FREDY MWANYUMBA

FREDY MWANYUMBA page hii ni kwaajili ya neno la mungu.hivyo inahitajika msaada wenu ku like na ku share ili kwa pamoja tupate kulijua neno na kulijadiri kwa pamoja

PRAY FOR MOROGORO
10/08/2019

PRAY FOR MOROGORO

29/09/2016

USINGIZI WA KIROHO

Mtumishi Gasper Madumla

Bwana Yesu asifiwe…

Kuna mambo mengi sana yanatokea tunapokuwa tumelala kiroho.Adui huamka tunapokuwa tumelala.
Dhumuni la adui ni kuharibu,
kwa kuiba kile tulichopewa na Bwana Mungu,maana kile tulichopewa na Mungu ni kitu chema sana

*Hivyo kunam-badilishano usio wa halali tunapokuwa tumelala kiroho.Ubadilishano huu ni wa kutumia nguvu za giza/nguvu za kimapepo(A demonic change)

*Wakristo wengi leo wamebadilishiwa vitu au mambo yao ya thamani walipokuwa wamelala pasipo kujijua.Siku ya leo nataka uyajue haya,na tunaanzia kwa andiko hili;

Tunasoma 1 Wafalme 3:19-20;
“ Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia.
Akaondoka kati ya usiku,
akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu.”

*Katika andiko hilo, tunaona habari za wanawake wawili makahaba. Ambao walikuwa wakiishi nyumba moja.Wote wawili wakafanikiwa kuzaa watoto,baada ya kuzaa,mmoja wapo alimlalia mtoto hata kufa nyakati za USIKU.

Biblia inatuambia wakati wa usiku ndipo pakatokea UBADILISHANO/EXCHANGE baina ya mtoto aliyekufa kwa mtoto asiyekufa(1 Wafalme 3:20)

• Mbadilishano/exchange huo ulitokea nyakati za usiku wakati mama wa mtoto asiyekufa alipobadishiwa mtoto wake na kupewa mtoto aliyekufa.

Hivi ndivyo adui afanyavyo wakati tunapokuwa tumelala,
-anajaribu kukuchukulia mtoto wako aliye hai na kukupa aliyekufa,
-anajaribu kukubadilishia Ndoa yako aliyo hai,na kukupa iliyokufa,
-anajaribu kukubadilishia kazi yako nzuri na kukupa mbaya,
-anajaribu kuondoa kizazi kilichowekwa na Mungu ndani yako,na kukupa UTASA.N.K

• Adui ni muongo siku zote,akitaka ukubaliane naye kirahisi kwa kukubadilishia kitu kizuri kwa kitu kibaya.

*Mungu hajakupatia kitu kinyonge,
*Mungu hajakupatia Ndoa yenye matatizo,
*Mungu hajakupatia kazi yenye misukosuko,
*Mungu hajakupatia afya ya magonjwa,
*Mungu hajakupatia kuishi katika umasikini,BALI ADUI NDIYE ALIKUBADILISHIA NYAKATI ZA USIKU ULIPOKUWA UMELALA USINGIZI WA KIROHO.

Haleluya…
Jina la Bwana lisifiwe…

Tazama andiko hilo vizuri (1 Wafalme 3:16-20),
utagundua kwamba haikuwa rahisi kwa mama yule aliyebadilishiwa mtoto wake,maana watoto wote walikuwa ni wachanga mno.

Hivyo adui akapata mwanya wa kutaka kumlazimisha yule mama akubali kumchukua mtoto ambaye si wake,ambaye ni maiti.

Na ndivyo Adui afanyavyo kwetu sisi tunapokuwa tumelala katika usingizi wa kiroho,yeye adui hutulazimisha kukubaliana naye kwa mazingira aliyoyaandaa yeye,akijua kwamba itakuwa si rahisi sisi kugundua.

Sasa angalia;
1 Wafalme 3 :21
“ Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa.”
Neno linaposema,

“Nilipoondoka asubuhi…” Hapa maana yake ni kwamba ASUBUHI ni mahali ambapo pana MWANGA wa kutosha,ambao ulimfanya yule mama aliyebadilishiwa mtoto wake kumtambua kwa haraka alipomtizama sana.

Sasa Bwana Yesu Kristo ndiye asubuhi yetu,Yeye Yesu Kristo ndiye MWANGA wetu unaotupa kutambua UBADILISHAONO HUO ULIOFANYIKA USIKU.

Kwa maana nyingine ni kwamba yule mama aliyebadilishiwa mtoto wake,hasingeweza kumtambua mtoto wake nyakati za USIKU,
Hivyo alihitaji mwanga ili aweze kumtizama vizuri mtoto wake,kisha amtambue.

Vivyo hivyo sisi wenyewe hatuna UWEZO wa kutambua mambo yetu yaliyobadilishwa katika ulimwengu wa roho pasipo kuwepo NURU,ambayo hiyo NURU ndiye Yesu Kristo.

Ninaomba usikose fundisho hili,Maana nitakapomalizia nitafanya maombezi kwako
Mawasiliano yangu ni 0655-111149 (gasper madumla)

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.

21/09/2015
13/09/2015

(ZABURI 119:105 NENO LAKO NI TAA YA MIGUU YANGU NA MWANGAZA WA NJIA ZANGU) OMBI LANGU KWA MUNGU SHETANI ASIWEZE KUKUTAPISHA KILE CHAKULA CHA KIROHO ULICHO SHIRIKI KTK IBADA YA LEO YAANI NENO LA LEO AMINA

07/09/2015

k**a kuna mwanafunzi alijiandikishiaga chuoni na wakati wa kupiga kura atakuwa kwao lingine aende kwa mkurugenzi au ofisi ya kata/wilaya aliyopo sasa ili wambadilishie taarifa zake ili aweze kupiga kura sehemu aliyopo:- sambaza ujumbe huu kwa wanafunzi wa chuo na rafiki zako kwenye magroup.

