02/03/2023
Madhabahu ya Maarifa ya Neno la Mungu- Mbeya Tanzania:
SEMINA YA WAZAZI KWAAJILI YA MAISHA YA WATOTO.
Waebrania 2:13
Siku ya Kwanza:
Kristo Yesu atukuzwe mwana wa Mungu karibu katika Semina hii ambayo Wazazi tunapokea Maarifa ya Neno la Mungu kuhusu kuwaombea watoto wetu mbele za Mungu. Sikiliza somo hili Kwa Sauti AUDIO VOICE kupitia LINK hii ya group la Telegram https://t.me/+YkJw-aXXKXDohkt_
MASWALI YA KUJIULIZA K**A WAZAZI KWAAJILI YA MAISHA YA WATOTO WENU MLIONAO KATIKA FAMILIA.
Kuna maswali ambayo nataka sisi k**a Wazazi tuweze kujiuliza ambayo yanagusa maisha ya watoto wenu tulionao katika Familia.
SWALI LA KWANZA:
Je msingi wa kuoana kwetu na kuzaa kwetu watoto ulikuwa unasimamiwa na mungu yupi rohoni?.
Ruthu 4:13 Isaya 8:3 Zaburi 11:3 1Wakorintho 3:10-11
🔶 Wakati nyie Wazazi mnaoana ni mungu yupi rohoni aliwapngoza kuoana? Na wakati mnazaa watoto ni mungu yupi alihusika katika kuzaa kwenu watoto? Kwenye ulimwengu wa roho Mungu katika Yesu Kristo na Shetani/miungu wanahusika sana katika kuoana Kwa wanadamu na kuzaa watoto Kwa wanadamu.
Kuna msingi ambao Wazazi waliutengeneza walipokuwa wanaoana na kuzaa watoto ambao Leo umekuwa sababishi la matatizo Kwa watoto wao. K**a Mungu katika Yesu Kristo hashirikishwi katika eneo la kuoana na kuzaa watoto mnatengeneza tatizo kubwa rohoni kwaajili ya maisha ya watoto wenu mtakaokuwa nao katika familia yenu.
Mungu ndiye mwanzilishi wa Familia hivyo vijana wawili wanapotaka kuoana lazima wamshirikishe Mungu Kwa asilimia zote pia Kwa kuwa watoto tunapewa na Mungu hawa waliooana wanapotaka watoto kwenye Ndoa Yao ni lazima wamshirikishe Mungu Kwa asilimia zote pia katika jambo hili
Ila sivyo ilivyo wanadamu wengi wanapotaka kuoana wanamuweka Mungu pembeni na kujiamulia wao wenyewe kuoa/kuolewa na hata wakitaka watoto kwenye Ndoa Yao Mungu anawekwa pembeni ndio hapo unawakuta Wana ndoa wanaenda Kwa waganga wa kienyeji kutafuta watoto au wanaenda kwenye makaburi Kuomba wapate watoto na wengine wakiwa na mimba wanatumia vitu vya uganga wa kienyeji na mtoto akizaliwa huwafunga hirizi na vitu vya kimila. Mambo haya yanawajenga watoto wao katika msingi mbovu ambao unakuja kuyaghalimu maisha ya watoto wao hapa duniani.
☑️ Biblia inasema Yesu Kristo ni Msingi kwahiyo watu wakioana lazima Ndoa Yao waijenge kwenye msingi wa Yesu Kristo kabla hawajazaa watoto na wakizaa watoto nao wajengwe katika msingi unaoitwa Yesu Kristo, Wazazi wakifanya hivyo wanasababisha watoto wao maisha Yao kuongozwa na msingi wa Yesu Kristo nao wataishi k**a Mungu alivyowaleta hapa duniani.
