06/06/2026
🕊️ 𝗨𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗜 𝗞𝗔𝗠𝗔 𝗪𝗜𝗧𝗢, 𝗦𝗜𝗢 𝗖𝗛𝗘𝗢
📖 Marko 10:42–45
'Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi'.
𝗨𝘁𝗮𝗻𝗴𝘂𝗹𝗶𝘇𝗶: 𝗠𝗴𝗼𝗴𝗼𝗿𝗼 𝘄𝗮 𝗩𝘆𝗲𝗼
Shalom wapendwa. Leo tunazungumzia msingi muhimu katika maisha ya kanisa, taasisi, na jamii: "Uongozi ni Wito, Sio Cheo." Wengi hudhani uongozi ni kiti unachokalia, lakini ukweli ni kwamba uongozi ni alama unayoiacha katika maisha ya watu. Katika ulimwengu wa sasa, tunashuhudia mgogoro mkubwa wa utambulisho kwa viongozi, ambapo Position (Cheo) imetangulizwa mbele ya Divine Mandate (Wito wa Kimungu).
𝗧𝗼𝗳𝗮𝘂𝘁𝗶 𝘆𝗮 𝗺𝘀𝗶𝗻𝗴𝗶 𝗻𝗶 𝗵𝗶𝗶:
- 𝗖𝗵𝗲𝗼 (𝗣𝗼𝘀𝗶𝘁𝗶𝗼𝗻): Ni nafasi rasmi ya nje inayotolewa na wanadamu. Ni "lebo" ya muda. Unaweza kuitwa mwenyekiti, mkurugenzi, au mchungaji, lakini hayo ni majina tu.
- 𝗨𝗼𝗻𝗴𝗼𝘇𝗶 (𝗟𝗲𝗮𝗱𝗲𝗿𝘀𝗵𝗶𝗽): Ni uwezo wa ndani wa kushawishi, kuelekeza, na kuhamasisha watu kuelekea kusudi.
Mtu anaweza kuwa na cheo lakini asiwe kiongozi—huyo ni "bosi" tu anayetegemea mamlaka ya ofisi. Lakini mtu mwenye uongozi anaweza hata aswe na cheo rasmi, lakini sauti yake inasikilizwa na maisha yake yanabadilisha wengine. Biblia inatufundisha kupitia Daudi (1 Samweli 16:7): “BWANA hautazami k**a mwanadamu atazamavyo; maana mwanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huitazama moyo.” Kabla Mungu hajampa Daudi kiti cha enzi, alimthibitisha kwanza akiwa malishoni anachunga kondoo kwa uaminifu.
Hii ndiyo Theology of Character (Teolojia ya Tabia) inayotangulia Theology of Authority (Teolojia ya Mamlaka).
𝟭. 𝗨𝗼𝗻𝗴𝗼𝘇𝗶 𝗸𝗮𝗺𝗮 𝗪𝗶𝘁𝗼 (𝗩𝗼𝗰𝗮𝘁𝗶𝗼)
Uongozi wa kweli ni wito, mwaliko wa Mungu (Vocatio) unaokusukuma kutimiza kusudi hata pasipokuwa na anayekuona. Mtu mwenye wito hafanyi kazi kwa ajili ya makofi, umaarufu, au vyeo, bali kwa sababu hawezi kuacha kufanya kile Mungu ameweka ndani yake k**a moto wa Spiritual Compulsion.
Tazama mfano wa Nehemia: Hakusukumwa na nafasi yake ikuluni, bali na maumivu ya Yerusalemu iliyobomoka. Wito huwa mkubwa kuliko starehe na maslahi binafsi. Yeremia 20:9 anasema: “Ndipo nikasema, Sitamtaja wala sitasema tena kwa jina lake. Lakini neno lake lilikuwa moyoni mwangu k**a moto uwakao uliofungwa ndani ya mifupa yangu.”
Hivi ndivyo uongozi unavyopaswa kuwa, moto unaoungua ndani.
𝗠𝘁𝘂 𝘄𝗮 𝘄𝗶𝘁𝗼 𝗵𝘂𝗷𝗶𝘂𝗹𝗶𝘇𝗮: "Nawezaje kuwa wakili mwema wa neema ya Mungu (Steward of God’s Grace)?"
𝗠𝘁𝘂 𝘄𝗮 𝗰𝗵𝗲𝗼 𝗵𝘂𝗷𝗶𝘂𝗹𝗶𝘇𝗮: "Watu watanisaidiaje?"
Wito wako haupimwi kwa ukubwa wa jukwaa, bali kwa uaminifu wako katika kile ulichopewa (Faithfulness in Stewardship) (Mathayo 25:21).
𝟮. 𝗠𝘁𝗲𝗴𝗼 𝘄𝗮 𝗖𝗵𝗲𝗼 (𝗧𝗵𝗲 𝗧𝗿𝗮𝗽 𝗼𝗳 𝗛𝘂𝗯𝗿𝗶𝘀)
Cheo si kibaya; jamii na kanisa vinahitaji viongozi kwa ajili ya Ecclesiastical Order (Utaratibu wa Kanisa). Lakini cheo huwa hatari pale kinapokuwa lengo badala ya chombo cha huduma. Mtego mkubwa wa cheo ni kiburi (Hubris), ambacho Mithali 16:18 inasema: “Kiburi hutangulia uharibifu, na roho ya majivuno hutangulia maanguko.”
