Mkote global

Mkote global Taifa la Ufalme wa Mbinguni

20/01/2026

1. Kitu ambacho mwanadamu kapoteza katika maisha yake ni Ufalme wa Mungu.
- ufalme ndio msingi mkubwa zaidi wenye uwezo wa kumfanya mwanadamu ( a) aweze kuishi kuishi kwa amani ( b) aweze kumzalia Mungu matunda ,
anasema, "Yohana 15:16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

huwezi mzalia Mungu matunda endapo ukiwa nje ya Ufalme wake.

kwasababu hizi.
1: Mtu ni roho ana Kaa ndani ya mwili na ana nafsi.
2: Nguvu ya kufanya kazi duniani na kuleta matokeo inatoka katika ulimwengu wa roho.
3: Mtu akiwa duniani, akitaka kufanikiwa kwa jambo lolote, lazima apate msaada katika ulimwengu wa roho, /
Mungu hakumuumba Mtu kufanikiwa duniani bila msaada wa rohoni/ ulimwengu wa roho.
anasema "Waebrania 11:3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.

kwa hiyo Sasa Mtu kufanikiwa duniani pasipo msaada wa Mfumo wa ufalme wa Mungu ni ngumu, lakini pia hakuna mafanikio nje ya Mfumo wa Ufalme wa Mungu yatakayo mwacha Mtu salamaa, lazima yamwangamize tu;
anasema, "Mithali 1:32 Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.

Cha kufanya ni
kuutafuta Hadi tuupate Ufalme wa Mungu kwenye Kila eneo la maisha yetu, ndio suluhisho pekee alilo Baki nalo Mtu.
eg: Luka 15:4, 8
4 Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?

8 Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?

10/01/2026

UFALME KWANZA - MATHAYO 6: 33

Ni somo ambalo tutajifunza kwa mfululizo na pointi, ambazo zitatupatia kulielewa hili somo, angalau kwa sehemu atakayo tujalia Mungu wetu wa Mbinguni.

1. Kuutafuta Ufalme wa Mungu na haki yake, ni agizo ambalo wanadamu wote tumepewa.

2. Mtu aliwekwa duniani kwa makusudi maalum ya Mungu mwenyewe,
-kusimamia ufalme wa Mungu na ukuaji wake hapa duniani / kuwa wakili wa Mungu hapa duniani.
- 1 Wakorintho 4:1-2
1 Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.

tupo hapa duniani k**a mawakili wa alituweka, tupaswa kufanya Yale ya aliye tuweka sio ya kwetu.
-
Waebrania 13:21
awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, (naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake), kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina.

jambo analotaka Mungu ni kuona anatawala na dunia pia kupitia mtu.

3. Ni jambo Moja tu ambalo wanadamu tumeambiwa tulitafute, { nalo ni Ufalme na haki}
- lakini wanadamu tunatafuta maisha, pesa nk, ambavyo ni sio maagizo ya Mungu kwetu kuyatafuta.

4. Kinacho Fanya Ufalme na Haki vionekane ni vigumu kuvitafuta kwa wengibwetu, ni kwa sababu wengi tuna mambo mengi ambayo tunayatafuta,
lakini ametupatia jambo Moja tu la kulitafuta { Ufalme na Haki}
Bwana Yesu alisema hivi,
Mathayo 6:24
Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashik**ana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
- tunayo yatafuta hayo yanatuweka kwenye huo utumishi wa tunacho kitafuta

5. Ufunuo wa Yohana 3:15-16
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri k**a ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

- Moja ya sababu inayo leta uvugu vuga katika Misha ya watu ni , mambo mengi tunayo yatafuta,
ni kwa sababu hayo mengine tunayo yatafuta yanataka mda wetu, nguvu, akili nk. na Mungu Naye anataka hivo pia,
- Sasa ni unawezaje kujigawa ukawarisha wote wawili, jua ni ngumu Sana, lazima mmoja atafurahi na mwingine utamkera tu.

6. Kumbuka uvugu vugu Hauna matokeo yanayo eleweka, hayatajulikana ni ya Ki Mungu au dunia kwa sababu hayatakuwa upande wa Mungu.
- kwa hiyo faida ambazo ulitakiwa uzipate kwa Mungu hutazipata, na uzuri wa kimahusiano baina Yako na Mungu hutauona,
...............

01/01/2026

Have a blessed year

Address

Makambako

Telephone

+255769345986

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mkote global posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Mkote global:

Shortcuts

Share