Kyela Mjini SDA Church

Kyela Mjini SDA Church Karibu Katika Page Ya Kanisa La Waadventisa wa sabato Kyela Mjini, Southern Highlands Conference.

02/07/2026
Karibuni Sana Sana
17/06/2026

Karibuni Sana Sana

Shiriki sasa
27/03/2026

Shiriki sasa

12/03/2026

SHC Pastors Singing During Burial Service of Pastor Joseph Msambwa, Who Died By Accident, Held on Njombe SDA church, March 8, 2026

SIKU 10 ZA MAOMBI-KUFUNGULIWAFUNGAMANA NA VIPAUMBELE VYA YESU “Iliwapasa wanafunzi kuendelea mbele na kazi yao kwa jina ...
08/01/2026

SIKU 10 ZA MAOMBI-KUFUNGULIWA

FUNGAMANA NA VIPAUMBELE VYA YESU

“Iliwapasa wanafunzi kuendelea mbele na kazi yao kwa jina la Yesu Kila neno na tendo lao lilitakiwa kuwavuta watu kwenda kwa Kristo, k**a jina lenye nguvu za kuweza kumwokoa mwenye dhambi. Imani yao ilitakiwa kujikita Kwake aliye chimbuko la rehema na uwezo.
Kupitia jina Lake wangepeleka maombi yao kwa Baba nao wangejibiwa. Walikuwa wanatakiwa kuwabatiza watu kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Jina la
Kristo ndiyo ingekuwa kauli mbiu yao, kitambulisho kinachowatofautisha na wengine, kifungo cha umoja wao, mamlaka ya kila tendo lao na chanzo cha mafanikio yao. Chochote kisingetambuliwa katika ufalme Wake kisichochukua jina na neno hili kuu.” (Matendo ya Mitume, Sehemu ya Kwanza, uk. 22)

SIKU 10 ZA MAOMBI – KUFUNGULIWAKaribu katika KUFUNGULIWA. Tunaishi katika nyakati ambazo zinaashiria kwa wazi kwamba Yes...
07/01/2026

SIKU 10 ZA MAOMBI – KUFUNGULIWA

Karibu katika KUFUNGULIWA. Tunaishi katika nyakati ambazo zinaashiria kwa wazi kwamba Yesu anakuja hivi karibuni. Ndiyo maana, katika Siku 10 za Maombi mwaka huu, tunalenga kwa makusudi “kumwalika Roho Mtakatifu abadilishe maisha yetu binafsi pamoja na ulimwengu tunaouishi”. Hii ni safari ya siku kumi ya kumtafuta Mungu kwa unyenyekevu, maombi ya kina, na uamsho unaoongozwa na Roho Mtakatifu.
Kabla ya Yesu kuondoka duniani, aliwaachia wafuasi Wake ahadi kubwa sana. Aliwaambia kuwa angemwomba Baba awape Msaidizi mwingine, Roho wa kweli, ambaye angekaa nao hata milele. Baadaye tena, kabla hajapaa mbinguni, Yesu aliwaagiza wanafunzi Wake wasitoke Yerusalemu bali waingojee Ahadi ya Baba, yaani ubatizo wa Roho Mtakatifu. Hii inaonesha wazi kuwa maisha ya ushuhuda na ushindi hayawezekani bila nguvu ya Roho Mtakatifu.
Hata hivyo, ni jambo la kusikitisha kwamba zawadi hii iliyoahidiwa kwa watu wa Mungu mara nyingi imebaki katika kiwango cha mazungumzo tu. Tunaisoma, tunaijadili, na tunaifahamu kinadharia, lakini mara nyingi hatufikii hatua ya kuifungua na kuishi ndani ya uhalisia wake. Matokeo yake ni ukame wa kiroho, udhaifu wa imani, na kukosa nguvu ya kweli katika maisha ya Kikristo.
Ni muhimu kutambua kwamba ni Roho Mtakatifu pekee anayeweza kuifanya upya mioyo yetu yenye dhambi na kutupatia moyo mpya. Ni Yeye pia anayebadilisha watoto wetu, kuwalinda, na kuwalea katika baraka za Mungu. Zaidi ya yote, ni Roho Mtakatifu anayethibitisha ndani ya mioyo yetu kwamba sisi ni watoto wa Mungu na kutuunganisha na familia ya mbinguni. Habari njema ni kwamba Mungu yuko tayari kabisa kutupatia Roho Mtakatifu kwa wote wanaomwomba kwa dhati.
Ellen G. White anaonya kwamba pale ambapo hitaji la Roho Mtakatifu linapochukuliwa kuwa jambo dogo, hujitokeza ukame, giza la kiroho, kushuka kwa hali ya imani, na hatimaye kifo cha kiroho. Anauliza kwa masikitiko kwa nini watu wa Mungu hawana njaa na kiu ya karama hii, kwa nini hawaombi, hawazungumzii, wala hawahubiri kwa uzito juu ya Roho Mtakatifu, ilhali hii ndiyo njia pekee ya kupokea nguvu kutoka juu.
Biblia inatupatia mfano wa kusisimua katika 1 Samweli 14 kupitia kisa cha Yonathani na mbeba silaha wake. Wakati Mfalme Sauli alikuwa amekaa bila kuchukua hatua, Yonathani alichochewa na imani yake kwa Mungu akaamua kutoka katika eneo la usalama na kukabiliana na jeshi kubwa la Wafilisti. Wakiwa wawili tu, lakini wakiwa wamejitoa kikamilifu kwa Mungu, Bwana aliingilia kati na kuleta tetemeko la Mungu lililotetemesha kambi yote ya adui. Imani ya watu wawili ilimpa Mungu sababu ya kuitikisa ardhi.
Mungu bado anatenda kazi hata leo. Swali ni hili: ni nini kitakachompa Mungu sababu, kwa siku kumi mfululizo, kufanya ardhi itetemeke tena? Miaka elfu mbili iliyopita, waumini wapatao 120 walikusanyika katika chumba cha juu huko Yerusalemu, wakathubutu kuamini ahadi ya Yesu na kuingojea kwa uvumilivu. Roho Mtakatifu alipomiminwa siku ya Pentekoste, waliibadilisha dunia kwa ushuhuda wao, upendo wao, ujasiri wao, na kujitoa kwao.
Roho Mtakatifu anapenda kufanya kazi kutoka ndani kwenda nje. Ndiyo maana Siku 10 za Maombi si tukio la kawaida tu, bali ni mwaliko wa kuanza mtindo mpya wa maisha ya maombi, utii, na uamsho wa kweli. Mungu bado yuko tayari kumimina Roho Wake—kinachohitajika ni mioyo iliyo wazi na tayari kupokea

KARIBU SIKU 10 ZA MAOMBI YA KUFUNGULIWA

Karibu sana Kyela Mjini SDA Church, Leo Ibada ya Maombi ya Siku kumi inaanza, Njoo Tushiriki kwa Pamoja Mibaraka Hii, Ha...
07/01/2026

Karibu sana Kyela Mjini SDA Church, Leo Ibada ya Maombi ya Siku kumi inaanza, Njoo Tushiriki kwa Pamoja Mibaraka Hii, Hakika Tutafunguliwa

Address

Kyela

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kyela Mjini SDA Church posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share