30/07/2026
Bwana Yesu asifiwe!
Katika muendelezo wa kichwa Cha kijarida hicho, Cha KUKAMILISHWA KATIKA ROHO, pia Kuna:
KUZALIWA MARA YA PILI KWA MAJI NA KWA ROHO.
Ubatizo wote unahitajika katika maisha Yako, yaani kubatizwa Kwa MAJI na kubatizwa Kwa Roho, kwani ni ukamilifu wako katika roho Kwa agano jipya.(Yohana 3:5-6).
Warumi 6:4-5 inazungumzia ubatizo wa maji k**a ishara kufa na kufufuka pamoja na Yesu.
Katika kitabu Cha Luka 3:16, Yohana anazungumzia ubatizo wake wa maji Kwa watu, na ubatizo wa Yesu wa Roho mtakatifu, akisema, Mimi nawabatiza Kwa MAJI lakini yuaja mwenye nguvu kuliko Mimi ambaye Mimi sitahili kulegeza gidamu za viatu vyake, yeye atawabatiza Kwa Roho mtakatifu na moto.
Lakini pia katika kitabu cha matendo ya mitume, tunaona watu wakikamilishwa katika Roho Kwa kubatizwa, walipokutana na Paulo, "Ikawa Apolo alipokuwa korintho, Paulo akiisha kupita Efeso; akakutana na wanafunzi kadhaa wa huko; akawauliza, Je mlipokea Roho mtakatifu mlipoamini? Wakajibu, La, hata kusikia Kwamba Kuna Roho mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, Basi mlibatizwa Kwa ubatizo Gani? Wakasema wa Yohana.
Paulo akasema, Yohana alibatiza Kwa ubatizo wa Toba, AKIWAAMBIA watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani Yesu.(matendo ya mitume 19:11-7)
Basi waliposikia HAYO , wakabatizwa Kwa JINA la Bwana YESU. Na Paulo alipokwisha kuweka mikono yake juu Yao; Roho mtakatifu akaja juu Yao; wakaanza kunena Kwa lugha na kutabili. Walikuwa wanaume 12.
Kwahiyo hapo:
1. Kuna ubatizo uliofanywa na Yohana (wa maji Yani kutubu na kumwamini Yesu ajaye.
2. Kuna ubatizo unaofanywa na Yesu) wa Roho mtakatifu.(Kubatizwa Kwa JINA la YESU)
N.B kutokana Neno Hilo hapo juu, Watu wengi, yaani mafarisayo, masadukayo, wakuu wa makuhani na wanasheria walikuwa wamebatizwa ubatizo wa maji ule wa Yohana, tatizo lilikuwa kukubali kubatizwa ubatizo wa Roho mtakatifu, yaani wa Yesu. Na hata Leo ndivyo ilivyo makanisani.
Kwahiyo hata Petro alipokuwa akisema tubuni, mkabatizwe kwa JINA la YESU, haukuwa ubatizo wa maji, sababu ubatizo wa Yohana wengi walikubali na kwenda Kubatizwa. Tatizo lilikuwa katika ubatizo wa Roho mtakatifu. Huku wakiamini Masihi aliyesemwa na Yohana yani Yesu bado kuja.
YESU ATUSAIDIE TUTAFUTE SANA KUKAMILISHWA NAYE!
BARIKIWA NA UWE NA SIKU NJEMA