Neema ya Kristo

Neema ya Kristo NEEMA YA BWANA WETU YESU KRISTO NA PENDO LA MUNGU NA USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE. 2WAKORINTHO 13:14

05/08/2026
*UAMINIFU wa THAMANI*“Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. Akaja yule aliyepokea talan...
28/07/2026

*UAMINIFU wa THAMANI*
“Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako” (Mathayo 25:19-21).

Neno uaminifu ni hali ya mtu kutenda jambo fulani kwa namna ambayo mtu mwingine atamwamini. Kwa lugha nyingine, uaminifu ni HALI ya moyo ambayo itampelekea mtu kuthamini NA kutii utaratibu au jambo la mtu mwingine, “hata k**a hapati faida binafsi” ila anafanya kwa ajili ya mwingine.

Kila nisomapo huu mfano wa talanta najikuta napata somo jipya. Huyu bwana aliporudi “baada ya siku nyingi”, (inamaana hakuwepo hawa jamaa wakifanya kazi), alitoa ZAWADI au alimpandisha cheo huyu jamaa wa talanta 5 aliyezalisha 5 zingine. Angalia tena hapa “Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako”. Huyu mtumwa alikuwa na sifa 2, kwanza ni WEMA, na pili ni UAMINIFU. Angalia tena hapa, bwana wake akarudia tena neno “uaminifu” na kusema ” ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako”! Ina maana kilichomvutia sana bwana wake na kuona huyu jamaa amestahili KUPANDA cheo ni UAMINIFU! Ukiangalia yaliyo msibu yule jamaa wa talanta 1 utagundua aliitwa “MWOVU”, japo kwa mtizamo wa kawaida, alikuwa “mwaminifu” kutunza kilicho cha bwana wake! Sasa angalia hapa, huyu wa talanta 5 alifanya KAZI akaleta FAIDA, huyu wa talanta 1 hakufanya KAZI, “hakupoteza hela ya watu (mtaji) ila pia hakuleta faida”! Akaadhibiwa.

Unapofanya JAMBO la faida (kuzaa matunda), kwa KUAMUA kwa uhuru wako bila kusimamiwa au watu kuona, hilo ni jambo KUBWA! Hawa jamaa wote hawakusimamiwa, bwana wao alisafiri; baada ya SIKU NYINGI alirudi kufanya hesabu. Najaribu kuwaza k**a huyu mtumwa aliyepewa talanta 1 angesimamiwa ingekuwaje? Nashawishika kujibu kwamba “angezalisha pia”, ila sio kwa “kuamua mwenyewe”! Kuna “uaminifu wa thamani” na “uaminifu wa sababu”. Watu wengi ni waaminifu kwa sababu fulani, ila k**a wangekuwa mahali peke yao, wangefanya tofauti! Ni kwa sababu tu “mtu fulani” yupo ndio maana ulijizuia kufanya jambo fulani! Huu ni uaminifu pia ila SIO wa thamni mbele za Mungu.

Nitakupa mfano. Umewahi kufikiri ni watu wangapi wengeenda mbali kabisa na wake/waume zao halafu wakasimama waaminifu? Girl/boyfriends maana hawana la kujitetea pia, wanahusika. Nazungumzia watu ambao “imewapasa” kuishi maisha masafi ila UAMINIFU ni jambo zito. Hebu fikiri mtu anajisifia kwamba mimi sitaanguka katika zinaa/uzinzi, na anawashangaa na “kuwasema” wenzake wakianguka badala ya kuwaombea. Subiri kujaribiwa kuna kuja, kaa sawa. Ghafla! mume/mke anapata shule nje ya nchi, hujakaa sawa mijamaa/wadada wanaanza kuku-beep, hujakaa sawa unaanza kupita vipindi vigumu, wanaokuja kukusaidia ni wale wa jinsia tofauti na wewe, ghafla! tu. Unagundua uko mbali na hakuna “ushahidi”, unaamua kuchukua hatua ngumu za kuvunja UAMINIFU kwa mwenzako na kwa Mungu. Sawa utatubu, utajikausha. Mwenzako akirudi, unaanza kuchachamaa tena, unashambulia wengine walioanguka, unakuwa moto moto na kweli huanguki tena, ila Mungu akiangalia anagundua jambo. Uaminifu wako ni kwa mumeo/mkeo na sio kwa Mungu, maana “bwana wako alipokawia hukuweza kuwa mwaminifu”! Bwana anakupita, hupandi cheo. Mungu akiangalia anaona unafiki tu. Angalia tena uaminifu “ulio wa thamani” maana yake. Wakati hakuna mtu anakuona, unafanyaje?

