Casfeta-Tayomi UDSM MCHAS

Casfeta-Tayomi UDSM MCHAS We are welcoming you to join us in our page and Services.

This is an organization of born again students from University of Dar Es Salaam (UDSM) Mbeya College Health and Allied Science (MCHAS) --UDSM MCHAS Found in Mbeya Region Tanzania.

REHEMA & KWELI ZA BWANAKuna mambo 5 yanayompa mtu kutembea chini ya rehema (mercy), neema ( grace) na upendeleo wa kiung...
06/08/2024

REHEMA & KWELI ZA BWANA

Kuna mambo 5 yanayompa mtu kutembea chini ya rehema (mercy), neema ( grace) na upendeleo wa kiungu ( divine favor)...

Mungu amejitambulisha kuwa mwenye huruma nyingi

Kutoka 34:6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;

[ And the LORD passed by before him, and proclaimed, The LORD, The LORD God, merciful and gracious, longsuffering, and abundant in goodness and truth, ]

Lakini....

Usiseme Mungu ni wa huruma na rehema hivyo ukawa mjinga kiasi cha kuwa na mwenendo wa kudumu usiopatana na injili ambayo kwayo uliokokewa...

Ingawa Bwana husamehe na ni mwenye huruma ila hawi radhi na wapumbavu siku zote....

Ni Bwana mwenye huruma na rehema nyingi huyu huyu ambaye kwa Manung’uniko aliwazuilia wana wa Yakobo kuiona nchi ya Ahadi akamruhusu Rahabu kahaba badala yake....

Ni Mungu huyu huyu...

Hata hivyo kuna namna nne zinazovuta huruma na rehema za Kimungu juu ya mtu kiasi cha kutoruhusu mkono wake au wa shetani umguse mtu huyo....

1. Jifunze kuungama (confess)

Hii ni hatua ya kwanza na ya muhimu kila mara nafsi yako inapokuhukumu (convict) kuhusu mwenendo fulani usio sawa. Dhamiri ya mtu ni sauti ya mtu wa ndani na itakwambia ukweli siku zote kuliko ukweli anaoweza kukwambia mtu yeyote. Jifunze kumweleza Mungu ukubwa wa kosa lako kinagaubaga bila kulipamba au kulifunika-funika (covering) wala kujitetea.

Hilo ndio maana ya Ungamo. Kutambua kosa lako na kuliungama k**a lilivyo ni hatua ya kwanza ambayo huvuta huruma, rehema, neema, upendeleo na kibali cha kiungu juu ya mtu.

2. Tubu (Repent )

Toba (Repentance) ni kuacha (forsake).

Ni kuamua toka moyoni na kwa nia dhabiti kuacha njia mbaya.

It is an intentional and total change from evil..

Wakati ungamo (confession) mi ukiri wa ulimi, toba ni badiliko ya jumla la kitabia/kimwenendo.

Ikiwa unakiri dhambi ile ile kila siku mbele za Mungu, huo sio udhaifu tena bali kifungo wala hiyo sio toba bali ungamo.

Ni sawa umekiri kuwa unatembea na mme wa Mtu, bado Mungu anakuhesabu kuwa mwasherati na mzinzi hadi utakapokuja mbele zake na kumwambia Bwana nimeacha.

Mungu hahitaji maneno zaidi k**a anavyofurahia kitendo hiki cha mtu kuacha njia zake mbaya...

Kwahiyo

Ungamo + Toba = Rehema + Mafanikio

Mithali 28:13

Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.

[ He that covereth his sins shall not prosper: but whoso confesseth and forsaketh them shall have mercy.

Sio kuungama tu bali na kuacha kabisa...

Mungu ni rafiki wa watu wanaoungama na kuacha njia zao mbaya kuliko watu wanaojihesabia haki kila kukicha....

Ati Mungu ni rafiki wa Daudi muuaji....

Kuacha njia mbaya ndio toba....

3. Jifunze Kusamehe ( Forgive)

Mungu huwapenda watu wenye huruma na wepesi wa kusamehe...

Usisamehe hutasamehewa...

K**a unataka kuishi maisha ya kibali, rehema na upendeleo wa Mungu, jifunze kuwasamehe ndugu zako hawa wanaokuudhi na kukukosea kila siku...

Msamaha wetu wa kibinadamu huruhusu mtembeo wa rehema na msamaha mkubwa wa kiungu juu yetu....

Mathayo 6:14-15

"Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu"

[ For if ye forgive men their trespasses, your heavenly Father will also forgive you: But if ye forgive not men their trespasses, neither will your Father forgive your trespasses. ]

Daudi alimsamehe Sauli wala hakuwalipiza kisasi adui zake wa waziwazi.....

4. Jifunze kumtii Mungu

Isaya 1:19 K**a mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
Isaya 1:20 bali k**a mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.

[ If ye be willing and obedient, ye shall eat the good of the land: But if ye refuse and rebel, ye shall be devoured with the sword: for the mouth of the LORD hath spoken it]

Utii ni alama muhimu ya mwana wa Mungu.

Ingawa Mungu ni mwenye rehema lakini roho mbaya ( evil spirit) ilivyomwingia Sauli hata asimsikilize Ssmweli nabii wake Mungu alimkataa.

Hivyo hivyo kwa Yuda wa Iskariote..

Mungu anafurahishwa na utii wetu kuliko kazi zetu tunazoita za kumvunia watu...

Anatamani kuvuna moyo wako kabla ya kukutumia kuvuna wengine...

5. Uwe Mnyenyekevu ( Be humble).

Isaya 66:2b

"...lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu"

[..... but to this man will I look, even to him that is poor and of a contrite spirit, and trembleth at my word.]

K**a ilivyo hekima, unyenyekevu ni roho pia na unaweza kwa kiasi fulani 'kujifunza kuwa'. Mungu anawapenda na kuwahurumia mno watu wanyenyekevu kwa neno neno lake wanapolisikia kutoka kwa kinywa cha nabii wake au kutoka kwake.

Mungu huwapenda watu wanaoukubali msalaba na neno k**a ukamilifu wa njia zao kuliko kutegemea akili zao wenyewe.

Watu waliopondokeka mioyo na sio wajuaji wasiotaka kufundishwa na mtu au Bwana...

Hakuna namna rehema za Mungu zitafanya kazi kwa mtu aliyeshupaza shingo yake...

