Pastor Ulenje

Pastor Ulenje HII NI ZAIDI YA PAGE
NI MADHABAHU YA KUPOKEA UAMSHO WA MAOMBI NA MIUJIZA.
2025 Mungu anataka sana Kanisa kurejesha Matumaini yao katika Maombi.

Karibu Tujifunze na Tuombe Pamoja.

Newday-NewpowerPRAYER DEVOTION Fri 10 Julai 2026ANA HERI MTU YULE ANAYEAMINI KABLA YA KUONA Pt 2_“(k**a ilivyoandikwa, N...
10/07/2026

Newday-Newpower

PRAYER DEVOTION
Fri 10 Julai 2026

ANA HERI MTU YULE ANAYEAMINI KABLA YA KUONA Pt 2

_“(k**a ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, *ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.”*_
‭‭Rum‬ ‭4‬:‭17‬ ‭SUV‬‬

👉 Mungu tunayemwabudu ni Mungu ayatajaye mambo yasiyokuwapo kana kwamba yamekuwapo; ili Ibrahimu aweze kuwa baba wa mataifa mengi, ilimlazimu kuungana na Mungu.

🌺 Ibrahimu alijifunza kumuamini Mungu ambaye; anatamka vitu ambavyo havipo kana kwamba vipo; anamwambia utakuwa na uzao k**a mchanga wa bahari, anamwambia k**a nyota zilivyo pasipo idadi machoni pako; ndivyo itakavyokuwa uzao wako.

🤔 k**a kweli unataka kutembea na huyu Mungu na kupokea muujiza wako; basi lazima ujifunze kutazama ushindi wako na muujiza wako kana kwamba umekwisha tokea tayari; na ukaanza kumshangilia Bwana kana kwamba unacho ulichoomba.

🔥🥰 Hapo nakwambia wazi utatokea muujiza wako.

MUNGU AKUBARIKI KWA KUSOMA (1 TIMOTHEO 4:13)

Maombi ya Leo;
_Baba uliye mbinguni naomba nisaidie kutazama mambo yasiyokuwapo kana kwamba ninayo._

🎻 Pastor Ulenje
*GOD ANSWERS PRAYERS*

🔥

Newday-NewPowerPRAYER DEVOTION Thus 9 Julai 2026ANA HERI MTU YULE ANAYEAMINI KABLA YA KUONA._“Yesu akamwambia, Wewe, kwa...
09/07/2026

Newday-NewPower

PRAYER DEVOTION
Thus 9 Julai 2026

ANA HERI MTU YULE ANAYEAMINI KABLA YA KUONA.

_“Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.”_
‭‭Yn‬ ‭20‬:‭29‬ ‭SUV‬‬

🙆🏻‍♂️👉 Yohana 20:25 inasema “Basi wanafunzi wengine wakamwambia Thomaso, Tumemwona Bwana. Akawaambia, *Mimi nisipoziona* mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, *mimi sisadiki hata kidogo.”*
😒🤔 K**a unataka kumuamini Mungu basi shika neno hili, ukishasema “nitaamini nikiona” hiyo siyo imani; au unasema “nimeamini ila nikiona ndiyo nitaamini vizuri” hiyo siyo imani.

🌺🔥 Yesu anamwambi Thomaso *“wa heri wale wasioona wakasadiki”* maana yake yule ambaye ataamini *kabla hata hajaona* huyo ndiye atakayeondoka na baraka yake.

🥰📚📖 Leo ukiingia kusoma neno, lisome kisha ingia kuomba, baada ya hapo tamani moyo wako uamini kupokea, na hata kumshukuru Mungu wako kwa matokeo.

UBARIKIWE SANA KWA KUSOMA (1 TIMOTHEO 4:13)

*Maombi ya Leo;*
_Eh! Baba wa Mbinguni naomba nisaidie kuwa na imani yako yenye matokeo._

🎻 Pastor Ulenje
*GOD ANSWERS PRAYERS*

🔥

NewDay-NewPower PRAYER DEVOTION Mon June 22NAMNA NYEPESI UNAWEZA KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU.Karibu tujifunze kanuni zinawez...
22/06/2026

NewDay-NewPower

PRAYER DEVOTION
Mon June 22

NAMNA NYEPESI UNAWEZA KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU.

