27/10/2024
ADUI HUTUMIA VIFUNGO VYA KIROHO K**A SIRAHA YA KUTUKANDAMIZA
Vifungo vya kiroho vina vyanzo vyake ambavyo huusiana na;
1. Vizazi tulivyo toka , vifungo hivi vinakandamiza maeneo yafuatayo katika maisha ya mtu
Ndoa, Elimu, Familia, Afya, na Uchumi.
2. Vifungo vinavyo tokana na eneo au mji
3. Vifungo vinavyo tokana na Nguvu za giza, utenda kazi katika biashara huletwa na waganga na wachawi . Vifungo hivi tutavishinda kwa kutumia jina na damu ya yesu.
MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA KATIKA VITA VYA KIROHO
1. Sio kila wakati ni vita , vita vina mda wake Luka 22:53. Lazima uelewe ni wakati gani kuzimu inapambana na wewe Luka 4:13. Watu wengi wanashambulia katika mda wasiodhani 1Wathesalonike 5:3
Kushinda vita vya kiroho kunahitaji
Ufahamu wako, Hekima, na Nguvu ndani yako
SIRAHA AMBAZO SHETANI HUTUMIA KUTUSHAMBULIA
Maneno, Rungu ( kukata tamaa), Shetani hutushambulia kutokana na matajio tulionao Mithali 13:12, na Udhaifu wako, ni mlango mkubwa ambao shetani anatumia kukushambulia hiyo tambua udhaifu wako.
SILAHA ZA KUZITUMIA KUSHINDA VITA VYA KIROHO
1. UPENDO, Warumi 12:21
2.AMANI, Yohana 14:27
3. UVUMILIVU
4. UTII
5.IMANI 1Yohana 5:4
6. MATOLEO
SUNDAY SERVICE
Mch LUSAJO HEZRONE