Efatha Church Mbinga

Efatha Church Mbinga NENO EFATHA LILITAMKWA MARA MOJA TU NA BWANA YESU KATIKA KITABU CHA MARKO 7:34. MBINGA FUNGUKA. Nini kinafanyika? Kuwafanya watakatifu wawe na umoja.
6. HALELUYA!

Saa imefika ya kuileta injili halisi ya YESU KRISTO wilayani Mbinga. Mungu alipomuita Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira kwa kazi ya kuliandaa kanisa lenye NGUVU ili hatimaye Injili iwaokoe waliokusudiwa, kwa wakati na majira yake sasa tumefika Mbinga. Kuikomboa Mbinga na watu wake Kutoka madhalimu yote ya shetani Kupitia mahubiri ya Neno la Imani, k**a Biblia isemavyo "Imani chanzo chake ni k

usikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo" WARUMI 10:17. Kwa kuwa wengi wanampenda Yesu Kristo hivyo tunafundisha mafundisho maalum ya kukulia wokovu, na jinsi ya kuishi na Nguvu ya ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye chanzo cha Hekima, maarifa na Mafinikio Yote ya Mwanadamu. Huduma ya Efatha ni maono aliyopewa Mtumishi wa Mungu, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira ambayo ndani yake kuna kusudi la Kiungu. Ili kufanikisha kusudi hilo, MUNGU alimpa Mtume na Nabii vipengele 10 vya kutekeleza ambavyo kwa pamoja ndivyo vinavyoumba Huduma ya Efatha.
1. Kuikomboa Tanzania ili iweze kusimama mbele za kiti cha hukumu na kupokea baraka za MUNGU.
2. Kuliandaa kanisa la YESU KRISTO kwa ajili ya kunyakuliwa lisilo na mawaa wala makunyazi.
3. Kufanya Kanisa la YESU KRISTO liwe na Mamlaka.
4. Kudhihirisha uweza katika KRISTO YESU, kwa Ishara, Miujiza, Uponyaji na Ukombozi wa Roho, Nafsi na Mwili.
5. Kumzalia BWANA matunda yaani kuwaleta watu kwa YESU.
7. Kupokea vipawa vya MUNGU k**a mahitaji yetu, ROHO MTAKATIFU, lugha mpya na kuvigawa.
8. Kusimamia kazi ya MUNGU na kuruhusu maongozi ya ROHO MTAKATIFU yaweze kutenda kazi.
9. Kuhakikisha kuwa malango ya kuzimu yananyamazishwa.
10. Kuwa tayari wakati unaofaa na usiofaa kuhubiri NENO la MUNGU

Usisite, njoo ukutane na Neno lenye kukutoa shimoni yaani dhambini. MBINGA MBINGUNI NI KUWA NA YESU.

Address

Precious Area, Kihaha
Mbinga
TZA

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00
Saturday 08:00 - 17:00
Sunday 00:00 - 17:00

Telephone

+255754711034

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Mbinga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share