Mgao Remmy

Mgao Remmy Christian's Teachings

Bwana Yesu asifiwe sanaa,Hallelujah. Nitumie nafasi hii kumshukuru Mungu wetu wa Mbinguni kwaajili yako pia kwa kukuweze...
01/01/2026

Bwana Yesu asifiwe sanaa,Hallelujah.
Nitumie nafasi hii kumshukuru Mungu wetu wa Mbinguni kwaajili yako pia kwa kukuwezesha kufika mwishoni mwa mwaka huu tena,tunajua ni kwa neema tu,ni kwa neema tuu, na hivyo nikuombe na nikukaribishe katika kipindi hiki kifupi cha kutafakari,
Tuombe;
Bwana Yesu! Nashukuru kwaajili ya kila mmoja ambaye anapata nafasi ya kusoma jambo hili kwa leo katika wewe,Naomba neema,baraka,ufahamu wa ndani na hekima zako ziende juu ya kila mmoja naaam ! Msaada wako uende juu yake hata apate kitu cha kujifunza katika wewe kwa Jina la Yesu-Amen
Kwa somo lenye kichwa cha -

TUMIA UTOAJI WA SADAKA YAKO K**A SILAHA YA UJEZI
VOL;01

Niaze kwa kuuliza maswali haya ya kutafakari.
Umewahi kujiuliza sadaka ni kitu gani? au Sadaka ni nini? Au kwanini Sadaka?
Bila majibu mazuri ndani yako kwenye hayo maswali,ni vigumu sana kutoa sadaka na ikawa sadaka kwa Mungu wetu. Sijasema huwezi kupeleka/kuleta kitu au fedha kwenye chombo kinaitwa chombo cha sadaka
Sadaka haiwezi kuitwa sadaka kwasababu ya kuwekwa kwenye kapu la sadaka.

Hebu tusome misitari hii kwenye kitabu cha Mwanzo 4;3-5
Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.

Ukisoma vizuri hii mistari unaona ..
Kwanza; Biblia inasema wote walitoa au walileta kwa lengo la sadaka kwa Bwana, Kwahiyo Bwana alikuwepo mahali pale sadaka zilitolewa na hawa ndugu.

Pili; pamoja na kutoa au kuleta sadaka hizo mbele za Bwana, unaona tofauti ya matokea yao,baada ya kutoa ni kwamba sadaka ya Habili ilipokelewa na sadaka ya Kaini haikupokelewa au Bwana hakuitakabali sadaka yake.
Na hii tofauti iliathiri maisha yao jumla kuazia wakati huo.
Kila unapo ona mahali sadaka inatolewa kumbuka picha ya jambo hili moyoni mwako.

kwa kusoma hii misitari huoni tofati ya Habili na Kaini kwasababu wote walikuwa na sadaka na wote walikuwa mbele za Bwana au walitoa sadaka kwa Bwana,kwa sasa tungesema wote walikuwa kanisani na walitoa kwenye madhababu moja.

Swali langu, ni kitu gani kiliwatofautisha kiasi cha Sadaka ya mmoja kutakabaliwa na mwingine kukataliwa?
Na nirudie tena kuuliza kuwa sadaka ni kitu gani? au Sadaka ni nini? Au kwanini Sadaka?

Kumbuka lengo kubwa la somo hili ni kuimarisha mahusiano yetu na Bwana kupitia utoaji wa sadaka hasa wakati Roho mtakatifu anatusukuma katika kujenga upya au kukarabati maeneo tunayo hitaji msaada tunaoweza kuupata kwa njia hii,
Inaweza kuwa kujenga au kusuka upya maisha yetu ya kiroho au misuli ya utumishi au imani au nafsi zetu au maono yetu au biashara au chochote unahitaji Mungu aingilie kati upate msaada wake. etc

Tusogee hatua kidogo,kwa kusoma Waebrania 11;4 nayo inasema hivi..
Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.