Mithali 29:1 Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa.

[ He, that being often reproved hardeneth his neck, shall suddenly be destroyed, and that without remedy.]

Dr. Kazabao Edson
+255763575550

MASWALI NA MAJIBU KUHUSU IMANI Vs MAYENDO KATIKA WOKOVU WA MTU KWA MKTADHA WA KITABU CHA WARUMI 4.DADA IRENE:Mimi utanis...
30/04/2024

MASWALI NA MAJIBU KUHUSU IMANI Vs MAYENDO KATIKA WOKOVU WA MTU KWA MKTADHA WA KITABU CHA WARUMI 4.

DADA IRENE:
Mimi utanisaidia tu kunielewesha warumi sura ya 4 yote kwa kweli nachanganyikiwa nayo nikisoma kwa utulivu ndio nazidi kuvurugwa

MAJIBU:

Sura ya 4 ya kitabu cha Warumi kilichoandikwa na Paulo inafundisha kitu kimoja tu, HAKI KWA NJIA YA IMANI ( Righteousness by Faith )

Mwandishi anaanza kwa kumuongelea Ibrahimu jinsi ambavyo alihesabiwa haki kwa imani ( 4;1-5) huku ikiyahesabu kutokuwa kitu matendo ya sheria katika kumhesabia haki Ibrahimu ila imani yake juu ya Ahadi ya Mungu.

Mstari wa 4:6-8 Paulo anainukuu Zaburi 32 maneno ya Daudi ambaye akisha kuuona udhaifu wa matendo ya sheria ukilinganisha na haki na utakatifu wa Mungu akayaona ni kitu kisichoweza kumuokoa mtu, akasema heri yake mtu yule aliyestririwa makosa naam heri yake yule ambaye Mungu hamhesabu mkosa ( Si kwamba si mkosa, bali Mungu hamhesabu kuwa mkosa).

Daudi aliiona neema. na aliitamani...

Waebrania 11:39
[39]Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi;

Chini yake Mstati wa 9 hadi 12 Mwandishi anarudi kwa Ibrahimu kuwa alihesabiwa haki hata kabla ya Sheria ya Musa (torati) tena hata kabla ya kutahiri ili hao wasioishika sheria wala kutahiriwa ( mataifa) waipokee haki kwa njia ya imani juu ya ahadi ya Mungu. Tena akatahiri k**a agano ili hata awe baba yao pia wanaotahiri ( Wayahudi). Lakini yeye akahesabiwa haki kwa imani ( Kuna maelezo mengi Roho ananiambia nafupisha)

Tena mwandishi ili kuweka sawa zaidi akaelezea namna Ibrahimu alivyoamini juu ya ahadi ya kupata uzao k**a mchanga wa bahari ijapokuwa umri wake ilipata miaka 100 na mkewe Sarah alikuwa amekoma siku za k**e. Kwa njia hiyo Ibrahimu akalala bila kuiona ahadi lakini akamtumaini Mungu hata kufa. Hivyo akawa baba wa imani na leo ni baba wa mataifa. ( 4:18-22)

Nini maana yake?

Sisi tumeupokea wokovu wa bure kabisa ambao gharama Amelipa Kristo mwenyewe na kuhesabiwa haki kwetu si juu Tena ya matendo Mangapi mazuri au mabaya tumetenda tangu kuzaliwa ( K**a waaminivyo Waislamu) bali ni juu ya ahadi ya Mungu kutuokoa kwa kuwa tumemwamini mwanaye yeye aliye na ndugu yetu wa kwanza kati ya uzao wa wenye haki...

DADA IRENE:

Min Kazabao Edson asante kaka kwa mafafanuzi ya kunifungua! Nilipokua nachanganywa zaidi ni pale kwa tunahesabiwa haki kwa njia ya imani na sio kwa matendo ya sheria! Sasa nkawa nawaza kwamba hata ufanye uovu namna gani ukiendelea kufanya uovu lakini ukawa na imani kwamba Yesu ni Bwana na kuamini kwamba alimaliza yote pale msalabani basi unahesabiwa haki kwa io imani na sio yale matendo unayoendelea kuyafanya!

MAJIBU:

Ireen George Ukweli ni kwamba kwa habari ya Matendo ya sheria ( torati) hakuna mwanadamu hawezaye kuhesabiwa haki mbele za Mungu si mimi, Petro, Paulo, Daudi, Mchungaji wako, wewe au yeyote. Imani yetu juu ya Kristo mkamilifu ndio wokovu wetu.

Je, kwa kusema hivyo nimesema matendo si kitu?

La, sijasema hivyo...

Sisi tulio ndani ya Kristo tunaye Roho, msaidizi wetu. Yeye hutubeba katika udhaifu huu wa matendo yetu hata kuutia wema na haki mtembeo wetu katika mwili.

Twatenda mema si kwa sabsbu sasa imekuwa asili yetu bali kwa sababu yule aliye asili ya mema yu ndani yetu, akifanya hima kila wakati kutukumbusha yatupasayo kurenda ( Yoh. 16:13-14), naam yeye hututia hata katika kweli yote.

Sisi si wakamilifu k**a Baba isipokuwa kupitia ndugu yetu na mzao wa kwanza wa wakamilifu Yesu hivyo sasa tumekuwa wakamilifu. kupitia yeye ( Wakolosai 1:15-18, ufunuo wa Yohana 1:5)

Mathayo 5:48
[48]Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, k**a Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Ukichunguza huu mstari, Mwinjilisti Mathayo ananukuu Maneno ya Yesu ya Mahuniri ya mlimani namna ambayo Mkristo imempasa kuishi na kutenda ( Matendo yake). Ni namna ambayo kwa asili yetu ya mwili haiwezekani bali kwa Roho tu.

Basi tumekuwa wakamilifu kupitia huyu mjumbe wa mwisho Roho Mtakatifu.

Kuhitimisha!

1. Kristo hakuja kuitamgua torati bali kuhtimiza. Yeye alitimiza sheria yote, ili hao wamwaminio ijapokuwa hawakuitimiza yote wahesabiwe haki. Hiyo ndio inaitwa neema. Wokovu ni neema.

2. Neema hii yatufundisha kuukataa ubaya na kuishi kwa kiasi katika ulimwengu huu mwovu( Tito 2:11-12) na si kutufundisha tu, bali hata kututia nguvu ya kushinda tunapoomba (Luka 22:40 ).

