Kituo cha uinjilishaji na maombezi ya wagonjwa

Kituo cha uinjilishaji na maombezi ya wagonjwa Kituo cha uinjilishaji na maombezi ya wagonjwa kipo Jimbo katoliki la Mbulu mawasiliano 0787554057🇹

Pumzika kwa amani mama yetu Mpendwa Anna Paulo Akinaay vita umevipiga na mwendo umemaliza Akina
21/12/2023

Pumzika kwa amani mama yetu Mpendwa Anna Paulo Akinaay vita umevipiga na mwendo umemaliza Akina

Tunawashukuru WAWATA wa Dekania ya Katesh kwa Kutenda matendo ya huruma kuja kuwatembelea Wasiojiweza, walemavu na wazee...
14/12/2023

Tunawashukuru WAWATA wa Dekania ya Katesh kwa Kutenda matendo ya huruma kuja kuwatembelea Wasiojiweza, walemavu na wazee wasio na watu wa kuwatunza pamoja na wagonjwa. Mungu awabariki kwa kile walichokitoa wazidishiwe Amina.
1. Parokia ya Endasack.
2. Parokia ya Nangwa.
3. Parokia ya Measkron.
4. Parokia ya Simbay.
//
We thank the WAWATA Dekania of Katesh for doing acts of compassion to visit the Indigent, the disabled and the elderly who have no one to take care of them as well as the sick. God bless them for what they have given and be multiplied Amen.
1. Parish of Endasack.
2. Parish of Nangwa.
3. Parish of Measkron.
4. Parish of Simbay.
ASANTENI SANA MUNGU AWABARIKI. 😊 😃

09/11/2023

Kituo
Ni

MASOMO YA MISA, JUMAPILI, OKTOBA 1, 2023YesterdayMASOMO YA MISA, JUMAPILI, OKTOBA 1, 2023JUMA LA 26 LA MWAKA ________MWA...
01/10/2023

MASOMO YA MISA, JUMAPILI, OKTOBA 1, 2023
Yesterday

MASOMO YA MISA,
JUMAPILI, OKTOBA 1, 2023
JUMA LA 26 LA MWAKA
________

MWANZO
Dan. 3:31, 29, 30, 43, 42

Ee Bwana, yote uliyotutendea, umeyatenda kwa haki, kwa kuwa sisi tumetenda dhambi, wala hatukuzitii amri zako. Ulitukuze jina lako na kututendea sawasawa na wingi wa huruma zako.
________

SOMO I
Eze. 18:25-28

Bwana ameniambia hivi: Ninyi mwasema, Njia ya Bwana si sawa. Sikiliza sasa, Enyi nyumba ya Israeli; Je! Njia yangu siyo iliyo sawa? Njia zenu sizo zisizo sawa? Mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, atakufa katika uovu huo; katika uovu wake alioutenda atakufa. Tena, mtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai. Kwa sababu atafakati, na kughairi, na kuyaacha makosa yake yote aliyoyatenda, hakika, ataishi, hatakufa.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
________

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 25:4-9, (K) 6

(K) Kumbuka rehema zako, Ee Bwana.

Ee Bwana, unijulishe njia zako,
Unifundishe mapito yako;
Uniongoze katika kweli yako,
Na kunifundisha:
Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu. (K)

Ee Bwana, kumbuka rehema zako na fadhili zako.
Maana zimekuwako tokea zamani.
Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu,
Wala mausi yangu,
Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako,
Ee Bwana, kwa ajili ya wema wako. (K)

Bwana yu mwema, mwenye adili,
Kwa hiyo atawafundisha njia wenye dhambi.
Wenye upole atawaongoza katika hukumu.
Wenye upole atawafundisha njia yake. (K)
________

SOMO 2
Flp. 2:1-11

Ikiwako faraja yoyote katika Kristo, yakiwako matulizo yoyote ya mapenzi, ukiwako ushirika wowote wa Roho, ikiwako huruma yoyote na rehema, ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo yaw engine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushik**ana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo k**a mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
________

SHANGILIO
Yn. 15:15

Aleluya, aleluya,
Ninyi nimewaita rafiki,
kwa kuwa yote niliyoyasikia
kwa Baba yangu nimewaarifu.
Aleluya.
________

