RhapsodyMan

RhapsodyMan Influencing the world with the rhapsody of realities, reaching the unreached , touching the untouched.

Preaching the gospel using the world number one daily devotional.

Uzima wa milele... Uzima wa Mungu.
31/05/2024

Uzima wa milele... Uzima wa Mungu.

Listen to "Alikuja kwetu katika Roho Mtakatifu.mp3" from Amedeus Live on Anchor:
21/02/2024

Listen to "Alikuja kwetu katika Roho Mtakatifu.mp3" from Amedeus Live on Anchor:

Elewa muunganiko wa Bwana wetu Yesu Kristo na Roho Mtakatifu, ni muunganiko wa Ajabu na kipekee. Bwana Yesu ni mfariji aina ile ile k**a Roho Mtakatifu, hao wawili ni kitu kimoja. Roho Mtakatifu ni Baba aliyekuwa ndani ya Bwana Yesu, yeye ndiye Bwana Yesu alikuwa akishuhudia kwamba nayatenda yale ni...

15/02/2024

╔════════════════╗
RHAPSODI YA UHAKIKA
KWA WASOMAJI WA AWALI
╚════════════════╝

👤MCHUNGAJI CHRIS

Alhamisi 15

UNAWEZA KUONA NINI?

Tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele (2 Wakorintho 4:18).

K**a unahisi dalili za homa mwilini mwako, je, mara moja unajiona mwenyewe hospitalini au ukiyakosa masomo shuleni? Au je, unatunza akilini picha ya uponyaji na ukamilifu wako, bila kujali jinsi unavyoweza kuwa na unahisi?

Musa alipotuma watu kumi mbili kwenda kuipeleleza Kanaani, ni Yoshua na Kalebu tu walioona ushindi; wale kumi waliobaki waliweza tu kuona matatizo na kushindwa (Hesabu 14:9). Yoshua na Kalebu walitazama kwa macho ya imani na kuona uwezekano.

Jifunze kuona kwa macho ya imani, licha ya hali inavyoweza kuonekana kuwa ngumu kiasi gani. Kumbuka, “…K**a ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye.” (Marko 9:23 NEN). Kwa hiyo, jizoeze mwenyewe kuona uwezekano tu; ona mafanikio, uponyaji, na ushindi.

📖ANDIKO LA KUSOMA
1 Yohana 5:4

🔉SEMA HIVI
Kwa macho ya imani, ninaona uwezekano wa mafanikio, uponyaji, na ushindi. Haleluya!

Sala Ya Wokovu
“Ee Bwana Mungu, ninamwamini kwa moyo wangu wote Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Ninaamini kuwa alikufa kwa ajili yangu na kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Ninaamini kuwa yu hai leo hii. Ninakiri kwa kinywa changu kuwa Yesu Kristo ni Bwana wa maisha yangu kuanzia leo. Kupitia Yeye na katika Jina Lake, nina uzima wa milele; nimezaliwa upya. Ahsante Bwana, kwa kuiokoa nafsi yangu! Sasa, mimi ni mwana wa Mungu. Haleluya!”

Upeleke kwenye kiwango kingine ushiriki wako kwenye Injili kwa kushiriki kwenye ReachOut World Extrvaganza na Mchungaji Chris. Anza sasa hapa bit.ly/RoWLive

Dhamini usambazaji wa Rhapsodi ya Uhakika: Anza leo hapa👉🏾
http://services.tniglobal.org/?center=eastafricacenter4

Jiunge nasi kujifunza Neno la Mungu
WhatsApp:
https://chat.whatsapp.com/FuQEUI0Yg7P0C0mOOkGGd7

Lisikilize Neno la Mungu kwako
Tumeitwa Kutumika https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Tumeitwa-Kutumika-e2e2uld

Vurugu na Hasira-TeeVo
https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Kataa-Vurugu-na-Hasira---Rhapsodi-TeeVo-e2e2v0c

Kuangaza Kupitia Roho Mtakatifu
https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Kuangaza-Kupitia-Roho-Mtakatifu-e2e537d

Yesu Kristo - Wasifu wa Mungu https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Yesu-Kristo---Wasifu-wa-Mungu-e2e9t01

Uchunge Ulimi Wako https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Uchunge-Ulimi-Wako-e2e9sq7

Lulu nzuri na ya Thamani https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Lulu-nzuri-na-ya-Thamani-e2e9slo

