Prophet AJ Mazengo

Prophet AJ Mazengo Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Prophet AJ Mazengo, Religious organisation, www. facebook. com/Prophet AJ Mazengo, Kisesa.

This is the only OFFICIAL page for Prophet AJ Mazengo and the general overseer of AJ Mazengo Ministries, Follow today, and receive biblically grounded teachings that will change your life and help you on your journey to eternal salvation in Christ.

Bwana Yesu asifiwe.Kanisa la True Light Church Dar es salaam tunaomba kipekee kukukaribisha kwenye semina ya Maalumu ya ...
03/04/2026

Bwana Yesu asifiwe.

Kanisa la True Light Church Dar es salaam tunaomba kipekee kukukaribisha kwenye semina ya Maalumu ya Pasaka ambayo itafanyika siku ya Ijumaa pamoja na Jumapili .

Mtumish wa Mungu Askofu Lotha Laizer kutokea Arusha atakuwa mgeni akifundisha na kuombea watu kwenye semina hii.

Kwenye semina hii Mtumishi wa Mungu atakufundisha NAMNA DAMU YA YESU INAVYOWEZA KUKUSAIA KUTOKA KWENYE VIFUNGO VYA SHETANI.

Watu wengi hawajui Namna Damu ya Yesu inavyoweza kuwasaidia kumshinda shetani na Kila njama zake .

Ufunuo wa Yohana 12:11
[11]Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
And they overcame him by the blood of the Lamb, and by the word of their testimony; and they loved not their lives unto the death.

Semina hii itafanyika Ijumaa ya Pasaka tarehe 3/4/2026 Kuanzia saa kumi jioni na Jumapili ya Pasaka Kuanzia saa nne Asubuhi .

Ni siku mbili tu za KUJUA Siri za rohoni za Namna ya Kumshinda Shetani na Njama zake .

Kwenye semina hii tutakuwa na Waimbaji mbalimbali wakiongozwa na Wana wa Asafu .

Nikuombe popote ulipo USIKOSE kwenye semina hii muhimu .

WAALIKE WATU WENGI KADIRI UWEZAVYO .

Wako ,
Prophet AJ Mazengo
Mchungaji Kiongozi
True Light Church _Worldwide .
MAWASILIANO 0716854881

JESUS IS ALIVE COME AND SEE

28/02/2026

Bwana Yesu asifiwe.
Kipekee Naomba kukukaribisha kwenye KONGAMANO LA WATUMISHI WA MUNGU WOTE TANZANIA .Kongamano hili linaenda Kwa jina la FLYING WITH WINGS MINISTERS CONFERENCE ambalo litafanyika jumapili hii tarehe 01/03/2026 Kuanzia Saa Nane Mchana kwenye Kanisa la True Light Church _Tegeta Kwa Ndevu Darajani.

Kongamano hili litahudhuriwa na Wazee wa zamani ,Mababa zetu wa Sasa na Kizazi kipya ambacho ndiyo kinachipukia na kinaandaliwa kuchukua kijiti .Niwaombe Wazee wetu Mababa Askofu ,Mitume , Manabii , Wainjilisti , Wachungaji,Walimu , Viongozi wa Makanisa na Watumishi wote wa Mungu mnaopatikana kwenye mji wa Dar es salaam na nchi ya Tanzania kuhudhuria Kongamano hili la siku Moja .

Haya ni Majira ya Kanisa la Tanzania kusimama pamoja Kwa ajili ya ufalme wa Mungu na kazi yake .

Tutakuwa na muda mzuri wa Kujifunza Neno la Mungu Kwa kina zaidi .K**a una kiu ya kuacha alama Kwenye uso wa nchi uliyopewa uimiliki Usipange kukosa .

Wako ,
Prophet AJ Mazengo
True Light Church World wide
MAWASILIANO Vd 0769684881 Tg 0716854881

KWA GARAMA YOYOTE USIKOSE

27/02/2026

Bwana Yesu asifiwe.
Kipekee Naomba kukukaribisha KWENYE KONGAMANO LA WATUMISHI WA MUNGU WOTE TANZANIA .Kongamano hili linaenda Kwa jina la FLYING WITH WINGS MINISTERS CONFERENCE ambalo litafanyika jumapili hii tarehe 01/03/2026 KUANZIA Saa Nane Mchana kwenye Kanisa la True Light Church _Tegeta Kwa Ndevu Darajani.