INJILI
Mt. 21:28-32

Yesu aliwaambia wakuu wa makuhani na wazee, Mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. Akajibu akasema, naenda, Bwana; asiende. Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda. Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Bwana Yesu akawaambia, Amin, nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini; nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

Wanafunzi wa shule ya Dr Orson waliokuja kuwatembelea watu wasiojiweza katika asasi hii CHODEP. Mwenyenzi Mungu awabarik...
03/09/2023

Wanafunzi wa shule ya Dr Orson waliokuja kuwatembelea watu wasiojiweza katika asasi hii CHODEP. Mwenyenzi Mungu awabariki na waweze kufanya vizuri katika mosomo yao waweze kufaulu katika mitihani yao ya kidato cha sita na kidato cha nne kupitia njia ya Kristo Bwana wetu Amina.

12/07/2023

Kaka Paulo hakika umetuacha umetangulia mbele za haki uliotuacha tunae majonzi na masikitiko Pumzika kwa Amani 😓😓😭😭😭Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa milele umuangazie Apumzike kwa amani.Amina.

20/06/2023

Tunamshukuru Mungu ilikuwa ni siku ya furaha kwa watoto wa utoto Mtakatifu wa parokia ya Mt Theresia wa mtoto Yesu Bashay Mangisa kuwa pamoja na watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu walio katika kituo hiki cha uinjilishaji na maombezi kwa wagonjwa tunamshukuru Mungu. tunawashukuru na sisiomba kwa Mungu ili wakue katika upendo wa Mungu. Pia tunawashukuru akina mama wa makundi maalum kutoka Karatu mjini kwa kuja kuwalea watoto na kuwatafutia baraka za Mungu kwa kuwaletea mahitaji mbalimbali. Mwenyenzi Mungu awape afya njema na abariki kazi ya mikono yao. Mawasiliano ya shirika hili ni 0756207272 na 0787554057. [email protected]. Asante na karibuni sana.

//

We thank God it was a happy day for the children of the Holy childhood of the parish of Bashay Mangisa to be with orphans and children living in difficult circumstances who are in this evangelization and intercession center for the sick we thank God we thank themand we pray to God that they may grow in God's love. We also thank the mothers of special groups from Karatu town for coming to look after the children and seek God's blessings by bringing them various needs. Our God grant them good health and bless the work of their hands. The contacts of this organization are 0756207272 and 0787554057. [email protected]. Thank you and very soon.

11/06/2023

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya siku hii ya leo ya ekaristi takatifu wagonjwa pamoja na wasiojiweza waliadhimisha siku hii wakiwa katika Asasi hii ya huduma ya uinjilishaji na maombezi ya wagonjwa na wasiojiweza. Ibada iliyoongozwa na padre James Yarrot.

08/04/2023

Tunawashuru sana mliotoa misaada kwa kipindi chote mwenyenzi Mungu awe pamoja nanyi Amina mbarikiwe sana mungu awajalie nguvu zaidi katika mikono yenu Amina. 🙌 🙌 🙌

Kumbukumbu
08/04/2023

Kumbukumbu

MARIOLOGYMARIAMARIAMU-MIRIAM MARA AVE MARIA (UTANGULIZI)Salamu Maria tutakayo tafakari umejaa mawazo Roho ya kibiblia na...
08/04/2023