Haki inakufanya Jasiri https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Haki-inakufanya-Jasiri-e2ebl4m

Alibatilisha Mauti https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Alibatilisha-Mauti-e2ef5iq

Hamna Haja Wasiwasi https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Hamna-Haja-Wasiwasi-e2egm8e

Yeye Yuko Juu ya Yote https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Yeye-Yuko-Juu-ya-Yote-e2eqgoo

Kuinuliwa Kwako https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Kuinuliwa-Kwako-e2ev7co

Angaza k**a Mwanga https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Angaza-k**a-Mwanga-e2evlf7

Maisha Bora https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Maisha-Bora-e2fa6s3

Kuishi katika Jina lake Lisiloshindwa https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Kuishi-katika-Jina-lake-Lisiloshindwa-e2fchh4

Tiketi ya Kupokea kila Baraka https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Tiketi-ya-Kupokea-kila-Baraka-e2ffjbl

Vitu vyote vipi chini ya Miguu yako https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Vitu-vyote-vipi-chini-ya-Miguu-yako-e2fld52

Afya Njema ni Haki Yako. https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Afya-Njema-ni-Haki-Yako-e2flrb3

Mito ya Uponyaji https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Mito-ya-Uponyaji-e2fchco

Tufuatilie
https://amedeuslive.blogspot.com/2024/01/dhamini-teevo-leo.html

Mungu akubariki

Listen to the most recent episode of my podcast: Yesu Kristo - Wasifu wa Mungu https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Ye...
12/01/2024

Listen to the most recent episode of my podcast: Yesu Kristo - Wasifu wa Mungu https://anchor.fm/amedeuslive/episodes/Yesu-Kristo---Wasifu-wa-Mungu-e2e9t01

Inapatikana kwenye castbox, google podcast, Amazon music and Spotify.

Mgundue Bwana Yesu kwa viwango vya juu zaidi na vipya mbali zaidi ya ulivyokuwa unamdhania au kumfikiria. Yesu ndio wasifu wa halisi wa Mungu. Yesu ndiye taswira ya halisi ya Mungu Baba, ukimwona Yesu umemwona Mungu Baba. Jifunze zaidi katika rhapsodi hii ya leo, toleo ya Watu wazima. Tafakari kweli...

Listen to the most recent episode of my podcast: Kataa Vurugu na Hasira - Rhapsodi TeeVo
06/01/2024

Listen to the most recent episode of my podcast: Kataa Vurugu na Hasira - Rhapsodi TeeVo

Usiruhuru Harisa wala Vurugu zikutawale. Wewe ni mwenye haki wa Mungu ndani ya Kristo Yesu.... hii ndio asili yako. Sikiliza kweli hii kutoka katika Rhapsodi ya Uhakika Teevo, kitabu mahususi kwa ajili ya Teenegers, kinachoandikwa na Mchungaji Chris Oyakhilome. Wasiliana nasi kwa namba hizi kupata n...

Habari za Leo mpendwa katika Bwana. Tafadhali kila Mmoja wetu naomba ahusike kwa kadri ya neema ya Mungu maishani mwako....
21/06/2023

Habari za Leo mpendwa katika Bwana. Tafadhali kila Mmoja wetu naomba ahusike kwa kadri ya neema ya Mungu maishani mwako. Tuchapishe na kusambaza nakala hizi, watoto wetu katika shule za msingi na walioko mitaani wanapaswa kupata nakala hizi, tunawekeza kwenye kesho ya familia zetu, jamii na taifa letu!
Nakala moja ni sh.5000, (ni colored printed kwa sababu ya vikaragosi vilivyotumika kuwasilisha Ujumbe kwa rika hili).
Inawezekana wewe ni *Mwalimu wa Sunday school au kiongozi katika Kanisa la watoto, au muumini wa kawaida, mzazi au mlezi* tafadhali fanya kitu, hamasisha wengine pia wachangie na wahusike kwenye kampeni hii! Kila vitabu viwili utakavyolipia tutakupatia kimoja! Hii ni kwa sababu tunakwenda mashuleni na uhitaji ni mkubwa Sana wa vitabu hivi.
Tumia lipa namba hii: 8177098 kuwasilisha mchango wako.
Mungu akubariki sana kwa kushiriki katika kampeni ya Uinjilisti kwa watoto wetu.

