ELCT-North Eastern Diocese

ELCT-North Eastern Diocese ELCT-NED LUSHOTO TANGA TANZANIA
[email protected]

Dodoma, 31 Agosti 2026 — Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs)...
31/08/2026

Dodoma, 31 Agosti 2026 — Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) Tanga, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 31 Agosti 2026 yupo Bungeni Dodoma katika ziara maalum yenye lengo la kushirikisha na kuwaalika viongozi pamoja na wadau mbalimbali kushiriki katika Harambee ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, inayolenga kuchangia na kuboresha Vituo vya Huduma na Diakonia katika Dayosisi.

Katika ziara hiyo, Askofu Dkt. Mbilu amekutana na Wabunge wote wa Mkoa wa Tanga, ambao wamepokea kwa uzito mkubwa wito na mpango huo wa Dayosisi.

Wabunge hao wameonesha utayari wa kutoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha Harambee hiyo, wakitambua umuhimu wa kuboresha huduma za kijamii na kiroho zinazotolewa kupitia Vituo vya Huduma na Diakonia.

Aidha, katika ziara hiyo , Askofu Dkt. Mbilu amepata fursa ya kukutana na viongozi mbalimbali, akiwemo , Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa M***a Zungu, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mheshimiwa Mary Chatanda, Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Awesso, pamoja na Waziri wa ElimuMheshimiwa Prof. Adolf Mkenda.

Harambee hiyo ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki inatarajiwa kufanyika tarehe 20 Septemba 2026, Jijini Tanga, ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki unawakaribisha waumini, Wanadayosisi, taasisi, viongozi, wafanyabiashara, wadau wa maendeleo na watu wote kuungana pamoja katika kufanikisha Harambee hii muhimu.

Ushiriki wa kila mmoja, kwa namna yoyote ile, utakuwa sehemu ya kujenga na kuimarisha Vituo vya Huduma na Diakoni ili viweze kutoa huduma bora, zenye tija na zinazogusa mahitaji ya jamii.

Tufuatilie/Wasiliana nasi.
INSTAGRAM - / elctned
FACEBOOK ACCOUNT North Eastern Diocese
FACEBOOK PAGE - ELCT-North Eastern Diocese
YOUTUBE - / KKKT DKMS Online TV

WEBSITE: www.elctned.org

Email: [email protected]
SIMU: 0743 399 798
BANK NMB
Jina: ELCT NED HARAMBEE KUU ACCOUNT
Acc.No. 41610058009,
Branch: Lushoto
BANK: CRDB

Jina: ELCT NED HARAMBEE KUU ACCOUNT
Acc No: 10457136884
Branch: Lushoto

WAKRISTO WAHIMIZWA KUTUBU NA KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU; KKKT-DKMs YAADHIMISHA MIAKA 30 YA USHIRIKIANO NA UEMHandeni, Ta...
02/08/2026

WAKRISTO WAHIMIZWA KUTUBU NA KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU; KKKT-DKMs YAADHIMISHA MIAKA 30 YA USHIRIKIANO NA UEM

Handeni, Tanga | 2 Agosti 2026

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewahimiza Wakristo kumrudia Mungu kwa toba ya kweli na kuacha dhambi, akisisitiza kuwa baraka za Mungu hupatikana kwa wale wanaoishi maisha ya utakatifu na kumtii Kristo.

Akihubiri katika Ibada ya Jumapili, Siku ya Bwana ya Tisa Baada ya Utatu, iliyofanyika Usharika wa Handeni, Jimbo la Magharibi, tarehe 2 Agosti 2026, Askofu Dkt. Mbilu alisema kuwa wokovu ni wa leo, hivyo kila Mkristo anapaswa kutumia fursa ya neema kwa kumgeukia Mungu.
Alisema kuwa wapo watu wanaotarajia kupokea baraka za Mungu huku wakiendelea kuishi katika dhambi, jambo ambalo haliendani na mafundisho ya Neno la Mungu.