3. Soma wewe...
Waefeso 2:8-10
[8]Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
[9]wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
[10]Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

JE, MATENDO MAFU KWA MWENYE IMANI HAYANA MADHARA KWA UMILELE WAKE AAMINIYE?

1. Hakikisha taa yako ina mafuta muda wote maana hujui ni siku gani atakayokuja mwana wa Adamu ( Math. 25: 1-13 )

2. Usilale kesheni ( Be watchful), jichunguze maana hujui siku wala saa ( Marh. 25:13)

3. Mathayo 5:16 na 1Petro 2:12
[16]Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

1 Petro 2:12
[12]Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.

Ubarikiwe!

Dr. Kazabao Edson

VITA VYA KIROHO [ Spiritual Warfare ]Nukiu muhimu kutoka kwangu..."Wakati Wokovu ni Zawadi tuliyopewa bure kutoka msalab...
27/04/2024

VITA VYA KIROHO [ Spiritual Warfare ]

Nukiu muhimu kutoka kwangu...

"Wakati Wokovu ni Zawadi tuliyopewa bure kutoka msalabani, Inahitaji WEREDI WA VITA kutawala na kumiliki kwa mwamini kabla ya ulimwengu ujao"

Andiko Rejea:

Waefeso 6:12
[12]Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya FALME na MAMLAKA, juu ya WAKUU WA GIZA hili, juu ya MAJESHI YA PEPO WABAYA katika ulimwengu wa roho.

ADUI NI NANI?

🛑1. SHETANI

Zekaria 3:1
Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na SHETANI amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.

1 Wathesalonike 2 : 18
Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na SHETANI akatuzuia.

Ni wazi kuwa vita yako kubwa k**a mwamini ni ile inayopiganwa moyoni ( The greatest battle a believer can face has its battlefield in the mind) katika kufanya maamuzi ya wema na ubaya.

Wakati Matendo mema au mabaya yanaweza kuwa au kutokuwa na madhara ya moja kwa moja kwa umilele wako bado kushindwa kuishi katika mema kutakuzuia uhalali na nguvu ya kutawala katika mwili na shetani atahakikisha mara zote unashindwa ili apate uhalali wa mashtaka yako.

Soma tena 1 Thes. 3:5

🛑2. MAMLAKA ZA GIZA.
Zimegawanyika katika makundi makuu 2

🎈A: VIIUMBE WASIO NA MIILI.

🔵i. WAKUU WA ANGA..

Danieli 10:12-13
[12]Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. [13]Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja.....

Hapo ni angani katika ulimwengu wa roho yuko mkuu wa giza (mfalme wa giza) anayetawala kuhakikisha maombi ya watakatifu walioko Uajemi hayazai kitu cha kumheshimisha Mungu...

NB: Najaribu kuandika kwa ufupi mno. Jitahidi kufikiri sana ili twende wote...

🔵ii. MAJESHI YA PEPO WABAYA

Huteka wa kipepo ( demonic possession) huvamia akili ya mtu (Mind) na hivyo kuathiri hisia (feelings), kumbukumbu (memory) na nguvu ya maamuzi (Will power). Mtu mwenye pepo ataugua ovyo (kwa savabu hana nguvu ya kiroho inayozuia magonjwa ), atachukua maamuzi ya hovyo na atafanya vitu ambavyo hata hapendi. Ni utendaji wa kipepo ndani ya mtu. Mtu kuwa shoga, malaya, kuua etc si Akili yake.

Magonjwa mengi ya akili, magonjwa ya kurithi na mengine mengi pamoja migogoro mingi ya ndoa ni kazi ya pepo wabaya. They simply control the mind....( Marko 10:1, 3:11-13, 6:7 Luka 4:36, 6:18, Matendo 8:7, 19:12.....)

Matendo ya Mitume 8:7
[7]Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa.

So, hawa uwete na kupoozwa kwao ilikuwa kwa sababu ya pepo wachafu ndani yao...tuko wote!

Baada ya kufanya kazi k**a tabibu kwa miaka sasa naweza kukiri wazi kwa ushahidi wa fikra zangu na macho yangu, kila ugonjwa huanzia katika ufahamu/moyo wa mtu na ikiwa pepo watapata nafasi humo mwili wa mtu umevamiwa.

Uzima wa moyo wa mtu ni afya mwilini mwake. Chochote kinachoweza kuingia katika ifahamu wako kinaweza kuharibu au kuuponya mwili wako....

🔵iii. FALME/ROHO KATIKA MAJI
[ Marine kingdom/Marine Spirits ]

Hizi ni roho za zinaa ( The spirits of lust) na kupenda fedha/mali ( covetousness) kuliko chochote.
Kwa pamoja tunaziita 'Mammons Spirits'na ziinafanya kazi kwa ukaribu mno na roho zidanyanganyazo ( seducing spirits).

Hizi roho ndio baba wa ushoga. ukahsba, uasherati katika nchi, kafara za mali na roho ya kupenda fedha hata kwa viongozi wa imani na Watakatifu ( 1 Tim 6:10)

🎈B: VIUMBE WENYE MIILI [ UZAO WA NYOKA ].

🔵i. WAKUU WA GIZA

Waefeso 6:12
[12]Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

[ For we wrestle not against flesh and blood, but against principalities, against powers, against the rulers of the darkness of this world, against spiritual wickedness in high places. ]

Wakuu wa giza ( Rulers of darkness )
Ni mfumo na watu kabisa wanaotumika kwa makubaliano na shetani ili kudhoofisha wana wa Mungu duniani. Mfano wa ni jamii zote za Siri ( Illuminat, Skull and Bones etc...) na wakuu wake ( Bahati mbaya wengine ni wakuu wa dini.)

Hawa ndio watawala wa ulimwengu huu. Hawa ndio remote ya ulimwengu na shetani anatawala kupitia wao. Ni mawaziri katika serikali yake.

Wanafanya kazi kwa ukaribu mno na mifumo mikuu ya dunia k**a UN na mashirika yake pamoja na mifumo yote ya vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, mifumo na Serikali za kila nchi.

🔵ii. FALME & MAMLAKA.