MARIOLOGY
MARIA
MARIAMU-MIRIAM MARA AVE MARIA (UTANGULIZI)
Salamu Maria tutakayo tafakari umejaa mawazo Roho ya kibiblia na kiinjili, kwani ni kingo kati agano la kale na agano jipya na torati mpya.
Maria ni kweli binti wa Kiizraeli ambapo roho (moyo) umejaa maandiko matakatifu katika ukimya wakumtafakari na kumfikia Mungu Maria ni msiri wa mungu (Mystique).
Tofauti na kiumbe (Binadamu)chochote anaweza kupenya maandiko matakatifu kwa vile toka kutungwa mimba kwake alishajazwa mwanga wa roho mtakatifu, roho huyo huyo aliye wasukuma waandishi wa vitabu vitakatifu kunena kwa jina la mungu.
K**a Waizraeli wengi Huchaji (Pieux) Wamcha Mungu Maria alikuwa anasubiri na kutamani ujio wa mwokozi na katika sala zake aliomba sana kwa moyo (Roho) wake wote ujio wa bwana na mwokozi wa Ulimwengu.
Ilijulikana karne hizo kwamba mabinti wadogo wa Izraeli na katika siri ya mioyo yao walisubiri na kutamani kuwa mama aliyetabiriwa aliyetangazwa ujio wa Kristo.
BIKIRA
Isipokuwa Maria pekee kwa upendo wake uliomwakia Mungu ali funga Nadhiri ya ubikira (usafi wa moyo), wala hajafikiria upendeleo wa bahati ya kuwa mama wa mwokozi mama wa mwokozi alikuwa amewaombea wengine mipango ya Mungu na yanaweza kukutana na malengo ya kibinadamu (Mungu akitaka) Mungu daima huchagua kisicho wezekana: na yule ambaye hakutegemea kibinadamu ndiye aliyechaguliwa kuonyesha nguvu ya Mungu. Kwa vile moyo wa haukuwa bila ukarimu na kwa vile umwilisha si nje ya kazi ya upendo ilibidi achaguliwe yule ambaye moyo wake umeja upendo. UPENDO uwezo wa kutoa na kupokea (to come out of one self and vice verses)
“SALAMU MARIA”
Mwanamke aliyepaswa kuuletea ulimwengu Mkombozi wake, lazima alitakiwa awe sehemu ya taifa teule la Mungu: na hayo yaliyotokea kwa Maria ambaye si tu alikuwa binti wa taifa la Mungu lakini pia alizaliwa nyumbani mwa Daudi.
Hakika katika injili ni Yusufu (Joseph) aliyewekwa wazi na Malaika Gabrieli kumtoa wazi (direct) wa Mbari ya Daudi mfalme mkuu, ambapo kwa Maria Madfhanio na si uhakika lakini watu wote wanaamini hivyo kwa vile alisindikizana na Yusufu wakati wa sensa ya Palestina kwa vyovyote ubaba halisi unampa mtoto wake haki ya Urithi, Yusufu hakika alikuwa mume wa Maariamu, kwa sababu ya uchumba waliokuwa nao.
Wakati wa upashaji habari Mungu alimtuma Malaika Gabrieli kujieleza kwa Maria, mpashanaji habari za matukio makubwa mpashanaji mashuhuri (mkuu) wa matukio ya kiimani (dini).
Masimulizi ya habari hiyo yako wazi, malaika anatumwa Nazareti kijiji cha Galilaya kilikuwa cha watu wakaaji fukara wakifanya wakifanya kazi kwa mikono yao kupata mahitaji ya kila siku. Maria pia alijishughulisha kupata mahitaji ya kila siku na ndipo hapo katika ufukara na unyenyekevu Mungu akamchagu yule atakaekuwa mama wa Mwokozi. Malaika Gabrieli alipofika alirudia salamu alizo pewa na Mungu kiasi kwamba tumedhiriki kusema maneno aliyosema siyo “Salamu Maria” bali:- Mungu anakusalimia Maria, kwa ajili hiyo tunarejea maandiko ya asili ya Kihispania {Dios te salve Maria} (Dieu te fr Salave Marie). Toka miaka mingi watu walitaka kutoa tafsiri ya salamu Maria ya Malaika. Mfano Mwinjili Luka anatumia neno: (Kaire) (Rejouis toi) mwenye heri.
Lakini kiunani hakizungumzi kule Nazareti bali Kiebrania na neno Kaire hakifanani kutakiwa amani neno Shalom ya Kiebrania inayofanana na salamu (Hujambo) Habari salama ya kiswahili chetu na Boujour ya kifaransa.