Unaaza kuona tofauti mojawapo ikiwa ni Imani waliyo kuwa nayo wakati wa kutoa.
Biblia inasema "kwa Imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko kaini.
Kwahiyo wote walikuwa na sadaka,ila siyo wote walikuwa na Imani.

K**a imani ndiyo tofauti yao, Kwahiyo ubora wa sadaka yeyote haupo kwenye unacho kitoa bali upo kwenye Imani.
Okay; Imani ndo nini?

Waebrania 11;1 inajibu kwakusema...
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

K**a Habili alimtolea Mungu kwa Imani na imani ni kuwa na uhakika wa mambo... ni bayana na yale.....

Kwahiyo Waebrania 11;4 tunaweza tukaisoma hivi
Kwa kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo(imani),Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.

Swali jingine linakuja "k**a imani ni kuwa na uhakika wa mambo,
“huu uhakika Habili aliutoa wapi kiasi cha kaini kuto kuupata “?

Warumi 10:17 inajibu kwa kusema
"Basi imani(kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo), chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo"
Kwahiyo k**a imani ni uhakika unao upata kwa kusikia ni lazima huku ni kusikia ambako ndani yako kunakupatia usikivu ambao ni maelekezo ya namna ya utendaji wa jambo

Kwahiyo moja ya tofauti ilikuwa kwenye kutekeleza maelekezo ya kutoa wanacho kitoa, Biblia ipo wazi kuwa Habili alitoa kwa imani ambayo ni maelekezo ambayo ameyapata kwa neno la kristo na kuwa maelekezo au muongozo ndani yake.

Siku zote kumbuka jambo hili "Fedha na dhahabu ni mali ya Bwana " chochote ni chake Bwana
Inapofika mahali anahitaji ukitoe kwake usije dhani kaishiwa au ana shida,bali anakuhitaji wewe kupitia hilo eneo.
Changamoto iliyopo ni mafundisho sahihi kwenye kutoa kiimani, kiasi ambacho kinapelekea wengi wakisikia kutoa wanajisikia vibaya na shida hii inaweza sababishwa na tuliopewa dhamana ya kufundisha au kueleza watu wa Bwana namna ya kumtolea Mungu wao.
Kuna wakati tunaelezea swala la kumtolea Mungu k**a vile ni kumpatia msaada huyu Mungu au k**a vile kuna jambo Mungu wetu kakwama anahitaji mchango ili avuke mahali alipo
Haiwezi kwenda namna hiyo huyu Mungu ni Mungu mtoshelevu anaye tamani nasi tutoshelezwe na baraka zake lakini pia atuimarishe kila eneo kuwa ushuhuda kwa ulimwengu
“maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.”
1 Wakorintho 10:26
Baada ya utangulizi huu,tuangalie mifano michache,namna ambavyo sadaka ilitumika k**a silaha kwa mtoaji katika kufikia lengo.


01; NAMNA AMBAVYO MUNGU ALIMTOA YESU KWAAJILI YETU.
Swala la Mungu kumtoa Yesu lilikuwa ni swala la kimkakati
Na moja ya mkakati ilikuwa ni kurejesha kilichopotea pamoja na aliyepotea
Tunasoma katika kitabu cha Yohana 3;16 inasema hivi …
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Msukumo mkubwa ulikuwa kwenye kurejesha kilicho potea ili kisipoteze,Biblia inasema ili asipotee, hebu sema asipotee ,asipotee...
Kwasababu anaye potea anapoteza pia alicho kibeba mpoteaji.
Au anaye potea maana yake amepoteza mwelekeo na njia
Au anaye potea maana yake amempoteza hata kiongozi wake
Au anaye potea maana yake amepoteza maelekezo ya kuyafuata.

