05/12/2024
UPENDO NI NJIA YA KUISHINDA DHAMBI
Warumi 5:8 " Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi."
Upendo wa Mungu ulifanya dhambi iliyokuwa juu yangu kuondolewa na kuokolewa na adhabu ya mauti. Kila mtu aliyewahi kuzaliwa katika Dunia hii alistahili kufa ,kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
Hakuna mtu angeweza kusimama kwa ujasiri mbele za Mungu . Lakini Upendo wa Mungu unaushinda dhambi iliyoleta mauti katika ulimwengu, Ungali ukiwa mwenye dhambi Kristo alikuja kufa kwaajili ya dhambi zako!! Hili ni pendo linalopita fahamu ,biblia inasema ni rahisi kwa Mtu kufa kwa ajili ya mtu mwema lakini si mtu mdhambi. Katika hili Mungu ametuonyesha Upendo wake kwetu upitao ufahamu.
Mungu baada ya kutuokoa sisi pia alitupatia nguvu hiyo hiyo ya Upendo wake ndani yetu
Warumi 5:5 "na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi."
Kupitia hili twajua ya kuwa nguvu kuu ya Upendo katika ulimwengu unapatikana ndani ya Moyo wa mkristo halisi aliyemwamini Mungu. K**a wakristo tuliojawa na pendo la Roho wa Bwana basi ni jukumu letu kuumimina Upendo huu katika ulimwengu huu ,tuwe kielelezo katika Jamii kwa Kuudhihirisha Upendo wa Kiungu ,Maana kupitia hili tutajuliwa kuwa tu wanafunzi wa Bwana wetu Yesu Kristo.
1 Petro 4:7 Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.
1 Petro 4:8 Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.