Kwa vyovyote tafsiri hizo hazijali pamoja na tofauti zao ndogo ndogo zinazokamilishana, kwani katika salamu yeyote zile kuna daima nia ya kumtakia amani na heri yule tunaemsalimia. Uhabarisho (“Lannouncietion”) na salamu hiyo ni kweli amani na furaha kwenu kwaajili ya ujio wa Masiha yaliyotangazwa (habarisho) kwa mama yetu kwa bahati wasanii wachonga sanamu sanamu za Maria wanamwakilisha uchaji heshima ya kupenya mioyo lakini itabidi kuwasamehi kwa kumtukuza na kumweka Maria kumpa awe na heshima inayofanana na ya mfalme na malkia wakati hayo yalifanyika katika nyumba ndogo na mazingira fukara na nyenyekevu ya Nazareti.
Hata hivyo kilichopewa kipao mbele ni ukuu (neema) alizojaliwa kiumbe huyo. Daima huenesha Malaika Gabrieli akimwinamia Bikira Maria kwa heshima kubwa malaika wa mbinguni kumpigia goti si maajabu ya pekee kwa roho ya Maria? Wasanii walilielewa hilo.
Malaika Gabrieli alimsalimia Bikira kwa jina lake. Sivyo kumwelewa na kumtambua? Kwanini asieleweke yungali ni mteule wa Mungu tangu milele?
Jina Maria ni jina lililojulikana sana kwa Waibrania. Na katika Agano la kale lilikuwa la dada wa Aroni. Katika injili Maria wa Bethania mama yake Yakobo kwa Kiebrania linatamkwa/ andikwa Myriamu au Mariamu na kwao lina Maana ya Malkia (Princess) au mama yetu (Dame) linatokana na neno Kiaramayo Mara lenye maana ya Bwana (seigneur) kwa hiyo kwa jina analo beba angeitwa mama yetu ( Notre-Dame). Zaidi ya yote maisha ya Maria haya kuwa bila tendo la mapendo kwa Mungu.
[PLEINE de GRACE] UMEJAA NEEMA
Hii haina maana ya kufananishwa na chombo chochote kisiwe na nafasi tena. Tuko kwenye uwanja wa neema, unaweza kuongezwa kadiri roho inavyokuwa kitakatifu/ ujazo tofauti kila wakati.
Hii ndiyo ilivyo kuwa hali ya Bikira Maria kwamba kwa uaminifu wake na ukarimu wa moyo amekuwa wa kupokea daima zaidi na zaidi neema za Mungu.
Hii neema ambayo si kingine kuliko Mapendo ya Mungu yanayozidi kupenya moyo wake kina na kumfanya kiumbe au uwazi zaidi au ukarimu.
NB: Maria alishakingiwa dhambi ya asili, tamaa,mwelekeo,matamanio si zaidi ya kuwa na kumpenda Mungu bila ya kubakiza kitu. Roho ya mtoto mdogo anaebatizwa hujaa utakatifu wa Mungu lakini tofauti na hayo anapashwa habari Bikira yeye ni mkamilifu katika kupokea ujumbe wa Mungu si tu kwa kukuba bali kuishi kwa kina mno.
Katika unyenyekevu wake wa kina mno Maria aliondoa/kuacha vyote vilivyo vya kibinadamu kwajili ya kuweka huru moyo (roho) kwa ajili ya yaliyo ya Kimungu (clivin).
Daima na milele hakuna kiumbe atakaye jazwa na roho wa Mungu k**a Maria Mtakatifu, kwa vile na kutakuwepo na kiumbe huru (dispenible) kuutatokea neema za mungu k**a Maria. Kwa neema zake (Mungu) hujiona (juzuta) ndani ya Maria na ndiyo huo wa neema unamfanya Maria umejaa neema machoni pa Mungu. Matokeo yake ni kwamba hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kustahili utakatifu kwa nguvu uweze kupokea uwezo wake chenye Kumpendendeza Mungu.
Ni bwana mwenyewe atakaeweza kushirikisha (particire) utakatifu wake oh! Ulivyopendekeza roho ya Maria ambapo upendo wa Mungu unakaa ndani mwake (Maria) kwa ukamilifu wa haki ya juu mno na waki pekee! Ndiyo sababu kumpitia karne zote kalchairi na wasanii walijaribu kuelezeeana kupitia lugha za picha wasifu wa Maria kwa maneno yaliyoonyeshwa vilevile hatima ya viwango vya lugha za binadamu.
Hakuna kuumbe chochote aliyekuwepo katika roho wa binadamu k**a Maria na hivyo ni pamoja na Maria ambapo watakatifu wa mungu (kanisa) waliweza kufungua mianyo yao kupokea neema za Mungu yeye ni mwanga na faraja inayomulika nguvu. Yeye ni mfano unaovulia na kuonyesha njia ya ukarimu. Yeye ni mwanga wa neema inayowaka katika giza ya Dhambi yeye ni faraja yake wanaoteseka na wanaopigana vita, yeye ni tabasamu ya wale waliao.
