08/06/2026
YESU KRISTO NI MSHAURI WA AJABU.
Hallelujah!
Ukisoma biblia katika kitabu cha Isaya 9:6 kinasema hivi;
"Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani."
Ukisoma vizuri mstari huo hapo juu mtoto anaye ongelewa hapo ni Bwana wetu Yesu kristo ambaye jina lake moja wapo ni mshauri wa ajabu.
Ukiangalia kwa makini maisha yetu ya Kila siku yamejaa changamoto nyingi sana ambazo kwa namna ya kibinadamu huwa ni ngumu kuzitatua, wakati mwingine huwa tunaangaika kwa wanadamu wenzetu ili watushauri namna ya kuzitatua changamoto zetu lakini tunijikuta Bado tunakwama.
Sina maana ya kwamba ni vibaya kupokea ushauri kwa watu ila kabla ya kuomba ushauri kwa watu muombe kwanza Bwana wetu Yesu kristo maana yeye ni mshauri wa ajabu anaweza kukushauri vizuri namna ya kutatua changamoto yako.