Uhalisia WA NDOTO Unazoota

Uhalisia WA NDOTO Unazoota Mwanzo 40:8 "Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasi

31/10/2024

Send your dream now ( Tuma ndoto yako sasa...)!

20/10/2024

WARUMI 8:28

Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

17/05/2022

6:14
14BWANA akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?

Mungu ni Pendo na pia Mungu ni Yule-yule jana, leo na hata milele. Naamanisha nini? Mungu anaijua jana yako, anaijua leo yako na pia anaijua kesho yako.

Hivyo basi kwa kuwa Mungu ni Pendo na anawapenda wanadamu, anapenda kuwaongoza wanadamu katika njia sahihi. Na njia ya msingi ambayo Mungu huwa anaitumia ni ndoto. Ndoto ni lango ambalo Mungu ama miungu huwa inatumia kuongea na wanadamu. Sasa, Mungu anaweza kukuonyesha kesho yako kwa kupitia ndoto but ukijiangalia kwa jinsi leo yako ilivyo, huwezi kuamini na kukubali kirahisi kuwa Mungu ndivyo anavyokuona na anakusudia uwe hapo kesho.

Mungu alipomtokea Gideon kupitia malaika na kuanza kumwambia Mungu alichomkusudia, Gideon alianza kuelezea udhaifu na mapungufu yake na kwa hivyo basi akajiona hawez kuwa hivyo Mungu anavyomwona.

Je, mangap Mungu amekuwa akikuonyesha kwa ndoto na ukadhani kuwa ni ndoto tu ama ukajidharau kuwa haiwezekani??

Cha msingi ni kuamini na kuanza kuipeleka hiyo ndoto yako kwenye uhalisia. Kumbuka Imani na matendo huenda pamoja na mwishowe matokeo udhihirika na kuwa halisi.

NB:: Usiache kuamini, kukiishi na kukitendea kazi( kukiweka kwenye matendo) kile Mungu anachokusemesha. Kwa sehemu kubwa, ndoto ni taarifa tu juu ya jambo fulani ambazo ni lazima ziwekwe kwenye matendo na matokeo yaonekane. Wengi wetu huwa tunashindwa ama tunasahau kuziweka hizo ndoto kwenye matendo huku tukiamini imeshakuwa na kumbe hapana. Siku zote kumbuka, IMANI PASIPO MATENDO IMEKUFA( HAKUNA MATOKEO/UDHIHIRISHO)

02/04/2022

NDOTO ZA ZINAZOHUSIANA NA SIMU:
K**a tujuavyo kwenye uhalisia kuwa simu inalenga mawasiliano. Hivyo basi ndotoni, simu inaweza ikaashiria/maanisha moyo, nafsi, mawasiliano baina ya mtu na mtu/watu, mahusiano, muunganiko wa kimwili/kiroho, kibali machoni pa watu na nadhalika.

Kuota mtu amepoteza simu, kuibiwa simu, kunyang'anywa simu na kadhalika, ina maanasha mojawapo ya hivyo vitu nilivyovitaja hapo juu, mtu hatokuwa navyo au atavipoteza kwenye uhalisia.

28/12/2021

KUOTA SHULE ULIYOWAHI KUSOMA NA HASA SHULE YA MSINGI

Zaburi 11::
2 Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta,
Wanaitia mishale yao katika upote,
Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.
3 K**a misingi ikiharibika,
Mwenye haki atafanya nini?

Hesabu 11:5 Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu;

Kuota shule ileile ambayo ulishawahi kusoma na hasa ya msingi, huwa inalenga kuwa kuna jambo ambalo liliwahi kufanyika miaka ya huko nyuma ama hv karibuni na hivyo basi limekuwa k**a ukuta mrefu wa kukuzuia na kuhakikisha husongi mbele kwenye maisha yako kimwili ama kiroho.

Mfano ibada ambazo mababu na mabibi walikuwa wakifanya miaka hiyo ni kizuizi, matamko au laana ambazo mtu aliwahi kutamkiwa, mtu aliibiwa kitu chake kimazingira na hicho kitu kikafanyiwa ushirikina na makosa mengineyo tu ya kibinadamu.