Ukisoma historia utagundua vita kubwa ya kanisa la kwanza haikuwa kitu kingine ila Falme na mamlaka za nchi k**a Rumi, Asia na Uyunani. Shetani akiwa adui yetu mkubwa mara nyingi atahakikisha anaweka watawala, wafalme na mamlaka inayoweza kumtii ili kukandamiza mfumo wa waamini.

Kwa kusema hivi, ni busara mno ikiwa moja ya maombi yetu itakuwa Mungu kuingilia kati kutuwekea watawala wasioweza kumtii ibilisi wala Amri kutoka kwa wakuu wa giza.

Nahitimisha nilichojifunza...

Nilikuwa najifunza, embu nisaidie zaidi hapa chini kwa kuelezea uelewa wako nijifunze zaidi..

Yesu akubariki...

Dr. Kazabao Edson

+255763575550

Sasa ukiwa na akili timamu unaweza kujiuliza maswali kadhaa:-i. Ni wapi imeandikwa tuuogope ulimwengu?2 Tim. 1:7Maana Mu...
13/03/2024

Sasa ukiwa na akili timamu unaweza kujiuliza maswali kadhaa:-

i. Ni wapi imeandikwa tuuogope ulimwengu?

2 Tim. 1:7

Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

[ For God hath not given us the spirit of fear; but of power, and of love, and of a sound mind.]

1 Yoh. 5:4
Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.

For whatsoever is born of God overcometh the world: and this is the victory that overcometh the world, even our faith.

ii. Je, tunazilinda roho zetu kwa kujiepusha na vyakula, mazingira na rangi za mavazi au kwa kuchunguza-chunguza wapi iliko 666?

iii. Je, Roho ndani yetu si hakika ya wokovu wetu?

Warumi 8:16,

Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

[ "The Spirit himself testifies (bear witnesses) with our spirit that we are God's children." ]

Kila unapoacha kumruhusu Roho au mtu akufundishe neno la Mungu kwa usahihi, naam ukiacha hata nodi moja tu hofu isiyo ya Mungu huzaliwa ndani yako, hakika ya wokovu wako itatiwa shaka kwa kuwa Roho hayupo na mashaka hayo utawajaza wanaokusiliza.

Ijapokuwa dalili hii nimeiweka mwishoni hata hivyo ni dalili ya mwanzo kabisa ya imani ambayo inaacha misingi na bado inakuwaga ya mwisho hasa kwa ukengeufu wa aina ya kiama ( Dooms-day cults).

Shetani ni mwerevu mno anapoleta uharibifu anaweza kuwafanya waamini wawe duni (kimuonekano, kifikra na kiushawishi) au akawafanya wajue kupitiliza mipaka na hivyo kuingia kiburi ( Mmeyaona haya kwa ndugu zangu wanaodai wanaijua mno neema)

Neno la Mungu halihitaji ulisaidie kulipazia sauti lilipokaa kimya au kulinyamazisha linapopiga kelele.

Extremity is a wrong game. There's always a biblical and universal standatd for every doctrine.

Msingi wa dalili hii ya 10 na ya mwisho ni kwamba, fundisho lolote linalokazia wewe kujitenga na watu (ulimwengu/mifumo), kazi au chochote kwa kudai vitakunyanganya wokovu wako ( hatima ya roho yako ) na huku Roho ndani hakushuhudii hivyo, sio fundisho la Kikristo.

Lakini usisahau Yesu anarudi upesi na mara wala sikushauri uupende ulimwengu ( 1Yoh. 2:15l Yesu azishuhudia kazi za Ulimwengu kuwa mbovu(Yoh. 7:7). Usiupende ulimwengu. Ishi kwa kiasi lakini si kwa hofu juu ya chakula na mavazi au kitu chochote kisichougusa usafi wa moyo wako

Yesu alijua tunaishi katika ulimwengu huu mbovu basi kila ukishikacho usiache kukifanyia ibada kabla ukitumie na hii si kwa ajili ya roho bali mwili. Kwa habari ya roho Kristo alishamwaga damu yake atunusuru na ulimwengu huu mbovu na uliojaa njama nyingi. Ishi kwa uhuru, neema na furaha tangu sasa. Furahini katika Bwana na Bwana tu, tena nasema furahini, mtu yeyote asikutie utumwani na katika hofu ya bure kwa elimu zake.

Wagalatia 1:3-4

Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, k**a alivyopenda Mungu, Baba yetu.

Ilinde nafsi yako kadri ya maongozi ya huyo Roho wa Bwana aliye ndani yako. Wala usiendelee kujifurahisha dhambini. Kristo ni Uhuru na uhuru ndani yake tu. Kristo ni amani na furaha. Ukikosa haya haupo kwa Kristo tena eh kondoo mwema, simama hapo hapo, ita, Bwana mwema akutafuta, amewaacha wale 99.

10. FUNDISHO KUHUSU NJAMA MBAYA (Fear of outside world & evil conspiracies )Umewahi kusikia mtumishi wa Mungu aliyekuwa ...
13/03/2024

10. FUNDISHO KUHUSU NJAMA MBAYA (Fear of outside world & evil conspiracies )

Umewahi kusikia mtumishi wa Mungu aliyekuwa vizuri kabisa ghafla anaanza kuwatisha watu?

Anawaambia ana ufunuo kuwa:-

Wasivae tena nguo nyeusi, wataenda motoni au ni za Freemason

Wasivae hiki au kile kwa kuwa ni vya shetani (Sitetei wale wasiojua kujistiri au wale hujipamba kupitiliza hadi inakuwa kero, kila mtimdo wanao)
Wasilale tena nyumbani mwao kwa kuwa huko shetani atawanasa.

Wasisalimiane na watu fulani.

Waache shule, kazi, ndoa n.k kwa kuwa huko wataanguka na mengine mengi.

Ghafla watu hawa huonekana duni kila kitu, wako nyuma ya kila teknolojia bora na kinachozaliwa ni kujitenga na kukaa mbali na watu kwa nia ya kulinda roho zao.

Mafundisho makubwa huwa ni njama ( conspiracy theories). Mtu aliyeacha njia ya Bwana atajitahidi kuonesha ulimwengu ulivyo kinyume naye na wafuasi wake tu. Mafundisho ya kulengwa kuonewa (Victim mentality ) au kufuatiliwa ili kudhulkwa ( Persecutory/ sierge mentality) huzaliwa pia.

