Shiloh United Worldwide Ministries / Prophet Dominic T Mwinyuka

Shiloh United Worldwide Ministries / Prophet Dominic T Mwinyuka Shiloh United Worldwide Ministries deals with SPIRITUAL MATTERS, DELIVERANCE and COUNCELING..

Kila mtu ana ramani yake anatamani kufika pale anapopenda.Hata k**a ramani yako itachelewa endelea kukaa kwenye hiyo ram...
07/09/2026

Kila mtu ana ramani yake anatamani kufika pale anapopenda.
Hata k**a ramani yako itachelewa endelea kukaa kwenye hiyo ramani, Daudi hakumuua tu Goliath bali alianza kuua simba na dubu wakati watu hawamuoni, Yusufu alikuwa mwaminifu akiwa mwenyewe ndio maana Mungu alimuinua, watu wengi wanapenda kuinuliwa mbele za watu lakini sio waaminifu wakiwa wenyewe.Mpe Mungu ramani yako na ya uzao wako (Habakuki 2:1-3)

UKOMBOZI WA KIZAZI CHANGU(BY PROPHET DOMINIC MWINYUKA)Mungu alipomuumba Adamu ndani yake aliweka mbegu ya mtu mwingine a...
06/09/2026

UKOMBOZI WA KIZAZI CHANGU(BY PROPHET DOMINIC MWINYUKA)

Mungu alipomuumba Adamu ndani yake aliweka mbegu ya mtu mwingine aliyeitwa Hawa kwa sababu hakutaka kuumba tena ili yule mtu mmoja aendeleze kuzaa. Kila kitu unachokifanya kina mbegu ya kitu kingine ndani yake,Vita vya kila kiumbe ni UZAO, usichoke kuombea kizazi chako.(Mwanzo 1:26, 28-29,5:1)

Vita vipo kwa uzao wa Adam
1.Baraka zangu ni za uzao, kila baraka za mtu ni za uzao, Mungu anapokupa nyumba lazima uwe na akili ya kugeuza ile nyumba iwe neema kwa uzao wako.(Mwanzo 12:6-7, 13:15)
Mungu wako pia anaweza akarithishwa kwa vizazi. (Mwanzo 17:7)

2.Vita vyangu ni vya uzao, anaweza akakosea mtu mmoja lakini Mungu akaachilia magonjwa ya kudumu.(Kumbukumbu 28:59)
Kwanini tunachukua laana na mapigo ya vizazi vyetu?
Dhambi za mtu hazirithiwi bali uovu ndio unaorithiwa, unaweza ukarithi uovu wa mababu kupitia jina la ukoo linalobeba tabia na mungu wa ule ukoo.(Maombolezo 5:7)

Kurudisha neno lililofukuza mema ya vizazi.
1.Mtu anaweza asikulaani wewe ila akalaani vitu au watu wanaokuzunguka, (Kumbukumbu 28:29)
2.Mtu anaweza kukatazwa asizikwe (2 Wafalme 9:10)
3.Mtu anaweza asilaaniwe ila yakalaaniwa mema yanayomjia (Isaya 47:15)
4.Ardhi inaweza ikalaaniwa ila wewe usiwe na hiyo laana, chochote utakachokifanya kwenye hiyo ardhi kinakataa. (Mwanzo 4:11, Yeremia 22:28-30)

SHALOM SHALOM Shiloh United Worldwide Ministries inakukaribisha kwenye ibada kubwa ya jumapili ya kwanza ya mwezi wa tis...
05/09/2026

SHALOM SHALOM
Shiloh United Worldwide Ministries inakukaribisha kwenye ibada kubwa ya jumapili ya kwanza ya mwezi wa tisa tarehe 6-9-2026 yenye kichwa kinachosema RAMANI YANGU YA UZAO

Vita vya kila kiumbe ni uzao, kila kitu unachokifanya kina mbegu ya kitu kingine ndani yake, kila baraka anazopewa mtu na Mungu ni za uzao hivyo ni lazima uzao uombewe.
Mbegu ili iwe bora lazima iendelee kuzaa na watu hutafuta mbegu njema na sio mbaya, mtu anaweza kurithi uovu au neema ya mtu ambaye hayupo tena kwenye mwili. Ile ramani ya uzao unayoitaka ni lazima uiombee, Mtumishi wa Mungu Prophet Dominic Mwinyuka amejiandaa vizuri kukuhudumia na kukuelekeza namna ya kuombea uzao wako.

Njoo na familia, ndugu, jamaa, marafiki bila kumsahau mwenye uhitaji, ipo neema mpya kwa ajili yako.

