03/11/2024
Bwana Yesu Asifiwe
Mimi pamoja na mke wangu Tunawasalimu kwa Jina Kubwa la Yesu Kristo
No 1
Somo tulilo nalo leo Ni mhimu saana Kila mtu aweze kulipitia kwasababu Ni somo ambalo lina sirii Nyingi Za ufalme wa Mbinguni, na namna shetani anaweza kukubana Kwenye Kipengele cha MAJIRA
SOMO
NAMNA SHETANI ANAWEZA KUKUFUNGA KWENYE NYAKATI NA MAJIRA ILII USIFANIKIWE KWA WAKATI
LUKA 19:41-44
[41]Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,
[42]akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.
[43]Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;
[44]watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.
👉 Alipouona Mji alianza kulia, Na ukisoma mistarii ya Nyuma kidogo utaona Yesu Wakati anawatuma wale wanafunzi wawili anawaambia Nendeni Mkamfungue mwana Punda, Na Baada ya wanafunzi kufanya hivyo Yesu aka panda yule mwana punda na alipopanda utaona Watu wa mjii wa Yerusalemu utaona namna walivyo Anza kushangilia na kupiga vigele gele na kutandika nguo zao chini ilii Yesu apite juu ya nguo zao Wakaanza kumuimbia na nyimbo kiujumla Wote walikuwa na furaha mnoo
Hadi mstarii wa 40 bado wanaimba nyimbo
Ghafla mstari wa 41
Yesu akaanza Kulia, na akatoa machozi
Sasa wametoka kwenye Furaha Alfu wale watu wa Yerusalem wanashangaa ghafla mtu anaanza Kulia
Na Sababu ya Yesu Kulia ni hii
Ni kwasababu Mjii HAUKUTAMBUA MAJIRA YA KUJILIWA
Sasa Cheki Ilionekana ni sababu ambayo haina mashiko kwa ule mjii wa Yerusalem
Na Biblia inazungumza wazi kabisa Yesu alizungumza Hata Wale watu aliokuwa nao Waliweza kusikia yale maneno
Na kwa wale watu ambao wanajua kufwatilia Wataona kuwa Ule Utabiri wa Yesu juu ya Mjii wa Yerusalem Ule Utabiri uliweza Kujitokeza Miaka 40 baadae ( 70 B.K)
WAKATI YERUSALEM ILIPO ANGAMIZWA NA JESHII LA KIRUMI NA MAELFU YA WAYAHUDI WALIUWAWA
Sasa angalia, watu hawa walikuwa na kosa moja Tu
KUTO TAMBUA MAJIRA YA KUJILIWA KWAO
Maana yake wangekuwa wanatambua majira ya kujiliwa kwao Wangeweza kujipanga, lakini hawakutambua majira
Ndio sababu Kuna Mambo unayapitia Leo ni kwasababu ya msimu uliopita Na Hukutambua majira ya kujiliwa kwako
-unapitia ni kwasababu hukujua uzuri au ubaya wa siku zijazo, Unaishi kwenye msimu mpya kwa kutegemea Majira ya Zamani
Ngoja nijaribu hii, Ukiwa Huna saa inayo kuongoza kuwa sasa hivii ni sangapii, Unaweza Zani Kila Mchana Ni Saa 6
Unaweza ishii kwa majira ya saa 6 wakati Sio saa 6 unakuta ni saa 8
Bado hujanielewa nasema hivii
Usitembee na historia ya mwaka jana ya kufeli, ukatembea nayo mwaka huu
Kwanini usitembee nayo? Ni kwasababu Jana Sio Leo
Ile kwamba Jana umeshindwa haina maana kwamba Na Leo utashindwa
Ilee kwamba Jana umelala na njaa haina maana Leo utalala na njaa
Kuna watu Mwaka Jana waliomba wapate mtoto na hawakupata Kwahyo hawaoni haja ya kuendelea kuomba tena eti kwasababu Jana hawakujibiwa,
Ngoja nikwambie huu ni wakati wako Wa Kujibiwa Maombi Yako Uliyo omba kwa muda mrefu
Kati ya kitu shetani anapambana nacho Kwenye Maisha ya Kila Mwanadamu ni hikii
SHETANI ANAPAMBANA NA MAJIRA NA NYAKATI ZILIZO BEBA MAJIBU YA MAOMBI YAKO YA MUDA MREFU Ndio maana Daniel aliona wakati wa kupokea majibu ya maombi yangu ni sasa kwahyo haijalishii k**a wakuu wa uajemi wameshikilia majibu yangu hapo juu ilaa mimi naomba mpaka majibu yapatikane, sio yapatikane kesho nataka yapatikane Leo
Nawewe pambana Mpaka majibu yapatikane Leo
K**a majibu yako yameshikiliwa kwa Jina La Yesu Yanaachiwa Leo
K**a ulikata Tamaa maana yake unamuachia Shetani ushindi Usikate Tamaa songa mbere na Bwana
Haijalishii umedhalauliwa Leo
Nasema Iko Kesho yako ya Kuheshimika na walio kudhalau
Iko siku yako ya heshima
Mungu akubarikii kwa kuendelea Kufwatilia Masomo Yetu,
SOMO HILII NI ENDELEVU HUU NI UTANGULIZI KWAHYO HAKIKISHA UNAFWATILIA KILA MUDA
KARIBU KWENYE GROUP LA WHATSAP
0742911147 TUMA MESEJI WHATSAP KUWA NIUNGE ntakuunga
Na page yetu ya Facebook Link yake hii hapa
Hakikisha una Like na Kutu Follow Ilii uwe wa kwanza kupata masomo Yetu
MT DANIELY SIAME
0742911147