Raudhwatul Muslimina Foundation - Rmf

Raudhwatul Muslimina Foundation - Rmf TAASISI YA HUDUMA ZA JAMII NA DINI

Tunawakaribisha wote katika KONGAMANO la sherehe za idilfitri katika viwanja vya MLILINGWA TARAFA YA NGERENGERE Morogoro
08/05/2021

Tunawakaribisha wote katika KONGAMANO la sherehe za idilfitri katika viwanja vya MLILINGWA TARAFA YA NGERENGERE Morogoro

baadhi ya matukio ya liyo jili kwenye kongamano lilofanyika katika viwanja vya tununguo tarafa ya ngerengere mkoani moro...
02/10/2019

baadhi ya matukio ya liyo jili kwenye kongamano lilofanyika katika viwanja vya tununguo tarafa ya ngerengere mkoani morogoro chini ya udhamini wa taasisi ya raudhwatu muslimina foundation RMF mwishoni mwa wiki iliyopita.
picha na habari zaid zita chapishwa kupitia ukura wetu huu usikose ku like na ku follow raudhwatul muslimina foundation RMF kwa taarifa muhimu za maendeleo ya uislamu na jamii kwa jumla

IMAMU AASEMA ANAIONA RMF MPYA YENYE MAFANIKIO INAKUJAImamu mkuu wa msikiti mkuu wa ijumaa ngerengere shekhe Seleman Made...
12/08/2019

IMAMU AASEMA ANAIONA RMF MPYA YENYE MAFANIKIO INAKUJA
Imamu mkuu wa msikiti mkuu wa ijumaa ngerengere shekhe Seleman Madege pichani amesema hana shaka juu ya ustawi wa taasisi ya RAUDHWATUL MUSLIMINA FOUNDATION RMF kwakuwa ina viongozi imara na waadirifu wenyenia yadhati yakufanya jambo kwaajili Ya ALLAH na sio kwa maslahi binafsi

Tangu ianzishwe imekuwa ikishughulikia mambo yake na kujisimamia na kujiendesha yenyewe lacha ya changamoto mbalimbali inazo zipitia hasa kubwa likiwa ni lauchumi, unajua kwenye hali mbaya ya uchumi ndio kwenye kipimo rahisi maana kuna wengine mda huo hawawezi kamwe kuvumilia na kuvumiliana watategeana majukumu mpaka wengine wajitoe kwenye kundi lakin licha ya uchanga wa taasisi na viongozi wake katika hili wamejitahidi sana
Wajibu wetu sasa nikujitoa kwa hali na mali tuichangie taasisi yetu Alisema shekhe madege wakati akitoa neno la ufunguzi wa sherehe za eidl udhhiya zilizofanyika katika uwanja mdogo kijiji cha ngerengere. Ambapo pamoja na mambo mengine kuliendeshwa harambee ya kuichangia taasisi kwa kutumia mitandao ya simu za mkononi kwenda kwenye akaunti ya RAUDHWATUL MUSLIMINA FOUNDATION RMF ambayo nambayake ni 3390482466 nae katibu wa RMF shekhe Shaaban Mssati alisema watu wanaweza kuichangia hata k**a sio leo nahivyo chamsingi ni kuwa nania yakufanya hivyo nawitumie namba hiyo popote walipo aidha mssati alisema kwenye mkusanyiko huo kiasi cha shilingi 89500 kimechangwa na wanaraji kitaongezeka mpaka itapo fikia mwisho wasiku yaleo kwani anaimani waliokosa fedha kwenye akaunti zao muda huu watachukuwa namba hizo nakuchangia baadae
RAUDHWATUL MUSLIMINA FOUNDATION RMF inakusudia kuanzisha huduma zakijamii na kidini kwa misingi ya dini na kwa maendeleo ya jamii yetu

Mkurugenzi wa taasisi ya RAUDHWATUL MUSLIMINA FOUNDATION RMF Shekhe Juma Mohammed Odda ametoa wito kwa waislamu wote pop...
07/08/2019

Mkurugenzi wa taasisi ya RAUDHWATUL MUSLIMINA FOUNDATION RMF
Shekhe Juma Mohammed Odda ametoa wito kwa waislamu wote popote walipo kuichangia taasisi hiyo ili kuiwezesha kufikia marengo yake ya kuanzisha na kuboresha huduma za jamii zinazo Simamiwa na kumirikiwa na RMF, Shekh Odda aliwaambia waumini katika msikiti mkuu wa ijumaa wa ngerengere kuwa ijumaa itakuwa ni siku maalum ambayo waislamu msikitini hapo watafanya harambee ya kuichangia taasisi hiyo kwakutuma fedha kwenye account ya Rmf ambayo imefunguliwa hivi karibuni katika benki ya Kcb tawi la morogoro