Hivyo, basi unapokuwa unaota ndoto za kuwa shuleni ni vyema ujitathamini na kujichunguza vya kutosha ili upate kujua sababu ya kuota kuwa shule na kingine ni lazima utafakari je huko shule unakiwa unafanya nini. Kumbuka dunia hii ni k**a shule tu!! So, kuota huko shule na umevaa sare( uniform) za shule hiyo, si mawazo na haiwez kuwa ni ndoto ya mawazo.... Ni lazima inakuwa inaashiria jambo kwenye uhalisia wa maisha yako ya kila siku.

Kwa sehemu kubwa ndoto za kuota uko shule ya msingi ukiwa umevaa uniform huwa zinaonyesha shida ya kiroho na kwa sehemu ndogo inayobaki huwa ni kwa sababu ya uzembe, kutokujua, au kukosa maarifa juu ya mtu anapaswaje kufanya ili avuke na kwenda hatua nyingine kwenye maisha yake kiuhalisia.

Hivyo, ni vyema kupima ikiwa ndoto hiyo inayojirudiarudia ni kwa sababu za kiroho au kuna eneo umekosa ufahamu( maarifa) namna ya kujikwamua!!

17/12/2021

NDOTO ZA VIATU
Viatu katika ndoto vinaweza maanisha maono/mipango/mitazamo/utayari/injili/wazo/ushauri.
Kutoka 3:5 na Yoshua 5:15. Hawa watumishi wote wawili tunaona waliambiwa wavue viatu vyao.Kwa nini? Ni kwa sababu mitazamo/mipango/mawazo yao yalikuwa kinyume na Mungu, so kuvua ilkmaanisha kuachana na hiyo mitazamo/mipango waliyokuwa nayo ili wapewe mipango mingine mipya na Mungu. Haikumaanisha kwamba walikuwa na dhambi na walitakiwa kutubu, hapana, sivyo. They were supposed to change their mind and surrender their every plan to God.

2 Samweli 15:30 Hapa tunaona Daudi akiwa amejifunika kichwa chake na kutembea peku( bila viatu). Hapa Daudi alikuwa amepinduliwa na mwanaye na kiti chake cha ufalme kimetwaliwa. So, kutembea peku inalenga Daudi alikuwa ametoka nje ya maono/kusudi/mpango ambawo kwa wakati huo alitakiwa kuwa.

Yoshua 9:5 " na viatu vilivyotoboka na kushonwa-shonwa katika miguu yao, na mavao makuukuu waliyokuwa wanavaa; tena mkate wote wa chakula chao ulikuwa umekauka na kuingia koga. " Huu mstari unawazungumzia Wagibeoni waliokuwa wamekwenda mbele ya Joshua na wana wa Israel waliposikia miji mingine imepigwa ili kunusuru maisha yako. Hawo watu waliamua kufanya agano na akina Joshua. Kwa kufanya agano na Joshua, ina maana walikuwa wameliacha agano lao. So, kuota ndoto za viatu ukiwa umevaa viatu vilivyotoboka, vilivyochakaa, vilivyo tofauti na kadhalika, inamaana adui anakubadilishia maono/mipango/agano/wazo na kadhalika ili usiwe k**a vile Mungu alivyokukusudia uwe

Kwa ufupi, ndoto za kuvaa viatu huwa zinakuwa na maana tofautitofauti kutegemea na mapito ya mtu husika. Kwa mfano wengine huwa wanaota wamevaa viatu vinavyoteleza, wengine vizito na vikubwa, wengine vinabana miguu na kumfanya atembee kwa shida, wengine ameazima viatu, mwingine viatu vyake havioni na kadhalika....

17/12/2021

NINI MAANA YA KUOTA UNAOKOTA PESA?

Biblia inasema pesa ni jawabu la mambo yote.... Pia inasema shetani anaweza kujigeuza kuwa malaika wa nuru( kwa maana ya kwamba shetani anageuza mambo kuwa kinyume chake) na pia kwenye zaburi 64:5 " Walijifanya hodari katika jambo baya;

Hushauriana juu ya kutega mitego;
Husema, Ni nani atakayeiona?"

