UWEPO WA MUNGU Ministry

UWEPO WA MUNGU Ministry Yesu yupo hapa

Maombi ya kupata mtotoEe mwenyezi Mungu, Mungu mwenye uwezo umba tena mtu ndani ya tumbo hili kwa mfano wako akawe mwema...
05/11/2022

Maombi ya kupata mtoto

Ee mwenyezi Mungu, Mungu mwenye uwezo umba tena mtu ndani ya tumbo hili kwa mfano wako akawe mwema, mwadilifu akikupendeza wewe na wanadamu maana hakuna aliyetasa katika Israel yote
Katika jina la Yesu kristo. Amina

Gusa 👇
https://chat.whatsapp.com/DqnURG9zI5VDlzMz8eGEL0

Kuoa au kuolewa (ndoa) kibiblia Mpango wa ndoa aliuanzisha Mungu mwenyewe kwenye bustani ya Edeni, kwahyo wazo la kuoa a...
02/10/2022

Kuoa au kuolewa (ndoa) kibiblia

Mpango wa ndoa aliuanzisha Mungu mwenyewe kwenye bustani ya Edeni, kwahyo wazo la kuoa au kuolewa sio fikra za mwanadamu bali ni mpango wa Mungu, kwahy k**a ni mpango wa Mungu mwenyewe makusudi ya kuoa au kuolewa kwako ni Mungu

Mwanaume anapotafuta kuoa hapaswi kutafuta mke mzuri, kwa sababu hakuna mtu mbaya, hapaswi kutafuta mke maarufu kwa sababu atakuwa anaoa umaarufu na siku ukipotea huo umaarufu ndoa nayo imepotea, hapaswi kuangalia umbo mfano tako, siku mkiishiwa pesa maana maisha ni kupanda na kushuka kwahyo hilo tako litapotea na ndoa itapotea maana ulioa tako sio mke sasa tako halipo ndoa ya nn

Mwanamke hupaswi kuolewa kisa umri umeenda,hupaswi kuolewa kisa rafiki zako wote wameolewa, hupaswi kuolewa kisa umechoka kukaa kwenu
Ukizingatia hayo👆utajikuta unaolewa na yeyote
Acha kuangalia kazi yake siku akipoteza hiyo kazi ndoa nayo hakuna

Nini cha kufanya, mwambie Mungu kwanza kuwa unataka kuoa au kuolewa yeye ndiye atasoti yupi wako ili kusudi la Mungu la kuanzisha ndoa likamilike sio kusudi lako wewe

Gusa link 👇 upate
https://chat.whatsapp.com/DqnURG9zI5VDlzMz8eGEL0

https://chat.whatsapp.com/DqnURG9zI5VDlzMz8eGEL0*hatari nne zinazoweza kutufanya tuondoke kwa Mungu*Hatari ya 1: kufuata...
16/09/2022

https://chat.whatsapp.com/DqnURG9zI5VDlzMz8eGEL0
*hatari nne zinazoweza kutufanya tuondoke kwa Mungu*

Hatari ya 1: kufuata maarifa ya kichwa badala ya maarifa ya moyo.

Je, kujifunza Biblia kumekuwa tu zoezi la maarifa ya kichwa kwako?ujuzi wa kichwa unamanisha kufikiria juu ya jambo fulani bila kulifanya. Inamanisha kujua lakini kutofanya. Si vibaya kujifunza Biblia,lakini watu wengi husimamia kwenye hatua ya "maarifa ya kichwa" na kamwe hawafikii hatua ya "maarifa ya moyoni"

Hilo ndilo lilikuwa tatizo la Mafarisayo katika karne ya kwanza. Yesu aliwaambia wasomi hawa kwamba walikosea kwasababu hawakuelewa maandiko au uweza wa Mungu (mathayo 22:29). Walikuwa wamekariri sehemu kubwa za Agano la Kale,lakini hawakuzitumia katika maisha yao. *Hilo na lisiwe kweli kwetu kamwe!*

Hatari ya 2: shughuli kuliko kujitolea kweli!

Kumtumikia Mungu unahitaji muda na nguvu. Utapanuliwa zaidi ya mapungufu yako ya kimwili. Hatari inayokuja kutotenga wakati wa kumtafuta Mungu badala yake unakuwa na mambo yako mengi huna muda na Mungu. Ni wajibu wako sasa hivi kujitolea kuwa na muda maalum kila siku wa kumtafuta Bwana

Hatari ya 3: kupoteza upendo wako wa kwanza

Kufanya kazi ya Mungu inapendekeza sana na kufanya vitu vyote vyema lakini bado ukikosa kile ambacho ni muhimu zaidi..hii ilitendeka kwa kanisa la Efeso. Kanisa hili lilikuwa na mwanzo mzuri sana. Lilikuwa na nguvu katika imani na upendo na lilikuwa linakuwa katika tumaini (waefeso1:15-18). Walivumilia nyakati nyingi ngumu. Hata hivyo waliacha upendo wao wa kwanza (1wakorintho13:1-3)
Hata wewe mwanzo ulianza vizuri sana mwanamaombi mzuri mwana sifa mzuri ibada hukosi lain leo huna hata kiu ya maombi hata usipoenda ibadani huoni tatizo. Maneno haya ya Yesu kwako
a) kumbuka: jinsi ilivyokuwa wakati ulinipenda mimi kwa moyo wako wote
b) tubu: ungama dhambi yako na umrudie Mungu
c) rudi: fanya mambo uliofanya mwanzoni. Rudi kwenye mambo ya msingi ya uhusiano wako na Mungu. Mtafute Mungu. Omba kwa dhati.soma Neno. Mzingatie yeye

Somo litaendelea
https://chat.whatsapp.com/DqnURG9zI5VDlzMz8eGEL0

Address

Morogoro
ZIP

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UWEPO WA MUNGU Ministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to UWEPO WA MUNGU Ministry:

Share