Vijana wengi wamejifariji kwamba wakioa/olewa wataweza kuwa “waaminifu”. Jua neno hili, ukiweza kuwa mwaminifu sasa, ni ishara kwamba hata kuko mbele utakuwa mwaminifu; ukishindwa kuwa mwaminifu sasa, hata ukioa/olewa unaweza pia ukashindwa kuwa mwaminifu. Zingatia neno hili, ukiwa peke yako (single) na ukawa mwaminifu, huo uaminifu wako ni wa THAMANI sana mbele za Mungu kuliko uaminifu “kwa sababu” umeoa/olewa. Siku hizi utasikia vijana wanapiga mahesamu ya kuoa/olewa ili kushinda tamaa za mwili; baada ya kuoa wanagundua tamaa za mwili na majaribu ya ngozo yameongeka maradufu! Kumbe ulipaswa KUSHINDA ukiwa peke yako ndiposa ushindi huwa dhahiri, kwamba hata sasa baada ya kuoa/olewa unashinda kwa sababu ya Bwana, na sio aibu au hofu ya mwanadamu mwenzio. Kushinda dhambi kwa sababu ya “hofu ya Mungu” ni tofauti na kushinda dhambi hiyo hiyo kwa sababu ya “hofu ya watu”. Thamani za ushindi hizi mbili ni tofauti pia.

Hili jambo la kukosa uaminifu ukiwa peke yako limedidimiza uchumi wa watu wengi. Mungu ameweka vitu “vichache” mkononi mwako, kisha akakaa mbali kuangalia utafanyaje. Ukamsahau Mungu na watu wengine, ukujipendelea kwa sababu uko peke yako na maamuzi yako! Nitakupa mfano mwingine. Umekaa katika nafasi ya maamuzi katika ofisi fulani. Hela zinapita hapo usoni kabisa, unafika mahali unachomoa kidogo na kuweka mfukoni, huku unajifariji eti “kila mtu anafanya hivyo”. Ghafla! Bwana (Yesu) anakuja kukagua mahesabu (moyoni mwako) ili aweze kukuinua katika kiwango kingine cha baraka. Ghafla! anagundua hakuna UAMINIFU, Bwana anapita. Unabaki hapo ukishangaa. Wakati unalalamika na kuonea wengine wivu wakiinuliwa, Roho Mtakatifu anakuonyesha moyo wako, unajua kabisa hata ile hatua uliyovuka ilikuwa sio baraka ya Mungu ila ulicheza faul mahali, unajua, na hilo ndio JIBU Mungu atakujibu ukiomba baraka, Atakufunulia moyo wako uone “mahali ulipoanguka ili utubu” ili akuinue tena. Nakwambia neno hili, ukivushwa na Mungu utajua ni Mungu, ukicheza rafu utajua ni rafu, Roho Mtakatifu hatakaa kimya, utajua tu. Uaminifu wa thamani. Unafanya nini ukiwa peke yako!

JIFUNZE KUOMBA KABLA MAMBO HAYAJA HARIBIKA.Watu wengi wamekuwa WAOMBAJI wazuri sana pindi waonapo mambo yao YAMEHARIBIKA...
28/07/2026

JIFUNZE KUOMBA KABLA MAMBO HAYAJA HARIBIKA.
Watu wengi wamekuwa WAOMBAJI wazuri sana pindi waonapo mambo yao YAMEHARIBIKA, au hayaendi sawasawa na MATARAJIO.
Mfano; WAKATI BIASHARA YAKO inakwenda vizuri unaweza jisahau na ukawa si mtu wa MAOMBI, si mtu wa IBADA, si mtoaji, lakini pale tu, BIASHARA inapo yumba, ndiyo wakati ambao UNAJIKUTA UNAANZA KUTUMIA nguvu KUBWA sana kumkaribia MUNGU.

