Ebenezer Gosper Ministries

Ebenezer Gosper Ministries Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Ebenezer Gosper Ministries, Religious organisation, Lushoto.

02/04/2026
Wagalatia 3:29 Na k**a ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
14/08/2025

Wagalatia 3:29 Na k**a ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Shallom Shallom Mwana Ngomeni JUMANNE YAKO IMEBARIKIWA SOMO: CHOCHOTE KISICHOKUBALIANA NA MAPENZI YA MUNGU JUU YAKO  HAK...
12/08/2025

Shallom Shallom Mwana Ngomeni

JUMANNE YAKO IMEBARIKIWA

SOMO: CHOCHOTE KISICHOKUBALIANA NA MAPENZI YA MUNGU JUU YAKO HAKITOSIMAMA.

Neno: Isaya 7:7 Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa.

Ukiisoma vyema hii sura utagundua mfalme Ahazi mwana wa Yothani na mwana wa Uzia alipokuwa mfalme wa YUDA kuna wafalme wawili waliopanga njama kinyume na Yuda nao ni Resini wa Shamu na Peka wa Remalia. Walipanga njama za kuiangamiza Yuda na watu wake. Ahazi mfalme wa Yuda akawa katika kuugua aliposikia habari hii. Moyo wake ulimuuma saana. Alikuwa ni mwenye maumivu na kuvunjika moyo ndipo Mungu akamtuma Isaya kwake na Isaya hakuwahi kupepesa macho kwa ujasiri akamwambia Mfalme Ahazi kuwa Jambo hili halitasimama wala halitakuwa. Unaposikia jambo kusimama maana yake ni *kuonekana* na kuwa maana yake ni *kuthibitika*

Mtu wa Mungu wakati natafakari Mungu juu yako Mwana Ngomeni nikasikia hili neno ndani yangu kuwa niseme nawe. Sijui unapitia nini au umesikia nn kinachouumiza moyo wako ila nsikia kukwambia hili neno unalolisikia k**a utisho kwako halitakuwa na halitasimama. Halitaonekana wala halitathibitika.

Na kwao wanaokupangia mashauri ya kigeni yenye asili ya Rasini na Peka kwamba upigwe katika biashara zako, Maisha yako, kazi zako, mifugo yako, Uzao wako, Afya yako nk nk nk hawataweza na kwamba jambo hili halitathibitika wala kuonekanani dauti za mfano wa simba aungurumaye.
Isaya 8:10
“Pangeni shauri, nanyi mtaangamizwa; semeni neno, neno hilo halitasimama, maana Mungu yu pamoja nasi.”

K**a ilivyokuwa kwa Ayubu 5:12
“Yeye huvunja shauri la hila, mikono yao isitimize makusudi yao.” Atavunja shauri lolote ambalo limefanya na kusimama kinyume nawe. Na kila mkono wenye kusudi ovu hautafanikiwa

Mithali 19:21
“Mawazo mengi yako mioyoni mwa wanadamu; lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.

Waweza omba hivi
Baba yetu uliyembinguni. Tunalitukuza na kuliinua jina lako takatifu. Ahsante kwa sababu ya asubuhi hii njema. Ahsante kwa sababu ya hakikisho la ushindi na ubatilisho wa mashauri yanayopangwa kinume nami na uzao wangu. Nakuomba neno hili likathibitike kwangu kuwa hakuna mipango ya kunisambaratisha itakayosimama au kuwa

Shallom

Kutoka 11:1 BWANA akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi...
02/08/2025

Kutoka 11:1 BWANA akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa.

Shallom Shallom Mwana Ngomeni JUMAMOSI YAKO IMEBARIKIWALeo ni jumamosi na kwa kawaida jumamosi na jumapili  tunajifunza ...
19/07/2025

Shallom Shallom Mwana Ngomeni

JUMAMOSI YAKO IMEBARIKIWA

Leo ni jumamosi na kwa kawaida jumamosi na jumapili tunajifunza kupitia shuhuda mbali mbali za watu wa Mungu ili kutujenga zaidi kiimani.

Mwaka 1985 mtumishi wa Mungu Dr Umar Ukpai na wenzie kadhaa walikuwa safarini China. Huko wakafika mpaka unaitwa Kuntung. Hapo kabla ya kuvuka msimamizi mmoja akawaambia tusingependa kuwajaribu na kuwafanya mkatenda dhambi.

Ikiwa mnajua kwenye mabegi yenu mmebeba Biblia zitoeni na mtafungwa kwa miaka 20. Mtumishi wa Mungu akashangaa na kumuuliza Mungu nifanye nini maana ukweli ni kwamba walikuwa wamebeba Biblia zao wote kabisa katika msafara ule.

Basi Mungu akasema na Dr Umar Ukpai waweza kuanza kunena kwa lugha na alipoanza kunena kwa lugha na wenzie wawili ambao walikuwa ni wamarekani wakajikuta wananena kwa Lugha pia. Na walipokuwa katika kunena kwa lugha ndipo mashine tano za upekuzi nazo zikazimama ghafula na wakaguzi wote wakashikwa na mshangao.

Akaja kiongozi wa wapekuzi na alipofika akawauliza nyie waganga na wachawi kutoka Afrika tunaowasikia? Wakamjibu ili amani iwepo turuhusu tupite. Wakaruhusiwa kupita na baada ya wao kuvuka kentung mashine zikawaka na kuendelea na kazi.