Matarajio yetu na maandalizi yetu ni kukusanya zaidi ya Watumishi 300 .K**a rafiki na mtoto wa Huduma ya True Light Church Naomba nisaidie kuendelea kuwaalika watu kadiri uwezavyo .

Naomba nisaidie kusambaza poster hizi Kila MAHALI .

Kwenye Kongamano hili tutakuwa na Mababa Askofu ,Mitume ,Manabii , Wainjilisti,Wachungaji,Walimu ,Watenda kazi na Viongozi wote wa Makanisa na WAIMBAJI wa nyimbo za Injili zinazofanya vizuri Kwa sasa Katika jiji la Dar es salaam

HAYA NI MAJIRA YA KUINUA KIZAZI CHA WATU WENYE MOTO WA KIUNGU

KWA GARAMA YOYOTE USIKOSE

26/02/2026
Kanisa la True Light Church Tlc  _Dar es salaam. linakuKaribisha kwenye Ibada maalumu ya UKOMBOZI WA FAMILIA .Mara nying...
21/02/2026

Kanisa la True Light Church Tlc _Dar es salaam. linakuKaribisha kwenye Ibada maalumu ya UKOMBOZI WA FAMILIA .
Mara nyingi adui hupambana na Msingi wa Familia Kwa sababu familia ndiyo lango la kutengeneza watu imara na watakaokuwa na matokeo Katika kizazi husika .

JUMAPILI hii Mtumishi wa Mungu ambaye amekuwa baraka katika ardhi ya Tanzania na nje ya Tanzania Bishop Laizer Pastor atatufundisha NAMNA UNAVYOWEZA KUINUA FAMILIA YENYE MISINGI IMARA na atafanya Maombi ya ubarikio Kwa familia yako Kwa ajili ya Mwaka 2026

Mara nyingi Adui hupambana na Familia na Uzao wa FAMILIA na hatma za wanafamilia .

Musa alipitia vita Katika umri wake mdogo .Yesu alikutana na vita Katika Mwanzo wake mdogo .
Samson alikutana na upinzani Katika Mwanzo wake mdogo.

K**a mkono wa Mungu usiposimama na wewe pamoja na Familia yako Kuna baraka ambazo Mungu amezikusudia Kwako na familia yako lakini hazitakaa zidhihirike katika macho ya nyama.

Ungana nasi Kwenye Ibada maalumu ya Familia Kwenye kanisa la True Light Church_Tegeta Kwa Ndevu Darajani.
Ibada hii itaanza saa tatu na nusu Asubuhi .

Wasiliana nasi Kwa Voda 0769684881 Tigo 0716854881

Wako,
Prophet AJ Mazengo
True Light Church (TLC)

Jesus is Alive ,Come and See

Kanisa la True Light Church Tlc _Dar es saleem linapenda kuwakaribisha Vijana WA ZAMANI na VIJANA wote wa sasa Yaani vij...
14/02/2026

Kanisa la True Light Church Tlc _Dar es saleem linapenda kuwakaribisha Vijana WA ZAMANI na VIJANA wote wa sasa Yaani vijana wa Gen A mpaka Gen Z kwenye kutaniko la waamini wapendanao katika Kristo Yaani USIKU WA NIMPENDAYE KATIKA KWELI.

3 Yohana 1:1 Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.

Huu ni Mwaliko maalumu KWAKO .NJOO tucheze rumba ya Yesu.Ni Jumapili HII kuanzia saa 12 jioni .

Tunakuomba uwaalike wale uwapendao katika Bwana.

