World Mission & Evangelistic Association

World Mission & Evangelistic Association World Mission & Evangelistic Association-Is non profit Organisation Preaching good news of the Kingdom of God, working hand to hand with Churches.

20/06/2024
From GLOBAL FIRE STARTER MINISTRIES, Forwarded by World Mission.Urgent Message of the People in Ukraine: The conditions ...
06/11/2022

From GLOBAL FIRE STARTER MINISTRIES, Forwarded by World Mission.
Urgent Message of the People in Ukraine:

The conditions in Ukraine right now; Temperatures are already below 32 degrees at night and more than 250,000 families with children, elderly grandparents, or disabled relatives are homeless due to the war.

We want to build 20 homes by winter, which is only 48 days away. Our prayer is that we can build even more. But we need your help NOW to meet this humanitarian crisis. We have a builder who can construct an insulated, tiny home for $5,000. We are excited to work with them to get as many families into homes before they freeze to death. YOU are literally someone’s answer to prayer by keeping them warm and alive this winter. Please be generous. For more information and to donate:

Our goal is to activate, equip, and catapult men and women of all ages to fulfill their Kingdom purpose. Learn more about our global efforts.

KUTO KUSAMEHE,UCHUNGU,HASIRA NA YANAYO FANANA NA HAYO NI HATARI KUBWA KWA MTU🔷Huharibu utu wa mtu.🔷Hufungua mlango wa ba...
09/09/2022

KUTO KUSAMEHE,UCHUNGU,HASIRA NA YANAYO FANANA NA HAYO NI HATARI KUBWA KWA MTU
🔷Huharibu utu wa mtu.
🔷Hufungua mlango wa baadhi ya magonjwa.
🔷Huharibu mahusiano.
🔷Ni kikwazo Cha kujibiwa Maombi.
🔷Ukishikilia hayo unajiweka kwenye mwelekeo ambao ni hatari katika maisha yako wewe mwenyewe.

USHAURI
🧲Amua leo kusamehe walio kukosea,hata K**a hawaja kuomba msamaha/Samehe bure kabisa.
🧲Achilia moyoni mwako Mambo Yale ambayo yamekuletea uchungu.
🧲Anza Safari mpya ya kupenda,wapende hata wale ambao Hakuna hata sababu ya Kuwapenda(watendee mema).
🧲Kumbuka Yesu pekee ndiye anaweza kukusaidia kushinda Hali hizi hivyo Anza kwa kutubu mbele zake na umwambie atawale maisha yako na akujaze Roho Mtakatifu na pendo lake;utaanza kuona chemichemi za maji ya uzima ndani yako.
RUMI 5:5

ANGALIZO
➖Usipokuwa makini na ukaendelea kushikilia Mambo hayo(Kutokusamehe,uchungu,hasira na maovu yote) si tu kwamba unapata hasara katika Ulimwengu huu bali unaweza kuja kujikuta unatengwa na Mungu milele.
🟣Kumbuka mara zote Mungu hawezi kukusukuma kuchukia mtu/watu wengine; Hivyo hiyo Hali ambayo inakusukuma usisamehe au usiwapende wengine Tambua kuwa shetani yupo kwenye biashara ya kutaka kuharibu maisha yako. (Lazima uamue kumpinga na kukataa misukumo yake kwenye maisha yako)
Yakobo 4:
7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
MAOMBI YANGU KWAKO
🟪Mungu akupe neema ya wewe kuanza kutembea kwa amani na watu wote na huo utakatifu,ambao pasipo huo hakuna atakaye muona Mungu.
=EBRANIA 12:14
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

MUNGU AKUBARIKI SANA.

World Mission Library
Email- [email protected]

Na Habari Njema ya Ufalme itahubiriwa kila Mahali Ulimwenguni mwote; Kila mmoja mahali ulipo una wajibu wa Kufanya kwaaj...
05/09/2022

Na Habari Njema ya Ufalme itahubiriwa kila Mahali Ulimwenguni mwote; Kila mmoja mahali ulipo una wajibu wa Kufanya kwaajili ya Ufalme wa Mungu.

