15/02/2023
BUSARA ZA WAHENGA
Wahenga husema, Usimpige nyoka mkia kabla haujajua kichwa kiko wapi π€π€π€π€
Siku zote ukiona panya anamcheka paka, ujue yupo karibu na shimoπππππ
Ukiona mtu anadharau wengine na kuwatenda vibaya, jua pengine anajua wapo wa kumteteaπ€π€π€π€π€π€
Wapo watu wanaoringia wengine kwa sababu tu wana maisha mazuri, na kuongea vibaya kwa sababu kuna mtu wa kumpigia kifua,π³π³π³π³π³π³π³π³
Tambua wapo wasioongea lakini wana vingi......πππππ
Kumbuka hata panya anaweza kumcheka paka kisa yuko karibu na shimoπππ na anaweza kukosea shimo akaambulia kujuta na hata kupoteza mkia wakeππππππππββοΈ
Usimdharau mtu kwa kuwa wewe ni kipenzi cha bossπ³π³
Waheshimu wote kwa sababu siku moja tutakufa piaπ€π€
WENU KATIKA KRISTO
RIZIKI KAVISHE
NILIYE MDOGO
π OF WISDOM π