05/09/2015

NAWAPENDA KTK UPENDO WA KRISTO USIKU MWEMA NA MUNGU AWE NANYI(Pia kumbuka kuombea TANZANIA yetu)

03/09/2015

CHANZO CHA NA UMOJA
Je ! Umewahi kufanya maombi juu ya hitaji lo lote ulilonalo bila mafanikio? Inawezekana umeugua, na umeomba uponyaji kwa Mungu lakini hali ya ugonjwa haibadiliki.
Inawezekana ya kuwa umeomba kwa Mungu ili Ndugu yako, mume wako au mke wako, au watoto wako waokoke. Na unashangaa kwa nini maombi yako hayajajibiwa.
Inawezekana ya kuwa umekuwa ukiomba juu ya mahitaji yako ya fedha lakini unaona siku zinapita na fedha haziji; badala yake unazidi kuingia katika madeni.
Ni kweli kabisa ya kwamba maombi yasipojibiwa, huleta hali ya kukata tamaa. Na Yesu Kristo mwenyewe alifahamu ya kuwa hali ya namna hii itakuja kutokea.
Kwa hiyo akasema; “Imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaa” (Luka 18:1)
Yesu Kristo aliyasema maneno haya akijua kabisa ya kuwa ni tabia ya Baba yake ambaye ni Baba yetu pia kujibu maombi ya watoto wake (Mathayo 7:7-11, 1Yohana 16:14; Yohana 16:23,24).
Je! Maombi ya Yesu Yamejibiwa?
Ukiangalia hali ya Mwili wa Kristo, yaani kanisa au hali ya wakristo unajaribiwa kutaka kusema maombi ya Yesu aliyotuombea umoja hayajajibiwa.
Hebu tafakari jinsi ambavyo faraka na chuki zinavyozidi katikati ya watu wa Mungu.
Kuna vikundi vingi sana vya wakristo ambavyo havipatani. Na pia kuna madhehebu mengi ya Kikristo ambayo hayapatani. Na pia kuna wakristo wengi sana ambao hawapatani, na hata kutoongea pamoja, wala kutembeleana wala kuomba pamoja.
Hali hii ni ya kusikitisha sana. Na pia ni hali inayotutia aibu. Na zaidi ya yote hali hii ya kutokuwa na umoja, inalichafua na kuliaibisha jina la Bwana.
Kwa sababu ya kukosa umoja katika huduma mbali mbali za kazi ya Bwana, watumishi wengi wameingia katika kushindana wala siyo kushirikiana. Kushindana huleta kiburi, kushirikiana ni matokeo ya kunyenyekeana.
Angalia, pamoja na mashindano, ubinafsi hujitokeza. Na palipo na ushirikiano, umoja hujitokeza. Mwili wa Kristo umeumbwa ukiwa na viungo vinavyotakiwa kushirikiana na wala si kushindana.
Huduma za Roho na Karama zake zimewekwa katika Kanisa au ndani ya wakristo ili kushirikiana na kufaidiana. Maana imeandikwa hivi:
“Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja; hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana,” (1Wakoritho 12:4-7).
Ikiwa ni hivi, mbona hali hii imefikiwa vizuri kati ya wakristo waliozaliwa mara ya pili huku wakiwa na Roho Mtakatifu aletaye umoja?
Je! tunaweza kusema maombi ya Bwana Yesu aliyotuombea umoja hayajajibiwa? Na k**a hayajajibiwa yatajibiwa lini? Na k**a yamejibiwa, mbona basi umoja huo hatuuoni?
Lakini nataka nikuambie ya kwamba maombi yote ya Bwana Yesu aliyokwisha kumwomba Baba, yamejibiwa. Tatizo liko kwetu, kwa kuwa hatujajua jinsi ya kupokea majibu ya maombi hayo.
Kumbuka Yesu Kristo aliwahi kumwambia Baba yake pale penye kaburi la Lazaro ya kuwa:
“Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya Mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.” (Yohana 11:41,42).
Na pia asingetuambia tulitumie jina lake na damu yake katika maombi k**a asingekuwa na uhakika ya kuwa ana kibali machoni pa Baba yake, na huwa anasikilizwa.
Ikiwa maombi ya Bwana Yesu aliyotuombea juu ya umoja yamejibiwa, basi tunatakiwa kuuona umoja katikati ya wakristo.
Lakini hali ilivyo na inavyoonekana sasa, umoja huo tulioombewa hauonekani. Wakristo wengi mahali mbali mbali duniani wametafuta kila namna ya njia ya kuleta umoja wa kweli bila mafanikio.
Hata injili haihubiriwi kwa nguvu, na kwa umoja k**a inavyotakiwa kwa sababu tu ya kukosa kushirikiana katika kuifanya kazi ya Bwana. Kila mtu au kikundi au dhehebu, linataka kufanya kazi hiyo peke yake. Ushirikiano ukiwapo mara nyingi ni wa maeneo machache, na wa muda mfupi tu.
Nini chanzo cha kutokuwa na umoja kati ya watu wa Mungu?
Je! Umewahi kujiuliza swali la namna hii? Ile tu kwamba unasoma somo hili, inamaanisha una haja na hamu ya rohoni ya kuona wote k**a wakristo tunasimama katika umoja.
Na ili tuweze kulitatua tatizo la kutokuwa na umoja, ni budi tujue chanzo cha tatizo lenyewe. Watu wengi wamekuwa wakijitahidi kutatua tatizo la kutokuwa na umoja kati ya wakristo bila ya kutambua kiini cha tatizo lenyewe. Na matokeo yake ni juhudi hizo kukosa matunda ya kudumu.
Dhambi ndiyo chanzo cha kukosa umoja
Unaweza ukamsingizia mwenzako au kikundi cha watu ya kuwa ndiyo chanzo cha kukosa umoja mahali ulipo. Hii si kweli, kwa kuwa chanzo cha kutokuwa na umoja katikati ya watu wa Mungu ni dhambi.
Vurugu, faraka, chuki na unafiki unaoonekana kati ya wakristo ni matokeo tu ya dhambi iliyokwisha ingia katikati yao.
Kumbuka ya kuwa unasoma somo hili si kwa sababu ni bahati yako au unajifurahisha; bali unasoma kwa kuwa Roho Mtakatifu ana makusudi na wewe kukutumia mahali ulipo. Utumiwe na Roho Mtakatifu kusimamisha umoja na wala si kuleta ugomvi na chuki.
Dhambi ni kitu gani?
Biblia inatuambia ya kuwa; “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.” (1Yohana 3:4)