Kwahiyo k**a Mung alitumia sadaka kurejesha alicho kuwa amepoteza ni dhahiri kuwa anaweza pia kutuongoza kutumia njia hii kurejesha tunachoweza kuwa tumepoteza

Inaweza kuwa hali zetu za mahusiano na yeye au kurejesha utumishi wetu au kuimarisha mamlaka yetu dhidi ya ufalme wa giza.
Kumbuka Yesu anasimama k**a mpatanishi ,mpatanishi ni k**a daraja ili kuhakikisha mwanzo inakuwa na mwisho na mwisho inakua na mwanzo
Tunasoma katika kitabu cha “1 Timotheo 2:5”
Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;

02; NAMNA SADAKA YA HABILI ILIVYO TUMIKA KUMJENGA
Natamani tujaribu kuona tofauti ya Habili kabla ya kutoa sadaka na yule Habili baada ya kutoa sadaka lakini usimsahau na Kaini yule baada ya kutoa sadaka kwa kutumia misitari huu

Waebrania 11;4 nayo yasema
“Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.

Yale maneno ya mwisho yanasema “ijapokuwa kuwa amekufa angali akinena “
Unaona sadaka ile aliyo itoa Habili Biblia inasema “ajapo kuwa amekufa angali akinena” maana yake ile sadaka ilikuwa na nguvu kiasi ambacho hata k**a Habili hayupo sadaka aliyo itoa itasema na kutekeleza maelekezo ambayo moyo wa mtoaji ulikuwa ukiyatimiza.

Jaribu kufikiria Habili alitoa sadaka hii kwaajili ya uzao wake,k**a ajapo kuwa amekufa angali akinena maana yake sadaka hii inaweza kushughulika nao kizazi hata kizazi

Hebu tusome misitari hii kutoka Zabari 89 inaposema...
Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu.
Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu.
Wanawe wakiiacha sheria yangu, Wasiende katika hukumu zangu,
Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo, Na uovu wao kwa mapigo.
Zaburi 89:20,21,30 na 32

Huyo ni Mungu anaye sema na kuahidi juu ya uzao wa Daudi ya kuwa hata k**a watajaribu kuacha njia za Bwana,yeye Bwana atawarudisha hata kwa fimbo,utumishi wa Daudi k**a sadaka kwa Bwana,Mungu aliridhia kiasi akamwahidi hayo juu ya uzao wake
Kwahiyo pia sadaka ilitumika kujenga mazingira ya Habili na kesho yake hata kizazi na kizazi.
Na
sadaka hiyo hiyo ilitumika kuvuruga au kubomoa kabisa mwelekeo wa kaini.kwahiyo unaweza kuitumia k**a nyezo kwa kufuata maelekezo unayo pewa wakati wa kutoa ili kujengamwelekeo au jambo ulilo nalo moyoni mwako.Ooooh Mungu aguse macho yetu

03; TUANGALIE MFANO WA SADAKA YA ANANIA NA MKEWE SAFIRA
Tuaze kwa kutumia misitari hii
Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali,
akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.
“Matendo ya Mitume 5:1-2"

Moja ya maneno ya msingi sana katika somo hili ni Yale maneno yanasema “akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake”
Akazuia,maana yake alikatalia/alificha baadhi ya thamani isiyotakiwa kuwa kwake akakaa nayo kwa mfano wa yake.
Na kitendo hiki cha kuzuia thamani,Paul akasema kwanini kumdanganya Roho mtakatifu (Kwahiyo maelekezo ya kutoa walipewa na Roho mtakatifu) unaona matokeo yake juu ya maisha ni kukatisha thamani yake ya kuishi "akafa palepale".

