CFL-Rhēma

CFL-Rhēma Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from CFL-Rhēma, Church, Kiteto/P. O. Box 74, Manyara.

🏹RHĒMA FOR LIFE MINISTRY🏹
"Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu"_Mathayo 4:4

📚 Challo Family Library (CFL)
🧭 Dira Ya Hekima
📞+255 769 743 737
📧 [email protected]
▶️ CFL Rhema
🌐 cfl.rhema.tz

🕊️ 📖   - Heri ya Pasaka.“Usiwe asiyeamini, bali aaminiye.” — Yohana 20:27 Baada ya Yesu Kristo kusulubiwa na kuzikwa, wa...
05/04/2026

🕊️ 📖 - Heri ya Pasaka.
“Usiwe asiyeamini, bali aaminiye.” — Yohana 20:27


Baada ya Yesu Kristo kusulubiwa na kuzikwa, wanafunzi wake walijifungia ndani kwa hofu. Walijikuta katika mshtuko wa kisaikolojia, hofu ya mamlaka ya Kirumi, na simulizi zinazopingana kuhusu ufufuo. Wengi walijua kwamba Mkombozi wa Israeli aliyeahidiwa ameaga dunia, hali iliyowachanganya. Ndani ya mazingira haya, Tomaso anatokea; mtu aliye na shaka ya wazi:
“Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari… mimi sisadiki hata kidogo.” — Yohana 20:25

Shaka yake si dhambi; ni chimbuko la imani, mwongozo wa akili inayotafuta ukweli wa kiroho. Tomaso ni mfano wa wanadamu wote waliopo katikati ya ushahidi na hitaji la uthibitisho.


1. Tomaso na Shaka ya Mwanadamu
Tomaso anawakilisha akili inayotaka ushahidi halisi. Wanafunzi wengine waliamini kwa kuona, lakini Tomaso alitaka confirmation ya kimwili, ikionyesha mgongano wa shaka na imani. Baadhi ya wanatheolojia walionekana kuhusika na hoja hii:

=>Rudolf Bultmann (Jesus Christ and Mythology, 1958) alihusisha simulizi za ufufuo na myth ya kiroho, kueleza uzoefu wa wanafunzi wake.
=>David Friedrich Strauss (Life of Jesus, 1835) aliona simulizi za ufufuo k**a myth ya imani ya Kanisa la kwanza, akitofautisha kati ya historia na tafsiri ya kiroho.

Hata hivyo, ushahidi wa kihistoria bado unathibitisha ufufuo, kwamba: kaburi lilikuwa tupu, wapo mashahidi wa kuona Yesu akiwa hai tena, na Kanisa lilianza kwa nguvu. Tomaso anatufundisha: shaka yenye msingi inaweza kuendeleza imani thabiti, si kizuizi.

2. Mantiki ya Imani
Yesu alimwambia Tomaso; “Usiwe asiyeamini, bali aaminiye.” — Yohana 20:27

Kauli hii ni mwongozo wa kiroho; shaka ni mwanzo wa imani, si mwisho. Imani haiishii kwenye ushahidi wa macho pekee; inaunganisha akili, moyo, na roho. Augustine (On Christian Doctrine, 397–426) anaita imani fides quaerens intellectum (imani inayotafuta ufahamu). Karl Barth (Church Dogmatics, III/1, 1960) anasema imani inakuza nakuimarisha akili hadi ukweli wa Kristo aliye hai, ikithibitisha kuwa imani si kupofusha au kuinyamazisha akili bali kuikamilisha ifanye KAZI kwa usahihi thabiti.

3. Ufufuo: Ushahidi na Nguvu
Ufufuo wa Yesu una maana tatu:
=> Ushindi juu ya mauti — mauti si mwisho wa historia ya mwanadamu.
=> Uthibitisho wa utambulisho wa Yesu — Yesu ni Bwana, si nabii tu.
=> Msingi wa imani ya Kikristo — Paulo anasema; “K**a Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure.” — 1 Wakorintho 15:14

Shaka ya Tomaso inawezesha kuunda imani yenye nguvu, inayobadilisha maisha na ushuhuda thabiti.

4. Paradoksi ya Imani
Yesu alisema; “Heri wale wasioona wakaamini.” — Yohana 20:29

Hii ni paradoksi ya kiroho; katika sayansi, kuona hupelekea kuamini; lakini katika imani, kuamini hupelekea kuona. Thomas Aquinas (Summa Theological, II-II, Q.2, 1265–1274) anafundisha shaka inaweza kuwa daraja la imani inayokua. C.S. Lewis (Mere Christianity, 1952) anaonyesha shaka ni mwanzo wa safari ya kiroho, si mwisho, na inaweza kubeba nuru ya kweli.

Hivyo mtu mwenye shaka asihukumiwe mapema ila kusaidiwa, na asipoelewa akaamini, Hilo ni tatizo lingine.


Kauli ya Yesu kwa Tomaso ni mwongozo wa vizazi vyote:
“Usiwe asiyeamini, bali aaminiye.”

Shaka si dhambi; ni daraja la imani ya kweli. Imani inaishi ndani ya roho, inaunganisha akili na moyo, na inapita historia. Ufufuo wa Kristo ni nguvu hai inayoweza kubadilisha shaka yetu kuwa imani thabiti, na maisha yetu kuwa ushuhuda wa milele. Tomaso anatufundisha kuwa, shaka yenye msingi inaweza kuwa mwanzo wa imani isiyopingika na kutoka mashaka hadi imani ni safari ya kiroho ya maisha yote.

Doubt is not the end, but the doorway to unwavering faith. _GDeBxhop.

🔚 Na Mtumishi: Gershom E. Challo
📞 0769 743 737 | 📧 [email protected]
🗓️ Aprili 05, 2026
📘 | 📚
_________________

LIGHT FROM BETRAYALWhat was meant for harm, God turned into salvation and light. This is exactly what befalls the wicked...
04/04/2026

LIGHT FROM BETRAYAL
What was meant for harm, God turned into salvation and light. This is exactly what befalls the wicked against God’s people even today. Thanks be to Almighty God. _ GDeBshop.

🕊️ 📖  TAFAKARI YA IJUMAA KUU:Maneno Saba ya Yesu Msalabani: Sauti ya Msalaba Inayofunua Upendo, Msamaha, na Ushindi wa W...
04/04/2026

🕊️ 📖
TAFAKARI YA IJUMAA KUU:
Maneno Saba ya Yesu Msalabani: Sauti ya Msalaba Inayofunua Upendo, Msamaha, na Ushindi wa Wokovu kwa Mwanadamu.

