Wiseman Tanzania Ministries

Wiseman Tanzania Ministries VISION

Loving God, Loving People, Loving Life

MISSION STATEMENT

To reach and influence the world by building a large Christ-centered, Bible-based family

SALAMU ZA MWISHO WA MWEZI JULAI NA MWANZO WA MWEZI AGOSTIShalom wapendwa katika Kristo Yesu!Tunamshukuru Mungu kwa kutuv...
31/07/2026

SALAMU ZA MWISHO WA MWEZI JULAI NA MWANZO WA MWEZI AGOSTI

Shalom wapendwa katika Kristo Yesu!

Tunamshukuru Mungu kwa kutuvusha salama mpaka mwisho wa mwezi Julai. Ni kwa neema na rehema zake tumeendelea kusimama, si kwa nguvu zetu bali kwa wema wake usio na mwisho.

Tunapoingia mwezi mpya wa Agosti, na tuingie kwa imani, matumaini na shukrani, tukiamini kuwa Mungu ametutangulia na ametuwekea mema. Mwezi huu uwe mwezi wa kufunguliwa milango mipya, ushindi, uponyaji, urejesho, mafanikio na kutimia kwa ahadi za Mungu katika maisha yetu.

MAOMBI

Baba, katika Jina la Yesu Kristo, tunakushukuru kwa kutuvusha salama katika mwezi wa Julai. Asante kwa ulinzi wako, rehema zako na upendo wako uliotudumisha kila siku.

Baba, katika Jina la Yesu, tunaweka mwezi wa Agosti mikononi mwako. Ututangulie katika kila hatua, fungua milango ambayo hakuna mwanadamu anayeweza kuifunga, na ufunge milango yote ya adui dhidi ya maisha yetu.

Baba, katika Jina la Yesu, tunaomba afya njema, amani, neema, hekima, mafanikio, ulinzi na baraka zako zitufuate katika mwezi huu mpya. Ondoa kila mpango wa shetani na utupe ushindi katika kila eneo la maisha yetu.

Baba, katika Jina la Yesu, tunatangaza kuwa mwezi wa Agosti utakuwa mwezi wa ushuhuda, mwezi wa kuinuliwa, mwezi wa mavuno na mwezi wa kuona mkono wako wenye nguvu ukitenda makuu katika maisha yetu.

Tunapokea yote haya kwa imani, katika Jina kuu la Yesu Kristo.

Amina!

Maandiko ya kusimama nayo mwezi wa Agosti

- Isaya 43:19 – "Tazama, nitatenda neno jipya..."
- Yeremia 29:11 – "Maana nayajua mawazo ninayowawazia..."
- Zaburi 121:7-8 – "Bwana atakulinda na mabaya yote..."
- Kumbukumbu la Torati 28:13 – "Bwana atakufanya kuwa kichwa wala si mkia..."
- Wafilipi 4:19 – "Na Mungu wangu atawajaza kila mnachohitaji..."
- Warumi 8:37 – "Lakini katika mambo hayo yote tunashinda kabisa...

23/07/2026
AMEFUFUKA! Jiwe lilitolewa, kaburi halikuweza kumshikilia na tumaini lilirejeshwa kwa wanadamu wote. Alichoahidi Mungu, ...
05/04/2026

AMEFUFUKA! Jiwe lilitolewa, kaburi halikuweza kumshikilia na tumaini lilirejeshwa kwa wanadamu wote.

Alichoahidi Mungu, alikitimiza.

Kilichoonekana kuwa mwisho haukuwa mwisho wake ,

Leo tunaishi katika ukweli wa ushindi wake kwa imani kwa sasa, na kutumaini yale yajayo.

📖 Mathayo 28:5-10

09/12/2025

MUNGU ANANIWAZIA MEMA: SEHEMU YA KWANZA (1)
katika somo letu tunaendelea na tafakari mbali mbali katika kitabu chetu cha YEREMIA 29:11, Endelea kujifunza nasi na Pastor Wiseman

08/12/2025

MUNGU ANANIWAZIA MEMA: SEHEMU YA KWANZA (1).
Karibu katika utangulizi wa somo letu la kinabii mwezi disemba, Na pastor Wiseman.

Address

Sae
Mbeya

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Telephone

+255736237329

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wiseman Tanzania Ministries posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Wiseman Tanzania Ministries:

Share