BWANA YU PAMOJA NAWE (SEIGNEUR ET AVEC VOUS)
katika litrujia ya kanisa huwa inawatakia inawatakia watu amani ya bwana kwa washiriki ibada ya mafumbo ya hasa nyakati za misa au nyakati ya sala maalum na sikukuu kubwa *2
Lakini Maria ni tofauti sana sikumtakia amani tu bali ni uendelevu wa kweli (realite). Hivyo malaika Gabrieli hamtakii amani bali anasalimia uwepo wa bwana ndani ya kiumbe hicho kilicho pendelewa (privilagie’e) kipekee kwani nani kuliko mama yetu (Notre-Dame) angeweza kuwa na uwepo wa bwana.
Ni utatu mtakatifu unaoshirikiana na Maria kwa kina na mapana yake roho ya Maria kwani yupo Maria na kila mojawapo na nafsi za Mungu mahusiano ya hali ya juu mno mpaka sisi tunadhiriki kusema Bikira Maria ni mama yetu wa utatu Mtakatifu (Mere de latrinite) tunaweza kusema bila kukosea kweli Maria ni binti wa baba wa mbinguni aliyekubali katika umilele wote umwilisho wa neno(verbed) ndani ya tumbo mwili wake na ukombozi ili katika sadaka ya kristo upendo uwe ushindi wa Dhambi.
Yeye ni mchumba wa roho mtakatifu kwani bila mapenzi ya binadamu bali kwa mapendo ya roho mtakatifu ya mwana wa Mungu Mimba ya mwana wa Mungu ikatunga tumboni mwake.
Tusisahau kwamba siyo rahisi binadamu kueleza kazi hizo nafsi hizo tatu za Mungu kuhusiana na Maria Kwani hiyo ni Dogma (ukweli wa imani Katoliki Dunia nzima).
Kwani umwisho ukombozi hazina maana k**a hazirejei upendo wa Baba Mwana na Roho Mtakatifu. Maria pia amehusishwa fumbo la Dogma ya Utatu mtakatifu.
Vous etes benie entre toates ure
(Barikiwa kuliko wanawake wote)
Femmes
Wote:-
Wakati Maria alipofikia Mwisho wa safari yake ya kwenda kumsalimia Binamu yake Elizabath, kulikuwa na maneno ya salamu za kubadilishana ambayo yataendelea hadi milele.
Hatimaye Elizabeth akiwa na msukumo wa pekee wa roho mtakatifu pamoja na mwanga wake, alitambua ndani ya binamu yake Maria uteule wa Mungu, bila hata kuelezwa umama wa Kimungu. Elizabeth alishafunuliwa kwamba binamu yake alishateuliwa kuwa mhitimisha malengo ya mapendo ya Mungu kwa binadamu.
Na ndiye kiumbe binadamu wa kwanza kunena {umebarikiwa} Baraka maana yake ni alama ya mahusiano pekee kati ya anayepokea na kutoa[Mungu] ambaye peke yake ndiye mwenye uwezo wa kutoa baraka Elizabeth tu aliyeweza kuelewa uhusiano huo unaomuunganisha Maria na Mungu kwakumtofautisha na wanawake wengine wote ambao Maria alipewa Heshima na nafasi ambayo mwanamke yeyote hajapewa daima.
Hivyo Bikira Maria ni mwanamke wa Juu mno pamoja na thamani zote anazoweza kumiliki kuwa nae kiumbe chochote. Kwahiyo Maria alitambulishwa Karne zote na atatambuliwa hivyo alivyo miaka yote kwamba ndani yake kuna kila heshima ya mwanamke aliyeheshimiwa bila kupingwa.
Yeye ni Mfano wa vizazi vyote kuwa mwanamke anaejitoa sadaka kwa vizazi vyote kwa wanawake wanaojitoa sadaka kwa Mungu (watawa) na pia mfano wa uzuri na upole ( tendresse) kwa kina mama wote Duniani na hata Mbinguni .
Nikweli kwamba maneno ya Elizabeth yanafanya mawingu ndani ya mioyo ya Wakristo (Umebarikiwa Kuliko Wanawake wote) pamoja na kwamba amezaliwa na Kuishi k**a wengine lakini yeye kilele cha mwisho cha uumbaji wa Mungu (chef-d-oeuvre de Dreu).
Ndani ya Maria Mungu akipata alichokidhamiria ndani ya utu wa watu. K**a ndani ya Eva aliukuta ubinafsi,(uaminifu)uliopuuzia/utu wetu kinsmen na Eva kwa Maria/ ulikuta/pata jibu la wema na upole uliopatanisha utu wetu(Mungu)
Yeye ni ujana wa asubuhi ya kwanza ya uumbaji yeye ni mlango wa furaha ya Mungu ambapo ndani yake Maria anakuta / pata tunda la kazi ya uumbaji aliyodhamiria katika umilele wake Mungu.