Maneno 7 ya Yesu Msalabani
1. Neno la MSAMAHA – “Baba, uwasamehe; kwa maana hawajui watendalo.” (Luka 23:34)
- Yesu anaonyesha rehema na msamaha hata kwa waliomsulubisha.
: Mkristo anafundishwa kuwa na moyo wa kusamehe hata kwa wanaomkosea, kwa sababu msamaha ni kiini cha upendo wa Kristo.

2. Neno la AHADI – “Leo utakuwa pamoja nami Peponi.” (Luka 23:43)
- Yesu anamwahidi wokovu mwizi aliyemwamini.
: Wokovu hutolewa kwa neema kwa wale wanaomwamini Kristo kwa toba ya kweli, hata k**a ni katika dakika za mwisho za maisha.

3. Neno la UPENDO na WAJIBU – “Mama, tazama mwanao… Tazama mama yako.” (Yohana 19:26–27)
- Yesu anamkabidhi mama yake kwa mwanafunzi wake akionyesha upendo na kuwajibika.
: Imani ya kweli inapaswa kuambatana na kuwajibika kwa familia na kuwajali wengine.

4. Neno la UCHUNGU – “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” (Mathayo 27:46)
- Yesu anaonyesha uzito wa kubeba dhambi za ulimwengu.
: Dhambi ina uzito mkubwa, na msalaba unaonyesha gharama ya wokovu wetu.

5. Neno la UBINADAMU – “Nina kiu.” (Yohana 19:28)
- Yesu anaonyesha mateso halisi ya kibinadamu aliyoyapitia.
: Kristo anaelewa udhaifu na mateso ya mwanadamu, hivyo tunaweza kumtegemea katika kila hali.

6. Neno la USHINDI – “Imekwisha.” (Yohana 19:30)
- Yesu anatangaza kuwa kazi ya ukombozi imekamilika.
: Wokovu wetu umejengwa juu ya kazi iliyokamilika ya Kristo, si juhudi za mwanadamu.

7. Neno la KUJITOA kwa Baba – “Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.” (Luka 23:46)
- Yesu anakabidhi maisha yake kikamilifu kwa Mungu Baba.
: Maisha ya mwamini yanapaswa kuwa ya kumtegemea Mungu na kujitoa kikamilifu kwake katika kila hatua ya maisha.

Kwa ujumla, maneno saba ya Yesu msalabani yanafunua moyo wa Injili: msamaha kwa wenye dhambi, tumaini la wokovu, upendo kwa wengine, uzito wa dhambi, udhaifu wa kibinadamu, ushindi wa ukombozi, na kujitoa kamili kwa Mungu. Hivyo msalaba unakuwa si tu mahali pa mateso, bali pia chanzo cha neema, wokovu, na ushindi wa milele kwa wanadamu.
'The Cross is the Forgiveness, Love and Victory' _GDeBxhop

🔚 Na Mtumishi: Gershom E. Challo
📞 0769 743 737 | 📧 [email protected]
🗓️ Aprili 03, 2026
📘 | 📚

🕊️ 📖  JUMAPILI YA MITENDE –> JUMAPILI YA PASAKA1. Jumapili ya Mitende (Palm Sunday)📖: Mathayo 21:1–11; Yohana 12:12–15Ye...
02/04/2026

🕊️ 📖
JUMAPILI YA MITENDE –> JUMAPILI YA PASAKA

1. Jumapili ya Mitende (Palm Sunday)
📖: Mathayo 21:1–11; Yohana 12:12–15
Yesu anaingia Yerusalemu kwa shangwe, akitambulika k**a Mfalme aliyeahidiwa. Hata hivyo, anakuja kwa unyenyekevu na si kwa nguvu za kisiasa.

Kiini: Ufalme wa Kristo ni wa kiroho, na wafuasi wake wanaitwa kumkubali kwa utii na si kwa matarajio ya kidunia.

2. Jumatatu (Holy Monday)
📖: Mathayo 21:12–22; Marko 11:15–19
Yesu anaitakasa Hekalu na kulaani mtini usiozaa matunda.

Fahari: Mungu anatafuta ibada ya kweli na maisha yenye matunda ya haki; dini ya nje bila uhalisia wa ndani hukataliwa.

3. Jumanne (Holy Tuesday)
📖: Mathayo 21:23–46; Mathayo 22–24
Yesu anafundisha Hekaluni akijibu maswali ya viongozi wa dini na kutoa mafundisho kuhusu ufalme wa Mungu, hukumu, na mwisho wa nyakati.

Fahari: Uongozi wa kweli wa kiroho unategemea utii kwa Mungu na utayari wa kuishi kwa haki mbele ya hukumu yake.

4. Jumatano (Holy Wednesday)
📖: Mathayo 26:14–16; Marko 14:10–11
Kipindi cha ukimya wa Yesu; wakati huohuo mpango wa kumsaliti unaandaliwa.

Fahari: Mpango wa wokovu wa Mungu unaendelea hata katikati ya usaliti na giza la mwanadamu.

5. Alhamisi Kuu/Amri (Maundy Thursday)
📖: Luka 22:14–20; Yohana 13:1–15
Yesu anaadhimisha chakula cha mwisho na wanafunzi wake, anaweka Sakramenti ya Meza ya Bwana, na kufundisha unyenyekevu kwa kuosha miguu yao.

Fahari: Upendo wa Kristo unaonekana katika sadaka na huduma; Kanisa linaalikwa kuishi katika ushirika, unyenyekevu, na kumbukumbu ya sadaka yake.

6. Ijumaa Kuu (Good Friday)
📖: Mathayo 27:32–54; Yohana 19:16–30
Yesu anasulubiwa na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi za wanadamu.

Fahari: Msalaba ni kitovu cha wokovu; mahali ambapo haki ya Mungu na neema yake vinakutana kwa ajili ya ukombozi wa dunia.

7. Jumamosi Kuu (Holy Saturday)
📖: Mathayo 27:57–66
Yesu yuko kaburini; ni siku ya ukimya na kutafakari.

Fahari: Hata katika ukimya na giza, mpango wa Mungu haujasimama; tumaini la ufufuo linakaribia.