*Sasa unaweza Kudhamini uchapishaji na usambazaji wa nakala hizi za rhapsodi ya Uhakika kupitia code namba: 8177098**ANZ...
05/06/2023

*Sasa unaweza Kudhamini uchapishaji na usambazaji wa nakala hizi za rhapsodi ya Uhakika kupitia code namba: 8177098*

*ANZA NA UJUMBE WA UPENDO*

Jumatatu, 05

Mchungaji Chris Oyakhilome, PhD

_*“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”*_ Yohana 3:16

Wakati wa kuhubiri Injili, baadhi ya Wakristo hukazia hasa somo la dhambi, wakikazia uhitaji wa watu kutubu dhambi zao. Ujumbe wa toba uliwafaa Wayahudi kwa sababu walikuwa chini ya Sheria. Kilichotakiwa kutoka kwao ni kugeuka kutoka katika uovu walipofanya dhambi, na kumwelekea Mungu.

Hata hivyo, wasio Wayahudi—yaani Mataifa—hawakuwa na kitu chochote cha kugeuka kwa sababu hawakuwa kamwe chini ya Sheria, ambayo (Sheria) yenyewe, ilikuwa hukumu yao. Biblia inasema, _*“Maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria”*_ (Warumi 5:13).

Ndiposa, Biblia inasema, _*“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”*_ (Warumi 3:23). Hii inajumuisha Wayahudi na Wamataifa. Ikiwa watu wa mataifa mengine hawakuvunja Sheria kwa sababu hawakupewa, je, dhambi yao ilikuwa wapi?

Tunajifunza katika kitabu cha Mwanzo kwamba Mungu alipowaumba Adamu na Hawa, walikuwa kwenye uwepo wa Mungu mtakatifu. Waliishi katika utukufu Wake. Lakini walikatiliwa mbali na utukufu huo Adamu alipomtenda Mungu dhambi.

Warumi 5:19 inasema, _*“Kwa sababu k**a kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.”*_ Kupitia kosa la mtu mmoja, watu wote walipungukiwa na utukufu, lakini sasa, katika Kristo, utukufu unarejeshwa. _*“…Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu”*_ (Wakolosai 1:27). Haleluya!

Hii ndiyo sababu mkakati wako wa Injili hupaswi kuanza na suala la dhambi; badala yake, unapaswa kuanza na ujumbe wa upendo. Huo ndio ufunguo; hivyo ndivyo Yesu alivyoiweka katika mstari wetu wa ufunguzi. Upendo ulikuwa msukumo Wake.

Tazama katika mstari huo kwamba hakusema lolote kuhusu dhambi. Hiyo ndiyo Injili ya Kristo. Ni ujumbe wa upendo na ujumbe wa uzima—uzima na asili ya Mungu—ambao mauti yake na kuzikwa Kwake na kufufuka Kwake kumefanya iwezekanike na kupatikanika kwa uzima huu kwa kila mtu anayeamini.

*| SALA*

*Baba Mpendwa, ahsante kwa upendo Wako ambao umedhihirishwa, kufunuliwa, na kukumbatiwa kwa vile ambavyo wengi ulimwenguni kote wanasikia na kupokea Injili ya kweli ya Yesu Kristo, na matokeo ya zawadi ya haki. Leo, wanaupata udhihirisho kamili wa upendo Wako thabiti na wa milele, utukufu wa neema Yako, katika Jina la Yesu. Amina.*

*Jifunze Zaidi:*

** Yohana 3:16 AMPC; 2 Wakorintho 5: 19-21 **

*SOMA MAANDIKO KILA SIKU*

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MWAKA-1:*_

Yohana 19:17-42 & 1 Nyakati 17-19

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MIAKA-2:*_

Marko 15:1-14& Kumbukumbu la Torati 3

*Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional*

*Weka maoni kuhusu utenzi wa leo kwenye _www.rhapsodyofrealities.org_*

_*Jipatie BURE Nakala yako ya mwezi FEBRUARI kwa LUGHA YA KISWAHILI na nyingine nyingi ikusaidie kukua kiroho:*_ http://...
17/02/2023

_*Jipatie BURE Nakala yako ya mwezi FEBRUARI kwa LUGHA YA KISWAHILI na nyingine nyingi ikusaidie kukua kiroho:*_ http://rhapsodyofrealities.tniglobal.org