Zaburi 125:1Wamtumainio BWANA ni k**a mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.
03/09/2026

Zaburi 125:1
Wamtumainio BWANA ni k**a mlima Sayuni,
Ambao hautatikisika, wakaa milele.

***NENO LA MWEZI SEPTEMBER***MWEZI WA RAMANI NINAYOITAKA(Habakuki 2:1-2)Kile kitu unachokitaka mwezi wa 9 kiweke kwenye ...
31/08/2026

***NENO LA MWEZI SEPTEMBER***
MWEZI WA RAMANI NINAYOITAKA(Habakuki 2:1-2)

Kile kitu unachokitaka mwezi wa 9 kiweke kwenye ramani, chochote unachokitaka kiongelee, ile ndoa, kazi, biashara, mume,mke unayemtaka muongelee, ndani ya mwezi wa uzao ongelea kile unachokitaka.
K**a aonavyo mtu nje ndivyo ndani mwake alivyo, jitabirie mwezi huu wa tisa ni mwezi wa ramani yako na uifanyie kazi kwa jina la Yesu.

Chochote unachokitaka anza kufanyia kazi, ile ramani unayoitaka Mungu akupe mwezi huu, ile ramani ya maisha yako omba upokee mwezi huu, ile njozi ifanye iwe wazi ili kila mtu apate kuisoma, Mungu akupe njia na akuinulie watu wa kuikamilisha hiyo ramani kwa jina la Yesu.

KARIBU KWENYE MWEZI WA RAMANI NINAYOITAKA.

2 Samweli 6:10-11[10]Basi Daudi hakutaka kulileta sanduku la BWANA kwake mjini mwa Daudi; ila Daudi akalihamisha nyumban...
31/08/2026

2 Samweli 6:10-11
[10]Basi Daudi hakutaka kulileta sanduku la BWANA kwake mjini mwa Daudi; ila Daudi akalihamisha nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti.
[11]Sanduku la BWANA akalitia katika nyumba ya Obed-edomu, Mgiti, muda wa miezi mitatu; naye BWANA akambarikia Obed-edomu, na nyumba yake yote.

LEADING FROM BEHIND PART 2"KUONGOZA KUTOKEA NYUMA SEHEMU YA PILI" (BY PROPHET DOMINIC MWINYUKA)Chochote unachokipata kab...
30/08/2026

LEADING FROM BEHIND PART 2"KUONGOZA KUTOKEA NYUMA SEHEMU YA PILI" (BY PROPHET DOMINIC MWINYUKA)

Chochote unachokipata kabla hujamtukuza mwanadamu mtukuze kwanza Mungu, unapoona mwingine amekutangulia kubarikiwa wewe pia unaweza ukafanikiwa. Wakati wote kuna nafasi juu ya kufanikiwa.(Mwanzo 4:1-5)
Biblia inasema Kaini alipoona sadaka ya ndugu yake imekubaliwa aliwaza je yake itakubaliwa? Kaini kabla ya kumuua ndugu yake alijiua yeye kwanza ndani.

Hata k**a upo chini ya jua ipo nafasi yako tena usijiue, je ulishawahi kujiua kwa kuona mafanikio ya mtu mwingine? Mungu anaweza kukupa maisha mazuri ya mbele wakati wanadamu wamekukatia tamaa, ukiona Mungu anakutoa kwenye uzuri wa macho upo uzuri anakupa uliojificha.
Kuna yule akuonaye zaidi ya wanadamu, hatazami k**a mwanadamu atazamavyo, Eli-Elion akuone tena. Kuongoza kutoka nyuma lazima uwe na moyo wa unyenyekevu ndani ya moyo wa unyenyekevu kuna kujazilizwa na kupewa package yako. Popote Mungu anapomuweka mtu wake hajakosea. Huwezi kutawala k**a bado mtawala yupo kwenye kiti chake, lazima ujifunze kutawala akiwa bado anatawala.(Mwanzo 16:5-11)

Pale mahali unapotaka kupaingia unahitaji UVUMILIVU TU na kujifunza sauti ya Mungu, yule ambaye alinyanyasika Mungu alienda kuuzidisha uzao wake. Vita unavyovipitia leo ni ukubwa wa utukufu wa kesho yako, kuna vitu vingine vigumu usiwaambie watu baki navyo k**a kiongozi na Mungu atakupa mwongozo wa kesho.

NAMNA YA KUONGOZA KUTOKEA NYUMA
1.Jiondoe kutoka kwenye historia ya nyuma/usijilinganishe maisha yako na ya sasa, futa historia ya nyuma. Uumbaji wetu si tumboni tu hata k**a umekua bado uumbaji wako unaendelea.
(2 Wakorinto 5:16-17, Zab 139:14-15)

2.Mwamini Mungu kwa yale usiyoyaona hata kwa macho ya nyama, Abraham alibarikiwa kwa kuona na yeye akaamini ndani ya moyo wake, wewe anza kuamini kwa kuona na Mungu atakuletea.
Hata k**a unachokigusa kinakufa unaweza kuongoza tena, ila unatakiwa uwe mwaminifu kwenye kila kitu unachofanya.