8. Jumapili ya Pasaka (Easter Sunday)
📖: Mathayo 28:1–10; Yohana 20:1–18
Yesu anafufuka kutoka kwa wafu, akishinda dhambi na mauti.

Fahari: Ufufuo ni ushindi wa mwisho wa Mungu na msingi wa tumaini la Kikristo; uzima mpya na wokovu kwa wote wanaomwamini Kristo.

Hitimisho la Kitheolojia (Theological Core)
Juma Takatifu linafunua siri kuu ya wokovu (mysterium salutis): Kristo alikuja kwa unyenyekevu, akafundisha ukweli wa ufalme wa Mungu, akatoa maisha yake msalabani k**a sadaka ya ukombozi, na akafufuka ili kuleta ushindi wa milele. Hivyo, safari ya Juma Takatifu inaonyesha kuwa njia ya utukufu wa Mungu inapitia msalaba na ufufuo.

Holy Week is the journey of the cross toward the victory of the resurrection. _ GDeBxhop

🔚 Na Mtumishi: Gershom E. Challo
📞 0769 743 737 | 📧 [email protected]
🗓️ Aprili 01, 2026
📘 | 📚

🕊️ 📖  𝐔𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐍𝐈𝐍𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐊𝐀 𝐇𝐔𝐔📖 Mithali 29:18"𝑃𝑎𝑠𝑖𝑝𝑜 𝑚𝑎𝑜𝑛𝑜, 𝑤𝑎𝑡𝑢 ℎ𝑢𝑎𝑐ℎ𝑎 𝑘𝑢𝑗𝑖𝑧𝑢𝑖𝑎; 𝑏𝑎𝑙𝑖 𝑎𝑛𝑎 ℎ𝑒𝑟𝑖 𝑚𝑡𝑢 𝑦𝑢𝑙𝑒 𝑎𝑖𝑠ℎ𝑖𝑘𝑎𝑦𝑒 𝑠ℎ𝑒𝑟...
03/02/2026

🕊️ 📖
𝐔𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐍𝐈𝐍𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐊𝐀 𝐇𝐔𝐔

📖 Mithali 29:18
"𝑃𝑎𝑠𝑖𝑝𝑜 𝑚𝑎𝑜𝑛𝑜, 𝑤𝑎𝑡𝑢 ℎ𝑢𝑎𝑐ℎ𝑎 𝑘𝑢𝑗𝑖𝑧𝑢𝑖𝑎; 𝑏𝑎𝑙𝑖 𝑎𝑛𝑎 ℎ𝑒𝑟𝑖 𝑚𝑡𝑢 𝑦𝑢𝑙𝑒 𝑎𝑖𝑠ℎ𝑖𝑘𝑎𝑦𝑒 𝑠ℎ𝑒𝑟𝑖𝑎.”

𝗗𝗜𝗕𝗔𝗝𝗜
Ndugu Mpendwa, neno la Mungu linatufundisha kuwa mabadiliko ya kweli hayaanzi na kalenda pekee, bali huanzia kwenye ufunuo wa Mungu unaopatikana moyoni mwa mwanadamu. Tunapoingia mwaka Mpya, swali la msingi si “Mwaka utakuwa vipi?” bali “Sisi tunaona nini?” Maono sio ndoto za kawaida, bali ni ufunuo wa kina wa mapenzi ya Mungu unaoongoza moyo, unaounda mtazamo wa maisha, na kuunda historia ya maisha yetu kulingana na mpango wa Mungu.

𝗠𝗔𝗔𝗡𝗔 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗢𝗡𝗢
Neno maono (ḥāzôn) lina maana tatu kuu:
 Ufunuo wa mapenzi ya Mungu – mpango na mwelekeo unaotolewa na Mungu kwa maisha ya mtu, si mawazo yetu ya kibinadamu.
 Mwelekeo unaotokana na Neno la Mungu – huonyesha njia sahihi, tofauti na mitazamo ya kiduniani inayolenga faida za muda mfupi.
 Ufahamu wa kusudi la Mungu – kuelewa “kwa nini” badala ya kufuata tu “vipi” katika maamuzi yetu ya kila siku.

𝗠𝗮𝘁𝗼𝗸𝗲𝗼 𝘆𝗮 𝗞𝘂𝗸𝗼𝘀𝗮 𝗠𝗮𝗼𝗻𝗼
Biblia inasema wazi: “Pasipo maono, watu huacha kujizuia.” Kukosa maono huleta:
 Kupotea kwa nidhamu ya maisha – mtu anakuwa k**a chombo kisicho na usukani.
 Maamuzi yasiyo na mwelekeo – kila uamuzi unategemea hisia za muda na hali ya sasa.
 Maisha ya mazoea – badala ya kusudi, mtu anaishi kwa mfumo wa roboti, bila kufuata mpango wa Mungu.

𝗠𝗮𝗼𝗻𝗼 𝗻𝗶 𝘂𝗸𝗼𝗺𝗮𝘃𝘂
Ukomavu haujengeki kwa umri pekee, bali kwa ukubwa wa maono. Kijana anaweza kuwa na maono makubwa ya kuongoza kizazi, huku mzee akiwa hana maono hata kwa kesho yake. Mtaalamu mmoja wa ndoa alisema: “Kuna tofauti kati ya mvulana na mwanaume. Mwanaume anajua kufuata maono ya mustakabali, mvulana huishi kwa ukosefu wa maono.” Ukimlazimisha mtu kuongoza bila maono, hata k**a ana umri mkubwa, hakutakuwa na tija.