"Baraka za Mungu zinapatikana pale mtu anapoamua kuacha dhambi na kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya," alisema Askofu Dkt. Mbilu.

Katika ibada hiyo, KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki pia iliadhimisha Miaka 30 ya Ushirikiano kati ya United Evangelical Mission (UEM) na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, ambapo Askofu Dkt. Mbilu aliishukuru UEM kwa mchango wake katika kuimarisha kazi za maendeleo ya Kanisa kwa kipindi chote cha ushirikiano huo huku akiwahimiza Wachungaji, viongozi na waumini wote kuendelea kuuombea ushirikiano huo.

Katika hatua nyingine ya ibada Askofu Dkt. Mbilu alitoa Tuzo ya Shukrani kwa Washarika wa Usharika wa Handeni baada ya kufanikisha kulipa kwa ukamilifu kiwango walichopangiwa cha mchango wa deni la Dayosisi, kiasi cha Shilingi milioni 97,600,000.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkuu wa Jimbo la Magharibi, Mch. Ishamael Ngoda, alisema mafanikio hayo ni ushuhuda wa neema ya Mungu na ushirikiano mkubwa wa waumini wa Usharika wa Handeni.

Alieleza kuwa safari ya kulipa deni hilo haikuwa rahisi, lakini ilifanikiwa kutokana na mshik**ano wa washirika, viongozi wa Kanisa na maelekezo ya uongozi wa Dayosisi.
"Tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii. Baba Askofu Dkt. Mbilu ameendelea kututia moyo kupitia miongozo na maelekezo yake katika vikao mbalimbali. Hakika, kiongozi hupimwa zaidi wakati wa changamoto, na Mungu ametuwezesha kushinda," alisema Mch. Ngoda.

Mch. Ngoda alibainisha kuwa baada ya kukamilisha jukumu la ulipaji wa deni la Dayosisi, Usharika wa Handeni sasa utaelekeza nguvu zake katika kuimarisha huduma za kiroho, shughuli za maendeleo na utekelezaji wa utume ambao Kanisa limeitiwa.
Pia aliwashukuru Washarika, Wazee wa Kanisa, viongozi wa jumuiya, wanajumuiya . wadau na waumini wote waliochangia kwa hali na mali hadi kufanikisha kukamilika kwa jukumu hilo.

Ibada hiyo ilihitimishwa kwa waumini wote wa Usharika wa Handeni kushiriki chakula cha pamoja k**a ishara ya shukrani kwa Mungu na kuadhimisha mafanikio ya kukamilika kwa ulipaji wa deni la Dayosisi katika ngazi ya Usharika, sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano kati ya UEM na KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki

21/07/2026
KATIKA PICHA: Ni Ibada iliyofanyika leo, tarehe 18 Julai 2026, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kask...
18/07/2026

KATIKA PICHA: Ni Ibada iliyofanyika leo, tarehe 18 Julai 2026, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs), Jimbo la Kusini, Usharika wa Ubiri, ambapo ilifanyika Ibada Maalum ya kustaafu rasmi kwa heshima Mwinjilisti Debora Eliamini Charamila baada ya miaka 10 ya utumishi katika Kanisa la Mungu.

Ibada hiyo iliongozwa na Dean Frank Richard Mntangi, akishirikiana na wachungaji pamoja na watumishi wengine wa kanisa. Ilikuwa ibada nzuri ya kumshukuru Mungu kwa maisha na huduma ya Mwinjilisti Debora, huku dayosisi ikitambua mchango wake mkubwa katika kuhubiri Injili, kulea waamini na kulitumikia kanisa kwa uaminifu na kujituma.

Katika ibada hiyo, Dean Mntangi alimtangaza rasmi Mwinjilisti Debora kuwa Mwinjilisti Mstaafu wa KKKT-DKMs, huku waumini wakimpongeza na kumshukuru kwa huduma yake ya uaminifu.