K**a utoaji wa sadaka uliweza kuondoa au kubomoa thamani ya kuishi kwao, basi kinyume chake isipozuiliwa k**a Roho mtakatifu anatusukuma kufanya inaweza kutumika kujenga thamani bora ya maisha yetu.
Kwenye hili tukio la Anania na Safira (Mdo 5;1-11) neno thamani limeandikwa zaidi ya mara tano
Hii inaonyesha namna thamani ikitumika ipasavyo inavyoweza kujenga au kubomoa kabisa hata thamani iliyopo

04; UTOAJI WA SADAKA ULIVYO TUMIKA KUJENGA MAISHA YA RAHABU NA FAMILIA YAKE. Tunaisoma kwenye kitabu cha "Joshua 2;12- 12" inasema hivi..
Basi sasa, nawasihi, niapieni kwa Bwana, kwa kuwa nimewatendea ihisani ya kwamba ninyi nanyi mtaitendea ihisani nyumba ya baba yangu; tena nipeni alama ya uaminifu;
ya kwamba mtawaponya hai baba yangu na mama yangu, na ndugu zangu wanaume na wanawake, na vitu vyote walivyo navyo, na kutuokoa roho zetu na kufa.
Wale wanaume wakamwambia, Uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati Bwana atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa ihisani na uaminifu.

Ukisoma habari hii ya Rahabu yote unaweza kuona kwa mazingira ya kawaida hawa wapelelezi wasinge fikia nyumbani kwa Rahabu,kwasababu ya tabia ile anajulikana nayo.
Lakini Mbinguni walijua kuwa Rahabu wa leo ni tofauti sana na Rahabu wa kesho,isipokuwa lazima apate mazingira ya kubadirisha ukurasa wa maisha yake.
Inawezeana tuna akina Rahabu wengi kwenye jamii zetu ambao kwakweli ukiwatazama kwa sasa siyo rahisi sanaa hata kueleweka kwa sababu ya mifumo yao ya kuishi,huyu Rahabu alikuwa na sifa ya ukahaba,haikuwa kitu rahisi sanaa kwamba kuna watumishi wa Mungu wanatembelea mji afu mwenyeji wao awe Rahabu,wakati mjini huko kuna watumishi wa Mungu tunaowajua wangeweza kuupokea huo ugeni.
IInawezekana wewe unasifa mbaya labda k**a Rahabu au unasifa ya mlevi,au mwizi au yeyote ile
Sikia;bado Mungu anaweza kukufungulia mlango ambao kila atakaye kuwa anakutazama asiamini k**a ndo wewe,na wewe waambie ndo mimi jamani Bwana wa majeshi amefumua-fumua nyaya zilizotumika kusuka maisha yangu na kusuka kwa upya hivyo nimekuwa kiumbe kipya nayo mambo yangu yamekuwa mapya, nayaweza yooote katika yeye.
Kwahiyo mabadiliko ya nyakati mpya za kujengwa upya Kwa maisha ya Rahabu Kulitegemea namna aliyo wapokea wapelelezi na kuwahifadhi katika nyumba yake k**a sehemu ya sadaka yake kwa Bwana
Na nguvu ya sadaka hii siyo tu kwamba ilibadirisha nyakati za maisha ya Rahabu tu,bali na familia yake yote iliingia kwenye maisha mapya ya baraka na ushindi kupitia Rahabu.
Umeona kwa Habili Biblia inasema ijapokuwa kuwa amekufa angali akinena, hii inaonyesha kwamba inaweza tengeneza mazingira mapya si kwa anayetoa tu bali hadi kizazi chake.

Inawezekana pamoja na changamoto yake Rahabu alikuwa akikaa anamwomba Mungu kwamba, Mungu nikumbuke na naomba unitoe kwenye hii tabia na aina hii ya maisha,kwasababu tabia yako isikuzuie kumwomba Mungu hata k**a unaomba kimya kimya nyumbani kwako, hata k**a umetengwa kanisani kwako,jifungie ndani omba Mungu, kwasababu Yesu yu apita mtaani kutafuta kilicho potea, Usiache tafadhali,usife moyo...your tomorrow is brighter than to day. Hallelujah, Hallelujah....