𝗝𝗜𝗡𝗦𝗜 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗧𝗘𝗠𝗕𝗘𝗔 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗞𝗔 𝗠𝗔𝗢𝗡𝗢
i. Maono huanza moyoni
Yesu alisema: “Jicho ni taa ya mwili; basi jicho lako likitakasa, mwili wako wote utakuwa mwanga” (Math 6:22). Maono sahihi huanzia pale moyo unaposafishwa na Neno la Mungu. Kila uamuzi, changamoto, na mahusiano yanapaswa kuongozwa na kile tunachoona moyoni.

ii. Maono yanahitaji kufanywa upya
Warumi 12:2 inatufundisha: “Msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu.” Maono ya Mungu yanapokea mchakato wa kugeuzwa upya, kuondoa mitazamo ya kiduniani, na kubadilisha mtazamo wa moyo. Hii huunda mtazamo wa kimbingu unaoleta mafanikio ya kudumu, na kuendeleza uongozi wa hekima katika familia, Kanisa, na jamii.

iii. Maono huzaa nidhamu na uwajibikaji
Mtu aliye na maono:
 Huamua kwa hekima na kusudi
 Huishi kwa kusudi la Mungu
 Huwajibika kwa matokeo ya vitendo vyake
 Hutoa mfano wa uongozi wa kiroho kwa vizazi vinavyofuata
 Huendeleza familia na jamii kwa mpangilio wa Mungu

iv. Umoja wa maono
Maono ya binafsi yanapaswa kuunganishwa na maono ya Kanisa na jamii. Mkristo aliye na maono anajitambua k**a sehemu ya mwili wa Kristo, akihudumia jamii kwa uaminifu na mshik**ano, huku maono yake binafsi yakisaidia kufanikisha mpango mkuu wa Mungu. Kwa hivyo, maono yako binafsi yanapaswa kueleweka na kuyatenda ndani ya mpango wa Mungu kwa familia, Kanisa, na taifa.

𝗧𝗔𝗙𝗦𝗜𝗥𝗜 𝗬𝗔 𝗠𝗪𝗔𝗞𝗔 𝗠𝗣𝗬𝗔
Kuingia Mwaka Mpya si namba ya kalenda tu, bali kipimo cha maono.
Kwa wenye maono: Mwaka huu utazaa mafanikio ya kiroho, fursa mpya zitaonekana, na mipango ya Mungu itafunuliwa kwa ajabu.
Kwa wasio na maono: Hatabmwaka mzuri kwao utakuwa mzigo, fursa zitapita, na maisha yataendelea bila kusudi. Kulazimisha Mungu aingie kwenye mipango yetu badala ya kuingia katika mipango Yake husababisha kushindwa, uchungu, na kupoteza maono.

𝗛𝗜𝗧𝗜𝗠𝗜𝗦𝗛𝗢
Badala ya kusema: “𝘉𝘸𝘢𝘯𝘢, 𝘵𝘶𝘣𝘢𝘳𝘪𝘬𝘪 𝘮𝘸𝘢𝘬𝘢 𝘩𝘶𝘶,” tuombe: 𝘉𝘸𝘢𝘯𝘢, 𝘵𝘶𝘱𝘦 𝘮𝘢𝘰𝘯𝘰 𝘠𝘢𝘬𝘰, 𝘵𝘶𝘴𝘪𝘱𝘰𝘵𝘦𝘦.”

𝗣𝗮𝗹𝗶𝗽𝗼 𝘂𝗳𝘂𝗻𝘂𝗼 𝘄𝗮 𝗠𝘂𝗻𝗴𝘂:
 Watu huishi kwa kusudi
 Mwaka huzaa matunda ya kiroho
 Kizazi kinapata uongozi wa hekima na uaminifu

Mwaka huu ni mwaka wa maono kwa wale watakaojitayarisha kupokea ufunuo wa Mungu na kuishi kulingana na mapenzi Yake. Maono ni habari ya mjini; bila hayo, hatuwezi kuongoza, kuathiri, au kuunda historia yenye maana.

𝙑𝙞𝙨𝙞𝙤𝙣 𝙞𝙨 𝙖 𝙩𝙚𝙡𝙚𝙤𝙡𝙤𝙜𝙞𝙘𝙖𝙡 𝙧𝙚𝙫𝙚𝙡𝙖𝙩𝙞𝙤𝙣 𝙤𝙛 𝙂𝙤𝙙’𝙨 𝙬𝙞𝙡𝙡, 𝙜𝙧𝙖𝙣𝙩𝙞𝙣𝙜 𝙝𝙪𝙢𝙖𝙣𝙞𝙩𝙮 𝙥𝙪𝙧𝙥𝙤𝙨𝙚𝙛𝙪𝙡 𝙙𝙞𝙧𝙚𝙘𝙩𝙞𝙤𝙣, 𝙙𝙞𝙨𝙘𝙞𝙥𝙡𝙞𝙣𝙚𝙙 𝙡𝙞𝙫𝙞𝙣𝙜, 𝙖𝙣𝙙 𝙢𝙤𝙧𝙖𝙡 𝙡𝙚𝙜𝙞𝙩𝙞𝙢𝙖𝙘𝙮 𝙞𝙣 𝙨𝙝𝙖𝙥𝙞𝙣𝙜 𝙝𝙞𝙨𝙩𝙤𝙧𝙮. - 𝗚𝗗𝗲𝗕𝘅𝗵𝗼𝗽

🔚 Na Mtumishi: Gershom E. Challo
📞 0769 743 737 | 📧 [email protected]
🗓️ Januari 01, 2026
📘 | 📚

Rhēma for LifeScripture interpreted by Scripture reveals God’s holiness, Christ’s lordship, and the clarity of divine tr...
02/02/2026

Rhēma for Life
Scripture interpreted by Scripture reveals God’s holiness, Christ’s lordship, and the clarity of divine truth.

 🕊️  HERI YA KRISMASI & MWAKA MPYA!Shalom Shalom! "Katika unyenyekevu wa hori, Umilele ulizungumza na mwanadamu.”Hebu tu...
25/12/2025


🕊️ HERI YA KRISMASI & MWAKA MPYA!

Shalom Shalom!
"Katika unyenyekevu wa hori, Umilele ulizungumza na mwanadamu.”

Hebu tutafakari kidogo 🤔;
Kwa nini Yesu, ingawa alikuwa Mungu, alilazimika kuzaliwa k**a mtoto na kuishi maisha ya binadamu wa kawaida! Na kuzaliwa kwake kulikuwa na maana gani kwa dhambi ya asili na mpango wa wokovu kwa mwanadamu! Kwa nini Maria alichaguliwa kuwa mama yake sasa!

Kuzaliwa kwa Yesu Kristo ni kitendo cha kipekee ambacho kinashirikisha falsafa na theolojia ya Kikristo. Kazi ya hypostatic union (Umoja wa asili mbili ndani ya Yesu, kiungu na kibinadamu), ni msingi wa kuelewa jinsi Mungu alivyokuwa karibu na wanadamu. Kuzaliwa kwake si tukio la kawaida; ni tukio lililojaa maana ya kiroho, kimaadili, na kifalsafa, ambalo linagusa maisha na wokovu wa kila mtu.

