21/11/2024
SOMO; KUTOKA KWENYE VIFUNGO VYA FAMILIA.
Mwanzo 12:13
"Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako."
Familia unayotoka wewe na ukoo unaotoka unahusiana na maisha yako, ndiyo maana Biblia inasema adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake, na unapoyaangalia maisha yako ya kila siku upo k**a ulivyo ni kwa sababu ya familia uliyotokea.
2Timotheo 1:5
"nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo."
Utaona hapa kwamba imani imeanzia kwa bibi ikaja kwa mama na inaenda kwa mtoto, kwa hiyo unaweza kuona kwamba kumbe kwenye familia kuna vitu vinaweza vikasafiri mtu hadi mtu. Ukija kuangalia kwenye familia yenu utaona kwamba kuna mambo yanayosafiri ambayo si mazuri utaona kwamba hamuwezi kukaa mahali pamoja kwenye familia, ama kufanya biashara kati ya ndugu na ndugu, yote ni kwa sababu ya roho iliyo nyuma ya familia kwa maana kila familia ina roho nyuma inayoiongoza.
Si kwamba wanaofanikiwa kwenye familia zao ndiyo wanaakili zaidi hapana, ila kuna roho iko nyuma ya familia ambayo inasababisha wafanikiwe ila kufanikiwa ama kutokufanikiwa kuna roho inayosimama badala yao. K**a hutaweza kufungua vifungo vinavyoikabili familia yenu tambua kwamba hutaweza kufanikiwa kwenye familia yenu.
Unaweza kuona kwenye familia mama aliolewa mke wa pili na mtoto anakuja kuolewa mke wa pili lakini kumbe sababu kubwa ni kwamba nyuma yake kuna roho inasababasha wawe hivyo walivyo.
MAMBO 4 AMBAYO NI MISINGI YA VIFUNGO VYA FAMILIA
1.Uchawi wa kifamilia
Familia nyingi leo zinateseka kwa sababu mwanzo wa familia hizo zilianza kichawi au kishirikina au kuna mkoba wa familia. Vitu k**a hivi vinasababisha familia ikae kwenye Kongwa la uchawi. Unaweza ukaona ndani ya familia kuna mtu mmoja amenunua uchawi, au amerithi kutokea mahali fulani. Vitu k**a hivi vinasababisha familia ikae kwenye vifungo vizito. Unaposema kuna mchawi kwenye familia yetu tambua kwamba kwenye hiyo familia kuna madhabahu ya kishetani na kuna njia ya kwenda kwa shetani. Ndani ya familia kukiwa na mtu ambaye ameokoka au ni mchungaji basi ujue madhabahu ya Mungu iko ndani ya familia na hakuna uchawi utakayoiweza.
2Wafalme 17:17
"Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha."
Hakuna kitu kibaya k**a Mungu akasirike kwa ajili ya familia yenu, tunamwona Samweli anamwomba Mungu kwa ajili ya Sauli ila Mungu anamwambia Samweli, Sauli simtaki nilishamkataa. Mungu akiona mchawi kwenye familia yenu anachukizwa na familia hiyo na utaanza kuona mabaya yanaanza kuwapata, utaona huyu aliye mchawi wa familia utaona kwamba akienda mahali kwenye kikao anang'ang'ania awe kiongozi ili aifunge familia na moja kwa moja anaitoa familia kwenye mikono ya Mungu, jambo la Muhimu ni kuung'oa uchawi na ushirikina kwa jina la Yesu. Ili ufanikiwe ni mahusiano yako mazuri na Mungu. Unakuta mabaya yanawapata ni kwa sababu ya kujichanganya na mambo ya kishetani, ni lazima utambue kwamba Mungu hajichanganyi na wabaya.
Kumbukumbu la Torati 18:10-12
10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
Unaanza kujiuliza, Kwanini Mungu hatendi nikimwomba?, ni kwa sababu ndani ya familia kuna waabudu sanamu, kuna wachawi na washirikina kuna waenda kwa waganga, lakini leo amua kuwaondoa wote waendao kwa waganga, na wachawi, sema leo asionekane mchawi ama mshirikina ama muenda kwa mganga ili Mungu akae kwenye familia yenu kwa jina la Yesu.
Usiwe na ndugu muenda kwa mganga kwa sababu utakuwa maskini kila siku. Kila kitu unachokiona duniani leo chanzo chake ni kwenye ulimwengu wa roho, lazima utambue kwamba kila tatizo linalokupata nyuma yake kuna mkono wa mtu unaotenda kazi ili usifanikiwe. Familia inapokaa pamoja ni uzima na baraka lakini shetani hataki mkae pamoja kwa sababu anajua mtafanikiwa.
Kwa kadri wachawi wanapokaa ndani ya familia yenu ndivyo milango ya baraka inafunga, ila kwa kadri unavyowaondoa wachawi kwenye familia yako ndivyo milango ya familia unavyozidi kufunguka kwa sababu Mungu amesema asionekane mchawi kwenu hivyo asipoonekana neema ya kufanikiwa inaonekana. Amua leo kuwaondoa wachawi, washirikina ama waenda kwa waganga kwenye familia yenu kwa jina la Yesu.
Nahumu 3:4
"Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake."