Unamkumbuka Ibrahimu huyu wa hapa Biblia inaposema,
Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.
akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako k**a nyota za mbinguni, na k**a mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;
Mwanzo 22:11-12;16-17

Huyu ni Mzee Ibrahimu ambaye inawezekana pia alikuwa anamwomba Mungu kwamba,Mungu ambariki kwa baraka nyingi zaidi,
Sijajua ilichukua mda gani,lakini Mungu alisikia maombi yake na ili kuzipata hizo baraka aliambiwa amtoe mwanae wa pekee yaani Isaka.
Mungu hakuwa anahitaji Isaka afe, bali kwa njia hii Mungu alikuwa anautafuta utaayari wa moyo wa Ibrahimu.
Na Ibrahimu alipo onyesha utaayari wa kumtoa Isaka,Ndipo unaona haya maneno mungu akiyasema kuwa “Sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu”
Siyo kwamba alikuwa hajui,bali ni kwamba sasa amejiridhisha ya kuwa ………
Kwahiyo sadaka ya namna hii imebeba msaada wa mpenyo wa ngazi mpya kibaraka,kiroho,au kimahusiano mapya na Mungu, mara nyingi Mungu anakuwa anawinda utaayari wako wa kutembea kwenye hiyo ngazi iliyo mbele yako.

Mungu akijiridhisha kuwa unao utaayari katika jambo hilo,ndipo anakufungulia mlango ili uingie katika msimu huo mpya kimaisha na kihistoria mpya
Mlango uliokuwa mbele ya Habili ulifunguka na upo wazi hata kwa kizazi chake ,kwanini?
Ni÷
“ijapokuwa kuwa amekufa angali akinena”
Mlango uliokuwa mbele ya Kaini alishindwa kuufungua akafungua upande wa laana,japo Mungu alimwambia kuwa “ukifanya vema hutapata kibali?” maana yake kibali kilikuwepo Ila hakuwa tayari nacho,K**a ilivyo kuwa kwa Anania na Safira.

Nani angekwambia ukaelewa kirahisi kuwa wakati Mungu anatafuta mtu wa kuwapokea watumishi wake “wapelelezi”kwenye mji wa Yeriko, wachungaji waliokuwepo mji wa Yeriko na wapendwa mbalimbali hawakuwa na utaayari ila Rahabu yule kahaba.

Fikiria baada ya Yeriko kuteketea,unakutana na ndugu zake Rahabu wanakwambia tulipona kwasababu ya Rahabu na unamjua Rahabu wa kabla ya hili tukio.
“Basi sasa, nawasihi, niapieni kwa Bwana, kwa kuwa nimewatendea ihisani, ya kwamba ninyi nanyi mtaitendea ihisani nyumba ya baba yangu; tena nipeni alama ya uaminifu; ya kwamba mtawaponya hai baba yangu na mama yangu, na ndugu zangu wanaume na wanawake, na vitu vyote walivyo navyo, na kutuokoa roho zetu na kufa”.
(Joshua 2;12-13)
Afu ukimuuliza Rahabu kwambai ilikuwaje? Akwambie alisikia msukumo ndani yake wa kuwakaribisha hao wapelelezi na akaomba na maombi ya kuhifadhiwa hai yeye na ndugu zake.

Ukipitia changamoto k**a hiyo,Kwa jinsi ya kawaida unaweza dhani umefikia mahali ambapo huna namna ya kung’aa tena zaidi kuliko wakati wowote
Au ndani yako unaona ndoto kubwa; na huoni namna inaweza kutimia hata kwa juhudi zote au ndani yako unaona kesho kubwa kwaajili yako au familia au kanisa au taifa na mataifa, please natumia wino huu kukwambia Usiogope .
Endelea kuomba bila kuchoka,amini Mungu anasikia
Zaidi jiombee usikivu na macho yako ya ndani kufunguka ili kuona milango ya kukuvusha ambayo Mungu anaipitisha kwako.
Na jifunze kuambatanisha kila sadaka na maombi yako
Na kutoa sawasawa na maelekezo unapewa isiwe kwa mazoea wala mapokeo wala mkumbo.
Mungu ni mwaminifu hakika atafanya mlango na kuandika jina jipya kwako.
Kwa leo naishia hapo,tutakutendea tena Mungu akitujaria
Happy new year🤝 ❤️
Have a victorious life in Jesus mighty Name.