Dhambi ni uasi. Ni kuasi maagizo ya Mungu. Ni kumuasi Mungu.
Dhambi ni kuenenda nje ya Neno la Mungu kwa kuwa imeandikwa “Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi”. (Warumi 14:23) Na kumbuka kuwa chanzo cha imani ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo (Warumi 10:17)
Umoja wa Kristo hauletwi na juhudi za wakristo. Umoja wa kikristo huletwa na Kristo mwenyewe aliye kichwa, kwa uweza wa Roho wake.
“Naye (Kristo) amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote HUSHIKANA katika yeye”. (Wakolosai 1:17)
“Maana k**a vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo. Kwa maana katika Roho mmoja sis sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani, ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.” (1Wakorintho 12:12-13)
Ikiwa ni hivi basi kitu gani kinatutenga na uwepo huu wa Mungu ndani ya Kristo katika Roho?
Biblia inatupa jibu inaposema, dhambi hututenga na uso wa Mungu.
“Tazama mkono wa Bwana haukupunguka, hata asiweze kuokoa; wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake usiuone hata hataki kusikia”. (Isaya 59:12)
Jambo hili la dhambi kututenga na uso wa Mungu limekuwa dhahiri tangu mwanadamu alipoumbwa.
Dhambi huleta utengano
K*tengwa na uso wa Mungu maana yake ni kutengwa na Kristo, kwa kuwa Kristo ndiye sura ya Mungu (2 Wakorintho 4:3,4).
“Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea ambao ndani yao Mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura ya Mungu.”
K*tengwa na uso wa Mungu ni kutengwa na sura ya Mungu. Kwa kuwa Kristo ni sura ya Mungu, basi kutengwa na sura ya Mungu ni kutengwa na uso wa Kristo ambaye ni sura ya Mungu.
Na kwa kuwa kila kitu hushik**ana katika Kristo, (Wakolosai 1:17) basi Kristo asipokuwepo mshik**ano au umoja hupotea.
Na biblia inatueleza ya kuwa dhambi hututenga na uso wa Mungu. Kwa hiyo dhambi huondoa uwepo wa uso wa Kristo katikati ya wakristo. Wakristo wanakuwa ni kwa majina tu, kwa kuwa sura ya maisha yao haimuonyeshi Kristo alivyo.
Hii hutokea kwa kuwa wanamwabudu Mungu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali naye.
Dhambi ni giza, na Nuru ni Kristo. Nuru ikitoka mahali, giza huingia.
Na muda si mwingi, utengano hutokea na kutokuwa na umoja kunakuwa dhahiri.
Labda umekuwa ukijiuliza kwa nini kikundi chenu cha maombi hakina umoja tena, mnagawanyika wala hamwaminiani tena. Na kwa sababu hiyo maombi yenu hayana nguvu. Je! hujui sababu ya hali hiyo? Sasa, nakuambia, funguka macho uone; kuna dhambi iliyoingia katikati yenu, na giza limewafunika.
Na giza likikufunika, maono ya kazi ya Mungu yanapotea. Na pia unakuwa huna uhakika na unachokifanya. Hata wewe mwenyewe unaanza kutokujiamini, hatimaye kupoa kiroho kunakukumba!
Kuna wakati fulani tulikuwa tunafanya maandalizi ya mkutano wa kiroho, uliokuwa uhahusisha wakristo wa madhehebu mbali mbali; Basi, kuna wakristo wa dhehebu fulani ambao walisema hawawezi kuomba pamoja kwa kuwa walikuwa hawaelewani kwa muda mrefu.
Hali ya namna hii ni ya kusikitisha sana.
Ngoja nikuulize swali: Je: Usipopatana na mkristo mwenzako hapa duniani unategemea kuwa mkifika mbinguni ndipo mpatane?
Yesu, Kristo alikufa msalabani akiwa DUNIANI na si mbinguni ili tuweze kupatanishwa na Mungu hapa hapa duniani – kabla ya kwenda mbinguni.
Biblia inasema kila alitajaye jina la Bwana, na auache uovu. Na kutokupatana na mkristo mwenzako au kutokuwa na Umoja na mkristo mwenzako ni uovu! Kwa hiyo kila alitajaye jina la Bwana na apatane na mwenzake.
Ndiyo maana imeandikwa; “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao.” (Waebrania 12:14)
Dhambi hutawanya Wakristo
Kitu gani kilichotokea wakati dhambi au uasi ulipoingia katikati ya wanafunzi wa kwanza kumi na wawili wa Kristo.
Kuna mambo muhimu hapa ambayo nataka tuyaangalie kwa makini kwa kuwa yatatusaidia kuweza kujua dhambi inavyoharibu umoja wa wakristo hasa katika huduma.
Dhambi ilipoingia katikati ya wanafunzi wa kwanza wa Kristo mambo yafuatayo yalitokea:
1. Shetani aliingilia kikundi chao kwa kumpitia mtu mmoja ambaye ni Yuda.
2. Usaliti uliingia; walimsaliti Yesu
3. Roho ya mauti iliwatembelea na kuondoka na mtu mmoja.
4. Wanafunzi walichukua hatua ya kumkana Yesu Kristo mbele za watu
5. Wanafunzi walimkimbia Yesu Kristo na kutawanyika.
6. Wito wa kumfuata Yesu na kuwa wavuvi wa watu ulipoa; na wakazirudia kazi zao za zamani ambazo walikuwa wanazifanya kabla ya Yesu kuwaita.
7. Waliingiwa na hofu na kukosa ujasiri.
Hawa wanafunzi ni wale ambao Yesu Kristo aliwatembelea mara kwa mara. Na pia walitembea na kuishi pamoja naye.
Na ndiyo hawa alioanza kuwaambia ya kuwa wamepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu. Walimwona Kristo akitenda miujiza, na wao pia walishiriki kuitenda.
Tena aliwahi kuwaambia ya kuwa amewapa mamlaka juu ya nguvu za shetani wala hakuna kitu ambacho kingewazuru (Luka 10:19).
Na vile vile hawa aliwaombea umoja na ya kuwa walindwe na yule mwovu.