Kwanza tunashukuru kwa kupata akaunti hii ya Rmf lakini naomba niwambie kuwa tunategemea michango kutoka kwenu hivyo ijumaa hapa hapa msikitini baada ya swala na kumalizika taratibu za kiuongozi ambazo huwa zinafanyika hapa kila ijumaa kitachofatia ni muda wajapo dk 25 ambazo katibu wa RMF atatuongoza kuichangia taasisi yetu kwa njia ya mitandao hivyo nawaomba sana msiniangushe wekeni pesa kwenye simu zenu iwe voda, tigo, airtel nk tutafanya kwa pamoja nawale walio mbali tafadharini tutatuma namba yetu mtumtumie kwa kadri allah alivyo wajaalia. Alisema Shekh Odda
nae Imamu mkuu wa msikiti huo shekh Suleimani madege (shekh Mabofi) aliwatoashaka waumini kuwa atawapanga viongozi wake ili kumaliza mapema majukumu ya kimsikiti ili kuwapa nafasi waumini kutekeleza ombi la RMF kwa mapema iliwaweze kuwahi kwenye majukumu yao bila ya kutumia muda mrefu sana msikitini hapo

07/02/2018

umoja wa makatibu wa miskiti ngerengere pamoja na taasisi ya raudhwatul muslimina foundation (RMF) tuna kusudia kuendesha semina elekezi kwa vijana na walimu wadini wanao fundisha somo la maalifa ya uislamu (vipindi vya dini) katika shule za msingi na secondary ngerengere.
semina hii yasiku mbili inatarajiwa kufanyika jumamosi na jumapili sawa na tarehe 10 na 11 wiki hii.
vijana wote walio tayari kushiriki semina hii ajisajili kwa katibu wa msikiti ulio karibu nae. mwisho wa kujisajili ni ijumaa saa 10:00 asubuhi. kaulimbiu ni
UTAYARI NA UTHUBUTU NDIO MAFANIKIO YA ZAMA HIZI ZENYE CHANGAMOTO.
wabillah taufiiq

04/11/2017

MKIFANYA HAYA TALAKA INAWANYEMELEA.

Tafiti mpya mbalimbali katika masuala ya ndoa na familia zimebaini kuwepo kwa sababu mbalimbali zinazopelekea wanandoa kuachana na kuvunja ndoa zao.

Account yako ya Furaha ya Ndoa inakuletea mambo 4 ambayo mara nyingi husababisha talaka kutokea katika ndoa nyingi:

1. KUMSHUSHA MWENZIO:

Ikiwa muda wote unaushusha na kuudharau uwezo wa mwenzio kwa makusudi au bila makusudi na kudhani kuwa wewe ni mwerevu zaidi yake, hilo linaweza kusababisha matatizo yanayoweza kuipeleka ndoa yenu kwenye talaka.

Epuka kumshusha na kumdharau mwenza wako.

Usimporomoshee maneno mazito yenye mtazamo hasi na maudhi.

Jaribu kuheshimu juhudi anazozifanya na ikiwa kuna kasoro fulani mueleze kwa namna nzuri na isiyokuwa na maudhi ndani yake.

2. UKOSOAJI ULIOPITILIZA:

Ukosoaji mbaya kwa mwenza wako unaweza kusababisha uhusiano wenu kuzorota. Jaribu kutumia lugha ya wanandoa inayolenga kuleta maelewano bila kumuudhi kwa ukosoaji wenye kuumiza na kuujeruhi moyo wake.

3. KUTETEA MAKOSA KWA UADUI:

Mara nyingi wanandoa hushusha mzigo wa lawama kwa wenza wao katika kutetea makosa yao.

Jiepushe kutetea makosa kwa njia hasi, kwa maana jambo hilo huwa na taathira hasi kwenye uhusiano wa ndoa yenu.

4. KUPUUZA:

Mara ngapi umempuuza mwenza wako pindi unapotokea mzozo na ukashindwa kuzungumza naye hata baada ya kupoa? Jiepushe na upuuzaji wa mizozo, daima fanya bidii kupata ufumbuzi na usiikimbie.

Matatizo yakilundikana huipeleka ndoa yenu shimoni.