Tuombe.
Bwana Yesu nashukuru sanaaa, nashukuru sanaa,kwaajili ya kila uliye mjalia neema somo hili kufika mikononi mwake naomba kikawe chakula bora ndani yake na sogeza hatua za kiufahamu kiimani kwenye moyo wake ambalo atasema Asante kwako,kwani umesema naye,ameona kitu cha kufanya,amepata mbinu mpya,umefungua moyo wake kukutazama kwa upya katika jambo hili,
Eeeeh Mungu Tembelea na kukagua kila hatua aliyotembea katika maisha yake yote ikiwa kuna mahali haufurahishwi napo,Naomba Rehema zako kwaajili yake,Naomba neema ya msalaba iende juu yake na msamaha wa yote katika Damu ya Yesu Kristo,apte kuvuka.
Na kila kilicho mzuia kikamwachie kwa Jina la Yesu wa Nazareth-
Akawe safi na kurejeshwa katika upya wote,na uzima wa milele ukawe juu yake naamu na kila Baraka ya Msalaba.AMEN

Ubarikiwe kwa kuutoa mda wako na Mungu akautazame k**a sadaka kwako.
By RM.
Emai: [email protected]
page:Mgao Remmy
WhatsApp +255759676771

Karibu katika ukurasa mpya wa “NIMEKUOMBEA “
< YouTube channel >
https://youtube.com/?si=J4wLiSj5w1COc5Pz
Naomba (share na subscribe) ni ukurasa tunaandaa kwa kazi ya mafundisho ya Neno la Mungu tu

Waimarishe Watu Wangu "Luka 22:32"

27/10/2024

Its all about a cost, "gharama, gharama.......🙏

KUOMBA KWA MDA MREFU NA KUNENA KWA LUGHA K**A SILAHA "TUNDUMA day 05"MUNGU awabariki na kuwatunza watu wa TundumaWaweza ...
07/06/2022

KUOMBA KWA MDA MREFU NA KUNENA KWA LUGHA K**A SILAHA "TUNDUMA day 05"

MUNGU awabariki na kuwatunza watu wa Tunduma

Waweza sikiliza 👇

MUNGU awabariki na awatunze watu wa Tunduma

27/03/2022
Vol.03  ANCHOR.FM
10/02/2022

Vol.03
ANCHOR.FM

Teaching

Vol 02.  ANCHOR. FM
09/02/2022

Vol 02.
ANCHOR. FM

Vol 02

This is the excerpt for your very first post....
01/02/2022

This is the excerpt for your very first post....

This is the excerpt for your very first post.

Somo letu linakichwa kinacho semaIMARISHA UTU WAKO WA NDANI ILI UISHI KATIKA MAJIRA NA NYAKATI ZA MUNGU KWAKO hebu tuang...
29/01/2022

Somo letu linakichwa kinacho semaIMARISHA UTU WAKO WA NDANI ILI UISHI KATIKA MAJIRA NA NYAKATI ZA MUNGU KWAKO hebu tuangalie mistari hii pamoja na mimi inayosema Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.2 Wakorintho 5:17 Unapo soma mistari hii unaweza kuona namna biblia inavyoelezea jambo moja muhimu hapa kuwa Mtu anapo kuwa ndani ya Kristo anakuwa kiumbe kipya na ili kuona k**a kuna upya biblia inasema Tazama/chunguza k**a ya kale yamepita au la, maana yake k**a ya kale hayajapita bado hujawa kiumbe/mtu mpya…...

Somo letu linakichwa kinacho semaIMARISHA UTU WAKO WA NDANI ILI UISHI KATIKA MAJIRA NA NYAKATI ZA MUNGU KWAKO hebu tuangalie mistari hii pamoja na mimi inayosema Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kr…

Address

Dodoma
Mbeya
41209

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mgao Remmy posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Mgao Remmy:

Share