Mafundisho yote hugeuka kuwa kiama ilivyokaribia na jinsi ulimwengu wote ulivyo wa shetani. Fundisho hili hutengeneza fikra kuu mbili. Mosi, wafuasi hujihisi hakuna mahali salama kwao zaidi ya pale walipo na wakitoka hapo wanaikosa mbingu. Mbili, wafuasi huhisi hakuna mtu mwingine anayeweza kuwaambia ukweli kuliko huyo. Tatu, Wafuasi huhisi hawatakiwi tena kujiendeleza (kielimu, kibinafsi, kibiashara, kindoa n.k) kwa kuwa mwisho umefika. Ni hatua hii watu huuza huacha shule, biashara na kuuza mali zote kumpa kiongozi wao na kuhamia kilingeni. Yanayofuata baada ya hapo huwa yanasikitisha mno.

Inaendelea...

9. KUKOSA UWAZI (Lack of transparency )🧱Mamlaka na aina ya mafundisho yasiyoweza kuhojiwa na mtu yeyote huibua mfumo wa ...
03/03/2024

9. KUKOSA UWAZI (Lack of transparency )🧱

Mamlaka na aina ya mafundisho yasiyoweza kuhojiwa na mtu yeyote huibua mfumo wa Siri wa uendeshaji. Hapo juu nimesema" Ghafla 'kilinge' hukosa uongozi maalumu. Kauli ya kwanza na ya mwisho huwa ni ni ya kiongozi mkuu tu ( One-man game)

Katika hatua hii uwazi katika matumizi ya fedha huibuka ghafla kwa kuwa hakuna anayeweza kuhoji tena. Ukengeufu na roho ya kupenda fedha ni mtu na pacha wake.

Katika hatua mbaya zaidi uwazi hupotea pia katika maadili. Ni katika hatua hii mtumushi wa Mungu huanza kumficha mkewe. Unaweza kufikiri hana mme/mke. Anaweza kutoa talaka na kanisa lisijue au likajua na asifafanue lolote, anaweza kutembea na mfuasi wake yeyote na ikiwa hajaoa basi balaa ni kubwa zaidi.

Ndugu yangu naomba ujue kuwa naandika haya kwa ajili ya kanisa ili mtu yeyote asipotee. Siandiki habari ya mtu yeyote wala siandiki kumfedhehesha mtu. Mambo haya nimejifunza muda mwingi mno nayo nimeyachunguza na kuona ni ya kweli kabisa. Naandika haya ili ikiwa utaona moja ya dalili hizi umsaidie ndugu yako katika Kristo bila kujali ukubwa wa matokeo yake.

Dalili moja muhimu ya ukengeufu ni kukosa uwazi wa kimahusiano na kifedha kwa kiongozi.

Naandika haya ili wewe mtumishi wa Mungu uilinde nafsi yako na wale wakusikilizao. Rudi nyumbani mpende mwenza wako na wanao, hapo ndipo kanisa linaanzia. Hakikisha nyumba yako wanajua kila kitu kukuhusu hasa mwenza wako. Hakikisha una uongozi na watu wanaoweza kukuhoji kuhusu mwenendo wako kimaadili na kifedha. Ni muhimu mno kwa usalama wa roho yako na wale wanaokufuata. Ok.

Uwe muwazi katika huduma yako ndani na nje ya kanisa. Kanisa ni taasisi, ni jamii ya watu (community based organization) sio duka lako. Jitahidi wewe, uongozi, wafuasi na walezi wako wote wanajua na kufurahia hatua za huduma yako. Sawa ndugu yangu!

Sasa tuendelee.

KUJIPA UPEKEE (Exclusivism)Wazushi huanza kwa kujitenga kifundisho na mara nyingi huyageukia mafundisho ya mashetani, ma...
29/02/2024

KUJIPA UPEKEE (Exclusivism)

Wazushi huanza kwa kujitenga kifundisho na mara nyingi huyageukia mafundisho ya mashetani, mapokeo/mafundisho ya wanadamu au mafundisho ya kwanza ya Ulimwengu (Rudiments of this world)

1Tim. 4:1
Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

[ Now the Spirit speaketh expressly, that in the latter times some shall depart from the faith, giving heed to seducing spirits, and doctrines of devils; ]

Wakolosai 2:8
Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure (Philosophy) na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu (tradition of men), kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu( Rudiments of this world) wala si kwa jinsi ya Kristo.

[ Beware lest any man spoil you through philosophy and vain deceit, after the tradition of men, after the rudiments of the world, and not after Christ.]

Watu wakianza kukengeuka huzusha mafundisho na tafsiri ambazo ni za kwao tu, zilizo elimu ya kibinadamu tu wala hazipatani na ufunuo wa kweli yote.

Lengo la mafundisho haya k**a nilivyotaja mwanzo huwa ni kufanikiwa kuwathibiti watu kiakili.

"Mtumishi huanza kuweka sheria ngumu kuzidi hata zile za Torati ya Musa. k**a za vichwani waweje, kimavazi ya kwao, k**a ni meupe huaminishwa ndio vazi la mbinguni lenye utukufu asijue kuwa unaweza vaa vazi jeupe na rohoni ukawa na gza, wengine marufuku mavazi ya maandishi. Wengine huenda mbali kukosoa hata biblia k**a kutoa ganda la nje jeusi" ( Maneno ya Kuhani Mwakalambo )

Lakini ghafla watu hawa hujaa kiburi na majivuno yaliyo kwa jinsi ya mwili kiasi kwamba mtu asiye wa dhehebu lao na asiyeenenda k**a wao humwona k**a mpagani na mchanga asiyejua kitu chochote.

Katika makala ya Kuhani Philemon Mwakalambo anaandika " Utaona mtumushi wa Mungu muda mwingi anaongea kuhusu mafunuo yanayozidi na kupita hata misingi ya kibiblia. Ukiona biblia anaanza kuiweka kando na kukosoa-kosoa ujue kaingiliwa na roho ya upotevu huyo"

Nataka nisisitize jambo moja muhimu hapa.

"Ujuzi wowote usiotokana na Roho Mtakatifu utakuletea kiburi usipokesha"

1Kor. 8: 1b..Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga.

[ ...Knowledge puffeth up, but charity edifieth.]