UNGANA NASI :
Uislamu Sahihi ni Qur'an na Sunnah

29/10/2017

MKE MMOJA ALIULIZWA:

Ni kipi kimemfanya mumeo akupende kiasi kwamba asione yeyote mwengine duniani wa kumsifia ila wewe, Ilhali wapo wenye uzuri kukuliko?

Akajibu

Hakika sikuwa mzuri wala sina uzuri wa kumfanya awe hivyo unavyosema.

Ninachofahamu ni kuwa:

Nimuonapo mume wangu anakuja au aniangaliapo usoni hutabasamu na kukunjua sura yangu.

Anapokuwa na jambo humsikiliza kwa umakini na huacha yote nimtekelezee aloniagiza ingawa nilikuwa na ya muhimu mengine.

Anaponipatia kingi au anileteapo zawadi humsifia na kuisifu zawadi hiyo hata ikiwa sio katika ninavyovipenda.

Anapokosa kikubwa akaniletea zawadi ndogo mfano wa p**i hutosheka na humuombea apate mengi na makubwa zaidi.

Humfanya yeye ndiye wa kwanza nyumbani kabla ya watoto na wengine wote.

Simkati neno hata k**a sipendi kulisikia

WAWEZA KUPTA MENGI ZAIDI:

Kwa kujiunga na group la facebook la Uislamu Sahihi ni Qur'an na Sunnah na pia kutembelea account ya Furaha Ya Ndoa ujuzwe kuhusu ndoa mwanandoa mwenzetu inshaallah.

Allah awe nanyi...

28/10/2017

UKUMBUSHO TU ALLAH ATUWAFIKISHE INSHAALLAH
🍎حكم عقد النكاح على امرأة حامل

🍎HUKUMU YA NDOA YA MWANAMKE MJAMZITO (MWENYE MIMBA)🍎.................................................................
KUHUSU KUMUOA MWANAMKE MWENYE MIMBA KUNA UCHANGANUZI KIDOGO WA KISHERIA K**A IFUATAVYO:

ج: الحامل من الزنى أو من غير الزنى، لا يجوز العقد عليها حتى تضع، لقول الله عز وجل:

☑JAWABU:

(1) MWENYE MIMBA INAYOTOKANA NA ZINAA AU HATA SIYO INAYOTOKANA NA ZINAA HAIJUZU KUMUOA MWANAMKE HUYO MPAKA AJIFUNGUE (YAANI AZAE MTOTO)

DALILI YA HILO NI MANENO YAKE ALLAH SUBHANA WATAALA:

 وَأُولاتُ الأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَنْ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ

"NA WALE WANAWAKE WENYE MIMBA BASI MUDA WAO WA EDA NI KULE KUJIFUNGUA MIMBA ZAO",

 ولقول الرسول صلى الله عليه وسلم:
 من كان يؤمن بالله واليوم الآخر فلا يسقي ماءه زرع غيره  ماؤه: منيه، وزرع غيره حمل غيره،

NA KAULI YAKE MTUME SWALA ALLAHU ALAYHI WASALAM:

"YULE MWENYE KUMUAMINI ALLAH NA SIKU YA KIYAMA BASI ASIMWAGE MAJI YAKE (YAANI MANII) KATIKA SHAMBA LA MWENGINE (KWENYE MIMBA ILOTIWA NA MTU MWENGINE)"

فإذا كانت حاملا من مطلق أو ميت، فليس لها أن تتزوج حتى تضع الحمل،

🔎HIVYO BASI IKIWA MIMBA INATOKANA NA MWANAMME ALIYEMWACHA HUYO MWANAMKE, AU INATOKANA NA MWANAMME ALIYEKUFA, BASI HAIJUZU MWANAMKE HUYO MWENYE MIMBA KUOLEWA NA MWANAMME MWENGINE MPAKA AJIFUNGUE MIMBA YAKE,

وإذا كانت حاملا من الزنى، فلا تتزوج لا بالزاني ولا بغيره حتى تضع؛ لأن رحمها مشغول بنطفة لا تنسب للزاني، ولا لغيره تنسب لأمه، فالزاني لا ينسب إليه الطفل،

👉NA K**A IKIWA HUYO MWENYE MIMBA INATOKANA NA ZINAA BASI HAIJUZU KUOLEWA NA HUYO ALIYEMTIA MIMBA KWA ZINAA AU HATA ASIYEKUWA HUYO, MPAKA AJIFUNGUE MIMBA YAKE,

