Efatha Church-Kyela

Efatha Church-Kyela Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Efatha Church-Kyela, Church of God, kyela, Kyela.

kanisa la Efatha Kyela lipo kata ya Ipyana 'B' kutokea mjini fuata barabara ya kuelekea bandarini hatua chache kutoka shule ya msingi Mpanda utaona kibao upande wa kulia
>kwa ukombozi, upony

SIKU YA ISHIRINI NA MOJA YA KUFUNGA NA KUOMBA.Leo tunakumbushwa kuwa kuishi kwa haki na uaminifu hutuweka chini ya ulinz...
21/05/2026

SIKU YA ISHIRINI NA MOJA YA KUFUNGA NA KUOMBA.

Leo tunakumbushwa kuwa kuishi kwa haki na uaminifu hutuweka chini ya ulinzi wa Mungu. Katika dunia yenye maadili yaliyopotoka, Mungu anatafuta watu wa kweli katika maneno na matendo yao.

Chagua leo kuishi kwa haki na uaminifu, ili uendelee kufurahia ulinzi wa Mungu na kumpendeza kwa maisha yako ya kila siku.

Mithali 12:21-22 (SUV) “Mwenye haki hatapatikana na msiba wo wote; Bali wasio haki watajazwa mabaya. Midomo ya uongo ni chukizo kwa Bwana; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake.”

*SIKU YA KUMI NA TISA YA KUFUNGA NA KUOMBA*Tunamshukuru Mungu kwa safari hii yenye neema na ushuhuda.  Mungu ametushika ...
19/05/2026

*SIKU YA KUMI NA TISA YA KUFUNGA NA KUOMBA*

Tunamshukuru Mungu kwa safari hii yenye neema na ushuhuda. Mungu ametushika mkono na ameendelea kutupatia nguvu, rehema na ufunuo mpya kila siku.

Hii ndiyo hatua ya mwisho na mara nyingi ni wakati huu ambapo adui hujaribu kutuvuruga au kutuletea uchovu wa kiroho. Lakini sasa si wakati wa kulegea; ni wakati wa kuzama zaidi katika uwepo wa Mungu. Anafanya kazi, hata k**a bado hujaona.

Tumia siku hii kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyokuleta mbali. Tafakari juu ya ukuaji wa kiroho, upendo mpya kwa Neno lake na amani ambayo amekujalia. Mungu aliyeanzisha, atakukamilisha. Kila ahadi yake ni ya kweli.

Wafilipi 1:6 (SUV) “_Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;_”

SIKU YA KUMI NA TANO YA KUFUNGA NA KUOMBALeo tumefika nusu ya safari yetu ya kufunga na kuomba na hii ni neema kubwa kut...
15/05/2026

SIKU YA KUMI NA TANO YA KUFUNGA NA KUOMBA

Leo tumefika nusu ya safari yetu ya kufunga na kuomba na hii ni neema kubwa kutoka kwa Mungu.

Kadri tunavyozidi kusonga mbele, ndivyo Mungu anavyoendelea kutuimarisha, kutufundisha na kutuandaa kwa mambo makubwa yaliyo mbele yetu. Mungu hakuiti urudi nyuma, anakuita usonge mbele. Adui anaweza kukukumbusha yaliyopita, makosa, maumivu au kushindwa kwako, lakini Mungu anaendelea kuzungumza kuhusu kesho yako yenye ushindi na tumaini.

Usikate tamaa katikati ya safari. Endelea kusimama katika maombi na Imani maana Mungu anayekuongoza hawezi kukuacha njiani. Kadri unavyoendelea mbele pamoja naye, ndivyo anavyofungua milango mipya na kukupeleka kwenye kiwango kingine cha neema na ushindi.

*SIKU YA KUMI NA NNE YA KUFUNGA NA KUOMBA*Leo tunaendelea kumtumaini Mungu, tukijua kuwa ana mpango mwema juu ya maisha ...
14/05/2026

*SIKU YA KUMI NA NNE YA KUFUNGA NA KUOMBA*

Leo tunaendelea kumtumaini Mungu, tukijua kuwa ana mpango mwema juu ya maisha yetu. Hata k**a unapitia changamoto au huoni majibu kwa sasa, usikate tamaa maana Mungu bado anatenda kwa wakati wake.