(Berie ehtre touted re femmes)umebarikiwa kuliko wanawake wote.
Hivyo kweli umetenganishwa hapohapo umeunganishwa na dada zake na kaka zake umetofautishwa kwa neema na heshima kubwa mno aliyopewa na umeunganishwa kwani yeye niwa kizazi cha wanadamu (sa race).
Hivyo yeye ni majivuno yetu (fierte) na matumaini yetu imemwelekea na kujimaliza kabisa kwa mungu lakini pia amejielekeza kwetu bila kujibakiza (ila sisi) yeye ni bustani ya siri isiyochafuliwa kutiwa doa na hila za kibinadamu ambapo utakatifu wa Mungu utapenya kwa kumwibua mwokozi wa Dunia.
Amebarikiwa kuliko wanawake wote na unaupa ulimwengu kumbukumbu ya usafi asilia na toba ya paradise iliyoacha /potea kwa ajili ya uzembe na tamaa ya kutaka kujitawala na kwa uwezo wa kufanana na Mungu kwa akili zetu wenyewe.
Yeye ni up linalochanua katika miiba. Yeye ni mwanga unaoangaza usiku kuikumbusha dunia (mwanadamu) kuwa yeye anaweza kutunza matumaini.
ET JESUS LE FRUIT DE VOS ENTRAIL EST BENI (Na yesu mzawa wa tumbo lako amebarikiwa)
Tukizingatia salamu ya Elizabeth akiwa na msukumo wa roho mtakatifu tunatambua kuwa anayakinisha(afirme) ukweli na akiupongeza umama wa Maria.
Yaani ukweli wa uwepo wa Yesu ndani ya huyu Mama na kuutukuza u ama huo, ambao k**a wengine (kina mama)unafanyika ndani ya tumbo la kiumbe (mama Maria).
Elizabeth alikuwa na uhakika wa Maria kujitolea ubikira wake kwa Mungu na ni Mungu na Roho Mtakatifu anaemsukuma kuzungumzia/ kuongea mimba hiyo ambayo mtoto Ataitwa Yesu.
Misemo(Expression) ni dhahiri na pengine tunashangazwa sana pamoja na hayo ya kibinadamu yanatuashiria umbile ya kifizikia na ya kibayolojia ya Mama anaembeba tumboni mwake.
Maria ni mama k**a kinamama wengine ,tofauti na mtoto aliye ndani ya tumbo lake haikutungwa kwa njia ya kibinadamu ( bila kuwa na mwanaumembona?). Lakini kwa Mapenzi ya Mungu nguvu na uwezo wa roho mtakatifu zilizomfunika kwa kivuli chake na nguvu yake ya kiumbaji. Mtu unatoa utomvu ili kutengeneza tunda lake Maria atatoa damu yake mwenyewe kwa mwana wa Mungu ili aweze kuimwaga msalabani uzao wa tumbo lake ni kweli mwana wa milele wa Baba neno wa Mungu lakini pia mwana wa Maria ,kiumbe cha Baba (reve)
Tunda la tumbo la Maria lililotugwa ndani ya tumbo la Bikira aliyeteuliwa na kuandaliwa na Mungu .Mungu hawezi kuingia kuishi ndani ya binadamu asiyekuwa na usafi ukarimu na upendo wa hali ya juu.
Elizabeti naye anambeba tumboni Yohani mbatizaji na atakuwa mfaidi wa kwanza wa mwokozi atakayezaliwa na Maria ulimwenguni.
John Batist aliruka kwa shangwe tumboni mwa Elizabeth tunakubali kwamba katika kuruka kwa shangwe huko tunagundua nafasi ya Maria. Hataendelea kukutana na roho za watu wanaomwomba bali daima zitakuwa na mwanawe ili kutukubalia (Fils pour le donner).
Maombi na due zetu kuruka huko kwa shangwe kwa wakristo kuna maana ya:- Ili kuwapelekea mapendo ndugu zetu ndugu zetu ni lazima kumwishe (posseder) Mungu.
Ndugu zetu hawataruka kwa shangwe furaha na amani na mapendo isipokuwa tukiwabebea /peekee kristo anaeishi (vivant) ndani mwetu.
SEHEMU YA PILI
(Ave Maria) (Sainte Marie Maire de Dieu) Maria mtakatifu mama wa Mungu.
Hapo sasa tunaanza kutafakari sehemu ya pili ya (Nakusalimu Maria). Wakati hapo awali tulikuwa tumefanya tafakari kutoka maneno ya biblia. Sasa tunaenda kurudia maneno ya watu wa Mungu ambayo waliyaingiza katika sala hii ya Maria kwa namna bora zaidi.
Sehemu ya kwanza sala yetu ilikuwa ya kusifu na sasa inakuwa sala ya kusihi kuomba. Hata hivyo sala hii ya kusikia niya kuumiza matumbo (emouvante) ambapo upande moja tunagundua ukuu (grandeur) ua tunayemsihi hali upande wa pili tunagundua mateso mahangaiko ya yule anaetumia sala hii.