2 Wathesalonike 3:16
Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.

Mungu akakujaalie kunena kwa lugha mpya ambako kuna majibu mengi zaidi kuliko vile tuezavyo. Kwa jinsi au namna yeyote Mungu akakupee amani ya Moyo.

Ikiwa kuna mashine inatakiwa kuzimwa ili wewe upite kwa amani basi ikawe hivyo kwako, Ikiwa kuna mtu anatakiwa kuondolewa katika nafasi yake ili wewe upite kwa amani na ikawe hivyo. Mungu asikupungukie, K**a kuna jambo linatakiwa kufanyika ili wewe uwe na amani basi na ikawe hivyo katika jina YESU KRISTO.

Omba hivi. Eee baba wa mbinguni nakushukuru kwa sababu ya asubuhi ya Leo. Nakuomba unijaalie nguvu kuweza kusonga mbele. Ikiwa kuna vikwazo huko mbele k**a ilivyokuwa kwa mtumishi wako Dr Umar Ukpai waweza nifanyia na mimi pia. Ili avuke mashine ziliacha kufanya kazi na mimi ili nifike ngambo ya hapa fanya lolote/vyovyote ili niwe na amani maana katika wewe kuna Amani yangu.

Mkwamila C C
Mtu wa Mungu
2025

Let's pray together everyday  from 21:30 hrs on my Ebenezer zoom Channel
10/07/2025

Let's pray together everyday from 21:30 hrs on my Ebenezer zoom Channel

My own prayer full girl. We pray and praise pamoja
20/09/2024

My own prayer full girl. We pray and praise pamoja

ELIMU BURE KUTOKA MKWAMILA COUNSELING CLINICMBOLEA , MAJI NA HEWA YA MAHUSIANOMawasiliano ndani ya mahusiano ni mbolea k...
23/08/2023

ELIMU BURE KUTOKA MKWAMILA COUNSELING CLINIC
MBOLEA , MAJI NA HEWA YA MAHUSIANO
Mawasiliano ndani ya mahusiano ni mbolea kuu ya mmea Upendo. Ili mmea ukomae unahitaji maji, hewani, na Udongo wenye rotuba au mbolea safi na mzuri.
Maji ndani ya mahusiano ni lugha mzuri ya ulimi. Jitahidi kuwa na nyama ya ulimi. Nyama ya ulimi ni lugha mzuri na ya kubembeleza. Usiwe just mpokeaji bali pia uwe mtoaji kwa maana ya usiwe ni mtu unayetaka kubembelezwa zaidi bali pia kuwa mbembelezaji wa mwenzi wako.
Achana na mambo ya mila na Desturi kuna maisha mapya ndani ya mahusiano ambayo yanatafunwa saana na mabadiliko ya mila , Desturi na tamaduni zetu. Usipombembeleza mpenzi wako na kumpatia nyama tamu ya ulimi huwezi kufurahia utamu na tamu aliyonayo maana atakupa kwa wajibu wala si wito. Ila pia wewe ukishindwa atapatikana wa kumbembeleza na kumpatia nyama tamu ya ulimi. Jiandae kwa maumivu k**a mpenzi wako atampata mwenye nyama ya ulimi.
Hewa ndani ya mahusiano ni ujinga na utaahira wa mwenzio. Usijifanye wewe ndiwe unajua Kila kitu. Kwamba Kila anachosema mwenzio anakosea. Mwache mwenzio aongee na kujiachia mbele zako. Mwache aongee kile moyo wake unataka aongee.
Mwache akuambie vile anajisikia na thamini mawazo yake. Ndani ya ujinga na utaahira wa mwenzio ndimo mwenye hewa ya mahusiano. Ukimnyima kuongea mwenzio hapo utakuwa umemnyima hewa na kwa sababu hiyo ndani ya moyo wake utapotea au kufa kabisa na kwa sababu hiyo akipatikana wa kumpatia hewa itakuwa imekula kwako. .
Jitahidi saana kumwachia mpenzi wako muda na nafasi ya kuongea na ikibidi fanya au kukiishi kule anachoongea na kukisema na kwa kufanya hivyo utakuwa umejihakikishia mahusiano yenye afya njema.
Jambo la mwisho katika mahusiano ni Udogo wenye rotuba au mbolea ya thamani. Mbolea au rotuba ya mahusiano ni mawasiliano. Ni muhimu ukampatia mpenzi wako nafasi mkubwa kwenye mawasilino yako. Awe wa kwanza kupokea cm na sms zako pia wa mwisho kabla hujalala. Mawasiliano yanamfanya mpenzi wako ajione ni wa thamani na muhimu zaidi kwako. Yanamfanfanya ajione hakuna k**a yeye kwako. Yanamfanya anajiona anaimiliki dunia yako.

Mkwamila C C .
Rafikiyo Wa Zamu
2023

       nawasalimu kwa jina la Wananchi wa Jangwani
22/07/2023

nawasalimu kwa jina la Wananchi wa Jangwani

Usikubali kuwa shahidi na muhili ya kushindwa kwa watu. Ukianza kufanya jambo wakikwambia hiwezi ni gumu waambie kwao ni...
08/07/2023

Usikubali kuwa shahidi na muhili ya kushindwa kwa watu. Ukianza kufanya jambo wakikwambia hiwezi ni gumu waambie kwao ni guru ila kwa Mungu anayeishi ndani yako ni jepesi na inawezekana. Ushindi is just maamuzi sio vile watu wanavyotaka iwe

Mkwamila C C
Rafikiyo Wa Zamu
2023

Address

Lushoto

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ebenezer Gosper Ministries posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share