Mwamini Mungu kwa moyo wote, maana mwisho wa safari yako itajaa ushindi, amani na kicheko tele.

Yeremia 29:11 “_Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi ni mawazo ya amani wala si ya mabaya._”

SIKU YA KUMI NA TATU YA KUFUNGA NA KUOMBAK**a dhahabu ipitavyo kwenye moto ili isafishwe na kuwa ya thamani zaidi, ndivy...
12/05/2026

SIKU YA KUMI NA TATU YA KUFUNGA NA KUOMBA

K**a dhahabu ipitavyo kwenye moto ili isafishwe na kuwa ya thamani zaidi, ndivyo na wewe unapopita katika mchakato huu wa kufunga na kuomba. Usihuzunike wala kukata tamaa, bali furahia maana Mungu anakutengeneza upate kuwa dhahabu safi mbele zake.

*SIKU YA KUMI NA MOJA YA KUFUNGA NA KUOMBA**Isaya 60:11* “_Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wa...
10/05/2026

*SIKU YA KUMI NA MOJA YA KUFUNGA NA KUOMBA*

*Isaya 60:11* “_Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku…_”

Tunapoingia katika wiki hii mpya ya safari yetu ya kufunga na kuomba; na tuweke imani yetu kwa Mungu kwamba ataifungua kila milango iliyokuwa imefungwa mbele yetu. Pale palipokuwa na kuchelewa, Mungu ataleta majibu. Pale palipokuwa na vikwazo, ataweka njia.

Wiki hii isiwe ya kawaida, bali iwe wiki ya neema, kibali, mafanikio na ushuhuda mpya. Mungu atawainua watu wake, atawaleta karibu na nafasi zao na kuwafungulia milango ambayo hakuna mwanadamu ataweza kuifunga.

Wiki hii iwe mwanzo wa ushuhuda mpya katika maisha yako.

Sunday service picture highlightsEfatha Church-Kyela
10/05/2026

Sunday service
picture highlights
Efatha Church-Kyela

Matukio katika picha Tarehe 09/05/2026Ziara ya Mchungaji kiongozi Mkoa wa Mbeya, Mch. Joshua Mwingira
09/05/2026

Matukio katika picha
Tarehe 09/05/2026

Ziara ya Mchungaji kiongozi Mkoa wa Mbeya, Mch. Joshua Mwingira

*SIKU YA TISA YA KUFUNGA NA KUOMBA*Katika nyakati za changamoto, usiharakishe kulaumu au kukata tamaa bali kaa chini uta...
09/05/2026

*SIKU YA TISA YA KUFUNGA NA KUOMBA*

Katika nyakati za changamoto, usiharakishe kulaumu au kukata tamaa bali kaa chini utafakari. Mara nyingi Mungu huzungumza kupitia mawazo ya utulivu na kukukumbusha kanuni sahihi za maisha.

Unapomruhusu Mungu akuongoze, atakupa hekima, njia sahihi na majibu ya kweli.

Mhubiri 7:14 “_Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri..._”

*SIKU YA NANE YA KUFUNGA NA KUOMBA*Yale yanayoonekana magumu leo, Mungu anayageuza kuwa ushuhuda kesho. Hakuna machozi w...
08/05/2026

*SIKU YA NANE YA KUFUNGA NA KUOMBA*

Yale yanayoonekana magumu leo, Mungu anayageuza kuwa ushuhuda kesho. Hakuna machozi wala maombi yako yatakayopotea mbele zake. Endelea kuwa mtu wa imani, maana Mungu bado anatenda na atakufikisha mahali pa ushindi.

Warumi 8:28 “_Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema._”

IBADA YA MFUNGO NA MAOMBI | SIKU YA 7 | 07.05.2026 Matukio katika picha.
07/05/2026

IBADA YA MFUNGO NA MAOMBI | SIKU YA 7 | 07.05.2026

Matukio katika picha.

Address

Kyela
Kyela
1203202

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church-Kyela posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category