08/06/2023
MCHUNGAJI KIONGOZI EBEN MSHIU.
SOMO: MKULIMA MWEMA.
Yohana 15:1-3 "Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia."
Mkulima ni MUNGU, Mzabibu ni YESU na wenye kubeba Matunda au tawi ni sisi. Mwenye shamba ama Mkulima ndio mwenye maamuzi ya kuchagua mazao gani ya kulima, na alime kwa kiasi gani, na anajua kwa zao alilopanda aweke mbolea gani ili mazao yastawi.
Lakini ili tawi listawi na kuzaa Matunda kuna kanuni za kufuata, hivyo MUNGU anapokutangazia ustawi, baraka na utajiri ili upokee unatakiwa ufuate utaratibu na kanuni za MUNGU. Mzabibu mwema ni wale wanaozaliwa wakiwa ndani ya YESU.Wewe k**a huwezi kuzaa bila shina lenye virutubisho unavyotakiwa kwa ajili ya Matunda.
MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUZAA MATUNDA
1.Hakikisha unazingatia kanuni za MUNGU, taratibu na maelekezo ya MUNGU.
2. Hakikisha unajitambua kuwa wewe ni nani, wewe ni sura na mfano wa MUNGU, kuwa unaweza kutawala na kumiliki vyote vilivyoumbwa na MUNGU.
3. Shika Neno lake na Amri zake, maisha yako ishi k**a Neno linavyosema, hakikisha moyoni mwako umeliweka Neno na tendea kazi Amri za MUNGU.