KIRI MAOMBI HAYA MZAZI:
Mungu katika Jina la Yesu Kristo sisi k**a Wazazi tunaomba Toba na rehema mbele zako kwaajili ya msingi mbovu tulioutumia katika kuoana kwetu na kuzaa kwetu watoto. Tunatangaza Kwa Jina la Yesu Kristo kuvunja Misingi yote mibovu ambayo inatumika kuwatesa watoto wetu katika maisha Yao hiyo Misingi ivunjike Kwa Jina la Yesu Kristo na kusambaratika kwenye maisha ya watoto wetu, na Leo tunakubali sisi Wazazi kuwajenga watoto wetu katika msingi wa Yesu Kristo Ili maisha Yao Yawe juu ya huu msingi wa Yesu Kristo siku zao zote katika Jina la Yesu Kristo tunaomba na kuamini Amen.
SWALI LA PILI:
Je ile madhabahu tuliyoitumia kufungia Ndoa ilikuwa na vitu vya upande wa mungu yupi rohoni?.
Ezra 3:2 Ufunuo 2:13 Waamuzi 6:25-26
🔶 Kipindi kile Wazazi mlipofunga ndoa Ile madhabahu mliyoitumia kufungia Ndoa yenu ilikuwa na vitu vya upande wa mungu yupi rohoni? Inapofika saa ya kufunga Ndoa wahusika wanaofunga Ndoa hawaingii kwenye maombi kumuuliza Mungu waende kwenye madhabahu ya kanisa gani kufungia Ndoa yao wao wanachofurahia ni kufungishwa Ndoa na kuwa mume na mke na matokeo yake Kuna madhabahu watu walizitumia kufungia Ndoa zimepitisha vitu visivyofaa katika maisha ya watoto wao navyo vinawatesa sana.
Sikiliza sio Kila madhabahu inayoitwa ya kanisa Iko na vitu vya upande wa Mungu aliye hai Kuna madhabahu nyingi tu zinaitwa za makanisa Fulani lakini rohoni hazijabeba vitu vya Mungu katika Yesu Kristo bali vimebeba vitu vya miungu na kuzimu Sasa nyie mkienda kufunga Ndoa yenu katika Madhabahu ya namna hii iliyobeba vitu vya kuzimu ni lazima mtakuwa mmeiingiza Ndoa yenu kwenye mtego hatari sana na watoto wenu mtakaowazaa kwenye hiyo Ndoa watasumbuliwa kimaisha na vitu hivyo vya upande wa giza.
Na wachungaji wanaofungisha Ndoa hawawasaidii Kwa kina vijana wanaotaka kuoana bali wanachofurahia ni kuongeza idadi za ndoa zilizofungwa makanisani kwao na mwisho wa siku unazikuta hizo Ndoa zimekuwa za mateso na maumivu Kwa hao watu.
☑️ Madhabahu mnayoitumia kufungia Ndoa nataka ujue kuwa inabeba Hatima ya ndoa yenu na maisha yenu katika Familia, ndio maana vijana mnaotaka kuoana hili jambo msijaribu kulifanyia mchezo mchezo ni lazima mkae katika Maombi kumuomba Mungu awaongoze katika Madhabahu ya kanisa gani kuitumia kufungia Ndoa yenu lakini baada ya kufunga Ndoa mfanye tena maombi ya kuiunganisha Ndoa yenu na watoto wenu mtakaopewa na Mungu katika Familia yenu na madhabahu ya Mungu katika Yesu Kristo kupitia Damu yake.
🔶 Sasa nyie Wazazi Kuna jambo la kufanya kwenye maombi Kwa watoto wenu kuwatenganisha na vitu vyovyote vya giza mlivyovibeba kipindi kile mnafunga Ndoa kwenye madhabahu Ili k**a viko vinavyofanya kazi Kwa watoto wenu viharibike kwao.
KIRI MAOMBI HAYA MZAZI:
Mungu Baba sisi k**a Wazazi tunaomba toba Kwa Damu ya Yesu Kristo kwako kutokana na kutokukushirikisha na kupata muongozo wako wakati ule tulipofunga Ndoa kwenye madhabahu ya kanisa, leo tunatangaza Kwa Jina la Yesu Kristo vitu vyovyote vinavyofanya kazi kwenye maisha ya watoto wetu ambao havitoki kwenye madhabahu yako Mungu bali vinatoka upande wa giza tunaviharibu katika maisha ya watoto wenu Kwa Jina la Yesu Kristo na tunawatenganisha watoto wetu na vitu hivyo vya madhabahu za giza Kwa Damu ya Yesu Kristo na Sasa tunayafungua maisha ya watoto wenu kutoka kwenye vifungo vyote vya uharibifu kwa Jina la Yesu Kristo tunawatangazia watoto wenu wapate kuwa huru kabisa maishani mwao nasi tunatangaza madhabahu yako Mungu uliye hai Katika Yesu Kristo ndio itakayosimama na maisha ya watoto wenu Kila siku Kwa Jina la Yesu Kristo tunaomba na kuamini Amen.