Dunia inafundisha "kuwa juu ya watu" na "kutafuta heshima", lakini Kristo aligeuza tafsiri hiyo katika Luka 22:26: “Bali ninyi msiwe hivi; bali aliye mkubwa kwenu na awe k**a aliye mdogo; na mwenye kuongoza k**a yule atumikaye.” Kiongozi wa cheo hulinda nafasi yake kwa siasa; kiongozi wa wito hulinda maono yake kwa tabia. Kumbuka, cheo kinaweza kuondolewa, lakini ushawishi wa kweli na hekima yako ni urithi wa kudumu wa kimaadili (Moral Legacy).
𝟯. 𝗞𝘂𝗿𝘂𝗱𝗶 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗠𝘀𝗶𝗻𝗴𝗶 (𝗧𝗵𝗲𝗼𝗹𝗼𝗴𝗶𝗰𝗮𝗹 𝗥𝗲𝗳𝗹𝗲𝗰𝘁𝗶𝗼𝗻)
Kila kiongozi anahitaji kutathmini moyo wake mara kwa mara kwa kujiuliza: "K**a nikiambiwa kesho sipo kwenye nafasi hii, je, bado nitakuwa na shauku ya kuleta matokeo?" K**a jibu ni hapana, basi umependa nafasi kuliko kusudi (Divine Purpose).
Unyenyekevu ni ngazi ya kweli ya kupanda katika ufalme wa Mungu. Kumbuka sifa za kiongozi wa kweli:
-𝗠𝗮𝗼𝗻𝗼 (𝗩𝗶𝘀𝗶𝗼𝗻): “Pasipo maono, watu huacha kujizuia” (Mithali 29:18).
-𝗨𝗮𝗱𝗶𝗹𝗶𝗳𝘂 (𝗜𝗻𝘁𝗲𝗴𝗿𝗶𝘁𝘆): “Uadilifu wa wenye haki utawaongoza” (Mithali 11:3).
-𝗠𝗼𝘆𝗼 𝘄𝗮 𝗵𝘂𝗱𝘂𝗺𝗮 (𝗗𝗶𝗮𝗸𝗼𝗻𝗶𝗮): Kristo alikuja kutumika, si kutumikiwa (Marko 10:45).
-𝗨𝗻𝘆𝗲𝗻𝘆𝗲𝗸𝗲𝘃𝘂 (𝗛𝘂𝗺𝗶𝗹𝗶𝘁𝘆): “Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawakuza” (Yakobo 4:10).
-𝗨𝗮𝗺𝗶𝗻𝗶𝗳𝘂 (𝗙𝗶𝗱𝗲𝗹𝗶𝘁𝘆): “Kilichotakiwa katika mawakili ni mtu aonekane kuwa mwaminifu” (1 Wakorintho 4:2).
-𝗨𝘄𝗲𝘇𝗼 𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗶𝗻𝘂𝗮 𝘄𝗲𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲:“Na mambo uliyoyasikia kwangu... hayo uwakabidhi watu waaminifu” (2 Timotheo 2:2).
𝟰. 𝗛𝗶𝘁𝗶𝗺𝗶𝘀𝗵𝗼 𝗻𝗮 𝗪𝗶𝘁𝗼 𝘄𝗮 𝗛𝗮𝘁𝘂𝗮 (𝗖𝗮𝗹𝗹 𝘁𝗼 𝗔𝗰𝘁𝗶𝗼𝗻)
Ndugu zangu, ninapohitimisha, nakusihi: Usiwe mtafuta vyeo; kuwa mtafuta wito. Cheo kinaweza kukufanya ujulikane, lakini huduma (Sacrificial Service) ndiyo itakufanya ukumbukwe. Cheo kinaweza kukufungulia mlango, lakini maadili (Ethics) yatakufanya ubaki ndani.
𝗝𝗶𝘁𝗮𝘁𝗵𝗺𝗶𝗻𝗶 𝗹𝗲𝗼: Je, unaongoza kwa moyo wa Kristo au wa dunia? (1 Petro 5:2–3). Usiombe kwanza cheo, omba kwanza Character transformation (Mabadiliko ya tabia). Usikimbilie kiti, kimbilia wito. Mwisho wa siku, watu hawatakumbuka ulikaa kwenye kiti gani, bali watakumbuka ulivyowatendea, ulivyowaongoza, na ulivyowasaidia kumkaribia Mungu.
True leadership is not a quest for a title to be served, but a divine call to sacrifice and serve others. _GDeBxhop
---------------
🔚
𝘕𝘢 𝘔𝘵𝘶𝘮𝘪𝘴𝘩𝘪,
𝘎𝘦𝘳𝘴𝘩𝘰𝘮 𝘌. 𝘊𝘩𝘢𝘭𝘭𝘰
0769 743 737
📧 𝘨𝘤𝘩𝘢𝘭𝘭𝘰30@𝘨𝘮𝘢𝘪𝘭.𝘤𝘰𝘮
🗓️ Juni 06, 2026
📘 #𝘎𝘋𝘦𝘉𝘹𝘩𝘰𝘱
📚 #𝘊𝘩𝘢𝘭𝘭𝘰𝘍𝘢𝘮𝘪𝘭𝘺𝘓𝘪𝘣𝘳𝘢𝘳𝘺