Karibu tujifunze kanuni zinaweza kukusaidia wewe au ukamsadia mwingine kupokea Roho Mtakatifu.

📚 Yohana 7:37-39
_[37] Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. [38] Aniaminiye mimi, k**a vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. [39] Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.

YESU ANASEMA MTU AKIONA KIU

✍️✍️ Maana yake ni hii; ni mpaka umeona kiu ndipo uende kwa Yesu kuomba Roho Mtakatifu; kigezo cha kwenda kwa Yesu kuomba Roho au kuombewa ni uwe na kiu.

🙌💯 Kuona kiu ni kuona shauku; ni kuwa katika hari ya kutaka Roho Mtakatifu, hata kuwa tayari kulipa gharama yoyote ili tu umpate, akuongoze, akutumie, na kuwa karibu na wewe.

👉🔉Nikwambia tu ukweli; kumpokea Roho Mtakatifu kuna gharama ya kulipa; siyo gharama ya msalaba, ila ni gharama ya kuacha mengine ili umpokee Roho Mtakatifu.

🫷🤔 Watu wengi wanamtaka sana Roho Mtakatifu ila hawampati ni kwa sababu hawapo tayari kulipa gharama; *na kwanini hawapo tayari kulipa gharama ni kwa sababu hawana kiu.*

MTU MWENYE KIU YUPO TAYARI KULIPA GHARAMA YOYOTE.

🔥🔥 Kiu ni k**a moto kwenye koo; huwezi kutulia mpaka umepata maji; tena siyo maji tu, maji mengi mpaka unafurika; hata k**a maji yatauzwa, utanunua, yako mbali, utayafata kwenda kuyachota.

K**A UNA KIU, KIWANGO CHA KUWA TAYARI KULIPA GHARAMA YOYOTE ILE ILI UMPATE ROHO KARIBU KUJIFUNZA (1 TIM 4:13)

Maombi ya Leo;
Bwana Yesu naomba unibatize na Roho Mtakatifu siku ya leo, hata kufurika.

🎻PastorUlenje
GOD ANSWERS PRAYERS

🔥

*“Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.”*‭‭Yn‬ ‭20‬:‭29‬ ‭SUV
20/06/2026

*“Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.”*
‭‭Yn‬ ‭20‬:‭29‬ ‭SUV

NewDay-NewPowerPRAYER DEVOTION Sat 13 June 2026ROHO MTAKATIFU ALIPO NGUVU ZA GIZA HAZIWEZI KAATangu kwenye agano la kare...
13/06/2026

NewDay-NewPower

PRAYER DEVOTION
Sat 13 June 2026

ROHO MTAKATIFU ALIPO NGUVU ZA GIZA HAZIWEZI KAA

Tangu kwenye agano la kare tunaona Sauli alipotokwa na Roho Mtakatifu basi roho mbaya ikamuingia, na Daudi ambaye tayari alikuwa na Roho wa Mungu alipopiga kinubi ile roho mbaya ikamuacha [1 Sam 16"13-17, 22-23].

💧⛲️ Pepo amtokapo mtu hupitia mahali pasipo maji - Math 12:43. Maji ni Roho Mtakatifu.

📚 Math 12:43 __
Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

📚 Yoh 7:38, 39 __
Aniaminiye mimi, k**a vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.

Maana yake mahali ambapo Roho yupo, pepo hawezi kupita hapo. Maji pia ni neno la Mungu na Roho - Yoh 6:63.

🔥 Yesu aliyejaa Roho Mtakatifu alipokuwa akifundisha roho chafu walipiga kerere na kuwatoka watu - Luka 4:14, 31-37, 40-41.

Pia tunaona wanafunzi walipojiwa na Roho Mtakatifu mapepo walianza kuwatoa watu mapepo - Mdo 5:16. Tunaona Yesu alitoa pepo kwa Roho wa Mungu - Math 12:28. Yesu anasema

📚 Luka 4:18
_Roho wa Bwana alikuja juu yake kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, kuwaacha huru waliosetwa._


KWANINI ROHO AKIWA MAHALI PEPO HAKAI

💥 Roho alikuja duniani ili kuondoa giza, kuondoa ukiwa - Mwa 1:1-3

__Mapepo ni giza, maana yake nuru ikiingia haijarishi wingi wa giza, linaondoka. na wingi wa giza ndiyo unafanya nuru kutawara.