Hapo sasa tunapata msigishano (conteste) inayoiuma roho kwa kina (emeut profondement) kwa vile watu wa Mungu wanavyompenda kwa upende wa namna yake bibi yetu.(Notre DAME) wanauelewa wazi ufukara na wa mateso (misere) ya kimwili na wa kiroho ya binadamu hapa ugenini.
Halafu tunajikuta mbele ya mkeka (Etalement) wa ukuu na uzuri unaotupaisha mbinguni.
Matokeo yake tunaelewa katika maisha ya kawaida hapa duniani fukara anavyosihi ukarimu wa tajiri au watu wakuu. Muombaji huwa yuko tayari kumpigia magoti tajiri au mtu mkuu na kumpa wasifu tajiri ili apate (ufadhili mradi) au anachokihitaji Tunasifia tajiri upate mradi wako.
Lakini kwa Bikira Maria sivyo ila tu unyenyekevu na upendo wa kutoka mioyoni mwetu.
Maria mtakatifu uliyemtakatifu na zaidi, wewe uliye Malkia wa Malaika na watakatifu wote wewe uliye na ukuu na thamani ya utakatifu wako inapita ukuu na thamani ya watakatifu wote pamoja na malaika wote.
Wewe ambaye utakatifu ni sifa na asilia (origirelle) wewe ambaye utakatifu una kuwa daima kwa kipimo cha uaminifu na upendo ambao daima unazidi kukua na kutanuka.
Wewe ambaye kimea (tige) cha maisha yake haijawahi kusinyaa. Wewe ambaye maisha yako yote ni mwendo wa kwenda mbele bila kurudi nyuma au kusita sita.
Kwa jinsi hii tunaweza kukuita Maria Mtakatifu katika ujumla wa ukweli maana halisi ya neno hilo (plenitude) kwa vile kiukweli Mungu peke yake ndiye Mtakatifu na hakuna aliyekubalikuishi kuingia utakatifu wa Kimungu zaidi yako.
Maria Mtakatifu nguvu ya sala tunayopata kwako kwaajili ya kuwaombea walio wakosefu inapata nguvu kutoka kwako kwaajili ya utakatifu wako.
Kiumbe chochote kinacho ishi utakatifu wa Kimungu kina mahusiano ya kipekee na Mungu na ndicho kinachompa nguvu ya pekee kuwaombea ndugu zako.
Hiyo nguvu ya kuwa mwombezi ni kubwa kadiri roho hiyo inavyozidi kuungana na Mungu. Mungu anakubali kwa upendeleo zaidi sala za yeye anaetimiza mapenzi yake. Bikira Maria hakuwahi daima kumkatalia chochote Mungu.
Mungu angewezaje kumkatalia kitu chochote? Ndiyo! (Oui) Maria Mtakatifu utuombee sisi (me’re de Deus)
Mama wa Mungu :-hazijaegemea tu utakatifu wa kiumbe huyo aliyependelewa na asiyewahi kumkatalia Mungu chochote lakini pia kwa kuegemea juu ya (maternite) umama wa Kimungu.
Hata katika hali ya kawaida ya maisha ya kibinadamu mwana asingeweza kumkatalia kitu mama yake. Je! Itafikirika vipi kristo kumkatalia Mama yake?
Turejee injili ya Yohana Mtakatifu halafu tusome masimulizi ya arusi ya kana ya Galilaya. Injili ya Yohana Mtakatifu 4:46 Basi alifika tena kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa Divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huki Kapernaumu.
Kwanza Maria anaemia pamoja na maneno makali ya majibu ya Yesu akasema kwa watu akawasihi fanyeni atakavyo waambia. Na hali akijua kwamba ameshakubaliwa ombi lake.
Mama wa Mungu, tunakuelekea wewe katika sala zetu tukiutambua moyo wako na nguvu yako juu ya mwao mpenzi.
Prior pour nous (Utuombee sisi)
Usuombee sisi ya salamu Maria inathamani ya kumheshimu ya Mwanzo kwa vile inaweka wazi nafasi ya (Bibi yetu) katika safari ya maisha ya kikristo.
Sala hii ya Bikira Maria inatupa nafasi ya Maria na inaonesha wakristo kwamba Bibi yetu ni kiumbe anayemuomba Mungu.
Lakini pia ni kiumbe aliyeandaliwa kipekee kuwa mama wa Kristo roho zenye huzuni ziwe na matumaini tusalipo (Salamu Maria) kwani majitoleo yetu hayo nje ya Mungu ila katika sala tunamsihi Bikira Maria atuongoze kwa mwanao.

