06/11/2022
JE WEWE UNAAMINI AU KUPINGA JUU YA UTATU?
U T A N G U L I Z I
Shalom ninyi mpendwao na mbingu, ninamshikuru Mungu Kwa jitihada unayoitumia kuutafuta ukweli. Katika mada hii tutazungumzia jinsi watu wengi wanavyoamini juu ya MUNGU MMOJA, hoja ambayo imeleta maswali mengi mno Kwa watu wengi.
Na kwasababu hiyo, nimeona watu wamekuwa na mashaka na uelewa finyu juu ya UUNGU WA YESU, NA ROHO MTAKATIFU.
Kabla sijaenda mbele niseme Kuwa SI FUNDISHO LA BIBLIA KUWA MUNGU NDIYE HUYO HUYO ROHO, NDIYE HUYO HUYO YESU YAANI NI MMOJA ANAYEJIGEUZA KULINGANA NA MAZINGIRA,
kwamba hapo nyuma alijifunua k**a Baba Aliyewatoa Israel Misri na kuiongoza nchi ya Israel (yaani kipindi Cha agano la kale) baadaye akaja akabadilika Kuwa mwanadamu yaani akawa Mwana na badaye yaani Sasa hivi amegeuka na Kuwa Roho Mtakatifu, LA HASHA MAANDIKO MATAKATIFU HAYAFUNDISHI HIVYO
Sasa baada ya kusoma vitabu kadha, nimekuja kufahamu baadhi ya mambo ambayo pengine, wapo baadhi ya watu ambao wanayatetea wakidhani kuwa wapo sahihi, na wengine wakiwaona hao wanayoyatetea kuwa hawapo sahihi.
Suala la utatu limekuwa pasua kichwa kwa watu wengi sana, na wengi miongoni mwetu tumekuwa tukitetea suala la utatu na kumbe namna tunavyoamini (kati yetu) msingi wake ni fundisho lililotoka kwa wakatoliki. Chukua utulivu, na umwombe Mungu sana ili yeye ajifunue kwako, na si hisia zetu zitawale. Ukisoma mpaka mwisho utanielewa maana yangu, maana pengine k**a haujasoma mpaka mwisho unaweza kufikiri kinyume na hatimaye ukawa na uelewa ulio kinyume na mtazamo wa maandiko matakatifu.
S E H E M U Y A K W A N Z A
JE UKATOLIKI UNAAMINI NINI JUU YA UTATU?
Ukatoliki wa Kirumi unafundisha kwamba Mwana anatoka kwa Baba na Roho Mtakatifu hutoka kwa Baba na Mwana: — na bado kuna Mungu mmoja tu! Hakuna Mwana bila Baba na hakuna Roho Mtakatifu bila ya Baba na Mwana. Kwa kiasi kikubwa, mizizi ya fundisho la Arianism (INAYOAMINI KUWA KRISTO SI WA MILELE) na Roho Mtakatifu asiyejitegemea {yaani anayemilikiwa na Baba na Mwana}, mafundisho yote yanapata chanzo chao katika fundisho hili la kipekee.
Ajabu ni kwamba, kuna wale miongoni mwetu leo ambao wanafundisha na kupinga dhana ya Utatu, wao hufundisha kwamba kuna nafsi moja tu ambayo ni ya milele Mungu! Mbali na Mungu huyo mmoja, hakuna Kristo wa milele na wala hakuna Roho Mtakatifu anayejitokeza kwa kujitenga k**a nafsi inayojitegemea. (IKIWA UNAAMINI HIVI, BASI UJUE KUWA IMANI YAKO NI CHANZO CHAKE NI UKATOLIKI)
Neno, trinitas, kwa mara ya kwanza lilitumiwa katika karne ya pili na watertullian; lakini fundisho hilo halikuundwa hadi karne ya nne.
Hapa chini Kuna nukuu 21 za namna wakatoliki wanavyoamini juu ya utatu, ingawa hatutazitazama na kuzimaliza zote
NUKUU ZA NAMNA WAKATOLIKI WANAVYOAMINI JUU YA UTATU MTAKATIFU
1. RC, WANAAMINI KUWA YESU SI SAWA NA BABA
👉 "Katika utbibitisho wa madai kwamba wengi wa mababa Wanakana usawa wa mwana pamoja na Baba, vifungu vimenukuliwa kutoka Justin (Apol., I, xiii, ###ii), Irenaeus (Adv. haer., III,viii, n. 3), Clem. Alex. (“Strom.” VII, ii), Hippolytus ( Con.Noet., 14), Origen (Con. Cels., VIII, xv).”—The Catholic Encyclopedia, 1914 Edition, art. “The Blessed Trinity.”
👆👆👆
Ikiwa unaamini Hivyo, kwamba Yesu hayupo sawa na Baba, Imani Yako ni ya kikatoliki
2. RC WANAAMINI KUWA: MWANA ALIUMBWA—“Maelezo ambayo yana taarifa kwamba Mwana aliumbwa hupatikana katika Clement wa Alexandria (Strom., V, xiv; VI, vii), Tatian (Orat., v), Tertullian (A’Adv. Prax.’ vi; ‘Adv. Hermong.’, xviii, xx), Origen (In Joan., I, n. 22).”— Ibid.