Kwa kawaida na mara nyingi ndoto za kuokota pesa huwa zinamaanisha kuwa mhusika( muotaji wa nyota), atapoteza pesa au vitu vya thamani kwa njia yoyote ile. Kuokota pesa ni mitego ambayo adui huwa anaitega na shabaha yake haswa ni mikono ya mhusika, kumpandikizia roho ya kutapanya/kuangusha/kupoteza au kutokushika pesa au kitu chochote cha thamani.

Wakati mwingine ikiwa mtu ilitakiwa apokee fedha au kitu chochote cha thamani siku za usoni, akiota tu ndoto k**a hii na akawa hajaishughulikia kikamilifu kwa wakati, huwa muotaji wa ndoto k**a hii hawez kupokea hicho kitu!!

NINI CHA KUFANYA UKIOTA NDOTO K**A HII?

Kwa kuwa shabaha ya adui inakuwa ni mikono ya mhusika, hivyo mhusika anatakiwa kuombea mikono yake kwa kuitakasa, kuondoa vinyago na sanamu, na kutangua manuizo( maneno) ambayo yalitamkwa kwenye zile ambazo zilionekana k**a ni pesa ndotoni na kujitamkia kupata, kukusanya, kutokupoteza na kadhalika.

14/04/2021

JE, MTU ALIYEOKOKA ANAWEZA KUFUATILIWA NA NGUVU ZA GIZA AU MIZIMU YA KWAO?

Zaburi 11:1-3
Zaburi 11:3 K**a misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?

Hii misingi ni mifumo au maagano na mapatano na nguvu za vita kwenye familia zetu, koo zetu, jamii zetu na makabila yetu. Kumbuka mwenye haki ni yule aliyepata neema ya Mungu kuwa mjoli wake au mtumishi wake au mtu wake.

Yohana 17:14-15, " 14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa si wa ulimwengu, k**a mimi nisivyo wa ulimwengu 15. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu".

Mizimu ni nini? Mizimu ni miungu iliyoabudiwa na inayoabudiwa na hujifunua kwa sura za wahenga{ ancestors) au mtu yoyote toka upande wa baba au mama aidha yu hai sasa au alishafariki.

Hii mizimu/miungu inaweza kuonekana kiuhalisia au kwa ndoto pia katika maumbo ya aina mbalimbali k**a vile nyoka, simba, chui, na kadhalika au babu, bibi ,shangazi, baba, mama na kadhalika aidha wako hai au hapana.

Ni kweli kuwa mtu aliyeokoka anaweza kifuatiliwa na nguvu za giza au mizimu. Kivipi? Kumbuka mwanadamu yuko katika utatu pia maana aliumbwa kwa mfano wa Mungu maana naye Mungu yuko katika utatu. Biblia inasema roho itendayo dhambi ndio itakayohukumiwa, so mtu anapoamua kumpokea Yesu awe Bwana na Mwokozi wake, roho yake ndo inaokoka bali nafsi na mwili wake unabaki katika hali ileile ya mwanzo. So nguvu za giza na hii mizimu inabaki na uhalali na kuishikilia nafsi yake, so maombi ya ukombozi( Deliverance) yanahitajika kuinunua nafsi yake, kuitakasa na kufuta kila hati ya madai, uhalali na vitu vyote visivyohitajika na mwili huwa unatiishwa tu kwa Neno la Kristo maana biblia inasema mtu akiipenda dunia hawez kumpenda Mungu.

Na kwa nini tunaziita nguvu za giza? Kumbuka nguvu za giza ni halisi ila zinatenda kazi nyuma ya pazia( bila mtu kujua/kufahamu, kwa kujificha) na ndo maana tunaziita giza. Giza ni kutokujua, kutokutambua kile kinachoendelea au kinachotokea au kinachotakiwa kujiri!

Address

Mbeya

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Uhalisia WA NDOTO Unazoota posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Uhalisia WA NDOTO Unazoota:

Share