29/12/2024
BIBLIA .....VS.....KATEKISIMU
Ifuatayo ni orodha ya amri kumi katika Biblia na Katekisimu (Katekisimu ya Wakristo Wazima, toleo la tatu, 1983, Peramiho Songea, 105. Amri za Mungu.)
BIBLIA, Kutoka 20:3-17. KATEKISIMU
1
Usiwe na miungu mingine ila mimi. 1
Usiabudu miungu mingine.
2
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. 2
Usilitaje bure jina la Mungu wako.
3
Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajae jina lake bure. 3
Shika kitakatifu siku ya mungu wako.
4
Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sitaBWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa. 4
Waheshimu baba yako na mama upate miaka mingi na heri duniani;
5
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako. 5
Usiue;
6
Usiue. 6
Usizini;
7
Usizini. 7
Usiibe;
8
Usiibe. 8
Usiseme uwongo wala usitoe ushahidi wa uongo;
9
Usimshuhudie jirani yako uongo. 9
Usitamani mke asiye mke wako;
10
Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako. 10
Usitamani mali ya mtu mwingine.
KANISA KATOLIKI LA ROMA LINAELEZA:-
• “Kanisa Katoliki ndio muasisi wa Jumapili, na madai yake ya kuitunza yanaweza kulindwa tu na mapokeo...kuanzia mwanzo hadi mwisho wa maandiko hakuna hata aya moja inayoruhusu uhamishaji wa ibada ya kila juma kutoka siku ya saba ya juma kwenda siku ya kwanza” Catholic Press, Sydney, Australia, August, 1900.
• “Ni kanisa katoliki lililobadilisha siku ya kupumzika kutoka Jumamosi hadi Jumapili siku ya kwanza ya Juma… Je, dunia yote inatii mamlaka ya kanisa lipi? Waprotestanti wanadai ya kwamba wanatii Biblia ilhali kwa kuitunza siku ya Jumapili, wanatii sheria ya kanisa Katoliki. Biblia inasema, “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase”, lakini kanisa katoliki linasema, “La, uitunze na kuitakasa siku ya kwanza ya Juma” na dunia yote inatii mamlaka ya kikatoliki!” (Papa Enright tarehe 15-12-1889).
• “Kwahiyo tangu siku hiyo aliyofufuka Bwana, Kanisa linatuita kila siku ya kwanza ya juma, ndiyo dominika, maana yake siku ya Bwana Jumapili.” Mithali ya waumini, uk 1.
• “Kutenda k**a Mungu ni mfano wa kutenda kwa kibinadamu. K**a Mungu alipumzimka siku ya saba, mwanadamu naye anapaswa kupumzika siku ya saba....Injili inataja matukio mengi ambayo Yesu analaumiwa kuvunja sheria ya sabato. Lakini Yesu kamwe hakuvunja utakatifu wa siku hii. Yeye kwa mamlaka anaipa sheria maelezo thabiti. “Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, wala si mwanadamu kwa ajili ya sabato.” Kwa huruma Kristo anahalalisha siku ya sabato kutenda mema kuliko mabaya, kuponya roho kuliko kuiua. Sabato ni siku ya Bwana wa huruma na ya kumheshimu Mungu. “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 2012, uk 483.
• “Sisi sote tunakusanyika siku ya jua, kwa sababu ndiyo siku ya kwanza baada ya Sabato ya Kiyahudi, lakini pia siku ya kwanza ya juma.” Katekisimu ya Kanisa katoliki,2012, uk 484.
• “swali:- Unayonjia nyingine yo yote kuthibitisha ya kuwa kanisa linayo mamlaka ya kuweka siku kuu ziamriwazo?
Jibu:- Lisingekuwa na mamlaka ya namna hiyo, lisingeweza kufanya kile ambacho wafuasi wa dini siku hizi hukubaliana nalo, lisingeweza kubadilisha kuadhimishwa Jumapili iliyo siku ya kwanza ya juma badala ya kuadhimishwa Jumamosi iliyo siku ya saba, badiliko lisilo na idhini yo yote ya maandiko Matakatifu.” Stephen Keenan, Doctrinal Catechism, pg 176.