KWA SABABU KIZAZI CHAKE KIMESHUGHULISHWA NA MBENGU ZILIZOINGIA KWA NJIA YA ZINAA, AMBAPO HAZI NASIBISHWI NA HUYO MZINIFU WALA NA ASIYEKUWA HUYO BALI HUNASIBISHWA MTOTO HUYO NA MAMA MWENYEWE,

👊MZINIFU HANASIBISHWI KATU NA MTOTO ALIYEPATIKANA KWA NJIA YA ZINAA,

مثلما قال النبي صلى الله عليه وسلم :
 الولد للفراش وللعاهر الحجر 

K**A ALIVYOSEMA BWANA MTUME SWALA ALLAHU ALAYHI WASALAM

"MTOTO HUNASIBISHWA NA KITANDA NA MZINIFU HAKI YAKE NI MAWE, (YAANI KWA NDOA TU NDIO MTOTO HUNASIBISHWA KWA BABA, NJE YA NDOA HAKUNA NASABA KISHERIA KWA BABA)"

YAANI HATA UKATIA MIMBA KWA MKE WA MTU BASI MWENYE KITANDA YAANI MWENYE MKE NDIO ATANASIBISHWA NA HUYO MTOTO BALI WEWE HAKI YAKO NI MAWE,

فالولد لأمه إذا كانت ليست للفراش، فإن كانت فراشا، فالولد لزوجها، والزاني له الحد الشرعي،

HIVYO BASI MTOTO HUNASIBISHWA KWA MAMA IKIWA SIO KWA NJIA YA NDOA,

AMA IKIWA NI KWA NJIA YA NDOA BASI MTOTO HUNASIBISHWA KWA BABA MWENYE MKE NA MZINIFU HUADHIBIWA KWA ADHABU YA KISHERIA (MAWE IKIWA ALISHAPITIA NDOA AU VIBOKO IKIWA HAJAPITIA NDOA)..............................................

فإذا حملت وهي ليست ذات زوج،

(2) AKIWA MWANAMKE HUYO AMEPATA MIMBA NJE YA NDOA,

فإنها لا يجوز تزوجها مطلقا، حتى تضع الحمل،

👉BASI HAKIKA HAIJUZU KUOLEWA MOJA KWA MOJA MWANAMKE HUYO MPAKA AJIFUNGUE MIMBA YAKE,

فإذا وضعت الحمل، جاز لها التزوج، بعد التوبة،

👍AKISHAJIFUNGUA MIMBA YAKE, BASI INAJUZU KWA MWANAMKE HUYO KUOLEWA BAADA YA KUTUBIA,

والرجوع إلى الله والإنابة ويجوز للمسلم أن يتزوجها بعد التوبة.

NA KUREJEA KWA ALLAH NA KUELEKEA KWAKE NA INAJUZU KWA MUISLAM KUMUOA BAADA YA TOBA AKIWA ASHAJIFUNGUA,

فتوى نور على الدربي

(الجزء رقم : 21، الصفحة رقم: 46)

[REJEA FATAWA NURU ALA DDARBI 📚📚]

JUZUU NAMBA 21, UKURASA 46,📂📂
--------------------------------------------------

27/10/2017

Kisa cha Nabii Ayyubu:

Ni somo kwa Wagonjwa, Wafiwa na waliofilisika!

Ibn Is-haaq amesema kuwa Ayyubu alikuwa ni mtu wa Urumi. Jina lake kamili lilikuwa ni Ayyub bin Musa bin Razih bin Esau bin Ishaaq bin Ibrahim. Mtu mwingine naye akasema, Ayyubu alikuwa akiitwa Ayyub bin Musa bin Rimil bin Esau bin Ishaaq.

Kumekuwa na maelezo mengine kuhusiana na nasaba yake. Ibn Asakir kasimulia kuwa mamaake Ayubu alikuwa ni binti wa Nabii Lut alayhis salam. Ikasemekana pia kuwa babaake Ayyub alikuwa ni mmoja wa wale waliomwamini Ibrahim pale alipotoswa kwenye moto.

Rai ya kwanza ndiyo inayokubalika zaidi kwa sababu Ayyubu alikuwa ni kizazi cha Ibrahim k**a Mwenyezi Mungu alivyosema katika Qur’an, Sura ya 6, aya ya 83-84.
Mwenyezi Mungu, Malaika wamsifu Ayyubu
Mwenyezi Mungu alimsifu mja Wake, Ayyub, “Bila shaka Tulimkuta ni mwenye subira, mja mwema; kwa hakika alikuwa ni mnyenyekevu sana.” (38:44)

Ayyubu alikuwa mwingi wa kuomba toba, mwingi wa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, mwingi wa subira na mwenye istiqama. Hii ndiyo sababu ya kupata kwake nusra na ndiyo siri ya kusifiwa hivyo na Mwenyezi Mungu.

