04/03/2019
(R I P) Yako mengi yanayotuchanganya hapa duniani na wengine tunaiga bila kujua yatokako, maana na faida yake, ilimladi ni fashion tu kwa wakati huo tunaiga tusionekane wahenga au washamba.
*R.I.Pāā*
!
*"PUMZIKA KWA AMANI" ā*
JE KUNA AMANI IPI KABURINI?
MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI.
HUKO MAHALA PEMA NI WAPI, NA JE! WAPO WASIOLALA MAHALA PEMA HUKO PEPONI?
*UTANGULIZI*
Limekuwa ni jambo la kawaida kuwaambia ndugu zetu waliolala ( wafu) wapumzike kwa amani ( R.I.P) na wengine wakaenda mbali zaidi kumsihi Mungu azilaze Roho hizo mahali pema, kibaya zaidi ni pale tunapoonesha Mungu akikupenda ati lazima akuue kwa msemo "TULIKUPENDA LAKINI MUNGU KUKUPENDA ZAIDI" Je! Mungu akikupenda lazima akuue, au ufe ili akuchukue?
BIBLIA INASEMA WAFU WAKO WAPI???
Mwanzo 3: 1 *"Kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi"*
Biblia inasema "WAFU WOTE WAPO MAVUMBINI HAIJALISHI WALITENDA MEMA AU MABAYA WANASUBIRI YESU AJAPO KUTOA HUKUMU"
R.I.P ( PUMZIKA KWA AMANI)
JE KUNA AMANI YEYOTE KABURINI MTU ANAPOKUFA? Muhubir 9:5 "Lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa"
WAFU HAWAJUI NENO LOLOTE WALA HAWANA MAWAZO WALA KUMBUKUMBU YA CHOCHOTE NI K**A MEZA, JIWE NA VIUMBE VYOVYOTE VISIVYO HAI! KWAHIYO KUWAAMBIA WALALE MAHALI PEMA HAKUNA WEMA WALA GHASIA KABURINI. WAFU WOTE HAWAJIELEW!!
JE TUKIWAOMBEA WAFU WANAWEZA KUFANYA TENA IBADA?* KUTUOMBEA?? AU TUKIWAOMBEA MUNGU ANAWEZA KUWASAMEHE? Zaburi 115.17 "Sio wafu wamsifuo BWANA, wala wo wote washukao kwenye kimya"
Zaburi 143:4 "Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake,Siku hiyo mawazo yake yapotea"
Mhubiri 9:10 "Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe"
HITIMISHO
O1. R.I.P.( PUMZIKA KWA AMANI)
Huu ni msemo wa kipagani tena unaokinzana na maandiko maana wafu hawajui chochote hivyo hakuna amani yoyote kaburini mfu hajitambui hajielew ni k**a kochi au peni hana ufahamu. Kwa hiyo kumwambia apumzike kwa amani ni kuongea na asiekusikia wala hajui uongeacho, mtendee mema kabla hajafa.
O2. MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI
a) Mungu hapangiwi pa kumuweka mfu, wala hana ghala au store ya kutunza waliokufa, wafu wote huozea kaburini ndiyo maana ya "mavumbi kuyarudia mavumbi"
b) Mfu akifa anarudi kuwa udongo
O3. MFU HAWEZI KUKUOMBEA WALA KUOMBEWA DHAMBI ZAKE ZIISHE
a) Wafu hawawezi kutuombea sio bikra Mariam mama wa Yesu wala mtakatifu yeyote aliyekwisha kufa anaweza kutuombea Kwa Mungu, Biblia inasema tuombe kwa jina la Yesu pekeee.. (Wafilipi 2:10)
b) Mtu akifa historia yake imefungwa hawezi kuombewa dhambi zikamtoka,
c) Ibada na maombezi ni kwa walio hai tu
IBADA ZA KUOMBEA WAFU NI UPAGANI NA MACHUKIZO KWA BWANA
WITO:
TUMKIRI YESU NA KUMFUATA TUKIWA HAI ILI HATA TUKIFA TUWE NA TUMAINI KUWA AJAPO MARA YA PILI ATATUPA MIILI YA KUTOKUHARIBIKA NA TUTAISHI NAE MILELE..!!
1 Thesalonike 4: 13 - 17 "13 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika k**a na wengine wasio na matumaini.
14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele."
Nakuachia swali la changamoto:
*K**a ibada ya kumuombea mfu ina maana kuna umuhimu gani wa kumtumikia Mungu ukiwa hai si usubiri tu ukifa uombewe dhambi zitoke? Je, nani atapewa adhabu ya moto na kupotea milele wakati wafu wote huwa wanaombewa?
Ebrania 9:27...... baada ya kifo ni hukumu.......
USINGOJEE KUFA ILI UOMBEWE AMUA LEO KUMFUATA YESU KRISTO AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO, LIPO TUMAIN NG'AMBO YA KABURI, HERI WAFU WAFAO KTK BWANA YESU.
ACHA KUDANGANYWA ATI UFANYE MAOVU YOTE MWISHO UOMBEWE TENA KWA KUMLAZIMISHA MUNGU AKULAZE PEMA PEPONI, HILO HALIPO HAKIKA, HATA WASWAHILI HUSEMA "SWALI KABLA HUJASWALIWA" HII HUMAANISHA IBADA YAKO KWA MUNGU NI MUHIMU KULIKO YA SIKU YA MAZISHI YAKO, IBADA INAYOFANYIKA KATIKA HUDUMA YA MAZISHI NI KWA AJILI YA WALIO HAI WATAFAKARI NJIA ZAO KABLA YA KIFO.
APANDACHO MTU NDICHO UTAKACHO VUNA
TAFAKARI.....