Hivyo:
Yesu, ingawa ni Mungu kamili, alichagua kuzaliwa k**a mtoto wa kibinadamu ili kushiriki kikamilifu hali ya binadamu, kushughulikia dhambi ya asili, na kuunda msingi wa wokovu. Kuzaliwa kwake k**a binadamu kamili kulikidhi mahitaji ya kifalsafa ya uwiano kati ya ubinadamu na uungu: Mungu anaonyesha unyenyekevu, haki, na upendo; huku k**a binadamu, akiwa mfano kamili wa maisha yenye maadili na ukamilifu wote.

Hypostatic union inathibitisha kwamba utu wa Mungu na utu wa kibinadamu vinaunganishwa ndani ya Yesu. Kupitia Maria, aliyechaguliwa kwa wema wake na unyenyekevu wake, kuzaliwa kwa Yesu kunakuwa kielelezo cha mpango wa kimungu. Hii inaonyesha falsafa ya msingi ya Kikristo: wokovu haujafanywa kwa nguvu tu, bali kwa mpango wa Mungu, kwa njia ya kielelezo cha binadamu aliye takatifu.

Msingi wa Biblia:
1. Luka 1:31–35
"Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu....”
- Hii inaonyesha mpango wa Mungu, kuzaliwa kwa kipekee lakini kwa njia ya kibinadamu.

2. Mathayo 1:21B
"...maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao".
- Hii ni kwamba Kuzaliwa kwa Yesu ni suluhisho la dhambi za wanadamu.

3. Yohana 1:14
" Naye Neno alifanyika mwili......”
- Hii inamaa kwamba Mungu aliingia alikuwa duniani k**a mwanadamu kamili, kushiriki hali yetu ya kibinadamu kwa ukombozi mkamilifu.

Hadhari,
Upande A wa Wazushi wanasema Yesu alikuwa mwanadamu bila kuwa Mungu na upande B kwamba Yesu alikuwa Mungu bila kuwa mwanadamu, na kwamba kuzaliwa kwake hakukuwa na maana ya kibinadamu. Hii inapotosha hypostatic union na mpango wa wokovu, ambao unahitaji Yesu kuwa Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja.

Ni vema kujua kuwa,
Kuzaliwa kwa Yesu k**a mtoto wa kibinadamu ni kielelezo cha unyenyekevu, upendo, na mpango wa Mungu kwa ajili ya wokovu. Hypostatic union inathibitisha kuwa Yesu ni Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja, na hivyo anaweza kufanikisha wokovu wa kila mmoja. Maria alichaguliwa kwa mpango wa kimungu, akidhihirisha usafi na mpango wa Mungu, na kuzaliwa kwa Yesu hakukuwahi kuwa jambo la kawaida, bali la kipekee lenye maana ya milele.

🎄 Heri ya Krismasi:
Wapendwa, wakati tunasherehekea kuzaliwa kwa Mwokozi wetu Yesu Kristo, tukumbuke kwamba uzuri wa Krismasi ni zaidi ya zawadi; ni fursa ya kutambua upendo wa Mungu, mpango wa wokovu, na unyenyekevu wa Mwanawe aliyezaliwa duniani kwa ajili yetu. Heri ya Krismasi kwa kila mmoja wetu, tukiwa na amani, upendo, na matumaini yasiyoyumba! - Much More Blessings!

“In Christ, Eternity remained God, yet chose to become human without ceasing to be God.”_GDeBxhop
---------------
🔚
𝘕𝘢 𝘔𝘵𝘶𝘮𝘪𝘴𝘩𝘪,
𝘎𝘦𝘳𝘴𝘩𝘰𝘮 𝘌. 𝘊𝘩𝘢𝘭𝘭𝘰
0769 743 737
📧 𝘨𝘤𝘩𝘢𝘭𝘭𝘰30@𝘨𝘮𝘢𝘪𝘭.𝘤𝘰𝘮
🗓️ Desemba 25, 2025
📘 #𝘎𝘋𝘦𝘉𝘹𝘩𝘰𝘱
📚 #𝘊𝘩𝘢𝘭𝘭𝘰𝘍𝘢𝘮𝘪𝘭𝘺𝘓𝘪𝘣𝘳𝘢𝘳𝘺

 🕊️  𝗙𝗨𝗠𝗕𝗢 𝗟𝗔 𝗧𝗛𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜📖  Mathayo 13:45-46"Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzur...
23/08/2025


🕊️ 𝗙𝗨𝗠𝗕𝗢 𝗟𝗔 𝗧𝗛𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜

📖 Mathayo 13:45-46
"Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua."

Yesu anatumia mfano huu kuonesha kwamba thamani ya kweli hupatikana kwa kitu kilicho adimu na cha kipekee, kiasi kwamba mtu yuko tayari kuacha vyote alivyokuwa navyo ili akipate. Lulu hiyo ni adimu, ghali, na yenye thamani isiyopimika; k**a ulivyo Ufalme wa Mungu.

𝐕𝐢𝐯𝐲𝐨 𝐡𝐢𝐯𝐲𝐨;
Kila kilicho na thamani ni ghali, na kila kilicho ghali huwa adimu (rare). Hivyo, rarity creates value; kilicho adimu ndicho kinachotengeneza thamani. Thamani ya mtu haipimwi kwa wingi wa mali au kwa urahisi wa kupatikana, bali kwa ubora na upekee wake. K**a vile lulu yenye thamani kuu au almasi adimu; havipatikani ovyo, bali vinachimbwa kwa gharama na kuthaminiwa kwa heshima kubwa.

Mwanadamu anayejitunza, kujiheshimu na kutokawaidisha mno maisha yake, hujengea nafsi yake hadhi ya pekee. Self-preservation creates value. Kwa hiyo, kuwa adimu si kujitenga, bali ni kujitunza; na hadhi hiyo ikupe heshima mbele za wanadamu na thamani ya kweli mbele za Mungu.