Na uwezo wa Mungu ulidhihirishwa waziwazi kwao, na hakika walifahamu ya kuwa Yesu Kristo, ni Masihi na Mwana wa Mungu aliyetumwa.
Kwa kuona yote hayo inashangaza kuona jinsi ambavyo dhambi ilivyoweza kupenya katikati yao na kuwafanya wamsaliti na kumkana Yesu na kisha kutawanyika.
Ingawa walimuahidi Yesu kuwa hawatamwacha hata k**a watapata shida, inaonekana wazi ya kuwa hawakuweza kuitimiza ahadi hiyo wakati Yesu alipok**atwa.
Hali ya namna hii imelikumba Kanisa wakati huu pamoja na vikundi vyake mbali mbali vya huduma.
Ukiangalia hali ya makusanyiko au vikundi vya maombi, huduma au madhehebu ya Kikristo inasikitisha.
Ni jambo la kawaida siku hizi kusikia na kuona magomvi yakitokea kati ya wakristo kwa wakristo.
Je! umewahi kujiuliza kwa nini umekata tamaa kuendelea kuhudhuria katika maombi na kufanya huduma na wenzako?
Je! Umewahi kujiuliza kwa nini wenzako fulani na baadhi ya watumishi wamerudi nyuma kiroho?
Je! Umewahi kujiuliza kwa nini vikundi vingi vimekosa ujasiri wa kutoka nje na kuhubiri badala yake wanajifungia ndani wakiomba kila mara?
Je! Umewahi kujiuliza kwa nini baadhi ya madhehebu ya Kikristo yamefarakana? Je! Unashangaa kuona wakristo wanasalitiana, wanakufa kiroho, wanakata tamaa, hawashirikiani, wametawanyika, na wengi kupoteza wito wao?
Sikiliza sasa jambo hili ambalo Roho wa Kristo analiambia kanisa; sikiliza jambo hili ambalo Roho wa Kristo anasema na wewe.
FUNGUKA MACHO UONE NA UFAHAMU kuwa kuna dhambi iliyo kati yenu.
Na kwa ajili hii uwepo wa Bwana umeondoka na mmebaki na mahangaiko.
Tazama tamaa ya Yuda ilivyotawanya kikundi cha wanafunzi wa kwanza na Yesu aliondoka kati yao hadi alipofufuka. Basi hata siku hizi kuna watu walio na tamaa mbaya walio katikati ya vikundi vya kiroho na ndani ya madhehebu. Na kwa kuwa hawataki kujionyesha na kwa kuwapitia wao shetani ameingilia vikundi vya kiroho.
Dhambi huondoa ushindi
Jambo mojawapo tunalohitaji kujifunza ni kwamba, katika vita vya kiroho usitegemee ushindi k**a Mungu hapigani upande wako.
Siri ya ushindi wa mkristo katika maisha ya kila siku ni uwepo na matumizi ya nguvu za Mungu zilizo ndani yake katika Kristo Yesu.
Ndiyo maana imeandikwa;
“Lakini katika mambo hayo yote tunashinda na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.” (Warumi 8:37)
Na tunashinda kwa kuwa tunaye Kristo ndani yetu na kati yetu, ambaye ni mshindi wa yote na katika yote.
Na jambo hili linakuwa dhahiri tunaposoma maneno haya;
“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” (Wafilipi 4:13)
Kwa hiyo nuru ya Kristo inapoondoka ndani yako kwa sababu ya kuasi kwako, giza huingia, na ushindi uliokuwa nao mwanzoni unapotea. Na utaona majaribu yakija huwezi kuyashinda k**a zamani, bali sasa yatakuangusha.
Na fahamu ya kuwa dhambi inayokuingia kwa siri, pia huondoa nguvu za Mungu ndani yako kwa siri. Utatambua kuwa Mungu hayuko pamoja na wewe utakapokwenda vitani au kazini na kushindwa kufanikiwa.
Hili ndilo lililomtokea Yoshua na wana wa Israeli, walipotaka kuuteka mji wa Ai.
Baada ya kupata mafanikio mazuri na ushindi kwa kuuteka na kuuangamiza mji wa Yeriko, Yoshua alituma baadhi ya askari wake ili wauteke mji wa Ai.
Askari hawa wa Israeli walipokwenda kwenye Mji wa Ai. Yaliwapata yafuatayo:-
1. Vita hiyo walipigwa na walishindwa mbele ya adui zao (Yoshua 7:5)
2. Wana wa Israeli walikimbia na kuwapa visogo adui zao (Yoshua 7:4)
3. Baada ya kushindwa kusonga mbele katika kuteka miji kuelekea Kaanani askari wa Israeli walikata tamaa ya kusonga mbele, na wakaingiwa na hofu (Yoshua 7:5) Sasa, nataka nikuulize maswali wewe unayesoma haya.
Je! Huwa unafanya nini unapoona wakristo unaowaongoza au wanaookuzunguka wakipigwa na kushindwa na hila za shetani?
Je! Huwa unafanya nini unapowaona wakristo wenzako wakikata tamaa kuendelea na wokovu kwa sababu ya kukabiliwa na majaribu?
Ni lazima uwe na majibu ya maswali haya. Kumbuka unawajibika kwa Mungu juu ya roho za watu aliokukabidhi. Ngoja nikuulize swali jingine.
Je! Huwa unachukua hatu gani unapoona ya kuwa katika kikundi chako nguvu za kiroho zimepungua na hata magonjwa na mapepo yana wachezea? Na wakati mwingine kushindwa kuandaa mikutano ya kiroho na huduma zingine za kiroho?
Je unaamua kukaa kimya na kuwaacha wakristo wapambane wenyewe?
Je! Joshua aliposikia habari za kupigwa na kukimbia kwa askari wake mbele za adui alichukua hatua gani?
Biblia inatuambia ya kwamba, “Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Bwana hata jioni, yeye na wazee wa Israeli wakatia mavumbi vichwani mwao” (Yoshua 7:6).
Kwa nini walifanya hivyo? Ni ili wapate kumuuliza Bwana Mungu wao kwa nini wameshindwa (Yoshua 7:7-9)
Na Mungu alimjibu Yoshua.
Na wakati ambapo Roho wa Mungu aliniwezesha kuona kwa jinsi ya rohoni hali mbaya ya mafarakano kati ya wakristo au wale waliookoka na hasara zake, nilipata mzigo na uchungu mkali wa rohoni.
Niliazimia kufunga na kuomba kwa ajili ya kumuuliza Bwana juu ya hali na chanzo cha mafarakano yaliyopo kati ya wakristo, na kule kukosa umoja wa kweli.