NB: Ukishakuwa mtu wa mafunuo memgi nje ya nuru yote ya neno la Mungu ni rahisi mno kuvamiwa na roho zidanganyazo (seducing spirits)

Hapo juu nimegusia mafundisho. Kuna aina kuu 4 za mafundisho katika maandiko matakatifu. Jitahidi ujipatie kijitabu changu cha FUNDISHO ili uweze kujiepusha na mafundisho potofu ya siku zetu hizi na uweze kufahamu nini unatakiwa kushika k**a Mkristo ili uwe salama. Ilinde nafsi yako na uharibifu.

1 Tim 4:16
Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.

MAJIGAMBO (Arrogance)

Wakati ambapo tatizo hili huge ukali kuwa hata tatizo la akili ( delusion of grandeur) bado Kuna uwezekano mtu aliyevamiwa na roho ya ukengeufu na wafuasi wake wakaanza kujigamba.

Kujipa upekee huzaa majigambo (Arrogance), majuvuno na kujisifu na mara nyingi huanzia kwa kiongozi kwenda kwa wafuasi.

Biblia inasema "Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani" (1Sam.2:3)

Linaweza kuibuliwa fundisho maalumu la kuwaonyesha yeye na wote wanaomfuata ni malaika, viumbe maalumu wasio k**a binadamu wengine (Kitu ambacho ni sahihi, kiumbe mpya si mwanadamu wa kawaida, ila anatakiwa kuishi na wanadamu kawaida huku akiwavuta kwenye asili yake k**a Yesu alivyofanya).

Kiongozi anaweza kujipa cheo chochote hata kisichopatana na maandiko.

Hujiinua na kujivuna kuwa tofauti kabisa na mwanadamu wa kawaida. Anaweza kujiita mungu, yesu, Eliya au jina lolote na ukiona hivi ujue uharibifu wake umefika mwisho kwani Mungu hana kawaida ya kuwavumilia watu wa hivi.

Zab. 101:5b
Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitavumilia naye.

Utawaona wafuasi wakibishana na kila mtu njiani na kila penye mijadala wakijionyesha wao kuwa bora kuliko mtu yeyote na si kumvunia Bwana roho zinazopotea. Tabia hii ya kuwaona hawa waamini wenzao wamepotea na kupungua mno ndio hupelekea kujitenga au kutengwa mbali na jamii ya watu wao.

Ndugu yangu Mungu hakupendi wala kukuhesabu mwenye haki kuliko wengine kwa sababu wewe ni mwema na unatenda matendo mazuri kuliko wengine, bali kwa kuwa umemwamnini, yatosha!

War. 3:27
Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani.

[ Where is boasting then? It is excluded. By what law? of works? Nay: but by the law of faith.]

Yeyote aliyemwamni Kristo ni mtu bora mno, unaweza kuwa na matendo mengi nazuri unayotahidi kufanya lakini ikiwa hukumwamini Kristo, huna uzima wa milele. Kwahiyo imetupasa kuishi maisha matakatifu na ya utauwa kadri ya neema ya Kristo ndani yetu bila kuwahukumu kuwa si kitu wale waliopungua katika matendo ).

Shina moja la uharibifu si kupenda fedha tu bali hata kiburi na wanae yaani majigambo na majivuno. Bwana hawapenda wanyenyekevu, huwapinda wenye kiburi na dharau.

Haya sio maneno yangu ni maandiko matakatifu. K**a unadharau watu, huna akili.

Mithali 11:12

Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.

[ He that is void of wisdom despiseth his neighbour: but a man of understanding holdeth his peace.]

1 Tim 6:3_4
Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa,amejivuna; wala hafahamu neno lo lote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya;

1 Petro 5:5
Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.

Katika sura ya nne tutaangalia kwa undani aina za mafundisho kibiblia na athari zake.

HEBREW WOMEN FOUNDATION *Empowering Women to Lead, Serve, and Transform**INTRODUCTION*Imagine if the world were filled w...
17/02/2024

HEBREW WOMEN FOUNDATION

*Empowering Women to Lead, Serve, and Transform*

*INTRODUCTION*

Imagine if the world were filled with women like Kathyln Kuhlman, Marie Woodworth-Etter, Joyce Meyer, Felix Funke Adejume, Ruth Natasha, and Rose Shaboka of Tanzania. Their impact would be immeasurable, their influence profound, and their legacy everlasting. The Kingdom would surely flourish, hearts would be healed, and lives transformed. It is with this vision in mind that the HW Foundation emerges—a beacon of hope, a catalyst for change, and a nurturing ground for women destined to make a difference. With a mission to cultivate leaders, empower souls, and ignite the flames of passion and purpose, the HW Foundation stands as a testament to the power of women and their ability to shape the world for the better.

In Exodus chapter 3 verse 19, we see a powerful example of courage and resilience displayed by the Hebrew women in the face of adversity. Despite the oppressive circumstances they found themselves in, these women refused to succumb to fear or despair. Instead, they exhibited remarkable bravery and determination, even in the midst of great danger.

The significance of this passage extends far beyond its historical context—it speaks to the timeless truth that courage and faith are essential qualities for overcoming adversity and fulfilling our destinies. Just as the Hebrew women stood firm in their convictions and defied the oppressive decree of Pharaoh, so too must we, as modern-day women, be steadfast in our faith and unwavering in our pursuit of our God-given visions and dreams.

The Hebrew Women Foundation draws inspiration from the courage and resilience of these women, aiming to empower and equip women today to boldly pursue their visions and aspirations, regardless of the challenges they may face. Just as the Hebrew women refused to allow their children to be destroyed, so too must women today fiercely protect and nurture the dreams and destinies entrusted to them by God.

Through the Hebrew Women Foundation, women are encouraged to embrace their strength, resilience, and inherent worth as daughters of the Most High. They are equipped with the tools and resources needed to navigate life's challenges with courage and confidence, knowing that they are supported by a community of like-minded sisters who are committed to seeing them thrive.

In essence, Exodus chapter 3 verse 19 serves as a powerful reminder that with God's strength and guidance, women have the power to overcome any obstacle and fulfill their divine calling. Just as the Hebrew women defied Pharaoh's decree and preserved their children's lives, so too can women today rise above the forces that seek to hinder their progress and extinguish their dreams. Through faith, determination, and a commitment to supporting one another, women can truly become agents of change and transformation in their families, communities, and beyond.