👑 Roho anakuja na ufalme wa Mungu [ utawala, mamlaka, nguvu, utukufu wa Mungu] - Math 12:28, Mdo 1:4-8.

__infact. Adamu alikuwa na mamlaka pale alipokuwa na Roho wa Mungu ndani yake, Suali kadhalika.

🔋 Roho mtakatifu huja na nguvu za Mungu

mtu anapopokea Roho Mtakatifu anapokea na nguvu za Mungu, sababu Roho anakuja na nguvu za Mungu, ndiyo maana kuna sehemu anafananishwa na mkono wa Mungu - Luka 4:14, Mdo 1:8.

📚 Matendo 4:31
Mitume na kanisa wanapokea ujazo zaidi wa Roho Mtakatifu na Mdo 4:33 __wanatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi.

🔥 Roho anafananishwa na moto - Mdo 2:3, Math 3:11, Ufu 4:5.

📚 Ufunuo 4:5
Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.

__ndiyo maana tunapotamka moto mapepo yanapiga kerere, sababu Roho ni moto wa Mungu, mapepo hayawezi kustahimili.

🙌 Roho kuwa ndani ya mtu ni Mungu kuwa ndani ya Mtu

__Yaani Baba, Mwana na Roho kuwa ndani yake - 1 Yoh 3:24.

__Haiwezekani Mungu awe ndani yako na pepo wote pia, nop! lazima shetani atatafuta njia.

MUNGU AKUBARIKI KWA KUSOMA (1 TIM 4:13)

Maombi ya Leo;
Baba wa Mbinguni, naomba unijaze Roho wako Mtakatifu; nguvu za giza zisipate nafasi kwenye maisha yangu.

🎻PastorUlenje
GOD ANSWERS PRAYERS

🔥

NewDay-NewPower🧨PRAYER DEVOTION Thu 4 June 2026🔥UKIOMBA ROHO MTAKATIFU UTAPEWA.📚 Luka 11:13Basi, ikiwa ninyi mlio waovu ...
04/06/2026

NewDay-NewPower🧨

PRAYER DEVOTION
Thu 4 June 2026

🔥UKIOMBA ROHO MTAKATIFU UTAPEWA.

📚 Luka 11:13
Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?

Kati ya mistari ambayo ina nguvu sana kuzungumza kuhusu Roho Mtakatifu ni huu; kwa maana unafunua namna gani unaweza kupokea Roho Mtakatifu hata ukiwa mwenyewe.

✍️ Ukweli, watumishi wengi ukisoma historia zao; kuanzia na Martin Luther, John Wesley, Happy Hunters, Kathryn Kuhlmam, Benn Hinn, David Yonggi Cho. AA Allen na wengine walipokea Roho Mtakatifu walipojifungia ndani ya kuomba.

💥 Hata ukisoma uamsho uliotokea Azusa mwaka wa 1906 ukiongozwa na Mother of Pentecostalism Lucy Farrow na Williams Saymor utaona walijifungia ndani kwa siku 10 ili kufunga na kuomba, na siku ya 6 Roho Mtakatifu akawashukia.

🔥 Mbali na yote tazama chanzo cha uamsho wa wanafunzi pale Yerusalemu (Mdo 1:13-14, 2:1-4) utaona ni namna ile ile; walijifungia ndani ghorofani kwa siku 10 wakiomba na kusali na Roho Mtakatifu akawashukia na wakajazwa na Roho Mtakatifu.

👍 Amazing, Nawapenda sana, walipoingia kuomba tena na kumpazia Bwana sauti kwa moyo mmoja (Mdo 4:23-31) Roho Mtakatifu akawashukia tena na wakajazwa tena na tena mpaka mahali pale pakatikiswa.

UNAJIFUNZA NINI?