02/09/2015

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU BALI JAWABU LA ULIMI HUTOKA KWA BWANA MITHALI (16:1) NI WAKATI MZURI WA KUSEMA NA BWANA HAJA ZA MOYO WAKO NI KIPINDI CHA UCHAGUZI NI VYEMA UKAPOTEZA MUDA NA WAKATI WAKO KWAAJILI YA KUOMBEA NCHI YAKO NAJUA UNA MENGI YA KUOMBA LAKINI NCHI ISIPO KUA NA AMANI UTAFURAHIA VIPI AYO UNAYOOMBA? ANZA NA MSINGI KWANZA MENGINE YATAFUATA MAOMBI YAKO NI MUHIMU SANA ILI KWA PAMOJA TUSUBIRI JAWABU LA ULIMI KUTOKA KWA BWANA NA MUNGU AKUBARIKI AMINA

01/09/2015

MUENDELEZO WA SOMO LA NAMNA YA KUOMBA BY ASKOFU MWAKASEGE NILI WEKA PAGE MOJA KATI YA PAGE NNE NAMALIZIA PAGE TATU ZILIZO SALIA NA SOMO LETU LITAISHIA APO KAA TAYARI KWA SOMO LINGINE NA MUNGU AKUBARIKI WAWEZA KU COMENT POPOTE UNAPOHISI HAPAELEWEKI AMA KUNA LOLOTE ILI TUWEZE KUWEKANA SAWA SOMO JEMA-----Mweleze Mungu haja zako. Ongea na Mungu kwa uwazi na ukweli. Japo
anazijua haja zetu, lakini ameagiza kuwa tumwombe ndipo atafanya.
‘aombaye hupokea’ yaani; asiyeomba, hapati. Mungu anasema tumpelekee
hoja zenye nguvu (Isa 41:21). Omba vitu vizuri na mambo makubwa ili
upewe (pray for good things and big things)
5.FANYA MAOMBI YA VITA VYA ROHONI. *Efe 6:10-13 *2Kor 10:3-5
Baada ya kumwendea Mungu na kumweleza mahitaji yako, sasa simama k**a ‘mfalme’,
kwasababu wewe ni ‘mfalme’ (Ufu 5:8), tumia mamlaka yako ya kifalme, ongea na
hali/hitaji ulilokuwa unaliombea, na kwa mamlaka, amuru iwe k**a vile
ulivyoomba/unavyotamani. Ndio maana Bwana Yesu alipokabidhiwa mamlaka yote na
Mungu, naye akatukabidhi sisi (kanisa lake) “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga
nyoka na nge na nguvu zote za yule adui. Wala hakuna kitakachowadhuru” (Luk 10:19,
Yer 1:10, Yak 4:7). Tuma neno lenye mamlaka katika hali/jambo ulilokuwa unaliombea,
Amuru iwe vile ulivyokuwa unamwomba Mungu iwe. Kemea kila roho ya shetani
inayoweza kuwa inasababisha tatizo katika swala lako.
6.OMBEA ULINZI JUU YA ULIYOYAOMBEA. *Math 6:13a
Baada ya kupiga vita vya kiroho, weka ulinzi katika yale uliyoyaombea, ili shetani na
mapepo yake wasiweze kuirudia hali/jambo/mtu yule uliyemkomboa kwa maombi ya
vita. Yesu alisema shetani akifukuzwa mahali, haendi mbali, anasubiri kuona k**a
atapata upenyo wa kuparudia mahali pale alipokuwa kwanza. (Math 12:43-45). Kwahiyo,
usipoweka ulinzi, kuna uwezekano wa adui kurudi na kuliharibu zaidi lile jambo
uliloliombea na kulipata.
Kumbuka, unapoomba vizuri, unapokea papo hapo (katika ulimwengu wa roho), lakini
udhihirisho wake katika ulimwengu wa mwili, unaweza kuchukua muda fulani. Hivyo
katika muda huo wa kusubiri, shetani anaweza akapita na kuzuia au kuharibu kile
unachokisubiri kidhihirike katika ulimwengu wa mwili. Ndio maana Yesu alitufundisha
kuombea ulinzi, “tuokoe na yule mwovu” (Math 6:13a). Weka ulinzi juu ya mambo yako
yote. Jengea wigo wa moto wa mbinguni (2Fal 6:16-17), Yafunike kwa damu ya Yesu na
agiza malaika walinzi walinde mambo yako masaa yote. Omba hivyo kila siku. (Zab
34:7, Zab 91:9-11, Ebr 1:13-14)
MSIFU, MWABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Math 6:13b
Yesu alianza maombi kwa kumsifu Mungu na kumtukuza. Na ak**aliza maombi yake
kwa kumtukuza Mungu tena. Akasema “kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu ni zako,