👆👆👆
Ikiwa unakubali fundisho kwamba Kristo hajawahi kutokea tangu milele, WEWE NI MKATOLIKI MZURI. Jihadharini na makosa unayokubali kutoka kwa tabaka la walimu walio miongoni mwetu]
3.RC WANAAMINI KUWA: ROHO NI PUMZI YA KRISTO TU—“Inaeleweka katika mwanga wa Yohana 20:22 ambapo Kristo, akawatokea Mitume, akawavuvia na akawapa Roho Mtakatifu. Yeye {Roho Mtakatifu} ni pumzi ya Kristo (John Damascene, ‘Fid. orth.’, 1, viii), breathed by Him [Christ] into us (Cyril of Alexandria, ‘Thesaurus’; cf.Petav., ‘De Trin’, V, vii).”—Ibid.
4. RC WANAAMINI KUWA: KILA MKATOLIKI MWEMA LAZIMA AKUBALI KWAMBA ROHO MTAKATIFU ANATOKA KWA BABA NA MWANA,(YAANI NI PUMZI YA YESU NA BABA) NA SI NAFSI INAYOJITEGEMEA HANA KUWEPO TOFAUTI “Yeye [Roho Mtakatifu] huendelea, si kwa njia ya kizazi, bali Kwa maongozi, kutoka kwa Baba na Mwana Pamoja. Hayo ndiyo matakwa ya imani ya Imani ya Kikatoliki.”— The Catholic Encyclopedia, 1914 Edition, art. “Holy Ghost.”
👆👆👆
[K**A UNAKUBALI KUFUNDISHA KWAMBA ROHO MTAKATIFU SI NAFSI INAYOJITEGEMEA, NAFSI YA TATU YA UUNGU, WEWE NI MKATOLIKI MZURI. Jihadharini na makosa unayokubali kutoka kwa tabaka la walimu walio miongoni mwetu]
5. RC WANAAMINI KUWA: Mbali na Mungu, Roho Mtakatifu hajiwezi; yaani, Yeye hana nafsi inayojitegemea— “St. Gre Gory Thaumaturgus, au angalau Ekthesis tes pisteos, Ambayo kwa kawaida inahusishwa naye, inatupa hiki Kifungu cha ajabu (P.G., X, 933 sq.): ‘Mungu ni mmoja, Baba wa Neno lililo hai, la Hekima idumuyo. Bwana mmoja, mmoja wa mmoja, Mungu wa Mungu, asiyeonekana wa visivyoonekana…. Mmoja wa Roho Mtakatifu, akiwa na riziki Yake (akitegemea ufadhili) Kutoka kwa Mungu. . Utatu Mkamilifu, ambao katika umilele, utukufu, Na nguvu, hazigawanyiki, wala hazitenganishwi . . Utatu unaobadilika usiobadilika.” IBD
FUMBO HILI NDIYO FUNDISHO KUU LA IMANI YA KIKATOLIKI — “Fumbo la Utatu ni kiini cha Mafundisho ya imani ya Kikatoliki. Juu yake ni msingi wa mafundisho mengine yote ya Kanisa.” — St.Augustine (De Trin., lib.V, c. xiv, in P.L., XLII, 921), p. 16
Huu hapa ni muhtasari wa yale tuliyojifunza Katika sura hii: Ingawa wanatheolojia Wakatoliki wanazungumza Kuhusu “Nafsi tatu” katika Utatu wao, kwa hakika hawafundishi kuhusu nafsi tatu! Mwana ni kitu Fulani ambacho Mungu Anaendelea kuvumbua kutokana na “akili” yake mwenyewe (kinaitwa “kizazi cha milele”). Wote wawili wanapumua, kitu kinachoitwa “Roho Mtakatifu” ambacho si nafsi shirika tena. Ni udhihirisho tu wa “matakwa” ya Mungu. Kwa karne nyingi, wanatheolojia Wakatoliki hatua kwa hatua wamekuwa wakiunganisha Dhana za kipagani pamoja na tafsiri potofu ya Maandiko kuwasilishia ulimwengu maajabu ya uzuri Bandia wa ile kweli:
1. Mwana ambaye wakati wote hutoka kwa Baba. [yaani si kamili bila baba]
2. Roho Mtakatifu, ambaye si nafsi inayojitegemea, lakini hutolewa (kupumuliwa, au ni pumzi inayotoka kwa Baba na Mwana
3. Mwana ambaye ana maisha machache kuliko asili yake Na ni sehemu tu ya mchanganyiko wa “asili moja.”
Ni NDANI ya theolojia ya Kikatoliki ya Kirumi kwamba tunapata mbegu ya makosa ya kisasa KWAMBA Kristo alikuwa na mwanzo na si wa milele, na Roho Mtakatifu hayupo kabisa. Je, hivi ndivyo unavyotaka kuamini? makosa yanatokana na makuhani wa Kikatoliki au Biblia/Roho ya Unabii yenye ukweli kwamba Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni tofauti na ni nafsi ambazo zimejitenga kikamilifu, watakatifu kabisa, na kamili milele? "
KARIBU SEHEMU YA PILI AMBAPO NITACHAMBUA KWA KINA KUHUSU NAMNA AMBAVYO AYA YA WAKOLOSAI NA MITHALI ZINA YOTAFSIRIWA VIBAYA KUHUSU UUMBWAJI WA YESU