Mawaidha ya dini ya kiislamu

Mawaidha ya dini ya kiislamu Allah akujaalie msikilizaji wa mawaidha haya upate ibra mazingatio na ubadili muelekeo wa maisha yak

04/04/2024

KAMWE USIRUHUSU MTU AKUSH*TAKIE KWA MWENYEZI MUNGU

Asalam Aleykum
15/03/2024

Asalam Aleykum

10/03/2024

Ramadhan kareem

13/04/2022

Masha llah

05/04/2022

Mash Allah

19/08/2021
19/08/2021

Mashallah mawaidha mazuri sijawahi kusikia

SUNNAH KATIKA NDOTO Anachokiona mwenye kulala hakitoki nje ya hali tatu zilizokuja katika Hadithi ya Abuu Huraira RAA il...
19/08/2021

SUNNAH KATIKA NDOTO

Anachokiona mwenye kulala hakitoki nje ya hali tatu zilizokuja katika Hadithi ya Abuu Huraira RAA iliyopo katika mapokezi ya Muslim:

1 ✔Ndoto njema ambayo ni bishara kutoka kwa Allah SWT. Ndoto hii ina adabu zake na zitakuja.

2 ✔Ndoto ya kuhuzunisha ambayo inatoka kwa shetani. Ndoto hii haimdhuru mja k**a atafuata adabu zake, na zitakuja.

3 ✔Kuota yale aliyokuwa akiyazungumza nafsini mwake kabla ya kulala. Ndoto hii haina maana yoyote.

Na miongoni mwa Sunnah katika mlango huu ni yale mafundisho yalokuja katika Hadithi hizi zifuatazo:

Imenukuliwa kwa Abuu Salama RAA aliyenukuliwa kusema kuwa:

“Nilikuwa nikiota ndoto na kunipa ugonjwa”. Akasema: “Nikakutana na Abukatada (nikamwambia naye), akasema: “Na mimi pia nilikuwa nikiota ndoto na kunipa ugonjwa, mpaka nilipomsikia Mtume SAW akisema:

“Ndoto njema inatoka kwa Allah. Akiota mmoja wenu jambo analolipenda asimzungumzie ila yule anayempenda tu. Na akiota jambo asilolipenda anatakiwa apulize kushotoni kwake mara tatu, kisha aombe kinga kwa Allah dhidi ya shari ya shetani na shari ya alichokiota, wala asimhadithie yeyote, kwa sababu ndoto hiyo haitamdhuru”.

Na akasema Abusalama:

“Na nilikuwa naota ndoto nzito kwangu kuliko mlima. Tangu niliposikia Hadithi hii sikuijali ndoto hiyo”.

Imepokewa na Bukhari kwa nambari (5747) na Muslim kwa nambari (2261).

Na katika mapokezi mengine kuna nukuu kwamba:

“Ndoto njema inatoka kwa Allah na ndoto mbaya inatoka kwa shetani. Akiona mmoja wenu ndoto anayoiogopa basi apulize kushotoni kwake, na aombe kinga kwa Allah dhidi ya shari yake, kwa sababu haitamdhuru”.

Imepokelewa na Bukhari kwa nambari (3292) na Muslim kwa nambari (2261).

Na katika Hadithi ya Jabir RAA katika mapokezi ya Muslim, kuna nukuu kwamba Mtume SAW amesema:

“Na aombe kinga kwa Allah mara tatu dhidi ya shari ya shetani, na ageukie ubavu mwingine”.

Ameipokea Muslim kwa nambari (2262).

Na katika Hadithi ya Abusaid Alkhudriy RAA katika mapokezi ya Bukhari kuna nukuu kwamba:

“Anapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda, hakika hiyo inatokana na Allah, na amhimidi Allah kwa ndoto hiyo”.

Ameipokea Bukhari kwa nambari (7045).

Tunapata katika Hadithi zilizopita kwamba:

1 🌸Mwenye kuota ndoto nzuri ni Suna afanye yafuatayo:

Kwanza:

Amhimidi Allah kwa ndoto hiyo, kwa sababu inatoka kwake Sub-haanahuu Wata’aalaa.

Pili:

Aizungumze. Na asimzungumzie isipokuwa tu yule anayempenda.

2 🌸Na kwamba yule aliyeota ndoto ambayo haipendi, ni Suna kwake kufanya yafuatayo:

Kwanza:

Ateme cheche za mate, au apulizie mate upande wake wa kushoto mara tatu.

Pili:

Aombe kinga kwa Allah Aliyetukuka dhidi ya Shetani, na
dhidi ya shari ya alichokiota. Afanye hivyo mara tatu, kwa kusema:

“A’uudhu Billaahi Minash-shaitwaan, Wamin Sharrihaa” (Najikinga kwa Allah na shetani na shari ya nilichokiota) mara tatu.

Tatu:

Asimwambie yeyote. Akifanya hivyo, hakika haitamdhuru k**a alivyoeleza Mtume SAW . Na akizidisha juu ya hayo:

Nne:

Ageuze upande ambao alikuwa amelalia. Ikiwa alikuwa amelala
chali, alalie ubavu wake, n.k.

Tano:

Asimame na kuswali rakaa mbili.

Na inapatikana faida katika Hadithi zilizotangulia kwamba:

Ndoto ya Muislamu ni sehemu ya unabii, na kwamba mtu mwenye ndoto za kweli zaidi ni yule mkweli zaidi katika mazungumzo anapokuwa macho. Hali hii inatokana na athari kusema kweli na baraka zake kwa Muislamu, hata anapokuwa usingizini.

Address

Mbeya
31

Telephone

+255685293575

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mawaidha ya dini ya kiislamu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Mawaidha ya dini ya kiislamu:

Share