FAIDA YA KUWA KARIBU NA MTU ALIYE JUU YAKOKila nafasi unayopata kwenye maisha  kuwa karibu na mtu fulani wa juu yako huw...
22/08/2022

FAIDA YA KUWA KARIBU NA MTU ALIYE JUU YAKO

Kila nafasi unayopata kwenye maisha kuwa karibu na mtu fulani wa juu yako huwa inakupa faida kubwa ambayo inabidi uitumie kimkakati.

Faida mojawapo ya kuwa na mtu aliyekuzidi ni kujifunza kupitia yeye.

Kuna fursa unapewa kuwa msaidizi/chini ya wengine ili ujifunze,

Badala ya kuanza kupambana nao na kutaka kuwashusha au kufanya mbinu ukitamani waharibikiwe,

Tumia muda huo kujifunza ili zamu yako itakapofika usikosee walipokosea wao.

Usijikite katika kuwakosoa waliotangulia au walio juu yako, tumia makosa yao kujifunza ili na wewe usirudie. Watoto wengi walio mabingwa wa kukosoa wazazi wao kwa kutowaandalia maisha, nao wameishia kuwa mzigo kwa watoto wao.

Jifunze kuheshimu kila aliye juu yako hata k**a ukimuangalia unaona una uwezo kuliko wao.

Kuna wale ambao ukiwaangalia unaona k**a unastahili kuliko wao, badala ya kuwasema vibaya, chimbua ujifunze walifikaje hapo na utafute unachoweza kuiga.

Kumbuka, kuna watu ambao wako juu yako, hata ukiweka bidii ya kuwashusha nafasi walizoziacha hautazipata.

Kuwa chini ya mwingine ni fursa ya kukaa darasani kujifunza, itumie vyema ili zamu yako ikifika usichekwe.

IMEANDIKWA NA NDUGU JOEL NANAUKA.

UNAHITAJI MCHANGO WA WATU WENGINE.🟣Hata Uwe na uwezo mkubwa kiasi gani katika eneo lolote Unahitaji watu wengine.➖Namna ...
02/08/2022

UNAHITAJI MCHANGO WA WATU WENGINE.

🟣Hata Uwe na uwezo mkubwa kiasi gani katika eneo lolote Unahitaji watu wengine.
➖Namna Mungu alivyo tuumba alitufanya tutegemeane,hakuna ambaye alitengenezwa ajitosheleze mwenyewe bila kuhitaji mchango wa watu wengine.

➖Maisha yana thamani unapo itambua na kuthamini nafasi ya wengine katika maisha yako.

🟣Walio jikinai nafsi zao hudhani kwamba wao ni Bora kuliko watu wengine.
➖Hupenda kujitukuza na kuona wanatukuzwa na watu wengine.

➖Hutaka kuona kauli zao zinakuwa Sheria isiyo weza kurekebishwa au ikipingwa pale inapo bidi.

Mtazamo wa kujiona huhitaji mchango wa watu wengine ni mtazamo mbaya kabisa.
➖Utakufanya usiwe karibu na watu wengine.
➖Utazuia nafasi ya watu wengine kutumia uwezo walio nao Ndani Yao.

USHAURI
🔲Badili mtazamo wako Ndani yako juu ya watu wengine.
➖Ona kwamba hujakamilika bila kuhitaji wengine.
➖Tambua kuwa Kila mtu ni wa thamani, na kwa wale ambao Mungu anawaleta kwako basi wape nafasi ya kutumia uwezo ulioko Ndani Yao.
▪️Weka mlango wazi wao kukushauri
▪️Kukutia moyo.
▪️Kukuonyesha kuwa umekisea pale unapo kuwa umekosea Ili ujirekebishe.

Tambua kuwa wewe ni wa thamani,lakini pia Kila unaye muona anathamani sana; Wale walio karibu nawe wape nafasi ya kutumia uwezo ambao Mungu ameweka Ndani Yao.
➖Vipawa vilivyo Ndani Yao vitaibuka na kuanza Kutenda kazi kusudiwa.
➖Kila mmoja kwa nafasi yake atajiona ni wathamani.

NEEMA YA MUNGU IZIDI SANA JUU YAKO.