Mfano 2; Watu wengi wanapokuwa kwenye UHITAJI WA kupata wenza(Mume/mke), huu wakati huutumia kuwa karibu sana na Mungu kwa njia ya MAOMBI, kuhudhuria ibadani na kutoa pia, na Mungu kwa uaminifu wake Huwa hachelewi kuwafanyia njia, LAKINI BAADA YA KUIPATA NDOA mambo hubadilika, YULE ALIYE KUWA MUOMBAJI, majukumu yameongezeka haombi tena, IBADA si Muhimu kwake tena, mambo ya kanisa hayana maana kwake tena.

NINATAMANI NIKUKUMBUSHE, kuna gharama KUBWA ya kuilinda BARAKA YA MUNGU KULIKO KUIPATA, wengi hudhani tunahitaji Maombi mengi kwaajili yakupata NDOA AU MAFANIKIO, harafu tukisha vipata niwakati wa kuenjoy tu, jambo ambalo si kweli, TUNAHITAJI MAOMBI MENGI ZAIDI, IBADA NYINGI ZAIDI, UTOAJI MWINGI ZAIDI, wakati Mungu AMETUPA vilivyo vyake(ametubariki).

USIPO JIFUNZA KUIOMBEA SANA SANA NDOA YAKO SASA HIVI WAKATI MNAFURAHA NA AMANI, utajifunza kuiombea wakati imeharibika haina amani tena wala upendo ule WA mwanzo.

USIPO JIFUNZA KUIOMBEA BIASHARA YAKO LEO WAKATI UNAPATA FAIDA NA UNA MZIGO MKUBWA WA BIASHARA, utajifunza kuomba ukiwa huna hata huo MTAJI ULIONAO Leo.

USIPO JIFUNZA KUWA MWAMINIFU KWENYE ENEO LA UTOAJI LEO, utajifunza ukiwa huna hata cha kutoa na unatamani kutoa.

JIFUNZE KUOMBA KABLA HAUJA JARIBIWA,
Marko 14:38.
"Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu."

FANYA KILA NAMNA UNAYOIJUA ILI KUWEZA KUMKARIBIA MUNGU ZAIDI UKIWA HIVYO ULIVYO, usingojee MAMBO YAHARIBIKE NDIYO UTIE BIDII YA KUMTAFUTA MUNGU.

Pastor Bampele Nathanael
28 July 2023.

MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU 21, NUSU MWAKA YAPILI 2026.GOOD NEWS CENTRE MOROGORO +255 762 186 639SIKU YA KUMI NA TI...
17/07/2026

MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU 21, NUSU MWAKA YAPILI 2026.
GOOD NEWS CENTRE
MOROGORO
+255 762 186 639

SIKU YA KUMI NA TISA(19)
17.07.2026

Siku ya kumi na tisa ya maombi.
Kuharibu roho ya Kurudi Nyuma na Kukata Tamaa (Victory over Backsliding and Discouragement). Leo tarehe 17 Julai 2026, tunashughulika na hali ya kiroho na kisaikolojia inayomfanya mtu atake kuacha safari akiwa amebakiza hatua chache kuimaliza/kufika mwisho. Ni siku ya kuomba neema ya uvumilivu.

*MAANDIKO YA KUSIMAMIA*

Wagalatia 6:9 *Imeandikwa* "Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia mioyo."

Wafilipi 3:13-14 *Imeandikwa*
"13. Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; 14. nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu."

Wafilipi 3:13-14 *Imeandikwa* "...nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele, nakaza mwendo niifikilie fadhili ya dhawabu..."

Isaya 40:31 *Imeandikwa* "Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa k**a tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia."

*MAOMBI YA LEO*

1. *Mshukuru Mungu kwa Neema ya uvumilivu:* Mshukuru Mungu kwa kukuwezesha kufika siku ya 19. Ni neema yake pekee iliyokushika mkono tangu Siku ya 1 hadi leo tarehe 17 Julai 2026.

2. *Kukataa roho ya Kuchoka:* Kwa jina la Yesu, vunja kila roho ya uchovu wa rohoni na mwilini. Kataa sauti inayokuambia unapoteza muda au maombi haya hutapata majibu.

3. *Kusahau Yaliyo Nyuma:* Omba Mungu akusaidie kuacha kabisa kumbukumbu za kushindwa kwa miaka iliyopita. Tamka: "Sitaangalia nyuma tena, ninakaza mwendo kuelekea ushindi wa 2026!"