sasa na hata milele” ak**aliza. Kwahiyo nawe kwa kumaliza maombi yako, msifu na
kumshukuru Mungu tena, kwa ukuu wake, uaminifu wake, na ahadi zake juu yetu. Ndipo
ufunge maombi yako.
MUHIMU: TUMIA MAANDIKO KATIKA KUOMBA *Kol 3:16
-Katika kuomba kwako, mara zote tumia maandiko kumkumbusha Mungu ahadi zake .(Isa
43:26). Mungu analiangalia neno lake ili alitimize. Sababu pekee itakayomfanya Mungu
akupe alichoomba, ni ili kulitimiza neno lake. Hivyo, baada ya kumweleza unachohitaji
(kwa ajili yako au kwa ajili ya mtu unayemwombea) mpe Mungu andiko/neno lake
linalokupa wewe uhalali wa kuomba hicho kitu mbele zake na kupewa.
-Hata unapompinga na kumkemea shetani, baada ya kutoa amri yako dhidi yake, shetani
atasubiri kusikia andiko/neno linalomnyima yeye uhalali wa kushika alichoshika. Ndio maana
Yesu alimshinda shetani kwa neno la Mungu. Alisema “imeandikwa” na shetani akashindwa.
“Nao wakmshinda (shetani) kwa damu ya Yesu na kwa Neno” (Ufu 12:11)
MBINU ZA KUKUSAIDIA KUOMBA VIZURI KWA MUDA MREFU
1. CHAGUA MAHALI PAZURI PA UTULIVU. *Mk 1:35
ili uweze kuomba kwa utulivu na kwa umakini, chagua au tafuta mahali pazuri
patakapokupa utulivu katika kuomba (concentration in prayer). Ndio maana Mungu
alipenda kuongea na Musa juu ya mlima. (K*t 24:12-18). Hata Yesu alizoea kwenda
kuombea mlimani, mahali palipo mbali na vurugu za watu, alipenda kwenda
mlimani.
(Math 14:22-23). Tafuta mahali patulivu; chumbani, kanisani, mlimani (Math 6:5-6)
2. CHAGUA MUDA MZURI. *Mhu 3:1,7
Ili uweze kuomba kwa umakini mzuri, chagua muda mzuri ambao akili yako ma mwili
wako viko fresh. Usilazimishe kuomba hata k**a akili yako au mwili wako
umechoka sana. Kila jambo lina wakati wake. K**a umechoka sana, huo si muda
wa kuomba, bali wa kupumzika. Usilazimishe ratiba. ni bora upumzike ili baadaye
uweze kuomba vizuri baadaye. Usije ukajikuta unamkemea Yesu badala shetani.
Penda kuomba wakati una nguvu ya akili na mwili, ili uwe makini kuongea na
Mungu kwa akili timamu. Ndio maana Yesu alipenda kuamka alfajiri sana kwenda
kuomba mlimani. (Mk 1:35, Luka 4:42)
3. OMBA KATIKA ROHO (NENA KWA LUGHA). *Efe 6:18, Rum 8:26-27
Mbinu nyingine nzuri ya kuomba kwa muda mrefu na kwa ufanisi, ni kuomba kwa
Roho; yaani kuomba kwa kunena kwa lugha. Tunapoomba kwa akili za kibinadamu,
Mungu anasikia pia, lakini maombi yako yanakuwa na mipaka / limited kwasababu
akili ya mtu haijui kila kitu. Bali Roho wa Mungu anajua kila kitu. Naye hutupa
kipawa cha kuomba kwa lugha ya mbinguni iliyo bora zaidi. (Yuda 1:20, Mk 16:17,
1Kor 14:1-4, 15-16,7)
4. OMBA KWA KUFUNGA WAKATI MWINGINE. *Math 6:16-18
Kufunga kula kunasaidia kudhoofisha mwili, ili roho iwe makini zaidi kuongea na
Mungu kwa kina zaidi. Mwili huu siku zote haupendi kufanya mambo ya Mungu.
Na mwili ukiwa umeshiba, unakuwa na uchovu na uzito wa kufanya mambo ya
kiroho. Mbinu mojawapo ya kuudhibiti, ni kuunyima/kuupunguzia posho yake ya
chakula. Mwili ukidhoofika kiasi, roho yako inapata nguvu na upenyo mzuri zaidi
(Zab 35:13). Mashujaa wote wa imani walifunga na kuomba. Ndio maana Yesu
anasema ‘mfungapo’ akimaanisha ratiba ya kufunga, ipo. Inasaidia.
5. OMBA NA RAFIKI (PRAYER PARTNER). *Mhu 4:9-10
Neno la Mungu linasema, ni heri wawili kuliko mmoja. Kuna faida ya kuomba
pamoja na rafiki yako. Kwanza, mnapokuwa wawili au watatu, inaleta hamasa na