The HW Foundation under Kingdom Enlightenmed Network acknowledges the profound impact of some vital factors on the minds and behaviors of women in our generation. We recognize four primary channels through which the mind gets affected with the aim of letting the light in for transformation.

*1. Informations*

What we hear influences our thoughts and decisions. Prolonged exposure to negative or destructive information can lead to detrimental life choices, such as single motherhood or engaging in unacceptable behaviors. Faith, life and death are born of information thats the bible says Faith comes by hearing ( insert the respective Bible verse here) and life and death are within the power of tongue ( insert the respective Bible verse here). Human achievement os an average of informations he has. So the more righly informed and spritually enlightened are unlikely to fall into destruction sre demonic traps.

*2. Relationships:*

The relationships women form, whether intimate or platonic, play a significant role in shaping their experiences and outcomes while at colleges and campuses. Intimate relationships, in particular, can have profound effects on women's lives, often leading to distractions and deviations from their vision. Unhealthy or toxic relationships may result in unwanted pregnancies, abortions, and single motherhood, as well as spiritual backsliding and loss of focus. We must be mindful of the boundaries we set and the influences we allow into our lives through emotional and physical contact.

However, it's not only intimate relationships that pose a risk. Friendships with peers, whether of the same or opposite s*x, also play a crucial role in influencing women's behaviors and decisions. Bad peer influence and negative friendships can lead women astray, encouraging them to engage in behaviors that are detrimental to their well-being and future aspirations. Peer pressure to conform to societal norms or engage in risky behaviors can undermine women's confidence and self-worth, leading them to abandon their vision and compromise their values.

Therefore, it's essential for women to cultivate healthy, supportive relationships that uplift and empower them to pursue their goals and aspirations. Surrounding oneself with positive influences and like-minded individuals can help women stay focused on their vision and navigate the challenges of college life with resilience and determination.

By addressing the influence of relationships on women's lives, the Hebrew Women Foundation aims to equip women with the knowledge and resources to make informed choices and cultivate meaningful connections that contribute to their personal and spiritual growth.

*3. Visual stimuli.*

Our visual environment shapes our perceptions and attitudes. We must be discerning about what we expose ourselves to, as not all content is beneficial or conducive to our well-being. When it comes to visual stimuli, it's important to recognize the significant influence that movies, advertisements, and online content can have on women's lives, particularly during their time at universities or colleges. Many women are exposed to a variety of media, including movies and online videos, which may contain content that promotes harmful behaviors or ideologies.

Some movies contain advertisements or subplots that normalize unhealthy behaviors such as substance abuse, promiscuity, or even homos*xuality. Additionally, the accessibility of online po*******hy poses a significant risk, as some women may succumb to peer pressure or curiosity and end up consuming pornographic content, which can have detrimental effects on their mental, emotional, and spiritual well-being.

As an organization focused on the spiritual growth of born-again women, the HW Foundation aims to educate and empower women to be discerning and selective about what they watch and consume visually. We emphasize the importance of guarding one's heart, as the Bible teaches that the heart is the spring of life. By being mindful of the content they expose themselves to, women can protect their hearts and minds from negative influences and stay focused on their spiritual journey and vision for the future.

Through education, mentorship, and support, the HW Foundation equips women with the knowledge and tools they need to make wise choices about what they watch, ensuring that their visual consumption aligns with their values and aspirations. By promoting discernment and mindfulness in their viewing habits, we empower women to cultivate a positive and uplifting visual environment that contributes to their spiritual growth and well-being.

*4. Intuition:*

Our inner thoughts and instincts guide our actions. Renewing our minds involves evaluating our thought patterns and aligning them with our vision for a purposeful and impactful life. HW Foundation delve into the importance of renewing our minds and how it relates to empowering women to achieve their vision and overcome daily challenges.

HW Foundation prioritize the profound importance of renewing our minds as we navigate through life's journey. The concept of renewing our minds is deeply rooted in Scripture, and it holds tremendous significance for our spiritual growth and well-being.

In Romans 12:2, the apostle Paul exhorts us, "Do not conform to the pattern of this world, but be transformed by the renewing of your mind. Then you will be able to test and approve what God’s will is—his good, pleasing and perfect will." This verse highlights the transformative power of renewing our minds. It calls us to reject the mindset of the world and instead embrace a renewed perspective that aligns with God's will for our lives.

Renewing our minds involves a deliberate process of replacing negative thoughts, attitudes, weak doctrines and beliefs with God's truth and wisdom. It requires us to immerse ourselves in Scripture, prayer, and fellowship with other believers, allowing the Holy Spirit to transform our thinking and shape our perspectives.

The renowned theologian John Calvin once wrote, "The mind of man, though naturally confined to a narrow compass, is nevertheless, capable of transcending the limits of the world, and of learning by the Word of God the things which are in heaven." This profound insight reminds us that through the renewal of our minds, we gain access to divine wisdom and understanding that surpasses worldly knowledge.

Renewing our minds is not merely a cognitive exercise; it is a spiritual discipline that empowers us to discern God's will and navigate life's challenges with clarity and confidence. As women of faith, we are called to cultivate a renewed mind that is grounded in truth, filled with hope, and guided by the Holy Spirit.

The HW Foundation is committed to enhancing women's intuition, thought processes, and inner transformation through the power of renewing our minds. We provide resources, support, and guidance to help women immerse themselves in Scripture, prayer, and spiritual disciplines, enabling them to overcome daily challenges and pursue their God-given vision with courage and conviction.

As we embark on this journey of renewing our minds together, let us draw strength from the words of the psalmist in Psalm 119:105, "Your word is a lamp for my feet, a light on my path." May the light of God's truth illuminate our minds and guide us on the path of righteousness, enabling us to fulfill our purpose and impact the world for His glory.

The HW Foundation aims to transform women's lives by addressing these channels of influence, empowering them to live lives of vision, impact, and spiritual fulfillment. Through education, mentorship, and support, we seek to equip women to navigate the challenges of modern life with wisdom and resilience.

Join us on this journey of enlightenment, empowerment, and transformation, as we strive to unleash the potential of women and pave the way for a brighter tomorrow

*MISSION STATEMENT*

The HW Foundation is dedicated to raising a generation of spiritually, mentally, and socially strong Christian women who will lead, serve, and transform their communities. Drawing inspiration from Exodus 1:19, our mission is to nurture women who are as lively and resilient as the ancient Hebrew women, capable of overcoming the challenges of our modern world with grace and strength.