Pamoja na kustaafu kwake rasmi, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kupitia kwa Dean Frank Mntangi imeeleza kuwa itaendelea kutumia uzoefu na karama za Mwinjilisti Debora katika huduma mbalimbali za kanisa kadiri itakavyohitajika.

Tunamuombea Mwinjilisti Debora afya njema, nguvu na baraka za Mungu katika maisha yake mapya ya ustaafu.
“Na Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtapokea
taji ya utukufu, ile isiyokauka”, 1 Pet. 5:4

KATIKA PICHA: Ibada ya Jumapili – Siku ya Bwana ya 6 baada ya Utatu iliyofanyika KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,...
12/07/2026

KATIKA PICHA: Ibada ya Jumapili – Siku ya Bwana ya 6 baada ya Utatu iliyofanyika KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Jimbo la Pwani, Usharika wa Kana – Tanga na kuambatana na tendo la kubarikiwa kwa waliokuwa watheolojia kuwa wachungaji.
Waliokuwa Watheolojia waliobarikiwa kuwa wachungaji ni:

Ester Godwin Kivuma
Janeth Yakobo Doop
Mambazi Shemantu Mgonda
Yona Simon Mgonja
Ibada hiyo iliongozwa na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, akishirikiana na watumishi wengine wa Kanisa.

Tarehe: 12/07/2026
LINK YA PICHA ZA IBADA YA JUMAPILI YA TAREHE 12/07/2026 USHARIKA WA KANA.

https://photos.app.goo.gl/Lagmmr6kHPoqePvr5

Tufuatilie kupitia:

📘 Facebook Account: North Eastern Diocese
📘 page: ELCT – North Eastern Diocese
▶️ YouTube: KKKT DKMS Online TV
🌐 Website: www.elctned.org

03/07/2026

ASKOFU DKT. MSAFIRI JOSEPH MBILU AKIIMBISHA DARASA LA WANAFUNZI WA MUZIKI WA TARUMBETA WALIOHITIMU MAFUNZO YAO KKKT-DKMS USHARIKA WA HENGITI, LEO TAREHE 03/07/2026.

KKKT Marathon 2026-Kimbia kwa moyo, saidia kwa upendo
20/06/2026

KKKT Marathon 2026-Kimbia kwa moyo, saidia kwa upendo

KATIKA PICHA: Waumini wakishiriki Ibada ya Jumapili, Siku ya Bwana ya 2 Baada ya Utatu, iliyofanyika, KKKT Dayosisi ya K...
14/06/2026

KATIKA PICHA: Waumini wakishiriki Ibada ya Jumapili, Siku ya Bwana ya 2 Baada ya Utatu, iliyofanyika, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto, tarehe 14 Juni 2026.
Ibada hiyo iliyoongozwa na Dean Frank Mntangi akishirikiana na Chaplain wa Kanisa Kuu Lushoto Mch. Neema Kamendu, iliambatana na harambee ya kuchangia deni la Dayosisi ambapo jumla ya Tsh 9,025,000 ilipatikana. Kati ya fedha hizo, Tsh 8,580,000 zilichangwa taslimu na ahadi ni Tsh 445,000 .
Mgeni rasmi katika harambee hiyo alikuwa CPA. Peter John Singano, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, ambaye alichangia Tsh 5,000,000 kwa ajili ya deni la Dayosisi. Ibada na harambee hiyo zilidhihirisha ushirikiano na moyo wa kujitolea wa waumini katika kuendeleza kazi ya Mungu.
Tufuatilie kwenye mitandao yetu ya kijamii
INSTAGRAM - / elctned
FACEBOOK ACCOUNT North Eastern Diocese
FACEBOOK PAGE - ELCT-North Eastern Diocese
YOUTUBE - / KKKT DKMS Online TV
WEBSITE: www.elctned.org

Address

Lushoto
255

Opening Hours

Monday 08:00 - 22:00
Tuesday 08:00 - 22:00
Wednesday 08:00 - 22:00
Thursday 08:00 - 22:00
Friday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ELCT-North Eastern Diocese posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share