💖♥️ Kwa upendo wote kabisa 🥰 naomba niseme nawe 👧👦 my sisters and my brothers k**a utaamua leo kumpokea Roho Mtakatifu na kiwango cha kujaa; inawezekana, ni kuingia kuomba, na kiwango kimewekwa kibiblia ni siku 10; hata k**a uko bize namna gani k**a utajipa siku 10 kuomba kwa kufunga; hakika nakwambia utapokea majibu yako na utajaa Roho Mtakatifu.

💯 Yesu ameweka wazi; ikiwa sisi tulio waovu, tunajua kuwapatia watoto wetu vipawa vyema; Baba yetu wa Mbinguni ni zaidi atatupatia kipawa cha Roho Mtakatifu k**a tutamuomba.

Maombi ya Leo;
Nakuombea sana, k**a utajenga shauku ya kupokea Roho Mtakatifu basi ukapokee na kujaa hata kunena kwa lugha na kutenda miujiza. Amen 🙏

MUNGU AKUBARIKI SANA.

🎻PastorUlenje
GOD ANSWERS PRAYERS

🔥

NewDay-NewPower PRAYER DEVOTION Tue 02 June 2026IMANI YA IBRAHIMUWaebrania 11:8_Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, a...
02/06/2026

NewDay-NewPower

PRAYER DEVOTION
Tue 02 June 2026

IMANI YA IBRAHIMU

Waebrania 11:8
_Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako._

Imani ni kufanya kile Bwana amesema kwa imani; Mungu ameweka majibu ya maombi yako na majibu ya maisha yako kwenye neno lake.

💖 Ulipofika wakati wa Mungu kuanza kumtumia Ibrahimu na kumpatia maisha mapya; alituma neno lake kwa Ibrahim.

👋 Halikuwa neno rahisi; aliambiwa kwenda mahali ambapo Mungu atamuonyesha; sehemu mpya kwenye macho yake; na ngumu zaidi hakumwambia ni wapi anatakiwa kwenda; bali alimwambia nenda mpaka pale nitakuonyesha kuwa ndipo.

🔥 Lakini kwa Imani Ibrahimu akanyanyua ng'ombe zake, mke wake na wafanyakazi wake wote, na Lutu wakaanza safari asijue wapi anawapeleka, bali ana neno la Mungu pekee.

🏇 Kwa imani hiyo Mungu akamhesabia Ibrahimu haki; kwako leo, Je! Unaweza kumuamini Mungu hata k**a hajakwambia matokeo?

🎻🎉 Biblia ni kitabu chenye neno la Mungu, neno lenye pumzi ya Mungu (2 Tim 3:16) k**a utalisoma na kulitenda hakika utapata muujiza wa hilo neno; kwa maana kila neno ukilisoma lina jukumu la wewe kufanya na ahadi ya baraka, k**a utafanya jukumu basi baraka yake itakufikia

🤨 Usikae chini unasubiri Roho Mtakatifu aseme ikiwa kuna neno kwenye Bible bado hujaanza kuliishi; k**a Mungu ataona unadharau neno ambalo ameliandika, ni ngumu sana kukupatia neno la kusema.

SINA MAANA USITAKE ROHO ASEME, ILA NINA MAANA KILA NENO LA MUNGU LA KUANDIKWA NA KUSEMWA YANA THAMANI SAWA, UKIYAISHI UTAPATA MATOKEO.

Maombi ya Leo;
Nakuombea Bwana akupe ujasiri la kuliishi neno lake kwa kulitenda.


GOD ANSWERS PRAYERS

🔥

NewDay-NewPower Prayer Devotion Thu 28 MayESTA MWANAMKE SHUJAA WA MAOMBISijui unawaza nini unaposikia jina Esta; ila mim...
28/05/2026

NewDay-NewPower

Prayer Devotion
Thu 28 May

ESTA MWANAMKE SHUJAA WA MAOMBI

Sijui unawaza nini unaposikia jina Esta; ila mimi huwa nawaza dada fulani mnyenyekevu ila shujaa wa imani ndani yake; dada aliyekuwa na shauku ya Mungu ya kila siku.

🫶 Esta alimpenda Mungu na alimwamini Mungu; na alikuwa na shuhuda za kutosha kuhusu Mungu; kufunga na kuomba ilikuwa ni sehemu ya maisha yake.