• “Tunatunza Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu Kanisa Katoliki lilibadilisha taadhima kutoka Jumamosi kwenda Jumapili.” Peter Geiermann, CSSR, A Doctrinal Catechism, 1957 edition, pg 50.
• “Waprotestanti...wanaikubali Jumapili kunyume cha Jumamosi k**a siku ya ibada kwa kuiga Kanisa Katoliki lililo fanya badiliko hilo...kwa kuitunza Jumapili, wanakubaliana na mamlaka ya msemaji mkuu wa kanisa Papa.” Our Sunday Visitor, February 5, 1950.
• “K**a Waprotestanti wangefuata Biblia, wangeabudu siku ya sabato. Kwa kuitunza Jumapili wanafuata sheria ya kanisa Katoliki.” Albert Smith, Chancellor of the Archdiocese of Baltimore, replying for the Cardinal, in a letter dated February 10, 1920.
MADHEHEBU YA JUMAPILI, WAPROTESTANTI WANAKIRI:-
BAPTIST: “Ilikuwepo na ipo amri ya kutunza kitakatifu siku ya sabato, lakini siku ya sabato haikuwa ni Jumapili...Hakuna ushahidi wa maandiko wa badiliko la sabato kutoka siku ya saba ya juma kwenda siku ya kwanza ya juma.” Dr.E.T.Hiscox, author of the Baptist Manual.
CONGREGATIONALIST: “Ni wazi kabisa kwamba, ingawaje kwa uthabiti na kwa kujitoa tunaitumia Jumapili, hatuitunzi sabato...sabato ilitolewa kwa amri ya kimbingu. Hatuwezi kudai amri hiyo ya kimbingu kwa utunzaji wa Jumapili...Hakuna hata mstari mmoja katika agano jipya unaopendekeza kwamba tunapata adhabu yoyote kwa kukiuka kile kinachoitwa utakatifu wa Jumapili.” Dr.R.W.Dale, The ten Commandments, pg 106-7.
AFRICA INLAND CHURCH: “Siku ya sabato au Jumamosi baada ya kufa kwake, Yesu Kristo alikuwa kaburini. Siku ya kwanza ya juma yaani Jumapili alifufuka kutoka kwa wafu. Kwa kuwa Sabato ilikuwa Jumamosi kwa kalenda ya Kiyahudi, siku ya pili yake iliyotengwa na Mungu kuwa siku ya Pentekoste, ilikuwa siku ya Jumapili. Wayahudi walijua hivyo na Wakristo walijua hivyo.” Askofu Kitula wa AIC, Jumapili au Jumamosi? uk 45.
PROTESTANT EPISCOPAL: “Siku sasa imebadilishwa kutoka siku ya saba kwenda siku ya kwanza...lakini kwa kuwa hatuna maelekezo yoyote ya maandiko kwa badiliko hili, tunaweza kuhitimisha kuwa lilifanyika kwa mamlaka ya kanisa.” The Protestanti Episcopal Explanation of the Catechism.
PRESBYTERIAN: “Hakuna neno wala dokezo katika Agano Jipya kuhusu kutofanya kazi siku ya Jumapili.” Canon Eyton, Ten Commandments.
ANGLICAN: “Ni wapi katika maandiko tunaambiwa kwamba inatupasa kutunza siku ya kwanza (ya juma)? Tunaamriwa kutunza siku ya saba; lakini hakuna mahali tunapoamriwa kutunza siku ya kwanza.” Isaac Williams, Plain sermons on the Catechism, pg 334, 336.
METHODIST: “Ni kweli kwamba hakuna amri yoyote inayoruhusu ubatizo wa watoto. Kadhalika na utunzaji kitakatifu siku ya kwanza ya juma. Wengi wanaamini kuwa Kristo alibadilisha sabato. Lakini kutoka katika maneno yake mwenyewe tunaona kuwa hakuja kwa shughuli hiyo. Wale wanaoamini kwamba Yesu aliibadili sabato hoja zao zimejengwa katika mtazamo tu.” Amos Binney, Theological Compendium, pg 180-181.