4. *Omba Nguvu Mpya:* Mwombe Bwana akufanye upya k**a tai. Omba "upako wa uvumilivu" (endurance) ili umalize siku hizi 21 zilizobaki kwa kishindo na kuanza mwaka kwa kishindo.

5. *Kuharibu roho ya Kurudi Nyuma (Backsliding):* Omba dhidi ya majaribu yanayoweza kukurudisha kwenye dhambi au tabia za kale ulizozicha. Omba Mungu akutie nguvu ya kusimama imara.

6. *Kuvuna kwa Wakati Wake:* Simama juu ya ahadi ya Wagalatia 6:9. Tangaza kuwa wakati wako wa kuvuna matunda ya maombi haya umewadia na hautapita.

*OMBA*
"Mungu Mwenyezi, leo Siku ya 19 naja mbele zako nikitafuta nguvu mpya. Nakataa roho ya kukata tamaa na kuzimia moyo. Asante kwa neno lako linalosema nitavuna nisipozimia moyo. Mwaka huu 2026, sitarudi nyuma; nitasonga mbele hadi nishike taji yangu. Nifanye upya k**a tai ili nipige mbio bila kuchoka. Asante Bwana kwa kunipa ushindi mlangoni mwa kilele cha maombi haya. Amen."

MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU 21, NUSU MWAKA YA PILI 2026.GOOD NEWS CENTRE MOROGORO +255 762 186 639SIKU YA KUMI NA N...
16/07/2026

MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU 21, NUSU MWAKA YA PILI 2026.
GOOD NEWS CENTRE
MOROGORO
+255 762 186 639

SIKU YA KUMI NA NANE(18).
16.07.2026

Siku ya kumi na saba bado Mungu ameendelea kuwa MUAMINIFU, leo tunakwenda kuomba tena, tutaomba juu ya Kibali cha Pekee na Kuinuliwa kwenye huduma, kazini au kwenye biashara. Tunakwenda kunamlilia Mungu akatutofautishe na wengine. Katika soko lenye ushindani au mahali pa kazi penye watu wengi, unahitaji alama ya ubora kutoka kwa Mungu ili uonekane na kupandishwa daraja.

*MAANDIKO YA KUSIMAMIA*

Zaburi 75:6 - 7 *Imeandikwa*
"Maana siko mashariki wala magharibi,
Wala nyikani itokako heshima. 7. Bali Mungu ndiye ahukumuye;
Humdhili huyu na kumwinua huyu."

Danieli 6:3. *Imeandikwa*
"Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote."

Mwanzo 39:3-4 *Imeandikwa*
"3. Bwana wake akaona ya kwamba BWANA yu pamoja naye, na ya kuwa BWANA anafanikisha mambo yote mkononi mwake. 4. Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake."

*MAOMBI YA LEO*

1. *Mshukuru Mungu kwa nafasi aliyokupa:* Mshukuru Mungu kwa huduma, kazi uliyo nayo au biashara unayoifanya sasa. Mtukuze kwa kuwa Yeye ndiye anayekuwezesha.

2. *Omba Roho Bora (Excellent Spirit):* Mwombe Mungu akupe roho k**a ya Danieli roho ya kufanya mambo kwa ubora wa hali ya juu, ili ufanyike baraka kwenye maisha ya watu na watu wavutwe kwenye utumishi ulionao, au uweze kuonekana na viongozi na wateja kwenye biashara yako.

3. *Omba Kuinuliwa na Mungu:* Tamka kuwa kuinuliwa kwako hakutategemea kujuana na watu au upendeleo wa kibinadamu, bali kutatoka kwa Bwana. Omba Mungu akukumbuke katika msimu huu wa promosheni au upanuzi wa huduma yako, kazi yako, biashara yako na kila eneo la maisha yako unalostahili kuinuliwa.

4. *Vunja roho ya kudumaa:* Omba dhidi ya roho ya kukaa kwenye cheo kimoja au kiwango kilele cha huduma/utumishi, kiwango kimoja cha mapato kwa miaka mingi bila mabadiliko. Amuru kudumaa huko kuishe leo.

5. *Kibali Mbele ya Wakubwa/Wateja:* Omba Mungu akupe kukubalika, ili kila unachofanya kionekane kina thamani na sifa machoni pa wale wanaofanya maamuzi.

