28/02/2021
IBADA YA JUMAPILI TAREHE 28/2/2021 – KANISA LA EFATHA MWENGE.
MCHUNGAJI AIMANA DOMINICK.
Zaburi 119:121-126 “Nimefanya hukumu na haki, Usiniache mikononi mwao wanaonionea. Uwe mdhamini wa mtumishi wako, apate mema, Wenye kiburi wasinionee. Macho yangu yamefifia kwa kuutamani wokovu wako, Na ahadi ya haki yako. K**a zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako, Na amri zako unifundishe. Mimi ni mtumishi wako, unifahamishe, Nipate kuzijua shuhuda zako. Wakati umewadia Bwana atende kazi; Kwa kuwa wameitangua sheria yako.”
Ukiamua kuzifuata sheria za Bwana YEYE ataanza kazi ndani yako na yule anayekuonea katika maisha yako kwa sababu ya kuzaliwa kwako atapewa tangazo la kutokukufuatilia tena, nawe ndipo utaona FURAHA na USTAWI katika maisha yako.
UKIRI:
Bwana wa Utukufu kwa gharama yoyote nimeamua kuzitii sheria zako, kwa ajili ya hilo usiniache mikononi mwa wanaonionea; leo naomba uwe mdhamini wangu ili nikale mema uliyoniandalia ili wenye kiburi wasiendelee kunionea.
Bwana ukanitendee leo ili niendelee kutunza maagizo yako, kwa maana wewe umesema katika Zaburi 119: 126 “Wakati umewadia Bwana atenda kazi;………” Eeh Bwana niko tayari kuona kazi unayokwenda kutenda kwangu ili wale waliokuwa wananionea kutokana na kuzaliwa kwangu wasinionee tena, kwa maana nimeamua kuzishika sheria zako.
Katika mwaka huu wa KUSONGA MBELE nifanye NISONGE MBELE katika kila eneo la maisha yangu na sio kuwa wa kushindwa, mgonjwa, wa kurudi nyuma, n.k, na nikapate yale yote ambayo Bwana umeniandalia. Huu ndio ukiri wangu kwako Bwana.