🏹 Alikuwa na ufahamu kuhusu vita vya kiroho; alijua chochote mbele yake ni Mungu anakiongoza; ila pia alijua ili kuishinda mizimu ya Umedi na Uajemi basi ilihitaji kufunga na kuomba.

💥 Alitoa uzoefu wa maombi kwa Mordekai ambaye aliposikia habari mbaya akavaa magunia ishara ya kunyenyekea mbele za Bwana; ila Esta alienda mbali zaidi; alijumrisha na kufunga; tena alifundisha wajakazi wake wote; nina hakika na watoto wake; kuhusisha maombi na kufunga.

🧨🔥 Haleluya, maombi yamebeba nguvu; maombi yamebeba kibali; kwa maombi esta akapa kibali toka kwa Bwana; kibali ambacho hakiwezi shindwa popote na hakiwezi zuiliwa na yoyote.

🧡♥️ Kwenye maombi tunakusanya harufi nzuri kutokea kwa Bwana (Ufunuo 8:1-5) na hapo tunapata neema toka kwa Bwana (Ebra 4:12) hiyo inazalisha kibali kwenye maisha yetu.

🎻🎉 kwa kibali hiko; Esta akapita mbele ya mfalme; kinyume cha sheria; akamsh*taki yule adui wa Wayahudi Hamani; akaangamiza kizazi chake chote; akageuza huzuni ya Wayahudi kuwa sherehe.

UNATAKA KIBALI TOKA KWA BWANA; MAOMBI LAZIMA YAWE NI MAISHA YAKO.

Maombi ya Leo;

Eh! Bwana Yesu naomba nijalie neema ya kufunga na kuomba; usiniache pasipo kibali chako. AMEN 🙏


GOD ANSWERS PRAYERS

+255 683477827

NewDay-NewPowerPRAYER DEVOTION Tue 26 May🔥 UKIONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU UTAFANIKIWA 🔥Watu wengi wanatafuta mafanikio kup...
26/05/2026

NewDay-NewPower

PRAYER DEVOTION
Tue 26 May

🔥 UKIONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU UTAFANIKIWA 🔥

Watu wengi wanatafuta mafanikio kupitia nguvu zao, akili zao, elimu, au mahusiano yao; lakini mafanikio ya kweli yanapatikana pale mtu anapoongozwa na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu si nguvu tu, bali ni uwepo wa Mungu unaomwelekeza mwanadamu katika kusudi, amani, ushindi, na uhusiano wa kweli na Yesu Kristo.

1️⃣ Roho Mtakatifu ni wa zamani sana zaidi yako — alikuwepo kabla ya Adamu na kabla ya misingi ya dunia kuwekwa.

📖 Mwanzo 1:2 SUV
“Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.”

Kabla mwanadamu hajaumbwa, kabla dunia haijakamilika, Roho wa Mungu tayari alikuwepo. Anaijua mwanzo na mwisho kwa sababu alikuwa pale tangu mwanzo.

2️⃣ Roho Mtakatifu ana ufahamu wote kuhusu maisha yetu na kusudi la Mungu juu yetu.

📖 1 Wakorintho 2:10-11 SUV
“Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.”

Roho Mtakatifu anajua hatima yako, wito wako, mapambano yako, na mpango kamili wa Mungu juu ya maisha yako. Ukimruhusu akuongoze, lazima ufikie hatima yako.

3️⃣ Roho Mtakatifu anajua namna ya kutimiza kusudi la Mungu ndani yetu,

📖 Warumi 8:14 SUV
“Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.”

📖 Yohana 14:26-27 SUV
“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote…”

Unataka kufikia kusudi la Mungu huwezi kwepa kutengeneza nidhamu ya kuongozwa na Roho Mtakatifu kwenye maisha yako.

4️⃣ Furaha ya kweli inapatikana katika Roho Mtakatifu.

📖 Warumi 14:17 SUV
“Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.”

Furaha ya Roho Mtakatifu haitegemei mazingira. Ni furaha inayotoka kwa Mungu mwenyewe, inayobaki hata wakati wa majaribu. Haleluya.