6. *Kutofautishwa na Washindani:* Mwombe Mungu akupake mafuta ya utofauti (distinction). Katika watu mia moja wanaofanya kitu kilekile unachofanya basi wewe ukakimbiliwe, kwenye huduma, kazi au biashara.

*OMBA*
"Baba katika jina la Yesu Kristo, leo Siku ya 18 nakuja mbele zako nikiomba kuinuliwa. Wewe ndiye unayemtoa mnyonge mavumbini na kumketisha na wakuu. Naomba unipe 'Roho Bora' mwaka huu 2026 ili nitofautishwe kihuduma, kazini na kibiashara. Kila kizuizi cha kunifanya nibaki chini nakivunja katika jina la Yesu. Naingia katika msimu wangu wa kupandishwa na kuheshimiwa. Asante kwa kuwa kuinuliwa kwangu kunatoka kwako. Amen."
Fanya kile ambacho Mungu amekupa kufanya kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu kuliko kawaida. Kibali cha Mungu huambatana na juhudi za mwanadamu.

KWELI TANO KUHUSU UTAJIRI NA UMASIKINI1. HAKUNA ANAYEZALIWA TAJIRI AU MASIKINI, WOTE TUNAZALIWA TUKIWA NA NAFASI SAWA i)...
15/07/2026

KWELI TANO KUHUSU UTAJIRI NA UMASIKINI

1. HAKUNA ANAYEZALIWA TAJIRI AU MASIKINI, WOTE TUNAZALIWA TUKIWA NA NAFASI SAWA

i) Wote tunazaliwa uchi lakini hatuzaliwi watupu, tunazaliwa na vitu ndani yetu vinavyotosha kugeuza maisha yetu tukivitumia

ii) Uamuzi wa kubaki uchi unabaki mikononi mwa mhusika akishajitambua

2. UMASIKINI AU UTAJIRI SI MUUJIZA BALI NI MATOKEO YA MAAMUZI SAHIHI AU MABOVU MENGI ANAYOFANYA MTU

Maisha ni mchezo wa maamuzi ambao mtu anaucheza kwa masaa 24 (siku moja moja) ya maisha yake kila siku!
Maamuzi kuhusu FURSA, MUDA, RASILIMALI, FEDHA INAYOPITA MIKONONI MWA MTU NA MAHUSIANO NA WATU, hivi ndivyo huamua mtu awe masikini au tajiri baada ya kipindi fulani cha muda!

3. UMASIKINI AU UTAJIRI SI BAHATI NZURI AU MBAYA, MTU ANAKUWA TAJIRI AU MASIKINI KWA MAAMUZI YAKE YA DHATI YANAYOJIRUDIA!

Hakuna masikini aliyekuwa MASIKINI bahati mbaya, kila masikini anavunja KANUNI ZINAZOTAWALA MAISHA kwa mwendelezo na mfululizo!
Na kila TAJIRI anatajirika kwa kuzizingatia na kuziheshimu KANUNI ZINAZOTAWALA MAISHA ambazo masikini anazivunja!

4. MTU YEYOTE ANAWEZA KUANZIA ALIPO NA KUWA TAJIRI AU MASIKINI

TAJIRI anaweza kuamua kuishi kiholela nje ya KANUNI na baada ya muda mchache akawa masikini kabisa, kadhalika MASIKINI anaweza kugeuka na kuanza kuziheshimu KANUNI ZINAZOTAWALA MAISHA na baada ya MUDA atakuwa tajiri!
UMASIKINI na UTAJIRI ni k**a vazi ambalo mtu yeyote anaweza kulivaa au kulivua apendavyo mwenyewe!

5. UMASIKINI AU UTAJIRI HAUTEGEMEI SANA MAHUSIANO BINAFSI NA MUNGU BALI UWEZO WA MTU KUZIISHI KANUNI ZA MUNGU ZINAZOTAWALA MAISHA

Mfano Bakhresa au Mo Dewji hawajajaa maandiko, kunena kwa lugha, wala karama za Roho Mtakatifu, lakini NI MATAJIRI NA KUNA UWEZEKANO HADI YESU ANARUDI WATAKUWA WANAZIDI KUTAJIRIKA!