Malaika walikuwa katika kundi lao wakiwazungumzia viumbe wengine. Katika maongezi yao, waliwazungumzia waja wanyenyekevu jinsi walivyopata radhi za Mola wao, na wakawazungumzia wale waliotakabari jinsi walivyoghadhibikiwa na Mola wao.

Mmoja wa Malaika hao akasema: “kiumbe bora kabisa duniani hivi leo ni Ayyubu, mtu mwenye tabia njema ambaye kaonesha subira kubwa, na muda wote anamkumbuka Mola wake Mwingi wa Ukarimu. Ni mfano bora wa wenye kumwabudu Mwenyezi Mungu.

Malipo yake, Mola wake kamjaalia uhai mrefu, watoto wengi, na kamneemesha fungu la wenye kuhitaji na masikini. Anawalisha na kuwavisha masikini, na anawanunua watumwa na kuwaachia huru.

Kwa ukarimu na upole wake, anafanya wale wanaopokea zaka kwake wajione k**a vile wao ndio wanaomfanyia fadhila yeye.”
Ibilisi achukizwa na Maneno ya Malaika, Amwandama Ayyubu!
Ibilisi aliposikia yote hayo yaliyosemwa na Malaika katika kumsifu Ayyubu, akachukizwa. Akajipanga kumyumbisha Ayyubu ili aharibikiwe na kukufuru, basi akamwendea haraka.

Alijaribu kumvurugia Sala zake kwa kumnong’oneza mambo mazuri ya kimaisha lakini Ayyubu alikuwa ni muumini kwelikweli na hakuruhusu mawazo mabaya yambabaishe na kumvurugia Sala zake.

Jambo hilo likamkera zaidi Ibilisi. Sasa akaanza kujenga chuki mbaya sana dhidi ya Ayyubu. Ibilisi akalalamika kwa Mwenyezi Mungu kuhusu Ayyubu.

Akasema kuwa japo muda wote Ayyub alikuwa anamtukuza Mwenyezi Mungu lakini alikuwa akifanya hivyo bila ikhilasi ila kumpoza tu Mungu ili utajiri wake usiondoshwe. Akasema, ni riya tu aliyofanya Ayyubu, na hiyo ni kutokana na tamaa ya mali.. “Ukimuondoshea utajiri, utaona kuwa ulimi wake hautalitaja tena Jina lako na sala zake zitaishia hapo.”

Mwenyezi Mungu akamwambia Ibilisi kuwa Ayyubu alikuwa ni mcha Mungu kwelikweli. Hakumwabudu Yeye eti kwa sababu ya neema; ibada yake ilitoka moyoni kabisa na haikuhusiana na vitu vya kidunia.

Lakini, ili kumthibitshia Ibilisi kiwango cha ikhilasi na subira ya Ayyubu, Mwenyezi Mungu akamruhusu Ibilisi na wasaidizi wake wafanye chochote walichotaka dhidi ya utajiri wa Ayyubu.

Ibilisi akafurahi sana. Akawakusanya wasaidizi wake, na wakafanya ya kufanya kuhujumu mifugo ya Ayyubu, kuwahujumu watumishi wake na kuhujumu mashamba yake mpaka akabaki mee! Mtupu kabisa.

Baada ya hujuma hiyo, sasa Ibilisi akajitokeza kwa Ayyub akiwa k**a mzee fulani hivi wa kibinadamu mwenye busara zake, na kumwambia:

“Bwana wewe Utajiri wote umekutoweka, eti baadhi ya watu wanasema kuwa ulizidi sana kutoa-toa sadaka na unapoteza bure muda wako kwa kuswali-swali muda wote. Wengine wanasema eti Mungu kakukomoa ili awafurahishe maadui zako. K**a Mungu ndiye Mwenye uweza wa kukinga hasara, si basi angekukingia utajiri wako.”

Akiwa mkweli wa imani yake, Ayyub akajibu: “Kile ambacho Mwenyezi Mungu kakichukua kwangu ni mali Yake Yeye Mwenyewe. Mimi nilikuwa mtunza amana wa muda tu. Yeye humneemesha Amtakaye na Humnyima Amtakaye.” Baada ya kusema maneno haya, Ayyubu, kwa mara nyingine, akapomoka kumsujudia Mola wake.