“𝘽𝙚𝙞𝙣𝙜 𝙧𝙖𝙧𝙚 𝙢𝙖𝙠𝙚𝙨 𝙮𝙤𝙪 𝙫𝙖𝙡𝙪𝙖𝙗𝙡𝙚 ~ 𝙠𝙪𝙟𝙞𝙩𝙪𝙣𝙯𝙖 𝙣𝙙𝙞𝙠𝙤 𝙝𝙪𝙛𝙖𝙣𝙮𝙖 𝙢𝙖𝙞𝙨𝙝𝙖 𝙮𝙖𝙠𝙤 𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙮𝙖 𝙥𝙚𝙠𝙚𝙚.”_ 𝙂𝘿𝙚𝘽𝙭𝙝𝙤𝙥
---------------
🔚
𝘕𝘢 𝘔𝘵𝘶𝘮𝘪𝘴𝘩𝘪,
𝘎𝘦𝘳𝘴𝘩𝘰𝘮 𝘌. 𝘊𝘩𝘢𝘭𝘭𝘰
0769 743 737
📧 𝘨𝘤𝘩𝘢𝘭𝘭𝘰30@𝘨𝘮𝘢𝘪𝘭.𝘤𝘰𝘮
🗓️ 𝘈𝘨𝘰𝘴𝘵𝘪 23, 2025
📘 #𝘎𝘋𝘦𝘉𝘹𝘩𝘰𝘱
📚 #𝘊𝘩𝘢𝘭𝘭𝘰𝘍𝘢𝘮𝘪𝘭𝘺𝘓𝘪𝘣𝘳𝘢𝘳𝘺

 🕊️  𝗞𝘂𝘃𝘂𝗻𝗷𝗮 𝗞𝗶𝗯𝘄𝗲𝘁𝗮: 𝗡𝗴𝘂𝘃𝘂 𝘆𝗮 𝗨𝗽𝗲𝗻𝗱𝗼📖 Marko 14:3"Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulan...
12/08/2025


🕊️ 𝗞𝘂𝘃𝘂𝗻𝗷𝗮 𝗞𝗶𝗯𝘄𝗲𝘁𝗮: 𝗡𝗴𝘂𝘃𝘂 𝘆𝗮 𝗨𝗽𝗲𝗻𝗱𝗼

📖 Marko 14:3
"Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulani, alikuja mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi; akakivunja kibweta akaimimina kichwani pake.”

Upendo wa kweli haujibakizi; hutoa hadi mwisho. Mwanamke wa Bethania alipovunja kibweta chake cha thamani, alitangaza kuwa hakuna kilicho bora zaidi kuliko kumpa Kristo. Vivyo hivyo, tunapovunja vibweta vyetu;nguvu, muda, vipaji, hata tamaa zetu, harufu ya upendo wetu humjazia Mungu na kuwagusa watu.

:
Maisha bila kutoa si maisha halisi, bali kivuli chake. Kuvunja kibweta ni kukataa ubinafsi na kukumbatia utoaji usio na masharti, unaojenga Kanisa na jamii. Wakristo wanapomimina nguvu na ubunifu wao kwa Bwana sasa, wanakuwa nguzo thabiti za Kanisa la leo na la vizazi vijavyo.

"𝙈𝙖𝙛𝙪𝙩𝙖 𝙮𝙖𝙨𝙞𝙮𝙤𝙢𝙞𝙢𝙞𝙣𝙬𝙖 𝙝𝙪𝙠𝙤𝙨𝙖 𝙝𝙖𝙧𝙪𝙛𝙪, 𝙣𝙖 𝙢𝙤𝙮𝙤 𝙪𝙨𝙞𝙤𝙩𝙤𝙖 𝙝𝙪𝙠𝙤𝙨𝙖 𝙪𝙯𝙞𝙢𝙖." — 𝙂𝘿𝙚𝘽𝙭𝙝𝙤𝙥

:
Je, utahifadhi mafuta yako kwa ajili yako binafsi, au utayatoa kwa Kristo?.
---------------
🔚
Na Mtumishi,
Gershom E. Challo
0769 743 737
📧 [email protected]
🗓️ Agosti 10, 2025
📘
📚

Glory be to God!!
10/08/2025

Glory be to God!!

08/08/2025


🕊️ 𝗡𝗗𝗢𝗔: 𝗛𝗘𝗦𝗛𝗜𝗠𝗔, 𝗨𝗦𝗔𝗙𝗜 𝗡𝗔 𝗛𝗨𝗞𝗨𝗠𝗨

📖 Waebrania 13:4
𝘕𝘥𝘰𝘢 𝘯𝘢 𝘪𝘩𝘦𝘴𝘩𝘪𝘮𝘪𝘸𝘦 𝘯𝘢 𝘸𝘢𝘵𝘶 𝘸𝘰𝘵𝘦, 𝘯𝘢 𝘮𝘢𝘭𝘢𝘻𝘪 𝘺𝘢𝘸𝘦 𝘴𝘢𝘧𝘪; 𝘬𝘸𝘢 𝘮𝘢𝘢𝘯𝘢 𝘸𝘢𝘢𝘴𝘩𝘦𝘳𝘢𝘵𝘪 𝘯𝘢 𝘸𝘢𝘻𝘪𝘯𝘻𝘪 𝘔𝘶𝘯𝘨𝘶 𝘢𝘵𝘢𝘸𝘢𝘩𝘶𝘬𝘶𝘮𝘶 𝘢𝘥𝘩𝘢𝘣𝘶.

𝐢. 𝐃𝐢𝐛𝐚𝐣𝐢
Ndoa ni agano takatifu lililowekwa na Mungu tangu mwanzo, ikikusudia kuwa uhusiano wa heshima, uaminifu na usafi kati ya mume na mke. Katika Aya hii, Mungu anatufundisha mambo matatu ya msingi yanayohakikisha ndoa inabaki kuwa baraka na si laana: ndoa, kuyatunza yakiwa safi, na kutambua kwamba uvunjaji wa agano hili na Mungu mwenyewe. Fundisho hili linachambua kwa undani maana ya maneno haya matatu, likiweka wazi wajibu wa kila mtu; iwe ameoa, hajaolewa, au ni sehemu ya jamii inayoizunguka ndoa; na kutufundisha namna ya kulinda agano hili takatifu dhidi ya dhambi ya uasherati na uzinzi. Ni mwongozo wa hekima na onyo la Mungu kwa kizazi chetu, ili ndoa zetu ziwe mfano halisi wa upendo wa Kristo kwa Kanisa lake.

𝐢. 𝐇𝐞𝐬𝐡𝐢𝐦𝐚 𝐲𝐚 𝐍𝐝𝐨𝐚 (𝐌𝐚𝐫𝐫𝐢𝐚𝐠𝐞 𝐝𝐢𝐠𝐧𝐢𝐭𝐲 𝐢𝐧 𝐚𝐥𝐥)
Aya inaanza kwa kusisitiza heshima ya ndoa, na kusema iwe imetiwa thamani na watu wote. Maneno ” yanajumuisha:
• Wanaotaka ndoa (wapendanao wanaojiandaa kuingia ndoa),
• Walioona (wanandoa wenyewe), na
• Jamii kwa ujumla, pamoja na wale wasioingia ndoa; lakini wanaathiriwa na ndoa katika maisha yao k**a marafiki, familia, na viongozi wa jamii.