SWALI LA TATU:
Je sisi k**a Wazazi hatujaweza kuua Hatima za watoto wetu za Maisha kupitia ibada za miungu migeni?.
Kutoka 20:3 2Falme 17:17 Waamuzi 5:8 Kumbukumbu la torati 29:26 Zaburi 106:37 1Samweli 1:27-28
🔶 Hili eneo Wazazi wengi wamehusika kuweza kuua Hatima za Maisha za watoto wao kutokana na ibada za miungu migeni walizozifanya na wanazozifanya maishani mwao. Nataka utambue wewe mzazi kwamba kitendo Cha nyie Wazazi mliopewa na Mungu watoto mnapoamua kumuacha Mungu aliye hai Katika Yesu Kristo kumwabudu na kumtumikia na kugeukia miungu migeni kuiabudu na kuitumia kinatoa uhalali Kwa kuzimu kuvamia maisha ya watoto wenu na kuua Hatima zao na kuzifunga Hatima zao na kuzibadilisha Hatima zao na kuzuia Hatima za Maisha ya watoto wenu.
❌ Wazazi wanapotumia vitu vya uganga wa kienyeji na ushirikina maishani mwao wanasababisha kuua Hatima za Maisha za watoto wao.
❌ Wazazi wanapowaleta waganga wa kienyeji majumbani kwao na katika familia Ili kuwaagua watoto au kuzindika nyumba zao kitendo hicho kinasababisha kuua Hatima za Maisha za watoto wao.
❌ Wazazi wanapoenda kutafuta dawa Kwa waganga wa kienyeji za kupata mimba au kwenda makaburini kuwaomba wafu Ili wapate ujauzito kitendo hicho kinasababisha kuua Hatima za Maisha za watoto wao.
❌ Wazazi wanapozaa watoto na wakawafunga vitu vya uganga wa kienyeji au vya kimila k**a hirizi na kamba n.k kitendo hicho kinasababisha kuua Hatima za Maisha za watoto wao.
❌ Wazazi wanapoenda kuchukua dawa za kufukiza Kwa waganga wa kienyeji na kuwafukizia watoto wao au kuchukua dawa za kunywa zinazotoka Kwa waganga wa kienyeji au watu wa kimila na kuwanywesha watoto wao kitendo hicho kinasababisha kuua Hatima za Maisha za watoto wao.
Mambo yoyote ambayo Biblia k**a katiba yetu sisi haijaweza kuyaagiza tuyafanye Kwa watoto wetu lakini Wazazi wakayafanya Kwa watoto wao haijalishi sababu ni nini walizonazo hao Wazazi mambo hayo yaliyo kinyume na Neno la Mungu Wazazi mkiwafanyia watoto wenu na mkiyafanya kwenye familia yenu mnafungulia mlango wenyewe Kwa kuzimu na Shetani na maadui kuua Hatima za Maisha za watoto wenu
Ndio maana Leo ukiwatazama watoto wengi hapa duniani Kwa jicho la kiroho unaona vitu vingi haviko sawasawa maishani mwao na kuzimu imewak**ata watoto wengi na kuwavuruga kimaisha kwasababu ya uhalali walioutuo Wazazi wao. Unapoona Leo watoto wengi hawana mwelekeo wa kimaisha ila wanaendeshwa na Kila upepo unaotokea hapa duniani ni ishara Kuna mambo kwenye ulimwengu wa roho hayako sawa kwenye maisha ya watoto wengi.
