03/05/2026
UTANIOA AU UNANICHEZEA?
Kaswali ka kijinga sana haka
Mabinti niwaulize
K**a kijana amedhamiria kukuchezea na kukuacha, unadhani ukimuuliza swali k**a hili hata ulie machozi ya damu unadhani kuna mtu alishawahi kujibiwa anachezewa tu ili aachwe?
Jibu siku zote ni NITAKUOA SIKUCHEZEI
Atakuvuta kifuani, atakubembeleza.. atakwambia mpaka upo hapa nimekuchagua wewe. Unavyoniona unahisi labda nakuchezea? Hapo atakubusu kwenye paji la uso au mdomoni au shavuni.
Hapo itajihisi upo paradiso, utampa maji katika kisima chako. Atakunywa mara kadhaa
LAKINI, mpe muda. Atagundua amezoea anahitaji ladha nyingine.
Majibu utayapata ukishachezewa
Utakuja kugundua, ulikua na nafasi ya kugundua unachezewa bila hata kuuliza, majibu ulikua unayaona ni vile tu unachukuliaga mambo kirahisi na hupendi kushughulisha ufahamu. Huwa unatumia hisia zaidi kuliko akili
Usiendekeze hisia
Hisia huwa hazina jema, zimejaa ubinafsi kutaka kutulizwa bila kujali nini kitatokea baadaye na kitakachotokea zitakuacha katika hali gani!
Hisia huwa zinasaliti. Asubuhi zinakushawishi kufanya jambo jioni zinageuka maumivu zinautesa moyo
Ndio maana Mungu akampa mtu akili aweze kutambua jema na baya ili kuweza kuzidhibiti hisia.
Mara nyingi watu hudanganywa, uongo huamsha hisia za ukweli,
Unaweza kudanganywa unapendwa kisha wewe ukapenda kweli
Si kwa sababu unapenda panapopendeka bali hisia ndizo zinakutuma. Hisia huwa hazichagui mtu, mahali, mazingira au hali. Hujawahi kuona watu wanakutana kimwili vichakani bila kujali wataumwa na nyoka? Hujawahi kuona mtu analala na kichaa mchafu kabisa na hajali? Hisia hizo, usije ukazipa nafasi ya kukutawala sababu zenyewe popote kambi, popote weka tuweke!! Popote tu DJ tuondoke. Hizo ndo hisia sasa
Mh yaani hisia huwa hazieleweki zinataka nini, zinaweza kukataa ukweli zikavutiwa na uongo.
Hisia yaani, zinaweza kukufanya usisikilize mzazi aliyekuzaa ukamsikiliza kijana mliyekutana njiani tu wiki iliyopita mkapeana namba
Hisia zonaweza kufanya uone kila anayekutakia mema anakuchukia au anakuonea wivu
Unaweza kuacha vya thamani kwa sababu tu ya hisia.
Unaweza kutoroka kwenu na usiwaze wanaokuhusu watakua kwenye hali gani, hisia ni balaa
Mtaani wanasema, unatema big g kwa karanga za kuonjeshwa
Hisia zipo kukuonjesha tu na si kumaliza njaa yako
Vya kuonja havishibishi, Utahitaji kuonja kila wakati,
Ndivyo zilivyo hisia, haziridhiki, utazipa zinachotaka leo na kesho zitataka tena. Utakua mtumwa wa hisia
Lakini hisia huwa zina ushawishi lakini hazina nguvu mpaka pale umeziruhusu.. Ukishaziruhusu zinaanza kukutawala
Baada ya hapo hisia zinakutuma cha kufanya,
Kumbe shia sio hisia , shida ni hisia zisizodhibitiwa
Hisia zikemee
Hisia zikomeshe
Hisia zikomoe
Hisia ziwajibishe, ziambie zinaelewa na zinasikia
Lazima zijue hazina umuhimu huo ambao zinajipa
Lazima zijue wewe ndiye mtawala na zenyewe zinapaswa zinyenyekee na unachoamua ndicho kinachotoa uelekeo
Sasa wewe jikute mama huruma unazihurumia hisia
Hisia zinaweza kukugeuza ukawa k**a kifungashio cha maandazi, kila unachosukumwa unafanya!
Usisahau, hisia yoyote isiyo na jicho la kuona kesho ni utapeli
Utapeli wowote unashughulikiwa kisawasawa haijalishi ni tapeli la ndani yako au tapeli la nje. Kataa hisia za kitapeli. Unastahili kilicho bora
Hisia pekee zinazopaswa kujaliwa ni zile ambazo zimelenga kukutengenezea maisha bora
Yaani ingekuwa poa sana siku uamke usikie hisia za kuwa na kiwanja, usikie hisia za kuwa na nyumba, kufungua kampuni, biashara nk halafu uzitoe kwemye kundi la hisia uweke kwenye kundi la mambo yanayohitaji utekelezaji
Yale mahisia mengine ndio asilimia kubwa watu hukimbilia utekelezaji bila kujiuliza mara mbili mbili na mwisho hubaki katika majuto.. Huna nyota ya samaki wewe. Kaza mtu wangu k**a beki hazikabi kiviiiile si dhambi weka kufuli halafu tupa funguo tuokoe future
Niliwahi kusikia hadithi ya muwa kuzamisha meli
Nikasema heeee! Kivipi? Yawezekanaje Muwa mdogo kuzamisha li meli likubwa!
Nilipozama ndani nikagundua, vinavyoangushwa mara nyingi si vidhaifu na vinavyoangusha vyenye nguvu si vyenye nguvu
Unaweza kutafuna mua fakachu fakachu wakati unasikilizia utamu hadi kisogoni ndio meli inazama hivyo... Mua si gharama sana ila meli ni gharama. Tukiambiwa tupoteze kimoja mimi naona mua ungeachia tu space apo japo kuna mjinga mmoja asingekua tayari kuachilia utamu uende so hapo angekomaa na utamu na meli yake vyote kwa pamoja halafu kingetokea mshika mbili moja huponyoka na vile akili ni fupi kinachoponyoka ni kile kinachohitaji akili nyingi, sasa unaona hisia hazina gharama sana chenye gharama ni future lakini kwa bahati mbaya inaharibiwa kwa hisia za bei cheee
K**a vile ambavyo kamba inaweza kuwa imara lakini pale penye udhaifu pakakatika na kamba yote kuonekana haina maana ndivyo ilivyo!!
Hisia ni kasehemu kadogo tu k**a katone ka maji kwemye ndoo ndivyo zinaweza kufanya maisha yako yote yaonekane hayana maana
Si kwamba huna maana,
Lakini hisia zinaweza kufuta ile maana,
Hisia zinaweza kubadili utambulisho wako
Hisia zinaweza kukuondoa kwenye ramani ya maisha
Tanguliza mbele thamani yako
Hisia zisikufanye uweke rehani mwili wako
Zingatia kusudi lako kabla ya hisia za mwili wako
Hisia huwa hazidumu, usipoteze thamani yako ya kudumu kwa hisia za kupita!!
Waza kesho yako yenye uhakika unayoikabidhi mikononi mwa wanyang'anyi kwa sababu ya leo isiyo na uhakika.
Kwenye huu ulimwengu wa kuviziana, wajinga ndio waliwao... endekeza hisia kitakachoumia ni zaga halafu Utakufa vibaya!!