Lakini watu hawa WANAISHI KANUNI zinazotawala maisha k**a vile UTENDEAJI KAZI MAWAZO (Believing and working on every positive and constructive idea), BIDII YA KAZI (Hardwork), MATUMIZI SAHIHI YA FURSA (The best use of opportunities), MAHUSIANO SAHIHI NA WATU (They know how to relate with people based on their levels importance, status and positions), MATUMIZI SAHIHI NA BORA YA MUDA (Rightly investing, utilizing and redeeming time), na NYINGINE NYINGI....

NIMESHAKUPA PA KUANZIA,

JIFUNZE NA UAMKE,

CHAGUA UPANDE WAKO KATI YA UMASIKINI AU UTAJIRI,

HALAFU TUONANE MIAKA MITATU, MITANO AU KUMI IJAYO K**A BWANA YESU HATAKUWA AMERUDI KULICHUKUA KANISA LAKE!

RUKSA KUSHARE HII POST HASA NA WATU WALIOOKOKA WENGI UNAOWAFAHAMU ILI TULIAMSHE KANISA...

YOUTUBE: Pastor Dickson Kabigumila
(Video zaidi ya 2600)
Link ya Youtube hiyo ni hii chini:
https://youtube.com/?si=w1qBdbrxI9PZBl-s

MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU 21 NUSU MWAKA YA PILI 2026.GOOD NEWS CENTRE MOROGORO +255 762 186 639SIKU YA KUMI NA SA...
15/07/2026

MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU 21 NUSU MWAKA YA PILI 2026.
GOOD NEWS CENTRE
MOROGORO
+255 762 186 639

SIKU YA KUMI NA SABA(17).
15.07.2026

Siku ya kumi na saba tunakwenda kuomba juu ya Kibali cha Mungu na Kuunganishwa na Watu wa Hatima (Destiny Helpers). Leo tarehe 15 Julai 2026, tunaomba Mungu akukutanishe na watu ambao amewaandaa kuwa daraja la wewe kufika kwenye mafanikio yako(hatima yako). Hakuna mtu anayefanikiwa peke yake, kila mtu anahitaji mtu aliyetumwa na Mungu kwaajili yake.

*MAANDIKO YA KUSIMAMIA*

Esta 2:15, 17 *Imeandikwa* "...Esta alipata kibali machoni pa wote waliomwona... Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote... akampa taji ya kifalme kichwani pake."

Mwanzo 41:14, 39-40 *Imeandikwa* "Ndipo Farao akatuma, akamwita Yusufu... Farao akamwambia Yusufu... wewe utakuwa juu ya nyumba yangu." (Mungu alimtumia Farao kumwinua Yusufu).

Zaburi 102:13 *Imeandikwa* "Utasimama na kuirehemu Sayuni, kwa maana muda wa kuifadhili umewadia, naam, wakati uliowekwa."

*MAOMBI YA LEO*
1. *Mshukuru Mungu kwaajili ya watu walio wahi kusimama nawewe:* Mshukuru Mungu kwa ajili ya watu waliokusaidia huko nyuma. Mtukuze Mungu ambaye ndiye anayeunganisha mioyo ya watu.

2. *Kuomba Wasaidizi wa Hatima (Destiny Helpers):* Omba Mungu awaamshe watu waliopangiwa kukusaidia mwaka huu 2026 (kazini, kibiashara, au kihuduma). Tamka, Ee Mungu, mtume Farao wangu wa kunitoa gerezani anitafute sasa.

3. *Vunja roho ya Kujitegemea:* Omba dhidi ya roho ya kiburi inayokufanya uone kuwa unaweza kufanya kila kitu peke yako. Omba unyenyekevu wa kupokea msaada.

4. *Ondoa Vizuizi Kati Yako na Wasaidizi Wako:* Omba dhidi ya nguvu za giza zinazopandikiza fitina au chuki kati yako na watu wanaopaswa kukunyanyua. Amuru kila pazia lililokuwa linakuficha usionekane na wasaidizi wako liondoke.

5. *Kibali Mahali Unapohitaji Msaada:* Ikiwa una ombi la kazi, safari au mradi unahitaji ufadhili, omba kibali cha pekee machoni pa wale wanaofanya maamuzi.