❌ Je nyie Wazazi mnaosoma somo hili hamjahusika kuua Hatima za Maisha za watoto wetu? Mungu amesema yeye mwenyewe ndiye anayepaswa kuabudiwa na kutumikiwa na kusujudiwa lakini Wazazi wanapomkataa huyu Mungu katika Yesu Kristo na kuamua kuiabudu na kuisujudia na kuitumikia miungu migeni mnasababisha Hatima za Maisha za watoto wenu kushambuliwa na kuzimu.
Hivyo nyie Wazazi mnatakiwa kuingia kwenye maombi ya Toba mbele za Mungu kutubu Kwa mambo yote mliyoyafanya Kwa watoto wenu ambayo yalikuwa kinyume na Neno la Mungu. Baada ya hapo muombe Ukombozi wa Damu ya Yesu Kristo na kufunguliwa Kwa watoto wenu Ili waweze kuishi maisha Yao halisi ya uumbaji wa Mungu.
KIRI MAOMBI HAYA MZAZI:
Mungu katika Yesu Kristo mioyo yetu sisi Wazazi inajutia kutokana na mambo tuliyoyafanya kwenye maisha ya watoto wetu uliotupatia katika ndoa na familia Leo sisi Wazazi tunakubali kutubu kwako Mungu na Kuomba rehema zako kutokana na ibada za miungu migeni tulizozifanya na zikafungua mlango wa uhalali kwa Shetani na kuzimu kufunga na kuua na kuharibu Hatima za Maisha za watoto wetu tunaomba utusamehe Kwa Damu ya Yesu Kristo
Na tunatangaza Kwa Jina la Yesu Kristo Kila roho za kuzimu na roho za kishetani zilizok**ata na kufunga Hatima za Maisha za watoto wenu Leo nazilipua Kwa moto wa Yesu Kristo hizo roho na kutangaza watoto wetu kutoka kwenye vifungo vyote vya kuzimu Kwa Jina la Yesu Kristo
Ninatangaza Damu ya Yesu Kristo iwakomboe watoto wetu na kuwafungua watoto wetu na Hatima zao za Maisha walizowekewa na Mungu kwaajili ya maisha Yao tunazikomboa na kuzifungua Kwa Damu ya Yesu Kristo, nami nakuomba Mungu Baba watoto hawa uliotupatia katika Familia uwaongoze wewe na kuwafikisha katika Hatima zao za Maisha ulizowapangia maishani mwao Kwa Jina la Yesu Kristo Asante Kwa kuwa Mungu kwenye enzi yote umefanya jambo Jipya katika maisha ya watoto wenu nao wako huru Kwa Damu ya Yesu Kristo Amen.
SWALI LA NNE:
Je ni maisha ya aina gani mnayoishi nyie k**a Wazazi? Kumbukeni maisha mnayoishi yanawaathili watoto wenu katika Wema au katika ubaya.
Mithali 20:7 Isaya 14:21 Yeremia 22:29-30,21 Hosea 2:4 Malaki 4:5-6 2Falme 4:1-7 Ezekieli 16:44-45 Luka 1:5-6
🔶 Wazazi nataka niwaambie ukweli maisha mnayoyaishi yanawaathili watoto wenu katika Wema au katika ubaya inategemea nyie Wazazi ambao Mungu amewapatia dhamana ya hao watoto Kila siku mnaishi maisha ya aina gani. Unajua wako Wazazi ambao wanajiamulia kuishi tu aina yoyote ya maisha bila kujua kuwa maisha Yao hayo kwenye ulimwengu wa roho yanawaathili sana watoto wao.
❌ Wazazi wakiishi maisha ya dhambi yanawaathili watoto wao kupata mashambulizi ya maadui.
❌ Wazazi wakiishi maisha ya uongo na utapeli na dhuluma yanawaathili watoto wao katika ubaya.
❌ Wazazi wakiishi maisha ya ulevi yanawaathili watoto wao katika ubaya.
❌ Wazazi wakiishi maisha ya wizi yanawaathili watoto wao katika ubaya.
Ni lazima Wazazi mjichunge sana kutokana na maisha mnayoishi na vitu mnavyofanya kwenye maisha yenu kwasababu mnaweza kuwaathili watoto wenu katika Wema au katika ubaya.