Kipengele hiki kinafundisha kuwa ndoa si kitu cha aibu au cha kupuuzwa katika jamii, bali ni kitendo cha heshima, muhimu na cha kimaadili kinachopaswa kulindwa na kuthaminiwa na kila mtu. Katika muktadha wa Kikristo, ndoa ni kati ya mume na mke, na ni mfano wa uhusiano wa Kristo na kanisa (Rum 7:4; Efe 5:22-33), hivyo inapaswa kuenziwa na kuheshimiwa.
~ Marriage, therefore, is not merely a social contract but a divine covenant that demands honour from all; those entering into it, those within it, and the community at large that supports and witnesses this sacred union.

𝐢𝐢. 𝐔𝐬𝐚𝐟𝐢 𝐰𝐚 𝐌𝐚𝐥𝐚𝐳𝐢 (𝐓𝐡𝐞 𝐛𝐞𝐝 𝐮𝐧𝐝𝐞𝐟𝐢𝐥𝐞𝐝)
Sehemu hii inaelezea usafi wa mahusiano ya ndoa, hasa kuhusu usalama wa uaminifu na kutojihusisha na uasherati ndani ya ndoa. au kitanda ni mahali pa faragha ambapo uhusiano wa mume na mke unadhihirishwa. Kuwa safi kunamaanisha:
• Hakuna uasherati au uzinzi unaoruhusiwa,
• Kuna Uaminifu kamili na heshima kati ya wanandoa,
• Mahusiano hayo yanatakiwa kuwa ya kuaminika na yasiyoharibiwa na mtu mwingine wa nje.

Kwa mtazamo wa theolojia, hii inaonyesha kuwa tendo la ndoa ni iliyotengwa kwa wale walio ndani ya ndoa (1Kor 7:3-5). Hivyo, kitanda cha ndoa kinapaswa kuwa “ ,” kisichochafuliwa na dhambi ya uzinzi au uasi wa ndoa.
~ The "bed" as a symbol of conjugal intimacy must remain pure, reflecting faithfulness and holiness as ordained by God, protecting the sanctity of the marital union.

𝐢𝐢𝐢. 𝐇𝐮𝐤𝐮𝐦𝐮 𝐤𝐰𝐚 𝐖𝐚𝐚𝐬𝐡𝐞𝐫𝐚𝐭𝐢 𝐧𝐚 𝐖𝐚𝐳𝐢𝐧𝐳𝐢 (𝐉𝐮𝐝𝐠𝐦𝐞𝐧𝐭 𝐭𝐨 𝐰𝐡𝐨𝐫𝐞𝐦𝐨𝐧𝐠𝐞𝐫𝐬 𝐚𝐧𝐝 a𝐝𝐮𝐥𝐭𝐞𝐫𝐞𝐫𝐬)
Aya inahitimisha kwa onyo kali kuhusu adhabu ya Mungu kwa wale wanaovunja agano la ndoa:
: Wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi mara kwa mara nje ya ndoa, kwa makusudi (1 Thes 4:3-5).
: Wanaovunja uaminifu wa ndoa kwa kushiriki mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine asiye wake (Mhu 7:25).

Fundisho la theolojia ni wazi: Mungu ni mtakatifu na haki, na haavumili dhambi ya uvunjaji wa agano la ndoa. Hii ni onyo thabiti kwamba uzinzi ni dhambi yenye athari kubwa, si tu kijamii bali pia kiroho, ikizuia mtu kuingia katika ufalme wa Mungu (1 Kor 6:9-10).
~ God’s judgment on such sins underscores the holiness and seriousness of the marriage covenant, reminding believers to uphold purity and fidelity in their relationships.

𝟐. 𝐓𝐚𝐦𝐚𝐭𝐢
Aya hii inatufundisha kuwa ndoa ni kubwa inayopaswa kulindwa na kuthaminiwa na kila mtu katika jamii. Haijalishi mtu huyo ni nani; iwe ni yule anayetaka kuingia ndoa, wanandoa wenyewe, au watu wa kijamii; ndoa ni kitendo cha heshima na uaminifu unaopaswa kulindwa kwa bidii.
, k**a mahali pa faragha na waaminifu, yanapaswa kuwa safi, bila dhambi ya uzinzi wala uasherati.
Mwisho, tukumbuke kuwa Mungu ndiye Muamuzi wa mwisho wa tabia zetu, na kwa hakika waasherati na wazinzi. Hivyo basi, kila mtu ashike bidii katika uaminifu na usafi wa ndoa, akiheshimu agano hili la kiungu kwa unyenyekevu na hofu ya Mungu.
“𝑵𝒅𝒐𝒂 𝒔𝒊 𝒎𝒌𝒂𝒕𝒂𝒃𝒂 𝒘𝒂 𝒌𝒂𝒓𝒂𝒕𝒂𝒔𝒊, 𝒃𝒂𝒍𝒊 𝒏𝒊 𝒂𝒈𝒂𝒏𝒐 𝒍𝒂 𝒓𝒐𝒉𝒐 𝒍𝒊𝒏𝒂𝒍𝒐𝒅𝒖𝒎𝒖 𝒌𝒘𝒂 𝒖𝒂𝒎𝒊𝒏𝒊𝒇𝒖.” _ 𝑮𝑫𝒆𝑩𝒙𝒉𝒐𝒑

Mungu wa Mbinguni akubariki na kukujaalia heshima na adabu juu kuhusu eitha ndoa yako au ya mwenzako.
---------------
🔚
Na Mtumishi,
Gershom E. Challo
0769 743 737
📧 [email protected]
🗓️ Agosti 08, 2025
📘
📚

 🕊️ 𝗦𝗜𝗞𝗜𝗟𝗜𝗭𝗔 𝗧𝗘𝗡𝗔 𝗡𝗔 𝗧𝗘𝗡𝗔 👂‍🦻📖 Yakobo 1:19"Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kuka...
07/08/2025


🕊️ 𝗦𝗜𝗞𝗜𝗟𝗜𝗭𝗔 𝗧𝗘𝗡𝗔 𝗡𝗔 𝗧𝗘𝗡𝗔 👂‍🦻

📖 Yakobo 1:19
"Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika."

