11/03/2022
USIKATIE TAMAA KWENYE ENEO LILILO IBEBA HATIMA YAKO.
ilimgharimu Sauli kutembea mwendo mrefu akitafuta punda wa Baba yake waliopotea, haikuwa rahisi ni mwendo wa maeneo k**a matano usiku na mchana...haya ni majina ya maeneo au nchi alizopita Sauli KUTAFUTA Punda wa Baba yake waliopotea;
1.EFRAIMU2.SHALISHA 3. SHAALIMU 4.BENYAMINI 5.SUFU.
pamoja na kuzunguka maeneno haya yote matano hakuwaona Punda...!!!
SAULI ALIPOFIKA KWENYE NCHI YA SUFU AKACHOKA NA KUKATA TAMAA...jambo la ajabu *alipochokea ndiyo palikuwa mwanzo wa safari ya HATIMA YAKE*.
*Hata walipofika nchi ya Sufu, Sauli akamwambia yule mtumishi aliyefuatana naye, Haya, na turudi, baba yangu asije akaacha kufikiri habari za punda akatufikiri sisi*.
Naye akamwambia, Tazama, katika mji huu mna mtu wa Mungu, naye ni mtu mwenye kuheshimiwa; yote asemayo hutukia kweli kweli; basi, twende huko; labda yeye aweza kutuambia habari ya safari yetu tunayoiendea.
1 Samweli 9:5-6
JAMBO LA ajabu sana, walipofika SUFU Baada ya Sauli kuchoka, Mtumwa aliye ongozana naye alikuwa na jicho la ziada kuliko Sauli, akamwambia ..
"Katika Mji huu mna mtu wa Mungu, Mwenye kuheshimiwa, Yote asemayo hutukia kweli kweli"
Mtumishi wa nyumba ya Baba yeke Sauli anamuongoza Sauli, kwenye HATIMA yake, yaani KWA Nabii Samweli ILI amtie Mafuta awe Mfalme, hata wewe unahitaji mtu wa namna hii kwenye maisha YAKO...
"umewahi kufikiri hata mfanyakazi wa nyumbani Mungu anaweza kumtumia akakuongoza kwenye HATIMA YAKO"
acha kudharau watu.....
usikae na watu kwasababu wanavyo, kaa na watu kwasababu Mungu ametaka.
KUPOTEA KWA PUNDA ILIKUWA NI NJIA YA KUMPELEKA SAULIKWENYE MUUJIZA WAKE WA MAFUTA YA UFALME...!!!
KUNAGHARAMA UNAILIPA LEO KWENYE NAFASI FULANI, ILI KUTENGENEZA NAFASI IJAYO....ongeza jicho la rohoni.
USILIDHIKE ULIPO LEO, TUMIA PLATFORM HIYO KUTAFUTA UTAKAPOKUWA KESHO BILA KUJALI GHARAMA...
angalia maandiko yaliyo BEBA ujumbe wa habari hii yote;
Na punda za Kishi, baba yake Sauli, walikuwa wamepotea. Kishi akamwambia Sauli mwanawe, Haya basi, twaa mtumishi mmoja pamoja nawe, uondoke, uende ukawatafute punda hao.
Naye akapita kati ya nchi ya milima milima ya Efraimu, akapita na kati ya nchi ya Shalisha, lakini hawakuwaona; kisha wakapita kati ya nchi ya Shaalimu, wala huko hawakuwako; wakapita kati ya nchi ya Wabenyamini, lakini hawakuwapata.
Hata walipofika nchi ya Sufu, Sauli akamwambia yule mtumishi aliyefuatana naye, Haya, na turudi, baba yangu asije akaacha kufikiri habari za punda akatufikiri sisi.
Naye akamwambia, Tazama, katika mji huu mna mtu wa Mungu, naye ni mtu mwenye kuheshimiwa; yote asemayo hutukia kweli kweli; basi, twende huko; labda yeye aweza kutuambia habari ya safari yetu tunayoiendea.
Ndipo Sauli akamwambia mtumishi wake, Lakini angalia, k**a tukienda, tumpelekee mtu huyo kitu gani? Maana chakula kimekwisha vyomboni mwetu, wala hapana zawadi ya kumpelekea mtu wa Mungu; tuna nini sisi?
Yule mtumishi akamjibu Sauli, akasema, Tazama, mkononi mwangu nina robo ya shekeli ya fedha; nitampa huyo mtu wa Mungu fedha hiyo, atuambie njia yetu.
1 Samweli 9:3-8
Pamoja na Sauli kuchoka na kukata TAMAA kuwatafuta Punda, Yule Mtumishi aliyekuwa ameongozana naye alikuwa amebeba MAJIBU MENGI YA SAULI...!!!
UNAPOSOMA KWA KINA, UTAGUNDUA JAMBO LA MUHIMUSANA, MAHALI ALIPOCHOKEA NA KUKATA TAMAA SAULI, NDIPO PALIBEBA UNABII JUU YA HATIMA YAKE,
"Punda unao watafuta wamerudi nyumbani kwa baba yako, bali wewe ni mfalme wa Israel"
*Kesho, wakati k**a huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia*.
1 Samweli 9:16
pale alipo chokea Sauli, Nabii Samweli alikuwa akimsubiri ILI amtie Mafuta awe Mfalme juu ya Isael.
KUNA MAHALI PAMEKUCHOSHA SANA, NA TAKA NIKWAMBIE, *MAFUTA YAKUELEKEA MAHALI UNAPOTAKIWA KUELEKEA YAKO HAPO ULIPOCHOKEA*,
Maombi ya Leo;
1.Usiangalie kiwango cha kuchoka kwako juu ya eneo ulilopo, Omba Mafuta yakukufikisha kwenye HATIMA YAKO.
2.Omba Mungu akuinulie mtu mwenye jicho zaidi YAKO, amayeweza kuona uhusiano wa MAHALI ULIPOCHOKEA na unakoelekea.
Pastor GB Richard
Unshakable kingdom of Christ Ministries
More than Conquerors
[email protected]