*TUMEUNGANISHWA KWA ROHO NA NENO*

Ijumaa, 17

Mchungaji Chris Oyakhilome, PhD

_*…kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo. Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja*_ Yohana 11:51-52

Mistari hapo juu unaleta akilini maneno ya Yesu katika Yohana 10:16. Alisema, _*“Na kondoo wengine ninao, ambao si wa z**i hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja”*_ (Yohana 10:16). Alitoa kauli hii akiwazungumzia Wayahudi na Wamataifa ambao wangelimwamini. Alikuwa anaenda kuwakusanya wote pamoja k**a kundi moja na kuwa mchungaji wao. Ahimidiwe Mungu!

Jinsi gani Bwana Yesu anavyotaka Kanisa liwe wamoja! Anataka tuzungumze kwa sauti moja, tuwe na maono sawa tukijua kuwa tunaye Baba mmoja na Bwana mmoja, Yesu Kristo. Akiwaombea watoto wote wa Mungu kwa Baba, alisema, _*“…ili wawe kitu kimoja k**a nasi tulivyo mmoja”*_ (Yohana 17:22 BHN).

Ndoto ya Mungu ni kuwakusanya watoto Wake katika roho ya umoja. Usilichanganye hili na Dini Moja ya Ulimwengu ambayo wanautandawazi wanajiona bora zaidi wanajaribu kuiunda. Elewa kuwa Mungu anapofanya kitu, Shetani kila wakati anataka kuja na bandia Mungu anatukusanya pamoja, si lazima katika mwili, bali mioyoni mwetu—akituunganisha kwa Roho na Neno.

Leo, wengi wetu, watu wa Mungu duniani, tunafikiri vitu sawa kuhusu Bwana, tunampenda kwa njia ile ile kwa shauku sana, tunaihubiri Injili na kuvuna nafsi kuliko ilivyowahi kutokea. Tunapendana zaidi, na tunaielewa vizuri zaidi, siri ya mwili wa Kristo katika umoja wa roho. Hii ni ndoto ya Mungu, na kila mmoja wetu lazima ajibidiishe kwa ajili ya umoja wa Mwili wa Kristo.

Fikiria kuhusu hilo: kukiwa na wengi wetu tukiwa tunafanya kazi pamoja kutoka duniani kote, tumelifanya Neno la Mungu kupitia Rhapsodi Ya Uhakika lipatikane katika kila lugha iliyo hai duniani. Tumeunganishwa na Roho kwa ajili ya maono sawa na kwa ujumbe mmoja.

Kupitia Roho Mtakatifu, tunaelewa na kutangaza ujumbe mmoja. Hili litaendelea hata kipimo zaidi enzi ya Kanisa inavyokuja mwishoni. Utukufu kwa Mungu!

*| SALA*

*Mpendwa Baba, ninakushukuru kwa ukamilifu na kujengeka kwa mwili wa Kristo. Ahsante kwa uelewa wa kina uliowapa watoto Wako kuuelewa na kuushirikisha ujumbe mmoja, tunavyotimiza ndoto Yako, na kufikia umoja wa imani na wa maarifa ya mwana wa Mungu, hadi kimo cha ukamilifu wa Kristo, katika Jina la Yesu. Amina.*

*Jifunze Zaidi:*

** Waefeso 4:13; 1 Wakorintho 12:12-13; Wafilipi 1:27 **

*SOMA MAANDIKO KILA SIKU*

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MWAKA-1:*_

Marko 2:23-3:1-12 & Walawi 11-12

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MIAKA-2:*_

Mathayo 15:10-20 & Mwanzo 48

*Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional*

*Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye* _*www.rhapsodyofrealities.org*_

RHAPSODY OF REALITIES    FOR EARLY READERS     ════━🔍🔎━════🔖 Friday 17 Walking In Humility  Likewise you younger people,...
17/02/2023

RHAPSODY OF REALITIES
FOR EARLY READERS
════━🔍🔎━════

🔖 Friday 17

Walking In Humility

Likewise you younger people, submit yourselves to your elders. Yes, all of you be submissive to one another, and be clothed with humility, for “God resists the proud, but gives grace to the humble.” 1 Peter 5:5

🧏‍♂️ ○o。....。o○🤹
Pastor Chris Says
⊶⊷⊷⊷⊶⊷⊷⊷
Being humble is different from being timid. Humility according to God’s Word is when you submit yourself to God’s Word and do what it says.