𝐃𝐢𝐛𝐚𝐣𝐢
Katika maisha, hekima haipatikani kwa haraka ya kutoa majibu, bali kwa utulivu wa kusikiliza tena na tena. Dunia ya leo ina sauti nyingi, kelele nyingi, na mitazamo mingi; lakini ni wachache wanaojua thamani ya kusikiliza kwa makini kabla ya kutenda. Kusikiliza tena na tena si udhaifu wa kusuasua, bali ni uthibitisho wa akili iliyopevuka, roho iliyo tayari kujifunza, na moyo uliojaa busara.

𝐌𝐚𝐚𝐧𝐚 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐢𝐤𝐢𝐥𝐢𝐳𝐚 𝐓𝐞𝐧𝐚 𝐧𝐚 𝐓𝐞𝐧𝐚
Kusikiliza tena na tena ni utayari wa kufungua masikio na moyo zaidi ya mara moja, ili kutafakari kwa kina na kupata maana ya ndani ya jambo. Ni tendo la kurudia kusikia si kwa sababu hukusikia mara ya kwanza, bali kwa sababu unatamani kuelewa vizuri zaidi. Ni namna ya kuacha haraka, kuepuka jazba, na kuchagua hekima badala ya mazoea.

𝐉𝐢𝐜𝐡𝐨 𝐥𝐚 𝐤𝐢𝐛𝐢𝐛𝐥𝐢𝐚
Katika Maandiko, kusikiliza kunathaminiwa k**a lango la kuelewa na utiifu. Yesu alisema: “Yeye aliye na masikio, na asikie.” (Math 13:9). Hii haikuwa wito wa kimwili tu, bali ni agizo la kiroho; kwamba mtu anatakiwa kusikiliza kwa utulivu, kuelewa kwa moyo, na kutii kwa maisha.

Mungu haongei katika makelele, bali katika sauti ya upole na utulivu (1 Fal 19:12). Ni wale wanaojifunza kusikiliza tena na tena ambao huelewa mapenzi ya Mungu kwa usahihi na kwa wakati. Yakobo anaweka msingi wa hekima ya kimaadili kwa kusema: "Mwepesi wa kusikia, si mwepesi wa kusema, wala wa hasira.”
Hii ni dira ya mtu mwenye busara anayejua kwamba majibu sahihi hutanguliwa na usikivu sahihi.

𝐌𝐭𝐚𝐳𝐚𝐦𝐨 𝐰𝐚 𝐊𝐢𝐟𝐚𝐥𝐬𝐚𝐟𝐚
Katika falsafa ya kale,
~ Socrates alifundisha kuwa mwanzo wa hekima ni kutambua kuwa hujui kila kitu. Hilo hujidhihirisha si kwa kuongea sana, bali kwa kusikiliza kwa kina.
~ Plato aliamini kuwa kusikiliza tena huleta mwanga mpya kwa jambo ulilolisikia mara ya kwanza.
~ Aristotle alisema: "Akili iliyoelimika huweza kuzingatia wazo bila kulikubali mara moja."

Kwa hiyo, kusikiliza tena na tena ni tendo la hekima ya juu; si kwa ajili ya kurudia kusikia tu, bali kwa ajili ya kufikiri upya, kupima upya, na kuelewa kwa uzito zaidi.

𝐔𝐦𝐮𝐡𝐢𝐦𝐮 𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐢𝐤𝐢𝐥𝐢𝐳𝐚 𝐓𝐞𝐧𝐚 𝐧𝐚 𝐓𝐞𝐧𝐚
i. Hujenga uelewa wa kina na usio wa juu juu.
ii. Huongeza heshima kwa anayezungumza na kujenga uhusiano wa kweli.
iii. Huzuia uamuzi wa haraka, hasira, na makosa ya kihisia.
iv. Hukuandaa kutenda kwa msingi wa maarifa sahihi, si dhana au ushabiki.
v. Huimarisha usikivu wa kiroho kwa sauti ya Mungu, hata katika ukimya.
vi. Huonesha unyenyekevu wa ndani na kutojiamini kupita kiasi.
📖 Mtu anayejibu kabla ya kusikia, huo ni upumbavu na aibu kwake. {Mith 18:13}

𝐓𝐚𝐦𝐚𝐭𝐢 𝐲𝐚 𝐃𝐢𝐫𝐚
Mtu wa hekima hachukuliwi na haraka ya dunia, bali hujizuia, hujinyenyekeza, na husikiliza tena na tena. Katika kusikiliza mara ya pili, unaweza kugundua maana uliyokosa mara ya kwanza.

Katika kusikiliza mara ya tatu, unaweza kubaini sauti ya Mungu ikinena kwa sauti ya utulivu. Na katika kusikiliza kwa moyo, ndipo unapoelewa na kutenda kwa usahihi; Na hiyo ndio Dira ya Hekima ya mtu anayependa kutenda kwa maarifa badala ya hisia, na kwa ukweli badala ya pupa.

SIKILIZA TENA, TAFAKARI KWA KINA, NDIPO UTENDE KWA UJASIRI ULIOJAA BUSARA. _ 𝘎𝘋𝘦𝘉𝘹𝘩𝘰𝘱

Mungu akubariki na kukujalia KUSIKILIZA TENA NA TENA.
---------------
🔚
𝘕𝘢 𝘔𝘵𝘶𝘮𝘪𝘴𝘩𝘪,
𝘎𝘦𝘳𝘴𝘩𝘰𝘮 𝘌. 𝘊𝘩𝘢𝘭𝘭𝘰
0769 743 737
📧 𝘨𝘤𝘩𝘢𝘭𝘭𝘰30@𝘨𝘮𝘢𝘪𝘭.𝘤𝘰𝘮
🗓️ 𝘈𝘨𝘰𝘴𝘵𝘪 07, 2025
📘 #𝘎𝘋𝘦𝘉𝘹𝘩𝘰𝘱
📚 #𝘊𝘩𝘢𝘭𝘭𝘰𝘍𝘢𝘮𝘪𝘭𝘺𝘓𝘪𝘣𝘳𝘢𝘳𝘺

Address

Kiteto/P. O. Box 74
Manyara
CFL

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when CFL-Rhēma posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to CFL-Rhēma:

Share

Category