5️⃣ Uhusiano wetu na Kristo unashikiliwa na Roho Mtakatifu.

📖 Yohana 16:13-14 SUV
“Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote…”

“Yeye atanitukuza mimi…”

Bila Roho Mtakatifu, mtu hawezi kutembea kwa ukaribu wa kweli na Kristo. Yeye ndiye anayemfunua Yesu ndani yetu, anatubadilisha kufanana naye, na kuweka mioyo yetu karibu na Kristo.

✨ Ukijisalimisha kwa Roho Mtakatifu kila siku, atakuongoza kwenye maamuzi sahihi, atakulinda, atakutia nguvu, na atakupeleka kwenye mafanikio ya kweli katika kila eneo la maisha yako. Maisha salama na yenye ushindi ni maisha yanayoongozwa na Roho wa Mungu.

📖 Wagalatia 5:16 SUV
“Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.”

Maombi ya Leo:
Roho Mtakatifu nakupenda sana; naomba uongoze maisha yangu katika amani ya kweli, na kwenye njia ya kufikia kusudi la Mungu. Amen 🙏

pastorUlenje
GOD ANSWERS PRAYERS
+255 683477827

NewDay-NewPower PRAYER DEVOTION Wed 20 MayWEWE AMINI TU.Mk 9:23 SUVYesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aamin...
20/05/2026

NewDay-NewPower

PRAYER DEVOTION
Wed 20 May

WEWE AMINI TU.

Mk 9:23 SUV
Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.

Hakuna neno zuri na gumu kwenye Biblia k**a hili; maana unaweza fikiri umelielewa kumbe "hapana"

🤔 Kwa uelewa Yesu hakusema Yote yanawezekana; bali kasema "Yote yanawezekana kwake aaminiye.

Kuamini hapo ndiyo mada kuu ya Yesu.

🙆‍♂️ Tatizo ni moja Yesu anataka kuamini pasipo mashaka.

Mk 11:23 SUV
"...wala asione shaka moyoni mwake...

😞 Fikiri Petro mbele ya Yesu mashaka yalimzamisha.

Mbele ya Yesu Kristo, Petro alianza vizuri kutembea juu ya maji baada ya kuamini neno la Yesu; lakini alipoona shaka; akazama - Math 14:30.

🤔 Mashaka yanakuja pale unapoanza kuwaza itakuwaje/itatokeaje?

Unapoanza kuwaza itakuwaje/itatokeaje hapo ndipo unaanza kuona ugumu na ukubwa wa hitaji na mapito yako; hapo ndipo mashaka yanakuja na kuvamia moyo wako - 2 Wafalme 6 na 7.

🤨 Unamkumbuka yule akida wa mfalme mwenye mashaka?

Alimwambia Elisha _"...Tazama, k**a BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana?_ 2 Fal 7:2; kwanini alisema hivi? Ni kwa sababu alitazama uwezekano wa jambo hakumtazama Mungu.

🙌 Itawezekanaje/Itatokeaje ni sehemu ya Mungu siyo yako.

Wengi wanakonda na kuwa wanyonge sababu wanatazama itatokeaje/itawezekanaje; hiyo ipo kwenye kiwango cha akili ya Mungu siyo yako; yeye ndiye anajua muujiza wako utatokeaje.

👉 Haina maana usitumie akili zako.

Kuna yale ambayo Mungu anataka kutumia akili ambayo amekupatia; katika hayo ni utukufu kwa Mungu ukitumia akili; ila tazama usizitegemee akili zako hapo utavuka mipaka ya makusudi ya Mungu kukupatia akili na utaingia kwenye mashaka.

Nakushauri

Badala ya kuumiza kichwa itakuwaje; wewe nyenyekea Kwake Mungu Yeye atakupa akili ya kufanya na atakusaidia majibu kutokea.

Maombi ya Leo;

Nakuombea sana Bwana akupe moyo wa utulivu wa kuamini; hata eneo unaona shaka leo Roho wa imani akujaze imani.


GOD ANSWERS PRAYERS
+255 683 477827

🔥

Address

Kihonda Viwandani
Morogoro

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Pastor Ulenje posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share