13/04/2026
*KESHA LA ASUBUHI 2026*
_APRILI — MWITO WETU MKUU_
*JUMANNE, APRILI 14, 2026*
*_KAZI YA KULINDA MOYO_*
> *_Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. — Mithali 4:23._*
Bidii katika kuulinda moyo ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wenye afya katika neema. Moyo katika hali yake ya asili ni makao ya mawazo machafu na tamaa za dhambi. Unaposalimishwa kwa Kristo, lazima usafishwe na Roho Mtakatifu mbali na unajisi. Hili haliwezi kufanywa bila idhini ya mtu binafsi.
Roho inapokuwa imetakaswa, unabaki kuwa wajibu wa Mkristo kuulinda usinajisiwe. Wengi wanaonekana kufikiri kwamba dini ya Kristo haiwataki kuachana na dhambi za kila siku, kuachana na mazoea ambayo yameiweka roho katika utumwa. Wanakataa baadhi ya mambo yanayoshutumiwa na dhamiri, lakini wanashindwa kumwakilisha Kristo katika maisha ya kila siku. Hawaleti kufanana kwao na Kristo nyumbani. Hawaoneshi kujali kwa uangalifu katika uchaguzi wao wa maneno. Mara nyingi, maneno ya hasira, yasiyo na subira husemwa, maneno ambayo huchochea mawazo mabaya zaidi ya moyo wa mwanadamu. Watu k**a hao wanahitaji uwepo wa kudumu wa Kristo katika nafsi. Ni kwa nguvu Zake pekee ndipo wanaweza kuchunga maneno na matendo.
Katika kazi ya kuulinda moyo tunalazimika kuingia katika maombi papo hapo, pasipo kuchoka katika kuomba msaada toka kwenye kiti cha enzi cha neema.... Wale wanaobeba jina la Ukristo wanalazimika kumjia Mungu kwa bidii na unyenyekevu, wakiomba msaada.... Mkristo hawezi kila wakati kuwa katika mazingira ya maombi, bali mawazo na shauku zake zinaweza kuelekezwa juu daima.
*_Kuutunza moyo wako mbinguni kutakupatia nguvu katika neema zako na kuleta uhai katika majukumu yako yote. Kuifanya akili iweze kudumu katika kutafakari mambo ya mbinguni kutaleta uhai na bidii katika juhudi zetu zote. Juhudi zetu zimedhoofu na tunavipiga vita vya Ukristo taratibu mno na kuonesha uzembe na ulegevu, kwa sababu tunathamini kidogo mno tuzo ya mbinguni. Tunakuwa wadumavu katika mafanikio ya kiroho. Ni fursa na wajibu wa Mkristo kudumu kuongezeka katika kumfahamu sana Mwana wa Mungu, "hata kuwa mtu
Follow TUJIFUNZE NENO LA MUNGU. NA, CHIRONGE JMAGAI's WhatsApp Channel. *Jiunge katika Chaneli hii kwa ajili ya masomo mbalimbali ya Kiroho na jumbe za matumaini kila siku zitakazoletwa kwako nami, Chironge JMagai. Ubarikiwe.*
*KATIKA ROHO YA ELIYA.*
*Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana. Malaki 4:5-6.*
*"Wale watakaoandaa njia kwa ajili ya kuja kwa Yesu mara ya pili, wanawakilishwa na Eliya aliyekuwa mwaminifu, k**a vile Yohana alivyokuja katika roho ya Eliya kuiandaa njia kwa ajili ya ujio wa kwanza wa Kristo. Kazi ya Yohana Mbatizaji na ile ya wale ambao katika siku za mwisho watakwenda katika roho na nguvu ya Eliya kuwaamsha watu kutoka katika kutokujali kwao, zinafanana katika mambo mengi. Kazi ya Yohana ni kielelezo cha kazi ambayo inapasa kufanywa katika kizazi hiki. Somo kuu la matengenezo linapaswa lisisitizwe na mioyo ya watu iamshwe. Kiasi katika mambo yote inabidi kiunganishwe na ujumbe, kuwageuza watu wa Mungu kutoka katika ibada ya sanamu, ulafi, na ufujaji katika mavazi na mambo mengine. K**a vile Yohana Mbatizaji... alivyowakumbusha Amri Kumi, ndivyo tunavyopaswa kuutoa ujumbe kwa sauti isiyo na mashaka: “Mcheni Mungu na kumtukuza; kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.” Tunapaswa kujitahidi kuiandaa njia ya kuja kwa Kristo mara ya pili kwa umakini uliokuwa kwa Eliya na Yohana Mbatizaji." (Maranatha. Uk. 22)*
https://whatsapp.com/channel/0029Vb4gnrB5vKAFIY5r6R20
*(+255762895486.)*
🙏🙏🙏🙏. Join 9.2K followers for the latest updates.