🔶 Wazazi wanatakiwa kuishi maisha ya kumwabudu Mungu na kumtumikia Mungu aliye hai Katika Yesu Kristo Ili Wema wa Mungu uonekane katika maisha ya watoto wao.
🔶 Wazazi wanatakiwa waishi maisha ya Haki na uaminifu na kusema ukweli na maisha ya utakatifu Ili Wema wa Mungu udhihirike kwenye maisha ya watoto wao.
☑️ K**a umeamua na Kukubali kuingia kwenye Ndoa na kuzaa watoto ni lazima ukubali KUGEUKA na KUBADILIKA na kuishi maisha yanayoendana na katiba yetu ambayo ni BIBLIA na chochote ambacho Neno la Mungu limekataza usijaribu kufanya kabisa na yote ambayo Neno la Mungu limeagiza uyafanye hakikisha unayafanya.
Usijaribu kuishi Kwa kujifurahisha wewe mwenyewe mzazi na kuwafurahisha marafiki zako na wanadamu wengine wakati maisha hayo wanaathilika watoto wako ni heri usingeingia kwenye Ndoa na kuwa na Familia.
❌ Je wewe mzazi unatoa muda wako Kuomba pamoja na watoto wako katika familia?
Ni AIBU sana mzazi unakosa muda wa kukaa na watoto wako na Familia Yako na Kuomba nao pamoja lakini unaona muda wa kukaa na marafiki zako kijiweni.
❌ Je wewe mzazi unaenda kanisani pamoja na watoto wako na Familia Yako siku za IBADA?
Kuna Wazazi muda wa kwenda Kanisani hawataki kuongozana na watoto wao na familia zao ila Yuko tayari aongozane na marafiki zake au muda huo akae tu nyumbani bila kwenda Kanisani hiyo ni AIBU sana na unatengeneza kitu kisichofaa mioyoni MWA watoto wako.
❌ Je wewe mzazi Kila siku unatoa muda wa kukaa na kuongea na watoto wako na kubadilishana nao mawazo?
Ni AIBU mzazi huna muda wa kukaa na watoto wako na Familia mkapiga story na kujadiliana nao mambo kadhaa na kuwasikiliza changamoto zao ila unao muda wa kukaa kwenye baa kunywa pombe na marafiki zako na unarudi nyumbani Usiku watoto wameshalala, unawatengenezea aina gani ya mtazamo watoto wako?
❌ Je wewe mzazi unao muda wa kukagua mahali wanapolala watoto wako?
❌ Je wewe mzazi unao muda wa kujua marafiki walio karibu na watoto wako?
❌ Je wewe mzazi unao muda wa kuchunguza chakula wanachokula watoto wako?
🔶 K**a umekubali kuwa Mzazi narudia tena kusema ni lazima ukubali kutengeneza kizazi Cha Watoto ambao Mungu akiwatazama kwenye familia yenu hakika hatajutia kuwapitisha hao watoto kwenye Ndoa yenu na Familia yenu.
Ni lazima Sasa tukubali sisi Wazazi KUBADILIKA na KUGEUKA Kuna mambo tuachane nayo hata k**a yanatupatia Furaha sisi tujiulize jambo hili ninalotaka kufanya Je kwenye maisha ya watoto wako litawaathili katika namna gani ya Wema au ubaya? K**a unaona jambo hilo litawaathili watoto wako na Familia Yako katika ubaya liache na usijaribu kulifanya hata k**a marafiki zako wanakusisitiza ulifanye litupilie mbali kabisa.