ari ya kuomba zaidi. Si rahisi kujisikia mvivu unapokuwa na waombaji wenzako.
Pili; nguvu ya kiroho inaongezeka. Neno linasema, mwombaji mmoja anafukuza
adui elfu moja, bali wakiwa wawili, wanafukuza (sio elfu mbili) bali elfu kumi!
Shangaa! (Kumb 32:20) Hiyo ni kanuni ya mbinguni/kanuni ya Ki-Mungu. Kadri
mnavyoongezeka, nguvu ya Mungu huongezeka.
Kwahiyo, wakati mwingine, omba na rafiki yako, unayemwamini, unayeweza
kumshirikisha mambo yako ya binafsi. Mashujaa wengi wa imani, walikuwa na
marafiki wa kiroho. (Prayer Partners). Kwa Mfano:- Math 17:1-9
Musa - alikuwa na Joshua, Haruni na Huri
Eliya - alikuwa na Elisha
Daniel - alikuwa na Shadrack, Meshack na Abednego.
Yesu - alikuwa na Petro, Yakobo na Yohana.
Paul - alikuwa na Barnaba, Timotheo na Tito.
Wewe Je? Uko na nani katika urafiki wa kiroho?
K**a huna rafiki wa karibu wa kuomba naye, usikurupuke kujichaglia. Tulia
umwombe Mungu akupe mtu atakayekuwa wa msaada kwako. Mtu
mtakayefungamanishwa naye katika roho, hata k**a mmetengana kijiografia,
lakini katika roho, mko na umoja mzuri wa imani. (Math 18:18-19)
6. OMBA KATIKA MKAO UNAOKUPA UHURU NA NGUVU ZAIDI.
Katika kuomba kwa muda mrefu, mkao uliouzoea utakusaidia kwenda mwendo
mrefu. Yakupasa kujua nguvu yako na udhaifu wako (strong point and weak point).
Wakati wa kuomba, epuka mikao inayokuchosha haraka na tumia mikao inayokua
nguvu zaidi. Kwa Mfano:- Ukiwa umechoka, usipende kuomba kwa kupiga magoti
au kwa kuegemea kitandani. Ni bora uombe ukiwa umesimama au unatembea
tembea, ili kuepuka usingizi na uchovu. Waombaji hodari wanaujua mikao
inayowasaidia kuomba maombi marefu. Wengine hawana mikao maalum, bali
wakiwa katika maombi, huwa wanabadilisha-badilisha mikao ili wasichoke. Hiyo ni
mbinu nzuri pia.
Mifano ya Mashujaa wa imani;
Ibrahim – aliomba kwa kusimama (Mwa 18:22)
Daniel - aliomba kwa kupiga magoti (Dan 6:10)
Paul - aliomba kwa kupiga magoti (Efe 3:14)
Yesu - aliomba kwa kulala chini (Math 26:38-39)
Eliya - aliomba kwa kukaa chini na
kuweka kichwa kati ya miguu (1Fal 18:42)
Mimi - huwa napenda kuomba kwa kutembea tembea
Naweza kumaliza kilomita nyingi chumbani kwangu
Nikitembea huku nikiomba.
Wewe Je? Unaujua mkao wa nguvu? K**a hujui, Tafuta kujua.
OMBA NA MUZIKI LAINI KWA KUMWABUDU MUNGU.
Muziki wa kiroho, na wataratibu, unaweza kukutengenezea mazingira mazuri sana
ya kuomba kwa muda mrefu. Muziki wa kuabudu, unavuta uwepo wa Mungu kwa
namna ya pekee. Neno linasema, waimbaji na wanamuziki walipoimba na muziki
ukapigwa, nao wakawa k**a mtu mmoja, utukufu wa Mungu ukashuka na kulijaza
lile hekalu hata makuhani hawakuweza tena kuhudumu (2Nyak 5:12-14). Kule
mbinguni, kila malaika wa sifa, ana kinubi (zeze/gitaa). Elisha hakutoa unabii,
mpaka mpiga kinubi alipopiga kwa ustadi, ndipo mkono wa Bwana (Roho wa
Mungu) alipokija juu yake, naye akatabiri.
Najaribu kukuonyesha, kuna connection kati ya muziki wa kiroho na utukufu wa Mungu.
Kwahiyo, ukiweza kuomba huku umeweka kanda au CD ya nyimbo za kiroho za taratibu,
utapata (experience) hamasa ya kiroho (motivation) na utasikia una nguvu ya kuomba kwa muda
mrefu. K**a unaweza, tengeneza kanda au CD maalum yenye nyimbo nzuri unazozipenda
wewe, ili uwe unaipiga wakati wa maombi. Utajikuta unaweza kuomba kwa muda mrefu na kwa
bubujiko zuri zaidi