SOMO LA MSINGI-AHADI ZA MUNGU HAZIPOKELEWI KWA NJIA YA JUHUDI ZA MWILI WA NYAMA NA DAMU. (BY BISHOP COSTANTINE MKUDE)Wat...
30/08/2026

SOMO LA MSINGI-AHADI ZA MUNGU HAZIPOKELEWI KWA NJIA YA JUHUDI ZA MWILI WA NYAMA NA DAMU. (BY BISHOP COSTANTINE MKUDE)

Watu wengi wanadhani kupambana au kukazana kwa nguvu zao kunaweza kuwafikisha kwenye ahadi za Mungu la ahasha ila Mungu anampa yule ambaye hakutarajia kuzipokea. Biblia inasema Ibrahimu alikuwa anafikiria namna ya kuzaa kimwanadamu lakini uzao wake ulitegemea neno litokalo kwa Mungu.
Mungu aliwaona watoto wa Ibrahimu kupitia Isaka, lazima ufahamu Mungu ni wa miujiza, vile ambavyo havijaingia kwenye mikono yako ndivyo alivyowawekea wampendao. (Mwanzo 15:1-15)

Mtu wa Mungu anapoenda mbele za Mungu anategemea Mungu ndiye amwongoze na sio yeye ajiongoze mwenyewe, Mungu anaujua/kuuona mwisho wako, anaujua uzao wako na majukumu yake.
Ndoto ya kuwa mkuu alipewa Yusufu na utekelezwaji wa ndoto hiyo ni Yusufu kuchukiwa na ndugu zake. Njia zote za kukupeleka kwenye kuinulia hakuna iliyo na unafuu, Biblia imeonyesha njia zote za Yusufu kuinuliwa hazikuwa za kibinadamu na mapito aliyopitia Yusufu hayakumuua kwani mbeba maono hafi. (Mwanzo 37:1-28)

Unatakiwa uishi maisha ya kumtegemea Mungu ili akusaidie, hakuna mtu aliyeitwa na Mungu akaishia Jangwani. Unaweza ukawa na watu kanisani lakini hawamjui Mungu wanakushawishi na wewe uache tumaini lako, yeyote ambaye anabeza wokovu wako tengana naye. Ukiwekeza imani yako kwa Bwana utaona mkono wake ukifanya kazi kwenye maisha yako.
(1 Wakorinto 15:33)
Mungu anaweza kukuzuilia jambo fulani lakini lipo jingine jema amekuandalia kwa sababu wewe unaweza ukaona lakini usitazame. Mungu anaweza kukuzuilia kile unachokiona kinafaa sana kwa sababu yeye anaona mwisho wake rohoni.

WEKEZA IMANI YAKO KWA MUNGU ILI UFANIKIWE.

Shalom Shalom Shiloh United Worldwide Ministries inakukaribisha kwenye ibada kubwa ya ya junapili ya mwisho ya mwezi wa ...
29/08/2026

Shalom Shalom
Shiloh United Worldwide Ministries inakukaribisha kwenye ibada kubwa ya ya junapili ya mwisho ya mwezi wa nane, ya tarehe 30-8-2026 ikiwa ni sehemu ya pili ya kichwa kinachosema "KUONGOZA KUTOKEA NYUMA"

Mungu hawezi kumwinua mtu/au kumtambulisha bila kuleta neno la utambulisho, watu wengi wamejiua kwa sababu ya CV za watu jinsi wanavyowaona, lakini yule asiyefaa kwa wanadamu anafaa kwa Mungu.
Ibada hii itakupa neema mpya na kuinuka tena mahali ulipokata tamaa kupitia mtumishi wa Mungu Prophet Dominic Mwinyuka.

Njoo na familia, ndugu, jamaa, marafiki tumshukuru Mungu kwa pamoja na tuombe ulinzi kwa mwezi wa tisa.
WOTE MNAKARIBISHWA.

MWANAMKE HILI KONGAMANO SI LA KUKOSAWOTE MNAKARIBISHWA.
27/08/2026

MWANAMKE HILI KONGAMANO SI LA KUKOSA
WOTE MNAKARIBISHWA.

Address

MKUNDI-BANANA
Morogoro
70

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Shiloh United Worldwide Ministries / Prophet Dominic T Mwinyuka posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Shiloh United Worldwide Ministries / Prophet Dominic T Mwinyuka:

Shortcuts

Share