30/11/2016
*KATI YA YESU KRISTO NA MUHAMMAD (S.A.W.) NI NANI NABII YULE?*
*Katika Ulimwengu wa kimwili siyo rahisi kuweza kuelewa hiki ambacho nakizungumza, ila katika ulimwengu wa kiroho ni rahisi sana kuzitambua hila za muovu yule shetani! imekuwa ni kawaida sana kuwaona baadhi ya Waislamu wakijaribu kwa makusudi kabisa kuwapotosha waislamu wenzao na wakati mwingine kuwapotosha baadhi ya Wakristo, wale ambao kusoma neno la MUNGU kwao ni mtihani, wakifundisha yasiyowapasa! wakinukuu mistari hii 👇hii ndani ya BIBLIA.*
Yohana 1: 19 Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?
20 Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo.
21 Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.
22 Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako?
23 Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! K**a vile alivyonena nabii Isaya.
*Wakishasoma mistari hii wanasema kuwa, hapo kuna watu watatu!*
(1) KRISTO
(2) ELIYA
(3) KRISTO
*Wanasema kuwa, YOHANA yeye amekataa kuwa siyo mmoja katika wale watatu! hivyo wanaendelea kudai kuwa, Kristo na Nabii yule ni wawili tofauti, kwa sababu Yohana ametajiwa watu watatu na amekiri kuwa yeye siye! Ila Yesu yeye alipoambiwa kuwa yeye ni Kristo alikubali.*
Yohana 4:25 Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.
26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye.
*Wanasema kuwa, Yesu yeye ni Kristo, hivyo siyo Nabii yule, wanasema "Ni lazima tumtafute Nabii yule" Katika kumtafuta kwao, wanamdumbukiza Muhammadi, ukiwaomba ushahidi wa andiko ndani ya QURAN lisemalo kuwa Muhammadi ndiye Nabii Yule, hawawezi kutoa ila wanalazimisha dhana zao na Ujuzi wa kutunga maneno na kuyapangilia kwa ustadi mkubwa, kiasi kwamba k**a hujazama katika maandiko basi wewe unaenda na Maji!*
*JE! NABII YULE NI NANI?*
*kabla hatujamwangalia na kumjua ni nani kwa mujibu wa maandiko, tuwatazame wale walioenda kumuuliza Yohana wao wenyewe Walitoka wapi?*
Yohana 1:24 Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo.
25 Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?
26 Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi.
27 Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.
*Wale watu walikuwa wametoka kwa Mafarisayo, wakawa wanamshangaa Yohana ni vipi abatize wakati yeye siyo Kristo siyo Eliya wala Nabii yule? Inaonyesha wazi kuwa, wale nao pia hawakuwa wanamjua Yohana k**a Nabii aliyetabiriwa, Wao walijua atakaenza kubatiza ni Kristo na Nabii yule, Yohana akawajibu Amesimama yule wasiyemjua, huyo ambae atakuja nyuma yake ndiye Nabii yule ndiye Kristo. 👇*
Yohana 1:29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
30 Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
*Yohana 👆 Anawafahamisha kuwa huyu Yesu ndiye Muhusika ambae ninyi mlikuwa mkimuuliza, nikawapa habari zake, lakini wao hawakumjua pamoja na kwamba walijua ujio wake lakini bado hawakumjua kuwa ni Yesu, hawakutaka kukubali kuwa Yesu ni Kristo.*
Yohana 7:25 Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue?
26 Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo?
27 Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako.
*Watu hao 👆🏻 Bado hawakutaka kuamini kuwa Yesu ni Kristo, kwa sababu wao hawakujua kuwa Kristo ndiye huyo huyo Nabii yule, wao walijua kuwa Kristo na Nabii yule ni wawili tofauti, Swali la Kujiuliza Je! ni kweli Yesu ndiye NABII yule?*
Yohana 6:11 Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka.
12 Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee cho chote.
13 Basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia wale waliokula.
14 Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.
*Yesu Kristo ️👆 Ndiye Nabii yule, kwa nini ni Nabii yule kwa sababu, Ishara na dalili zake zipo sawa, unaweza kujiuliza, hao watu walijuaje kwamba, atakuja Nabii? ni hapa. 👇*
Kumbukumbu la torati 18:18 Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
*MUNGU 👆🏻alishawaambia Kuwa atawaondokeshea Nabii mfano wa Musa, japo katika andiko hili Waislamu hujaribu pia kumpachika Muhammadi wakisema, Musa alioa Muhammad nae alioa, Musa alipigana Vita Muhammadi nae alipigana Vita, hivyo ni vigezo vya kawaida visivyoendana kwani Kuoa kupigana Vita, siyo Vigezo vya Unabii mfano wa Musa, Daudi alioa na alipigana Vita, lakini yeye siyo mfano wa Musa! (NITAKUJA KUANDAA SOMO LA JE! MUHAMMADI NI NABII MFANO WA MUSA?) hapa tuendelee kuyaangazia maandiko ndani ya BIBLIA yamemtaja nani kuwa ndiye Nabii Mfano wa Musa?*
Matendo 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;
20 apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani;
21 ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.
22 Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, k**a mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.
23 Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake.
24 Naam, na manabii wote tangu Samweli na wale waliokuja baada yake, wote walionena, walihubiri habari za siku hizi.
25 Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa.
26 Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.
*Mtume Petro anatuambia kuwa, huyo nabii mfano wa Musa, ni Yesu Kristo, na Yesu alijithibitisha kwa kusema.👇🏼*
Yohana 3:14 Na k**a vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;
15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
*Maandiko yanazidi kutuonyesha kuwa aliye mfano wa Musa ni YESU. 👇*
Waebrania 4:1 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu,
2 aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, k**a Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.
*Hivyo watu wakawa wanamtazamia nabii huyo yaani Nabii yule ambaye alisemwa na Musa kuwa atakuja, Na alipokuja Yesu walinena. 👇*
Yohana 7:37 Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.
38 Aniaminiye mimi, k**a vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.
40 Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule.
*Waliotambua Utimilizo wa maandiko waliendelea kumtambua Nabii yule, 👇*
Mathayo 21:10 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu?
11 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.
*YESU NDIYE NABII YULE HAKUNA MWINGINE ALIYETAJWA KATIKA MAANDIKO KUSEMA KUWA NI NABII YULE WANAOSEMA NI NABII YULE NJE YA YESU WANASEMA KWA VINYWA VYAO PASINA USHAHIDI WA MOJA KWA MOJA K**A ULIVYO KWA KRISTO YESU!*
*Quran inamtumbua kuwa Muhammadi ni Nabii lakini haijawahi kusema ni Nabii yule, k**a kuna mtu ambae anao ushahidi ndani ya quran kuwa kuna aya imesema kuwa Muhammadi ni Nabii yule toa ushahidi hapa*
BY ABEL SULEIMAN SHILIWA.