Unapoviona vifo vyenye utata kwenye familia amini kwamba kwenye familia kuna mchawi wa familia. Mwanadamu ni k**a mashine hawezi kufa ghafla lazima kuwe na sababu ama mkono wa Mtu, uwo mkono wa mtu leo ukatwe kwa jina la Yesu. Haya matukio yasiyoeleweka lazima utambue kwamba kuna bibi wa kichawi, mtoto wa kichawi, mwanaume wa kichawi ama mwanamke wa kichawi ambao wanasababisha hayo yatokee. Wewe hujafanikiwa sio kwamba huna nyota ya kufanikiwa hapana ila kuna mchawi anayesababisha usifanikiwe, usimuache mchawi kutaabisha familia yako.
Mambo ya Walawi 20:27
"Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao."
Tumepewa maelekezo kwamba tuwapige kwa mawe, wewe umeacha wafilisti waendelee kukutesa leo achia jiwe limpate mchawi yeyote aliye kwenye familia, kwenye biashara aliye mahali popote pale kwa jina la Yesu. Yupo mchawi anayeng'ang'ana kuiangusha familia, ukiangalia kwenye familia kuna matabaka kwamba kuna wengine wanafanikiwa sana lakini wengine hawafanikiwi.
2.Mizimu/Mungu ya Kifamilia
Lazima uelewe kwamba tangu babu wa babu kuna ibada na pia kuna vitu huwa vinaabudiwa na ibada hizi ni za kishetani moja kwa moja zinamfanya shetani aimiliki familia yenu.
Mwanzo 31:30
"Basi sasa, umetoka kwa sababu umetamani sana nyumba ya baba yako. Mbona basi umeiiba miungu yangu?"
Kwa asili familia inaweza ikawa na Miungu ya kishetani, ama kuna vitu vinatuunganisha na shetani bila kujua. K**a familia yenu ina misingi ya kishetani lazima uwe na matatizo, Unakuta kuna mganga anaitwa ndani ya familia anaitwa ili aizindike familia na huku ndiko kuabudu mashetani na familia inakuwa na vifungo. Ki-mila cha kiafrika kina mahusiano moja kwa moja na mashetani. Misingi yetu ya kiafrika chimbuko lake limetokana na mashetani, Unakuta kwenye familia kinachotupinga sisi ni ile misingi ya kishetani ya familia.
Luka 3:23
"Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake k**a miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,"
Unaweza ukaona familia ya Yesu imeanza vizuri kabisa kwamba ukoo wake kuanzia huko nyuma kuna uhusiano na Mungu moja kwa moja lakini ukija kuangalia kwenye familia yako chimbuko la familia yako utakuta babu wa babu alikuwa anaabudu mizimu. Ukijikuta unapenda mila au ndani yako kuna aina fulani za mila mila utambue kwamba ndani yako kuna chembechembe za ushetani. Kinachofunga sana maisha yetu sisi ni mila za kifamilia, Unakuta kuna mtu mmoja kwenye familia anaenda kwa waganga anasababisha familia ifungwe iwekwe chini ya mamlaka ya giza. Unajikuta kwenye familia hamfanikiwi kwa sababu familia imekabidhiwa kwenye madhabahu za mizimu ya ukoo.
Kuna minyororo ya giza ndani ya familia ambayo inaleta matatizo, inaleta laana, inaleta mikosi kwenye familia kwa sababu ya uchawi uliyoko ndani ya familia na Mungu anaamua kutengana na nyinyi tambua kwamba hamtaweza kufanikiwa kamwe kwa sababu Mungu ameondoka kwenu.
Waamuzi 6:25-26
25 Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;
26 ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.
Mungu anataka kukutumia wewe lakini akiangalia anaona madhabahu nyingine iko ndani yako anaghairi kukutumia. Lakini unapoamua kuondoa madhabahu ya kishetani kwenye familia yako utaona Mungu anaanza kukutumia. Kuna watu wanakaa kwenye familia, kwenye maisha yetu na Tunaona wako vizuri lakini bila kujua huyo/hao ndiyo wanaoharibu familia. Unapoleta ndugu kwa pamoja unatafuta ugomvi na shetani, kwamba shetani hapendi kuona mnapiga hatua kwa sababu anajua mkikaa pamoja lazima maendeleo ya familia yataonekana. Utaona kwenye familia yule anayejitahidi familia ikae kwa pamoja, anayefanya mambo ya kuleta maendeleo kwa pamoja lazima shetani asababishe jambo baya limpate ama afe au augue kwa muda mrefu. Unakuta familia yenu hamuendi vizuri ni kwa sababu hamjamng'oa yule anayeleta kizuizi kwenye familia. Kwenye familia yako k**a hujafanikiwa kushinda vita ya ndani tambua kwamba hata vita ya nje hutaweza. Mafanikio yako, ushindi wako na baraka zako huanzia kwenye familia, k**a hujawashinda wachawi na waganga wa familia tambua kwamba hutaweza kushinda kamwe amua kuwaondoa wachawi na waganga wa kifamilia ndipo mtafanikiwa kwa jina la Yesu.
Ukiri
Damu ya Yesu imeniosha, damu ya Yesu imetakasa, damu ya Yesu imeniweka huru, leo nashindana na mamalaka zote za giza, mamlaka zote za mizimu, na mamlaka zote za balaa na mikosi nazipiga kwa damu ya Yesu, mahali popote nilipounganishwa na familia za giza, mizimu, uganga, mshirikina toka kwa damu ya Yesu, leo naingia kwenye familia yetu nateketeza kila vyanzo vya uovu, kila vyanzo vya giza, kila vyanzo vya kishetani, vyanzo vya kuzimu navipiga kwa damu ya Yesu, naviharibu kwa damu ya Yesu, navipasua kwa damu ya Yesu, Amen.