Pauvres pecheurs (wakosefu masikini)
Kweli vitu/ viwili vinavyokamilishana kwani mdhambi ni Maskini kuna kitu anapungukiwa anapungukiwa amani na furaha ya moyo / roho inayoishi na Mungu.
Anapungukiwa na uwema anaomsukumia awa peeked nduguze. Dhambi inamdhoofisha mdhambi na kumkosesha amani (Malheureux).
Watu wa Mungu walioelewa maneno hayo toka karne nyingi zilizopita kwamba mdhambi ni maskini wa heri.
Ahadi hiyo inaonyesha thamani ya Salamu Maria kuwa hiyo sala ina thamani ya pekee kwa vile anafunua maana ya dhambi na thamani ya neema kwa yule anae Sali sala hiyo pia inamweka mkristo katika hali ya unyenyekevu unaompa upendeleo katika maisha ya kiroho sala, Salamu Maria inajenga hali ya uaminifu una msukuma yeye anayesali apate nguvu ya wongofu unaohitajika daima ulio muhimu.
Mbele ya umaskini wa mdhambi huruma ya Maria ni kubwa kwa vile ni mama na mama daima anaupendeleo na msamaha na mtoto wake zaidi k**a ana maumivu na anapokosa heri na amani kwasababu ni mama wa Yesu amebarikiwa kiasi gani mapendo yana takiwa kwa ajili ya malipo ya dhambi.
Pia kwa sababu anaelewa mateso mengi hataki kwa namna yoyote kupoteza hazina ya huruma aliyopata mwanawe kwa kujimwilisha na kufa juu ya msalaba.
Huruma ni kubwa kwa yule amwonaye mwenye kuteswa anaemia goti miguuni pake.
Iliyo ndiyo kinachotukia katika sala ya (Salamu Maria) baada ya kusifu ukuu wa Maria tuna msihi atuinamie sisi tulio wa dhambi maskini.
Si tu utuombee kwa vile tumekosa, lakini pia utusaidie kumkalia shetani ushawishi wake.
Unaelewa udhaifu watu na tunaelewa tendo lako ni kuu kwa mwanao kwa vile amekushirikisha wakati wa kutoa sadaka ya ukombozi juu ya msalaba.
Tunaelewa kupitia historia ya kanisa kwamba majitoleo ya kimwana kwa bibi yetu katika mioyo yetu inajenga hali ya kuwa na nguvu na uwema.
Laity wakristo wote wangeelewa kuwa kwa kumwomba Bikira Maria wanapata mwangaza katika mioyo weupe angavu wa moyo wa Maria uliokingiwa dhambi ya asili.
(Maintenance et a l’heure) Sasa na Saa (de notre mort) ya kwetu kufa.
Huo sasa uliotamkwa (semwa) katika (Salamu Maria).
Itaendelee…

Address

Mbulu

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kituo cha uinjilishaji na maombezi ya wagonjwa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Kituo cha uinjilishaji na maombezi ya wagonjwa:

Share

Category