World Mission Library
Email : [email protected]

25/07/2022

MUNGU AMEWEKA HAZINA NDANI YAKO ILI IWE MSAADA NA FAIDA YA WENGINE.
🟣Ivi unatambua kuwa kilichoko Ndani yako si kwaajili yako pekee Bali ya watu wengine?.
➖K**a Ndani yako umewekwa uwezo wa kufundisha unahitaji watu Ili utumie uwezo huo kufundisha,na unapo fundisha wale unaowafundisha wananufaika na mafundisho yako.
➖Umewekewa uwezo wa kuimba?,Bado kupitia kuimba unaweza gusa maisha wengine kwa kuwatia moyo,kuonya,kuwavuta wamjie Mungu pia kuwajenga.
⭕Jichunguze; Chochote ambacho Mungu ameweka Ndani yako anataka kimletee yeye Utukufu kwa wewe unapo kitoa kuwahudumia wengine.

Warumi 12
5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;
7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;
8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.

JIULIZE...
🟥Umekuwa unatumia kile ambacho Mungu ameweka Ndani yako kwaajili ya kuwahudumia wengine?,Ili Mungu aendelee kupata Utukufu kupitia kile ameweka Ndani yako!!!!!.
➖Kumbuka usipo tumia kile kilichopo Ndani yako kuwahudumia wengine unasababisha jambo flani ambalo haliko sawa.
➖Tambua thamani ya mda katika kuachilia kile kilichoko Ndani yako,Usifikiri unao mda zaidi k**a unaupoteza mda ulio nao Sasa.
🟥Jikumbushe kuwa Kuna siku utatoa hesabu kwake yeye aliyeweka Ndani yako Ili utumie kuwagusa wengine.

Mathayo 25
15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
19 Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.

FAIDA ZA KUTUMIA KILICHOKO NDANI YAKO.
🟣Kupata furaha ya kweli na bubujiko la amani ikitokea Ndani na kuleta ustawi wa maisha ya kiroho na kimwili.

3 Yohana 1
2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, k**a vile roho yako ifanikiwavyo.
➖Wakati mwingine madhara ya kiafya yanaweza mpata mtu pale anapo acha kutumia kile ambacho Mungu ameweka Ndani yake.
🟣Inaleta furaha na Ustawi kwa wale ambao utawahudumia kupitia kilicho Ndani yako.
🟥MUNGU HUTUKUZWA SANA PALE AMBAPO WEWE UNATUMIA KILE AMEWEKA NDANI YAKO, NA KUTUMIA KILE MUNGU AMEWEKA NDANI KWA UONGOZI WAKE HUO NI UTII.

USHAURI.
Jijengee tabia ya kujitathimini mara kwa mara kuwa kile ambacho Mungu ameweka Ndani yako kwaajili ya kuwahudumia wengine umekuwa unakitumia sawa na Kusudi lake yeye aliye kuumba.

Neema ya Mungu iwe juu yako.

07/07/2022

Zaburi 29
11 Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani.

01/07/2022

Karibu na Wewe.

Waebrania 412 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena l...
30/06/2022

Waebrania 4
12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

➖Ni mhimu sana Kusoma Neno la Mungu na kulitafakari Kila Siku.
➖Unapokuwa na Neno la Mungu Ndani yako unakuwa na nguvu Ndani yako,Uzima wa Kimungu pia.

⭕Siku zote shetani atapambana na wewe usiwe na mda wa kulisoma Neno la Mungu na kutafakari maana anajua maisha ya mtu yanafanikiwa na kuchanua akiwa katika Neno la Mungu.
➖Adui atahakikisha mda wa kufanya mambo mengine unao,lakini mda wa kutulia katika Neno la Mungu unakuwa huna na Hata ukipata unautumia Kusoma juu juu.

🟥 KUMBUKA WEWE NI MSHINDI KATIKA KRISTO YESU
➖Hakikisha unashinda upinzani wa shetani unao kuzuia usiwe na mda wa kutosha Kusoma Neno.

2 Wakorintho 2
11 Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.

⭕Neema ya Mungu izidi sana juu yako katika kujaza Neno la Mungu moyoni mwako.
⭕Baraka zilizo katika Neno la Mungu zimiminike katika maisha yako kadri Unavyo zidi Kusoma Neno.

NAKUTAMIA WAKATI MWEMA.

Address

Mafinga
00255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when World Mission & Evangelistic Association posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share