KIRI MAOMBI HAYA MZAZI:
Mungu Baba ulituamini sisi Wazazi Katia Ndoa yetu na kutupatia watoto lakini sisi tumesababisha kuwaharibu watoto uliotupa kutokana na mwenendo na tabia za Maisha yetu sisi Wazazi na matokeo yake tumeyaathili maisha ya watoto wetu katika ubaya na Kuna mambo wanayapitia watoto wetu kwenye maisha Yao chanzo ni sisi Kwa kuwa Neno lako linasema apandacho mtu ndicho atakachovuna tunaomba toba na rehema mbele zako Mungu kutokana na maisha yetu sisi Wazazi katika ndoa na familia Kwa Damu ya Yesu Kristo
Tunakubali sisi k**a Wazazi Ee Mungu uigeuze mioyo yetu ikuelekee wewe na kukuabudu wewe na kukutumikia wewe nasi tutembee katika njia za Haki na kufanya matendo yaliyo mema maishani mwenu Ili watoto wenu wajifunze mambo mazuri kutoka kwetu Wazazi sio wajifunze mambo mabaya kutoka kwetu nakuomba Mungu utubadilishe na kutugeuze Kwa Jina la Yesu Kristo
Na Leo nakuomba Mungu Baba watoto uliotupatia katika Ndoa na Familia yetu tunawainua katika Madhabahu Yako kitu chochote wanachokipitia maishani mwao ambacho kimetokana na tabia zetu sisi Wazazi kuanzia Sasa kiweze kuondoa na kuwaachilia watoto wetu Kwa Jina la Yesu Kristo. Tunakuomba Mungu Baba uliyetupatia hawa watoto katika Ndoa na Familia uyakague maisha Yao na chochote kinachozuia kusudi lako kwao kisitende kazi tena kwao Ili watoto hawa waweze kulitumikia kusudi lako na kazi uliyowaleta waifanye maishani mwao hapa duniani waweze kuifanya Kwa Jina la Yesu Kristo
Sisi k**a Wazazi tunayabariki maisha ya watoto wenu na ulinzi wako uwe pamoja nao na madhabahu yako Mungu izidi kuwahudumia Kila siku watoto wenu kwenye maisha Yao katika Jina kuu la Yesu Kristo tunaomba na kushukuru Amen.
☑️ Hayo yalikuwa maswali 4 ambayo sisi k**a Wazazi tumepewa na Roho wa Mungu tujiuliza kuhusu maisha ya watoto wetu katika familia. Endelea kukaa kwenye maombi mbele za Mungu kadiri Roho Mtakatifu anavyowaongoza na lifanyie kazi somo hili la semina ya Leo.
Tuungane tena kesho katika sehemu yetu ya siku ya Pili, nakuomba washirikishe Wazazi wengine masomo haya na wale wanaotarajia kuwa Wazazi washirikishe pia masomo haya. Wewe mzazi hakikisha unamshirikisha mwenzi wako masomo haya.
Pia Kwa kusikiliza masomo haya ingia kwenye hiyo LINK hapo juu ya group la Telegram nimefundisha na kufafanua zaidi maswali hayo 4 na masomo Kwa njia ya AUDIO VOICE Kila siku nayatuma ndani ya group ninapotoka kanisani hakikisha Kila Usiku unasikiliza masomo haya kabla hujalala.
🔶 Tunazo siku 12 za Semina hii ya Wazazi kuwaombea watoto naomba usikose semina hii kila siku kwasababu Kuna mambo mengi ya kutusaidia sisi Wazazi Mungu ameyaweka moyoni mwangu Ili tushirikishane na tuweze kupata Maarifa ya Neno lake.
NIKUANDAE KWAMBA KATIKA SEMINA HII TUTAKUWA NA SADAKA YA KUTOA MBELE ZA MUNGU KATIKA MADHABAHU YAKE KWAAJILI YA MAOMBI HAYA TUNAYOWAOMBEA WATOTO WETU ENDELEA KUJIANDAA NA KUMUULIZA ROHO MTAKATIFU KWAAJILI YA SADAKA HII.
Kwa mawasiliano nami na Kushiriki Baraka za Mungu Kwa njia ya Utoaji Sadaka zako tumia namba hii ya utumishi +255 765 867574 na Sadaka zako zitafika madhabahuni pa Mungu kwaajili ya kufanya kazi zake.
Mimi ni Mwalimu wa Neno la Mungu la Maarifa
Samwel Kibiriti.
March 02, 2023
Mbeya Tanzania.
Tuungane katika Semina ya siku ya kesho na tuzidi kuombeana.