Ibilisi alipoona hivyo, akachanganyikiwa, na hivyo, akamwambia tena Mwenyezi Mungu: “Nimemvua Ayubu mali zote, lakini bado anaendelea kukushukuru. Lakini huyu anaficha tu huzuni yake, kwani kaweka akiba ya watoto wengi alionao. Mtihani halisi wa mzazi ni kwa watoto wake. Utaona jinsi Ayyubu atakavyokukufuru.”

Mungu akampa Ibilisi idhini lakini akamtahadharisha kuwa hiyo haitashusha imani ya Ayyubu kwa Mola wake wala haitampunguzia subira. Ibilisi akakusanya tena wasaidizi wake na kupanga hujuma zake. Akatikisa muhimili wa nyumba ambayo watoto wa Ayyubu walikuwa wakiishi na kusababisha jengo liporomoke na kuua watoto wote.

Kisha akaenda kwa Ayyubu kwa kujifanya yeye ni mwanadamu mwema aliyekuja kumfariji. Kwa sauti ya kumfariji, akasema, “Mazingira ambayo watoto wako wamefia yanasikitisha kwa kweli! Mungu hata hakulipi Sala zako sawasawa.” Baada ya kusema hivyo, Ibilisi akasubiri kwa hamu na matumaini kuwa sasa Ayyubu alikuwa tayari kumkufuru Mungu.

Lakini, kwa mara nyingine, Ayyub akamfadhaisha kwa kujibu: “Mwenyezi Mungu, wakati mwingine, hutoa, na wakati mwingine, hutwaa. Wakati mwingine, hufurahishwa na wakati mwingine, huchukizwa na matendo yetu. Mimi, iwe faida, iwe hasara kwangu, nitabaki kushik**ana na imani yangu na nitaendelea kumshukuru Mola wangu.” Baada ya kusema hivyo, Ayyubu akapomoka kumsujudia Mola wake. Ibilisi akakerwa mno na jambo hilo.

Ibilisi akamuomba Mungu: “Ewe Mola wangu! Mali ya Ayyubu imekwenda, watoto wamekufa, naye bado ana afya nzuri ya kiwiliwili. Maadam ana afya nzuri, ataendelea kukuabudu kwa matumaini ya kupata tena utajiri na kuzaa watoto zaidi, Nipe idhini juu ya kiwiliwili chake ili nikidhoofishe. Kwa hakika ataacha kukuabudu na hivyo atakuwa muasi.”

Mwenyezi Mungu akataka kumpa somo Ibilisi kwamba Ayyub alikuwa mja mchaMungu basi akamkubalia ombi lake la tatu lakini akamwekea sharti hili: Nakupa idhini juu ya mwili wake lakini sio roho yake, akili yake wala moyo wake, kwani humu ndimo inamokaa Ilimu yangu na dini Yangu.”

Akiwa amepata idhini hii mpya, Ibilisi akaanza mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya kiwiliwili cha Ayyubu, na akakijaza maradhi hadi kikakondeana na kubaki ngozi na mifupa mitupu huku akiugulia maumivu kadha wa kadha.

Lakini katika kipindi chote cha kuugulia, Ayyub alibaki na nguvu ya imani. Kwa subira ya hali ya juu, alihimili masaibu yote bila kulalamika, kusononeka.
Mja huyu mwema wa Mwenyezi Mungu hakukata tamaa wala hakuwaelekea wengine kuomba msaada, bali yeye alibaki kutumainia rehema za Mwenyezi Mungu. Ikafika mahala hata ndugu na jamaa wa karibu nao wakamtupa kabisa.

Ni mkewe pekee aliyebaki naye kwa huruma na mapenzi. Katika kipindi cha matatizo, mke huyu akaonesha huruma kwa mumewe na kumuuguza. Ndiye mwenza na mfariji pekee aliyebaki naye katika miaka mingi ya kuugua.

Ibn Asakir kasimulia: “Ayyubu alikuwa na mali za aina zote, watumishi, kondoo, mashamba makubwa ya Haran na watoto wengi. Neema zote hizo zikaondoshwa kwake, na akakumbwa na maradhi ya mwili.