For example, when the Bible says you should honour your elders (1 Peter 5:5), that’s not the time to choose who you’ll greet or not, no! Don’t think about how you feel, do the Word and honour ‘all’ your elders.

Learn to walk in humility for this is the path to greatness.

📚 Scripture Reading
⊶⊷⊷⊷⊶⊷⊷⊷⊷⊷
Hebrews 13:17

📣 Let’s Pray
:..。o○🗣○o。..
Dear Father, I receive Your Word into my spirit today and walk in humility always, in Jesus’ Name. Amen.

Rhapsody Dailies





EXCERPT FROM: Rhapsody of Realities for Early Readers

_*Jipatie BURE Nakala yako ya mwezi FEBRUARI kwa LUGHA YA KISWAHILI na nyingine nyingi ikusaidie kukua kiroho:*_ http://...
16/02/2023

_*Jipatie BURE Nakala yako ya mwezi FEBRUARI kwa LUGHA YA KISWAHILI na nyingine nyingi ikusaidie kukua kiroho:*_ http://rhapsodyofrealities.tniglobal.org

*KUACHILIA MISIMBO SAHIHI*

Alhamis, 16

Mchungaji Chris Oyakhilome, PhD

_*Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye (anayemwelewa); lakini anena mambo ya siri katika roho yake*_ 1 Wakorintho 14:2

Kuna vitu ambavyo havitatendeka kwa ajili yako maishani mwako na katika dunia hii mpaka utakapojifunza kutumia maneno ya misimbo. Paulo aliita hekima, mafumbo na siri za kiroho (1 Wakorintho 2:7).

Kwa mfano, unavyoanza kuomba katika roho, utafika mahali ambapo unapoanza kuviita vitu kutoka ulimwengu wa roho vije kwenye ulimwengu wa kawaida. Maisha ni ya kiroho na tunashinda kwa Roho.

Kupitia Roho Mtakatifu, unaweza kujua maneno sahihi ya kutumia katika sala. Maneno hayo ni misimbo ya kiroho. Anaweza atake urudie neno au kutoa sauti kwa kurudiarudia; hilo ni kwa sababu Anajua maelezo ya “msimbo.”

Roho Mtakatifu anajua mara unazoweza kuwa unahitaji kurudia maneno hayo ili yaunde msimbo sahihi. Katika sala, unaweza kuwa unazungumza maneno fulani au kutoa sauti fulani ambazo zinaweza kuhitaji ishirini na tano kati ya sauti hizo ili msimbo uwe kamili au umeunganika. Lakini ukiishia kwenye sauti ya ishirini na nne, haitafanya kazi, kwa sababu msimbo hautakuwa umekamilika.

Ni k**a kujaribu kuingia kwenye mfumo wa maneno ya siri au akaunti; huwezi kuingia kwa misimbo isiyo sahihi hata k**a ni herufi au alama moja iliyokosewa. Hivyo katika kuomba na kuviita vitu katika Roho, endelea hadi Roho aende kiwango kingine. Kumbuka, Yeye ndiye Anayekupa usemi.

Kuna mambo ambayo watu huyapitia maishani na hata k**a wamekuwa wakinena kwa lugha, kumeonekana kutokuwa na matokeo. Ni kwa sababu kuna msimbo kwenye ulimwengu wa roho ambao bado unakosekana. Tumia misimbo na utakuwa na mtoto uliyetamani kwa muda mrefu. Tumia misimbo na fedha zitakuja; utakuwa na ukumbi kwa ajili ya kanisa au biashara.

Nyumba unayoitamani iko ndani ya lugha hiyo ya msimbo; tumia misimbo sahihi na utakuwa nayo. Jibu la tatizo hilo liko kwenye “msimbo” lakini Roho Mtakatifu anaujua msimbo. Nena kwa lugha hadi upate misimbo kamili kutoka kwa Roho Mtakatifu na uiachilie.

