kuishi kinafiki. Hiyo ni mbaya zaidi. Nawashauri waache unafiki na waishi uhalisia wa wanachokiamini.

Wanaambiwa waachane na kujipamba lakini asili inagoma.(woman nature).
Wameumbiwa kujipamba..👇👇

Yeremia 2 : 32 - *"Je! Mwanamwali aweza kusahau mapambo yake,* au bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau mimi kwa muda wa siku zisizo na hesabu."

Anasahauje kwa mfano?!😇

Anyway, somo letu limeishia hapo kwa sasa.

Wale mliochukizwa na somo hili sababu ya misimao yenu ya kidini, niwaulize swali, 👇

Wagalatia 4 : 16 - *"Je! Nimekuwa adui wenu kwa sababu nawaambia yaliyo kweli?"*🤷‍♂️

Biblia inasema, 👇

Yohana 8 : 31 - 32 "Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; *tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru."*

Uhuru wa kweli unapatikana ndani ya Neno, sio kwenye misimamo ya kidini.

Bwana Yesu akubariki mpendwa..🙋‍♂️

Prepared by,

Amedeus J. Shio
0766 120 520

03/04/2020.

Address

Po Box 170
Morogoro

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Amedeus J.Shio Ministries posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Amedeus J.Shio Ministries:

Share