01/09/2026
Mkuu wa Jimbo la la Mlimba, KKKT Dayosisi ya Ulanga Kilombero, Mchg. Piana Mwenda akiweka wakfu vifaa vya kuwekea mishumaa madhabahuni pamoja na vitambaa vya ibada za Jumuiya, vilivyotolewa na Jumuiya ya Meta.
Jumuiya ya Meta walitoa vyombo vya kuwekea mishumaa madhabahuni kwaajili ya matumizi ya ibada usharikani na pia vitambaa vya ibada za jumuiya kwaajili ya kuwekwa wakfu tayari kwa matumizi ya ibada.
Haya yalifanyika kwenye Ibada ya Jumapili tarehe 30/08/2026, Siku ya Bwana ya 13 Baada ya Utatu.
Mchungaji Mwenda aliambatana na Kwaya ya Uinjilisti usharika wa Ruaha waliotembelea usharika wa Forest katika siku hiyo ya Jumapili.