*VISION STATEMENT*

Our vision is to create a world where women are empowered to live lives of purity, purpose, and service to the body of Christ. We aim to reduce the prevalence of single motherhood, abortion, and moral decay among women on campuses and in communities, while increasing female leadership and participation in ministry both locally and globally.

*OBJECTIVE*

1. To provide spiritual guidance and mentorship to women on campuses and in communities, helping them grow in their faith and relationship with God.

2. To address the unique challenges faced by women in academic settings through biblical teachings and discussions, fostering a supportive community of like-minded women.

3. To promote s*xual purity and holistic well-being among women, equipping them with the knowledge and resources to make healthy choices in their relationships and lifestyles.

4. To encourage women to actively engage in ministry and leadership roles within the body of Christ, empowering them to use their gifts and talents for the kingdom's work.
5. To collaborate with existing fellowships and organizations on campuses and in communities, uniting women across different backgrounds and denominations for mutual support and growth.

*PLAN OF ACTION*

HF Foundation involves reaching out to various universities, campuses, churches, villages, and schools to raise awareness and provide both spiritual enlightenment and counselling to women. This will be accomplished through conducting seminars, country crusades, and gatherings specifically targeted at young and middle aged women.

Additionally, seminars will also be held in churches to teach and preach to women, helping them renew their minds and focus on their goals despite the challenges they face. By reaching out to diverse settings and communities, the foundation aims to empower women from all walks of life and provide them with the resources they need to succeed through their mind transformations.

*LEADERSHIP STRUCTURE.*

Chairperson:
- The chairperson serves as the overall leader and organizer of the foundation.

- Responsibilities include coordinating activities, overseeing meetings, and representing the foundation in external matters.

- The chairperson will be chosen from among the fellowship leaders at various university campuses.

- Term of office: [ one year, renewable ]

Vice-Chairperson:
- The vice-chairperson will assists the chairperson in her duties and assumes leadership in her absence.

- Responsibilities include supporting the chairperson in organizing events, facilitating communication, and assisting with decision-making.

- The vice-chairperson will also be selected from among the fellowship leaders.

- Term of office: [one year, renewable]

Secretary:
- The secretary is responsible for maintaining accurate records of meetings, correspondence, and other administrative tasks.

- Responsibilities include taking meeting minutes, managing communication channels, and handling official documentation.

- Term of office: [one year, renewable]

*Treasurer:*
- The treasurer will oversee financial matters, including budgeting, fundraising, and financial reporting.

- Responsibilities include managing funds, tracking expenses, and ensuring compliance with financial policies and procedures.

- The treasurer will be entrusted with the safekeeping and management of the foundation's finances.

- Term of office: [one year, renewable]

*CONSTITUTION *

**Article I: Name and Purpose**

1.1 Name: The name of the organization shall be the E-Burimani Foundation, hereinafter referred to as the "Foundation."

1.2 Purpose: The purpose of the Foundation is to empower women through education, mentorship, and community engagement, with a focus on fostering spiritual growth, leadership development, and social impact.

*Article II: Vision and Mission*

*2.1 Vision:*
The Foundation envisions a world where women are empowered to realize their full potential and make meaningful contributions to society.

*2.2 Mission:*

The mission of the Foundation is to provide women with resources, support, and opportunities to thrive academically, spiritually, and professionally, thereby equipping them to lead with integrity and compassion.

*Article III: Leadership Structure*

3.1 Chairperson: The Foundation shall be led by a Chairperson, who shall oversee the organization's operations, provide strategic direction, and represent the Foundation in external matters.

3.2 Vice Chairperson: The Vice Chairperson shall assist the Chairperson in their duties and assume leadership in their absence, supporting the implementation of the Foundation's initiatives and programs.

3.3 Treasurer: The Treasurer shall be responsible for managing the organization's finances, including budgeting, fundraising, and financial reporting, ensuring transparency and accountability in all financial matters.

3.4 Secretary: The Secretary shall maintain accurate records of meetings, correspondence, and administrative tasks, facilitating communication and documentation for the Foundation's activities and initiatives.

3.5 Coordinator: The Coordinator shall oversee the implementation of various initiatives and activities across campuses and communities, mobilizing resources, engaging stakeholders, and maximizing the impact of the Foundation's programs.

*Article IV: Membership*

4.1 Membership: Membership in the Foundation shall be open to all individuals who support the mission and vision of the organization, regardless of gender, race, or background.

4.2 Responsibilities: Members shall actively participate in Foundation activities, promote its goals and objectives, and adhere to the principles of integrity, respect, and collaboration.

*Article V: Meetings and Governance*

5.1 Meetings: The Foundation shall hold regular meetings with the founder to discuss progress, make decisions, and plan future initiatives, with meeting agendas and minutes documented and distributed to members.

5.2 Governance: The Foundation shall operate in accordance with its mission, vision, and values, guided by principles of transparency, accountability, and ethical conduct.

*Article VI: Amendments*

6.1 Amendments: Any amendments to this constitution shall require a two-thirds majority vote of the Foundation's members, with proposed changes circulated in advance and discussed at a meeting before voting takes place.

*Article VII: Dissolution*

7.1 Dissolution: In the event of the Foundation's dissolution, any remaining assets shall be distributed to charitable organizations with similar missions, as determined by the Foundation's leadership and in accordance with applicable laws and regulations.

*Article VIII: Adoption*

8.1 Adoption: This constitution shall be adopted upon approval by the Foundation's members and shall serve as the governing document for the organization's operations and activities.

COUNTRY LEADERSHIP

Chairperson
Dr. Nice Zakaria
Phone: +255711298629

Vice Chairperson
Esther Mpollo
Phone: +255769622962

Secretary
Godbetter Simboy
+255743026209

Treasurer
Favour Raheem
+255629774185

Coordinator
Dr. Lydia Mwaikole
+255747696473

Contact us:
Hebrew woman Foundation
Email: hebrewomanfoundation .con
Phone:
Website:

Kingdom Enlightened Network Global ( KEN Global )
Phone: +255763575550
Email: [email protected]

Address

Mbeya Zonal Referal Hospital
Mbeya

Telephone

+255763575550

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Casfeta-Tayomi UDSM MCHAS posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Casfeta-Tayomi UDSM MCHAS:

Share