29/06/2026
KIJA MPUNZI AFUNGA PINGU ZA MAISHA
Mtangazaji Mahiri wa Hope Channel Tanzania,Awr Tanznia na Rock Fm radio Ndugu Kija Mpunzi amefunga pingu za maisha na Vumilia Kasili..
Tukio hili takatifu limefanyika tarehe 28/07/2026 Jijini Arusha.
Mch.Dr .David Mpwani mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista wa sabato Union ya kaskazini mwa Tanzania alitangaza rasmi kuwa Kija Mpunzi na Vumilia ni Mke na mume.Tukio hili linafunga na kufungua ukurasa mpya kwa vijana hawa ambao Mungu amewapatia kibali cha kumtumikia ndani ya kanisa la Waadventista wa Sabato.
Sisi watumishi wa Hope Channel Tanzania Awr Tanzania na Rock Fm tunaungana kwa pamoja na Maelfu ya wana jamii wanaokupongeza na Kukuombea heri, amani na upendo kwenye ndoa yenu.