6. *Kuwa Msaada kwa Wengine:* Mwombe Mungu akutumie wewe pia kuwa baraka kwa wengine, ili mbegu ya kusaidia unayoipanda izae matunda kwako pia.

*OMBA*
"Baba katika jina la Yesu Kristo, leo Siku ya 17 nakuomba unikutanishe na watu wa hatima yangu. Mwaka huu 2026, sitajihangaisha peke yangu; ninaomba kibali chako kinitangulie kwa watu wenye uwezo wa kunisaidia. Kila kizuizi kilichokuwa kinanitenganisha na wasaidizi wangu kiondoke kwa moto. Asante Bwana kwa sababu unainua watu wa kunishika mkono na kunivusha. Amen."

Zingatia kibali kinaambatana na tabia njema.

MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU 21, NUSU MWAKA YA PILI 2026.GOOD NEWS CENTRE MOROGORO+255 762 186 639SIKU YA KUMI NA SI...
14/07/2026

MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA SIKU 21, NUSU MWAKA YA PILI 2026.
GOOD NEWS CENTRE
MOROGORO
+255 762 186 639

SIKU YA KUMI NA SITA(16)
14.07.2026

Mungu ameendelea kuwa mwaminifu karibu katika maombi ya siku ya 16, leo tunakwenda
Kuharibu Roho ya Upinzani na Kukataliwa kwa Maombi. Leo tarehe 14 Julai 2026, tunashughulika na nguvu za giza zinazojaribu kuzuia majibu ya maombi yako yasikufikie, k**a vile "Mfalme wa Uajemi" alivyomzuia malaika aliyekuwa anamletea Danieli majibu.

*MAANDIKO YA KUSIMAMIA*

Danieli 10:12-13 *Imeandikwa* "...tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu... maneno yako yalisikiwa... Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja..."

Luka 18:7 *Imeandikwa* "Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku...?"

Zaburi 141:2 *Imeandikwa* "Sala yangu na ipae mbele zako k**a uvumba; Kuinuliwa mikono yangu k**a dhabihu ya jioni."

*MAOMBI YA LEO*
1. *Mshukuru Mungu kwa kukusikia:* Mshukuru Mungu kwa uaminifu wake. Mshukuru kwa sababu tangu Siku ya 1 ulipoanza kuomba, amesikia sauti yako.

2. *Kupigana na mfalme wa Uajemi:* Omba dhidi ya kila nguvu ya anga inayozuia majibu ya maombi yako ya siku hizi 16 zilizopita yasimfikie Mungu. Amuru kizuizi hicho kiondoke katika jina la Yesu.

3. *Kufungua Mbingu:* Mwombe Mungu afungue mbingu juu ya maisha yako. Tangaza kuwa mbingu zako hazitakuwa "shaba" (ngumu), bali zitakuwa wazi kupokea baraka zako za mwaka 2026.

4. *Kuvunja Roho ya Kuchoka:* Kataa roho ya ulegevu na kuchoka inayomjia mtu akiwa katikati ya safari ya maombi, Omba nguvu mpya ya kuendelea.

5. *Kuharibu roho ya mashaka:* Omba dhidi ya sauti za adui zinazokwambia "huwezi kujibiwa" au "Mungu hakusikii." Ng'oa shina la mashaka ndani ya moyo wako.

6. *Kuomba Malaika wa Majibu:* Mwombe Mungu atume malaika wake wa vita (k**a Mikaeli) kuja kushindana na vizuizi katika ulimwengu wa roho ili majibu yako yaonekane dhahiri sasa.

*OMBA*
"Baba katika jina la Yesu Kristo, leo Siku ya 16 nasimama kwa mamlaka, ninaamuru kila kizuizi cha angani kilichoshikilia majibu yangu kianguke sasa. K**a ulivyomsaidia Danieli, nisaidie namimi mwaka huu 2026, ninatangaza mbingu zangu ziko wazi, na maombi yangu yamefika mbele zako k**a dhabihu yenye harufu nzuri. Asante kwa sababu ushindi ni wangu leo. Amen."

Leo, jifunze kuomba kwa kumaanisha, usiache kuomba hadi uhisi amani ndani yako kuwa kizuizi kimeondoka.

Address

1703
Morogoro

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Neema ya Kristo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Neema ya Kristo:

Shortcuts

Share