Revelation Of Jesus Christ

Revelation Of Jesus Christ Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Revelation Of Jesus Christ, Religious Center, Mbeya.

25/10/2024

21/09/2024

Zaburi 511 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.2 Unioshe...
21/09/2024

Zaburi 51
1 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.

2 Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.

3 Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima.

4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.

5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.

6 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri,

7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji

8 Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi.

9 Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote.

10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu

11 Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.

12 Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.

13 Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako.

14 Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu, Uniponye na damu za watu, Na ulimi wangu utaiimba haki yako.

15 Ee Bwana, uifumbue midomo yangu, Na kinywa changu kitazinena sifa zako.

16 Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.

17 Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.

18 Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako, Uzijenge kuta za Yerusalemu.

19 Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki, Na sadaka za kuteketezwa, na kafara. Ndipo watakapotoa ng'ombe Juu ya madhabahu yako.

IMANIIMANI SI KUAMINI TU KATIKA KILE ULICHOOMBA BALI IMANI PIA NI KUWA TAYARI KUPIGWA, KUFA, KUCHEKWA, KUDHARAULIWA KWA ...
03/09/2024

IMANI
IMANI SI KUAMINI TU KATIKA KILE ULICHOOMBA BALI IMANI PIA NI KUWA TAYARI KUPIGWA, KUFA, KUCHEKWA, KUDHARAULIWA KWA AJILI YA YESU KRISTO UNAWEZA KUPATA FURAHA, AMANI NA UTAJIRI LAKINI PIA UNAWEZA KUPOTEZA KILA KITU KWASABABU YA YESU KRISTO AU KWA SABABU YA IMANI
Waebrania 11
Pastor Isack Mwampondele
RJC (Revelation Of Jesus Christ)

Neema Ya Mungu
29/08/2024

Neema Ya Mungu

Somo la leo Hakikisha unapotenda wema iwe siri yako wewe na Mungu wako Soma Mathayo 6:1-4Wengi leo wanapofanya wema au k...
13/03/2024

Somo la leo
Hakikisha unapotenda wema iwe siri yako wewe na Mungu wako
Soma Mathayo 6:1-4
Wengi leo wanapofanya wema au kusaidia mtu wanapenda watu ndiyo waone ili wao wapate sifa kwa watu lakini hayo yote siyo agizo la Mungu kulingana na maandiko.

Utaona leo watu wanaenda kuona yatima na wajane cha kwanza wanachokumbuka ni kupiga picha na kupost ili watu wajue kuwa wao wanasaidia watu, lakini neno linasema wafanyao hayo wamekwisha kupata thawabu yao kwa kwa hao wanaowasifia.

Ebu fikiri k**a mtu aje akupe msaada alafu akupige picha apost utajiskiaje au mtu anapompa msaada ndugu yako ampige picha amuweke mtandaoni sidhani k**a inapendeza hasa kwa wale wanaotamani kupokea thawabu kwa Mungu wao yaani wana wa Mungu
Mathayo 6
1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya k**a hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, k**a wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Watu wa Mungu tujitahidi kuishi na kuenenda sawa na neno hapo ndipo tutampendeze kuona mkono wa Mungu ukiwa pamoja nasi.

Pastor Isack Mwampondele
Rjc (Revelation Of Jesus Christ)

Address

Mbeya
53000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Revelation Of Jesus Christ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Revelation Of Jesus Christ:

Share