Ibada ya Jumapili Asubuhi itaanza SAA 3:00 Asubuhi mpaka saa 6:30 MCHANA

NA
Usiku WA Nimpendaye katika KWELI utaanza saa 12:00 jioni
NJOO Umependeza mpaka malaika wakushangae

Usiku huu utahudhuriwa na Watu maarufu na wenye mguso chanya katika KIZAZI HIKI Wewe ukiwa miongoni mwao

13/02/2026

POPOTE ULIPO KWENYE MJI WA DAR ES SALAAM

Karibu Jumapili hii kwenye USIKU WA NIMPENDAYE KATIKA KWELI
Usiku huu ambao ni maalumu kwa wale wapendanao na wampendao Kristo umeandaliwa na Idara ya Vijana ya kanisa .

Kwenye siku hii kutakuwa na keki maalumu ya KUMBUKIZI YA MIAKA KADHAA YA NDOA kwa Wana ndoa wazamani na wapya .

Tunaomba popote ulipo jiandae na MWANDAE na Mwenzako .

Wale mlioko single msiwaze itakuwaje yamkini Bwana akawa na JIBU lako siku hiyo na Yeye aliyezifanya mbingu atakushangaza .

Wazee wenzangu karibu tuungane na Vijana ili kuwatia akili ili wajue yawapasayo kutenda

NI JUMAPILI HII KUANZIA SAA KUMI NA MBILI JIONI

Ukibaki Nyumbani ni Kwa Hasara yako.

Kanisa la True Light Church Tlc _Dar es salaam linakukaribisha kwenye Ibada maalumu ya ARISE AND SHINE (IBADA MAALUMU YA...
07/02/2026

Kanisa la True Light Church Tlc _Dar es salaam linakukaribisha kwenye Ibada maalumu ya ARISE AND SHINE (IBADA MAALUMU YA KUINUKA NA KUANGAZA )

Kwenye Ibada hii ya kuuendea mwaka 2026 na kuiendea Nuru yako Kwa mwaka 2026 tutakuwa na Maombi maalumu kwa ajili ya Kuk**ata Malango ya Nuru Kwa mwaka 2026 .

JE ni Maeneo Gani unatamani Nuru ikuangazie Kwa mwaka 2026
JE ni kwenye biashara , Au kwenye ndoa , Au kwenye kupata uchumi imara au ni KWENYE kupata KAZI ?
JUMAPILI ya kesho Bwana atakushangaza.

BIBLIA inasema

Isaya 60:1-3
[1]Inuka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja,
Na utukufu wa BWANA umekuzukia.

[2]Maana, tazama, giza litaifunika dunia,
Na giza kuu litazifunika kabila za watu;
Bali BWANA atakuzukia wewe,
Na utukufu wake utaonekana juu yako.

[3]Na mataifa wataijilia nuru yako,
Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.

Mungu anatuasa huwezi Kuangaza mpaka ufanye tendo la IMANI la kuinuka .

Kuinuka kwako kunahusisha kumtafuta Bwana kwa Bidii sana ili Nuru yako iangaze katika mahali unapotamani.

Usikose Ibada hii muhimu itakayokupa Kuangaza na kuja kwa Nuru yako katika maisha yako kwenye Kila eneo la maisha yako.

Ibada hii itaanza saa tatu na nusu Asubuhi .

Fuatilia mambo haya ambayo Bwana alisema na Mtumishi wa Mungu Prophet AJ Mazengo Kwa ajili ya Taifa na  kanisa la mahali...
17/11/2025

Fuatilia mambo haya ambayo Bwana alisema na Mtumishi wa Mungu Prophet AJ Mazengo Kwa ajili ya Taifa na kanisa la mahali Pamoja la Kanisa True Light Church Tlc .
Mambo haya yalisemwa mwaka 2024 ,Kuna mengine ambayo Bwana anayatimiliza sasa au yanatokea sasa .

Bado tunayonafasi mbele za Bwana k**a taifa endapo Viongozi wetu wa kisiasa wataamua kuvaa magunia na kuomboleza k**a kipindi cha Yona na taifa la Ninawi .

Address

Www. Facebook. Com/Prophet AJ Mazengo
Kisesa

Telephone

+255716854881

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Prophet AJ Mazengo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Prophet AJ Mazengo:

Share