CHRISTIAN CHURCH: “Hakuna ushuhuda wowote kwa wakuu wote wa mbinguni kwamba sabato ilibadilishwa, wala kwamba siku ya bwana (jumapili) ilichukua nafasi yake.” Alexander Campbell, Reporter, October 8, 1921.
DESCIPLES OF CHRIST: “Hakuna mamlaka yoyote ya wazi katika maandiko ya utawazwaji wa siku ya kwanza kuwa ‘siku ya Bwana’.” Dr.H.Lukas. Christian Oracle, Januari 23, 1890.
MASHAHIDI WA YEHOVA: “Ijapokuwa Kristo alifufuka siku ya kwanza ya juma (ambayo sasa huitwa jumapili), Biblia haina agizo la kutenga siku hiyo ya juma kuwa takatifu. “Kutunzwa kwa jina lake la kipagani ‘Dies Solis,’ au ‘Siku ya jua’ kwaajili ya siku kuu ya Kikristo ya kila juma, kwa kadiri kubwa ni kwa sababu ya muungano wa upagani na [lile linaloitwa] wazo la Kikristo ambalo kwake siku ya kwanza ya jua ilipendekezwa na Kostantino [kwa amri mwaka 321 W.K] kwa raia zake, Wapagani na Wakristo pia, kwa kuwa ndiyo siku ya kuheshimiwa ya jua ....Huo ulikuwa mtindo wake wa kuzipatanisha dini zenye kutofautiana za Milki yake chini ya shirika moja la ujumla” Kutoa sababu kwa kutumia Maandiko, uk 251.
KORAN TUKUFU, INAELEZA:-
• Korani 2:65.
Na kwa yakinia mmekwisha kujua habari za wale walioasi miongoni mwenu, katika amri ya kuiheshimu Jumamosi. Basi tukawaambia: Kuweni manyani wadhalilifu.
• Korani 4:47.
Enyi mlio pewa Kitabu aminini tuliyoteremshia yanayosadikisha yale yaliyo nayo, kabla hatujazigeuza nyuso zenu tukazipeleka kisogoni, au kabla ya kuwalaani k**a tulivyo walaani wale walioharibu utukufu wa Jumaamosi. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima kufanywa.
154. Ufafanuzi kipengele C. Na baada ya kutua katika hiyo miji na vijiji, vya shamu, waliambiwa waiadhimishe siku ya Jumamosi. Kwa kuifanya kuwa siku ya ibada tu, si siku ya kufanya kazi, wakatiatia hila zao, mpaka ikawa siku ya kazi.
• Korani 7: 163.
Na waulize khabari za mji ulio kuwa kando ya bahari, wakiivunja Sabato
(Jumaamosi ya mapumziko). Samaki walikuwa wakiwajia juu juu siku ya mapumziko
yao, na siku zisio kuwa za kupumzika hawakuwa wakiwajia. Kwa namna hiyo
tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu.
• Korani 16:124.
Hakika siku ya Sabato (Jumaamosi) waliwekewa wale walio khitalifiana kwa
ajili yake. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka atahukumu baina yao Siku ya
Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitalifiana.
Swali ni je, lipi ni dhehebu la kweli la Ukristo?
Jibu ni Waadventista Wasabato. Kwa kigezo kipi?
Kwa kigezo cha kudumisha mafundisho ya Biblia.
Ili kuthibitisha ukweli huu chukua hatua Kusoma
Biblia na kuchunguza mafundisho yote ya
madhehebu ya Kikristo na kuyalinganisha na
Biblia. Mungu hatatuhukumu kwa kutojua
ukweli bali kwa kupuuzia fursa ya kujifunza
ukweli.
Kwa masomo mengine mengi karibu
YOUTUBE
https://youtu.be/r9fdLCLG9J8
AU website
Kujifunzabiblia.com
AU facebook
https://www.facebook.com/MUNGUazungumzanawatuwake
Be blessed 💖🥰🥰