Hakukuwa na hata kiungo kimoja kilichokuwa na afya isipokuwa moyo na ulimi, huku akitumia vyote viwili kumtukuza Mwenyezi Mungu, usiku na mchana. Maradhi yalimchukua muda mrefu hadi wageni waliokuwa wakimtembelea (kumjulia hali) wakachoka naye.
Rafiki zake wakajitenga naye, na watu wakaacha kumtembelea. Hakuna aliyemfariji isipokuwa mkewe. Akamuhudumia mumewe vizuri, akikumbuka fadhila na huruma ya mumewe kwake siku za nyuma.”

Basi Ibilisi akawa na hali ngumu. Akashauriana na wasaidizi wake, lakini hawakuweza kumshauri. Wakamuuliza: “inakuwaje ujanja wako unashindwa kufanya kazi kwa Ayyubu ilihali ulifanikiwa kumpoteza Adam, baba wa wanadamu, na kumtoa Peponi?”

Ibilisi akaenda kwa mke wa Ayyubu kwa sura ya mwanaume wa kibinadamu. Akajidai kuuliza: “Mumeo yuko wapi?” Mke wa Ayyubu akaonesha kiwiliwili ambacho aghalabu kilikuwa k**a mfu, chakachaka kabisa kitandani na kusema: “Yule pale, anapembea baina ya uhai na kifo.”

Ili kumuumiza kihisia na kumtia uchungu, Ibilisi akamkumbusha mke wa Ayyubu enzi za afya nzuri ya mumewe, enzi zao walipokuwa na mali na watoto. Tahamaki kumbukumbu ya uchungu ya miaka ya matatizo ikamzidia mke wa Ayyubu, na akaanza kububujikwa na machozi.

Akamwambia Ayubu, “(Mume wangu)! Hadi lini utaendelea kuvumilia mateso haya kutoka kwa Mola wako? Je, ndio basi jamani tubakie hivi hivi, moja kwa moja bila mali, watoto wala jamaa? Kwa nini usimuombe Mwenyezi Mungu atuondoshee machungu haya jamani?”

Ayyubu akavuta pumzi, na kwa sauti ya mbali ya mgonjwa aliye taabani, akajibu: “Ni Ibilisi tu huyo ambaye atakuwa amekuchochea wewe na kukufanya usononeke namna hiyo! Hebu niambie (mke wangu), ni kitambo gani mie nilifurahia afya njema na utajiri?

Mkewe akajibu: “miaka 80
Kisha Ayyubu akasema, “Nina muda gani tangu nilipoanza kuugua?
Mkewe akajibu: miaka 7
Ayyubu akamwambia mkewe: “Basi, k**a ndio hivyo (mke wangu), mimi mwenzio naona aibu kumuomba Mola wangu aniondoshee shida, kwani mbona sijataabika muda mrefu kulinganisha na miaka mingi ya afya njema na utajiri! Inaonekana wewe mwenzangu imani yako imedhoofu na huridhiki na Qadari ya Mwenyezi Mungu.

Nikipona mie wewe, naapa n’takuchapa mie, fimbo mia! Tena kuanzia leo sitaki tena kula au kunywa chochote mkononi mwako. Basi niache tu peke yangu, na mwache Mola wangu anifanyie chochote akipendacho.”

Akilia kwa uchungu na kwa moyo mzito wa huzuni na huruma (kwa mumewe), mke wa Ayyubu hakuwa na namna isipokuwa kuondoka na kwenda kutafuta mahali pengine pa kuishi. Huyu ni mtu wa mwisho tena, sasa Ayyubu kabaki peke yake, nani wa kumlisha, nani wa kumywesha, nani wa kumgeuza ubavu kitandani?

Katika hali hiyo ya kukosa kabisa msaada, Ayyubu akamuelekea Mola wake, sio kulalamika bali kuomba rehema Zake.
“Na (mtaje) Ayyubu alipomwita Mola wake (akasema): “Mimi imenipata dhara, Nawe ndiwe Unayerehemu kuliko wote wanaorehemu. Basi Tukamkubalia (wito wake) na Tukamuondolea dhara aliyokuwa nayo. Na Tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao.