*| SALA*

*Mpendwa Baba, ninaponena kwa lugha leo, mwangaza hunijia rohoni mwangu. Ninajua hatua za kuchukua kuhusiana na hali mahususi kuhusu maisha yangu; ninajua cha kufanya, wakati wa kukifanya, na jinsi ya kukifanya, kwa sifa na utukufu wa Jina Lako. Amina.*

*Jifunze Zaidi:*

** 1 Wakorintho 14:2 AMPC; 1 Wakorintho 2:11-13 **

*SOMA MAANDIKO KILA SIKU*

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MWAKA-1:*_

Marko 2:1-22 & Walawi 9-10

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MIAKA-2:*_

Mathayo 14:34-15:1-9 & Mwanzo 47

*Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional*

*Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye* _*www.rhapsodyofrealities.org*_

_*Jipatie BURE Nakala yako ya mwezi FEBRUARI kwa LUGHA YA KISWAHILI na nyingine nyingi ikusaidie kukua kiroho:*_ http://...
15/02/2023

_*Jipatie BURE Nakala yako ya mwezi FEBRUARI kwa LUGHA YA KISWAHILI na nyingine nyingi ikusaidie kukua kiroho:*_ http://rhapsodyofrealities.tniglobal.org

*JENGA KULINGANA NA MAELEZO*

Jumatano, 15

Mchungaji Chris Oyakhilome, PhD

_*…Musa alionywa alipokaribia kujenga hema, akiambiwa: “Hakikisha kuwa unavitengeneza vitu vyote kwa mfano ulioonyeshwa kule mlimani”*_ Waebrania 8:5 NEN

Mungu alipomwambia Musa ajenge hema, Alimpa maelezo dhahiri na kumwagiza ajenge kulingana na maelezo hayo: _*“Sawasawa na haya yote nikuoneshayo, mfano wa maskani, na mfano wa samani zake zote, ndivyo mtakavyovifanya”*_ (Kutoka 25:9).

Katika mwenendo wako na Bwana na kazi katika Ufalme Wake usikimbie tu na kila wazo kwa sababu hilo ndilo unalodhani ni zuri. Uwe na uhakika kuwa unafuata maelekezo ya Mungu; muundo na maelezo aliyoyatoa. Ni moja ya sababu inakulazimu kulijua Neno wewe binafsi.

Ndani ya Neno Lake utakuta sampuli, miundo na maelezo ya jinsi Anavyotaka tuishi, vitu Anavyotaka tufanye na jinsi ya kuvifanya. Mtunga zaburi alisema katika Zaburi 127:1, _*“BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wanafanya kazi bure…”*_; lazima tujenge sawasawa na mpango Wake.

Katika siku hizi za mwisho, Bwana Yesu analijenga Kanisa Lake. Alisema, _*“…nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda”*_ (Mathayo 16:18). Kuna maelezo tuliyopewa ndani ya Neno la Mungu yanayotuonesha jinsi Anavyolifanya hili. Biblia inasema (Kristo Mwenyewe), _*“…aliweka wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na walimu, kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za huduma, ili kwamba mwili wa Kristo upate kujengwa”*_ (Waefeso 4:11-12 NEN).

Mpango Wake ni kujenga kupitia viongozi hawa, lakini kila mmoja anahusika, kila mmoja wetu anachangia kwenye ujenzi wa mwili huu mkubwa wa Kristo: _*“Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo”*_ (Waefeso 4:16).

Kila wakati unapomwongoza mtu kwa Kristo unaongeza katika ujenzi wa Mwili wa Kristo, na ni jengo la kifahari sana. Haleluya! Endelea kufanya wajibu wako kwa kuvuna nafsi ziingie kwenye Ufalme. Utakuwa unachangia katika ujenzi huu wa jengo la kifahari sawasawa na maelezo yaliyotolewa.

*| SALA*

*Mpendwa Baba, ninakushukuru kwa uwezo wa Neno Lako rohoni mwangu. Mimi ni mtendaji wa Neno, sio tu msikiaji. Matokeo ya kuishi katika, na kwa Neno yanadhihirika dhahiri katika kila eneo la maisha yangu leo, katika Jina la Yesu. Amina.*

*Jifunze Zaidi:*

** Waebrania 8:5 AMPC; 1 Samweli 15:22 **

*SOMA MAANDIKO KILA SIKU*

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MWAKA-1:*_

Marko 1:21-45 & Walawi 8

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MIAKA-2:*_

Mathayo 14:22-33 & Mwanzo 46

*Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional*

*Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye* _*www.rhapsodyofrealities.org*_

Address

Chunya District
Mbeya

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when RhapsodyMan posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to RhapsodyMan:

Share