31/08/2015

NAMNA YA KUOMBA BY ASKOFU MWAKASEGE
- Hatua na vipengele muhimu katika kuomba -
MKARIBISHE ROHO MTAKATIFU. *Rum 8:26-27 *Yoh 14:16-17
Yesu alisema Roho Mtakatifu ni msaidizi wetu. Atatusaidia na kutufundisha yote, kwa maana
pasipo yeye, sisi hatuwezi neno lolote. Na sisi peke yetu hatujui kuomba ipasavyo, bali yeye
(Roho) ajua kutuombea kwa Mungu k**a vile Mungu apendavyo. Hivyo kabla ya kuanza
maombi au kusoma neno au ibada au safari au mitihani au kikao n.k. jifunze kujikabidhi kwa
Roho Mtakatifu, uombe msaada wake, akupe ufanisi/ubora katika yote yakupasayo kufanya.
Tambua Utu wake, Uungu na Uweza wake.
Jikabidhi katika Nguvu ya Uongozi wake.
Tii kila Uongozi anaokupa.
FANYA TOBA NA UTAKASO. *Isa 59:1-2, Yoh 9:31, 1Yoh 1:8-9,7
Sikio la Bwana si zito kusikia wala mkono wake si mfupi kushindwa kututendea mambo
tumwombayo, bali maovu yetu ndiyo yanatufarakanisha na Mungu wetu. Mungu
hawasikii wenye dhambi. Hivyo chukua muda wa kutafakari na kuungama dhambi zako
mbele za Mungu na kuzitubu kwa kumaanisha kuziacha. Mungu ni mwaminifu
kutusamehe na kututakasa na uchafu wote. (Isa 1:18). Lakini, kabla hujafanya toba yako
binfsi;
(i) - Kwanza, samehe wote waliokukosea, hata k**a hawajaja
kukuomba msamaha. Usipowasamehe waliokukosea, na Mungu
hataweza kukusamehe wewe. (Math 6:12,14-15)
(ii) - Ndipo nawe ufanye toba yako binafsi. Na Mungu atakusamehe kabisa.
Hata k**a ni nyekundu sana, zitakuwa nyeupe sana. (Isa 1:18, Isa 43:25)
3.MSIFU, MUABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Zab 147 na Zab 148
Msifu Bwana kwa Matendo yake makuu, mwabudu Bwana kwa uzuri wake na kwa sifa
zake. Mwadhimishe Mungu kwa Tabia zake, wema wake, fadhili zake na baraka zake
mbalimbali anazotutendea. Sifa yako ikifika vizuri mbele za Mungu, ndipo atakuwa
tayari kukupa haja za moyo wako. Haja zetu zimefichwa nyuma ya mgomgo wa sifa.
Ndio maana Neno linasema;
‘Nawe utajifurahisha kwa Bwana (kwa kumsifu, kumwabudu na kumshukuru), naye
atakupa
haja za moyo wako’ (Zab37:4).
Yesu anatuonyesha mfano; angalia sentensi yake ya kwanza katika kuomba kwake
imekuwa “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.” (Math 6:9). Anaanza maombi
kwa kumsifu Mungu. Msifu Mungu kwa kuimba na kwa kunena/kusema/kuelezea.
Mungu anataka kusifiwa na kutukuzwa. Ukifanya sifa nzuri, ya kuufurahisha moyo wake,
atakupa hata na vile ambavyo hukutegemea/hukuomba.
4.MWELEZE MUNGU MAHITAJI NA HOJA ZAKO. *Wafilipi 4:6-7,19 Isa 43:26
Mweleze Mungu zile hoja zilizokusukumwa kwenda kumwomba. Nenda mbele za
Mungu k**a ‘kuhani’ (1Pet 2:9). Kwa unyenyekevu na heshima. Lakini kabla ya
kumweleza mahitaji yako binafsi;
(i)Kwanza fanya ‘maombezi’ – ombea watu wengine; (1Tim 2:1-4)
Viongozi mbalimbali na wenye mamlaka, watumishi wa Mungu, marafiki
zako, wenye shida, ndugu zako, nchi yako, shule yako, shirika lenu, ofisi
yenu, chama chenu, n.k. Usianze kujiombea mwenyewe tuu, zoea
kuwatanguliza wengine.
(ii)Kisha fanya ‘maombi yako’– ombea haja za moyo wako. (Math 7:7-11)

Address

AIRPORT MWANJELWA
Mbeya

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when FREDY MWANYUMBA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to FREDY MWANYUMBA:

Share