Ni rehema inayotoka Kwetu, na, ni ukumbusho kwa wafanyao ibada” (21:83-84)
“Na mkumbuke mja Wetu Ayubu, alipomwita Mola wake, “Kwa yakini Shetani amenifikishia udhia na taabu. (Niondoshee Mola wangu maradhi haya yaliyonifika). (Mwenyezi Mungu akamwambia), “Uharakishe mguu wako (patachimbika chemchem chini yake, maji yake yatakuwa dawa yako. Basi haya maji baridi ya kuoga, na ya kunywa. Na Tukampa watu wake na wengine k**a wao pamoja nao, kwa rehema itokayo Kwetu, na (ipate kuwa) mauidha kwa wenye akili.” (38:41-43)

Ayyubu alifanya hivyo, na papo hapo, afya yake nzuri ikarejea. Wakati huo huo mkewe naye kule alikokuwa huruma ilimja kwa hali aliyomuacha nayo mumewe. Akashindwa kuendelea kukaa mbali na mumewe na akarejea ili kuomba msamaha na kuendelea kumuhudumia.

Alipoingia ndani ya nyumba, akashangaa kuona mabadiliko ya ghafla: Ayubu alikuwa bukheri wa afya k**a zamani! Akamkumbatia na kumshukuru Mwenyezi Mungu.”
Ayyubu alikuwa amekula kiapo cha kumwadhibu mkewe k**a angepata afya, lakini sasa hakutaka tena kumuumiza mkewe. Alijua kuwa k**a asingetimiza kiapo chake, basi angekuwa na hatia ya kuvunja ahadi yake kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa sababu hiyo, Mwenyezi Mungu, kwa Hikima na Rehema Zake zisizo na ukomo, akamsaidia mja Wake huyu mwema na akamnasihi hivi:
“Na kisha shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako (si fimbo), kisha mpige kwacho mkeo, wala usivunje kiapo.” (38:44).
IJUMAA MUBARAK

shekhe wa wailaya ya ngerengere JUMA MOHAMEDI ODDA amewatolea wito waislamu kuhakikisha wanaitumia vema fursa ya serikal...
22/10/2017

shekhe wa wailaya ya ngerengere JUMA MOHAMEDI ODDA amewatolea wito waislamu kuhakikisha wanaitumia vema fursa ya serikali ya kuwapatia elimu ya dini wanafunzi pindi wawapo mashuleni.
pichani ni shekh JUMA M. ODDA alie simama na MWALIMU RAMADHANI NKUSA alie kaa mwenye kitambaa began
hayo aliyasema juma mosi wikihii, katika hutuba yake akiwa mgeni rasmin katika maafari ya sita ya wanafunzi wa kiislamu wa shule ya secondary ya ngerengere day.
pia amewataka waislamu kujipanga hata ikibidi kwakuchangishana ili kuhakikisha walio pata nafasi ya kuendelea na masomo wanaipata fursa hiyo bila kikwanzo cha umaskini wa wazazi wao. nawale watao kosa nafasi basi wajiunge na mafunzo ya taaluma mbali mbali ilikujikwamua kiuchumi nakujenga taifa lenye nguvu kubwa za kiuchumi.
nae mwl mkuu wa shule iyo amesema amesikitishwa sana na muitikio mchache wa wailsamu kwenye maafari hiyo hali inayo wakatisha tamaa wanafunzi nakupelekea kuchukia masomo ya dini mashuleni ambayo amesema serikali katika mwaka 2018 imelitilia mkazo somo la dini.

Darul uluumy english medium nursery school ni shule inayo milikiwa na taasisi ya raudhwatul muslimina foundation RMF.shu...
17/10/2017

Darul uluumy english medium nursery school
ni shule inayo milikiwa na taasisi ya raudhwatul muslimina foundation RMF.
shule ipo kijiji cha mgude kata ya ngerengere takriban KM. moja toka stendi kuu ya mabasi ya ngerengere
shule inapokea watoto wenyeumri wa kuanzia miaka 3. na kuendelea
shule ni yadini na inapokea wasiokuwa waislamu bila kubaguliwa.
shule ina MAZINGIRA MAZURI viwanja vya michezo kwa watoto, ina walimu wenye weredi na wenye uzoefu na ubunifu.
fomu za kujiunga na shule zinapatikana sehemu zifuatazo
1. salmeen boking office ngerengere stend
2. msikiti mkuu wa ijumaa ngerengere
au wasiliana katibu wa taasisi ya raudhwatul muslimina foundation RMF kwa simu namba 0782379547
Au kwa maelezo zaidi wasiliana na mkurugenzi wa taasisi ya raudhwatul muslimina foundation RMF kwa simu namba 0683335335
au tuandikie kwa barua pepe [email protected]
Au tuandikie kwa sanduku la posta 31 ngerengere
Au fika makao makuu ya taasisi ya raudhwatul muslimina foundation RMF

Address

Morogoro

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Raudhwatul Muslimina Foundation - Rmf posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share